Sababu 3 kwanini Watu wanakudharau, wanakuchukulia poa, wanakupanda kichwani

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
16,464
35,691
Sababu ya kwanza mpaka ya tatu

1.UNAKUBALIKI UKOSOLEWA/KUPONGEZWA BILA KUFANYA UCHUNGUZI

Ni rahisi sana kukaribisha watu wenye nia mbaya ya kukudhuru na kukuangamiza kabisa katika maisha yako kama upo na tabia ya kukubali kusifiwa sana au kukosolewa kwa maneno makali sana bila kufanya uchunguzi.

Mtu kukusifia sana haina maana atakuwa na nia njema kwako, vilevile mtu kukukosoa haina maana upo na makosa au mapungufu yoyote.

Badala ya kukubali kukosolewa kwa maneno makali sana yenye lugha ya udhalilishaji, dharau, kejeli na vijembe kutoka kwa mzazi wako, mlezi, rafiki,mwenza wako, mshauri wao , mwalimu wako, mfanyakazi mwenzako, mwajiri wako, kiongozi wako wa dini, msomi au mtaalam wa fani au taaluma yako ,au supervisor wako n.k badala ya kujiona mkosaji,kujiona laana,kujiona kituko,kujiona kitu cha aibu mbele yake jaribu kuangalia nia ya mkosoaji wako.

Siyo kila mkosoaji wako anakuwa na nia njema kwako,wapo watu wanakukosoa kwa sababu ya chuki binafsi,,wivu,kinyongo,hisia za kisasi wala siyo kwa sababu ya dosari zako au makosa yako ya kiutendaji.

Wapo watu ni wakosoaji wako wakubwa kwa sababu ni washindani wako kibiashara,wengine kwa sababu wanataka ukate tamaa,wengine kwa sababu wamekata tamaa ya maisha wanataka kumaliza hasira na chuki zao kwako.

Badala ya kuumizwa na wakosoaji wako tenganisha wakosoaji wako sehemu mbili.
I.Mkosoaji mwenye nia njema - Huyu anakosoa kwa nia ya kujenga ,kwa nia ya kukusaidia ufanikiwe.Utamjuaje huyu anakosoa kwa lugha ya heshima,anakupa pongezi kwa utendaji wako,anaonyesha madhaifu yako bila kudharau,bila kukejeli bila kukushusha thamani,anaonyesha madhaifu yako kisha anatoa mapendekezo ya namna bora ya kuboresha kazi zako.Sikiliza sana maneno yake utafika mbali.

II.MKOSOAJI MWENYE NIA MBAYA,CHUKI NA WIVU NDANI YAKE

Huyu anakukosoa kwa lugha ya udhalilishaji ikiwemo matusi, kukashifu vibaya sana utu wako,anaweza kukashifu imani ya dini yako, anaweza kushambulia vikali sana kazi zako na utendaji kazi wako lakini ukihoji wapi kuna dosari katika kazi zako ili ufanye maboresho badala ya kujibu hoja atakuporomoshea matusi ya nguoni,kisha atageuza mada,atakujibu vibaya sana.

Ukimwambia atoe mapendekezo ya suluhu ya makosa au mapungufu yako hajui zaidi ya kukushambulia kwa maneno makali sana.

Mkosoaji wa aina hiyo ni ADUI mkubwa kwako na anataka kukudhuru na kukuangamiza kabisa.
Epuka kumnyenyekea,epuka kuomba msamaha,epuka kumpa ushauri,epuka kumbembeleza,epuka kutaka huruma yake au faraja yake kwa sababu hana nia njema bali anataka KUKUDHURU.

Ukijenga ukaribu naye atakuja kukudhuru siku za baadaye ukishampa taarifa zako za siri,tena atavunja ukaribu na wewe ghafla tu bila sababu zozote za msingi.

2.UNAAMINI SANA WATU WENYE MAMLAKA YA KIUONGOZI JUU YAKO BILA KUHOJI CHOCHOTE
Unaweza kuhatarisha maisha yako kama ni mtu ambaye unaamini sana Watu wengine kupitiliza.
Ukiwa mtoto unaamini mzazi wako anajua kila kitu, unaamini mzazi wako ni mwema sana kwako haijalishi ataongea au atakufanyia kitu gani unaamini anafanya kwa nia njema.

