Sababu kwanini Matajiri wengi hawaendi Makanisani, na wakienda wanaenda wakiwa wamechelewa sana

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,721
1. Waumini na watumishi, ombaomba. Kuna watu mabingwa wa kuscan watu wenye uwezo na kuanza kuwapiga mizinga. Wakati mtu kaja kuabudu waabuduji wenzake na watumishi wanamvizia wampige vibomu. Hali hii ikizidi inafukuza watu wenye uwezo kifedha. Inakuwa ni kero.

2. Mahubiri mengi yamelenga masikini wa vipato na magonjwa. Hivyo wanajisikia wapweke maana wanaingia kanisani na kiu ya kulishwa neno wanakutana na maneno yasiyowahusu.

3. Umasikini wa fikra kudhani kiongozi wa sasa lazima awe na pesa. Hivyo Wakikujua unapesa nyingi utatafutia kacheo hata kama hujui chochote. Ili wasiharibu wanaamua kukimbia au kujichelewesha.

4. Kanisa linakosa ladha maana hakuna maneno ya kuwachoma mioyo na dhambi zao. Maneno ya watumishi yatakuwa na tahadhari kali ili wasimkwaze mtu tajiri au maarufu kanisani. Anaingia na kuondoka na matatizo yake, haoni tofauti ya kanisa na vikao na wadau.
 
1: Waumini na watumishi, ombaomba. Kuna watu mabingwa wa kuscan watu wenye uwezo na kuanza kuwapiga mizinga. Wakati mtu kaja kuabudu ...
Unaposema kanisa unamaanisha dhehebu au chama cha wahuni fulani?

Hata ccm ina makanisa mengi tu hapa nchini, hebu funguka bado sijakuelewa ndugu
 
Maskini huenda kanisani kuomba miujiza.

Masikini mwenye hela haendi kabisa kanisani.

Tajiri huenda kanisani kutoa sadaka na kushukuru.
 
Back
Top Bottom