Lakini ukiwa mkubwa utabaini tofauti.

Siyo kila mtu mwenye mamlaka ya kiuongozi,au umri mkubwa unatakiwa kumuamini.
Kwenye kundi la kondoo mbwa mwitu anaweza kujipachika bila kujulikana...

Usimuamini mtu yeyote kupitiliza kwa sababu Watu wengi wanatumia fursa ya kuaminika sana kwenye jamii kuleta maumivu makali sana.

Mtu kuwa kiongozi wako wa dini, kisiasa,kuwa mzazi,mlezi, mwalimu wako, mshauri wako,bibi,babu ,mzee wa miaka 70 n.k bado haina maana kwamba mtu huyo ni malaika.

Mtu kuvaa nguo za gharama, kutembelea gari la kifahari,kuwa na muonekano mzuri sana,kuwa na kazi au cheo kikubwa ,mtu kuwa maarufu,mtu kuwa na nguvu ya ushawishi au wafuasi wengi sana haina maana kwamba yeye ni malaika bali anabaki ni binadamu kama walivyo binadamu wengine.

Unaweza kuibiwa, kudhulumiwa, kutapeliwa,kuporwa, kunyang'anywa mali,kusalitiwa na mtu ambaye kwako unamuheshimu kupitiliza kama mzazi , rafiki, ndugu wa damu, mwalimu wako, mshauri wako, mwajiri wako,mfano bora wa kuigwa (role model), mwenza wako, kiongozi wako wa dini.n.k

Kuamini watu wengine kupitiliza kunaweza kuhatarisha maisha yako.

3.HUWA UNAWEKA VISINGIZIO JUU YA MAKOSA NA TABIA ZA WAPENDWA WAKO

Sababu nyingine inayofanya watu wengine kukudharau,kukupanda kichwani,kukuchukulia poa,kukutumia kwa maslahi binafsi ni kwamba unaweka visingizio juu ya tabia za wapendwa wako wakifanya makosa tu unasema hawajafanya makusudi.

Kuna watu kwa sababu wanajua wewe ni mpole,upo na huruma sana,unasamehe makosa haraka, uvumilivu uliopitiliza,haupendi ugomvi wala migogoro wanatumia fursa hiyo kufanya makosa kwa makusudi kabisa kisha wanageuza kibao kwako.

Unakuta mtu anakutukana matusi ya nguoni kisha atageuza mada, atakujibu vibaya, mwengine anafanya makosa kwa makusudi kabisa kisha anajifanya amenuna anataka umuombe msamaha kwa makosa ambayo amefanya yeye.

Badala ya kuweka visingizio juu ya tabia za wapendwa wako acha wapate madhara ya tabia na makosa yao.
Kila mtu anawajibika juu ya tabia zake na makosa yake
mpendwa wako akifanya makosa anatakiwa kuwajibika kwa makosa hayo siyo kumkingia kifua ili kulinda heshima na taswira yake kwenye jamii.
 
Lisu ni mwenyekiti mpya chadema
 
Nimeipenda hii
 
kama huna P£$A hakuna atakayekuHE$HIMU, utadharaulika tu.
Na ukiamini kuwa ukiwa na pesa ndio utaheshimiwa ni ukosefu wa maarifa na fikra yakinifu,, Mwanadamu huwa hakuheshimu kamwe kama huna mamlaka juu yake!!

Its either umemuoa, umemuajiri, au unamdhamini kwenye jambo ambalo yeye na wengine hawawezi kulisimamia..

Hicho kipindi cha previllege kikiisha mwanadamu anachukua heshima yake anaweka mfukoni

Over.. Ndio maana ni watu wachache sana wanaweza kuacha kuhudhuria kikao ofisini kwao kisa baba yake kamtuma aende kiwandani kesho asubuhi akachukue machicha ya ng'ombe.. Why?? Jibu ni kwamba heshima ya baba iliishia pale walipoacha kula ugali wa shikamoo,, Japo deeply wanakosea sana but there is nothing you can do about it..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…