Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,057
- 55,952
1. Chini ya utawala wake kuna Ombwe la utawala bora na unaoheshimu sheria na katiba
Kitu cha msingi kabisa ambacho raisi anapaswa kukishika kama mboni ya jicho lake ni kutimiza kiapo alichoapa mbele ya Mungu, na wanadamu ni kuheshimu katiba, tumeona katika utawala huu mambo kadhaa yakifanywa bila kuheshimu katiba ya nchi wala kiapo kwa mfano kitendo cha kuzuia haki za vyama vya siasa kufanya shughuli halali za siasa zilizokuwepo kwa mujibu wa sheria na katiba ni mfano mmojawapo.
Lakini kibaya zaidi, wakati mwingine Utawala wa Magufuli ulienda extra mile ili kuzibadili sheria ambazo zinawapa haki watu wengine ili kupora haki hizo, mifano ya sheria hizo ni sheria ya takwimu ambayo waliitunga ili kuminya uhuru wa watu kupata na kutumia takwimu, lengo likiwa ni dhahiri kwamba serikali haikutaka ukosoaji kupitia takwimu zinazoonyesha failure katika utendaji wake wa kila siku.
Pia sheria ya juzi ya kuwapa kinga waziri Mkuu, Spika na naibu Spika ya kutoshitakiwa wao kama wao ni. mfano mmojawapo wa namna utawala wa Magufuli unavyojijengea mazingira ya kutotaka kuwa accountable kwa matendo ambayo huenda yakawa kinyume cha sheria!. Tukiacha hilo, hata usitishaji wa maslahi ya wafanyakazi wa umma ambayo yapo kwa mujibu wa mikataba ya ajira nayo ni mfano mwingine kwa nini utawala wa Magufuli umekuwa hauheshimu sheria za nchi wala kanuni za utawala bora.
Hata jinsi utawala wake ulivyoendesha uchaguzi wa serikali za mitaa, ni aibu kubwa mno, ule siyo uchaguzi ni uchafuzi wa demokrasia.
Hata kwenye hotuba yake ya kuvunja bunge, Magufuli hakugusia popote suala la utawala bora
2. Teuzi za Magufuli zinanuka udini
Mwanzoni mwa utawala wa Magufuli Waislamu walianza kunong'ona misikitini, kwenye vikao vyao vya kijamii kama vile harusi na misiba kuwa utawala huu unawaweka pembeni sana katika teuzi za shughuli ya umma.
Ukweli wa suala hili aliuona hata Profesa Kitila Mkumbo wakati huo mwanzoni kabisa mwa utawala huu mwaka 2016 hajapewa ulaji na kabla hajawahi kufikiri kuwa anaweza kuteuliwa, alipoandika makala juu ya utawala huu na aina ya teuzi ilizokuwa ikizifanya. Kitila aliandika kuwa ipo haja ya kubalance makundi mbalimbali ya kijamii katika kuunda serikali na utumishi wa serikali hiyo.
Tukiangalia teuzi alizozifanya Magufuli kiufupi Waislamu ni kiduchu ni kiduchu sana kuliko uwiano halisi wa jamii hiyo katika nchi. Swali la kujiuliza ni kuwa kwa nini kila teuzi anayofanya Magufuli inayoinvolve Waislamu na Watu wa dini nyingine kwa nini Waislamu wawe wachache always, kama hii siyo deliberate ni kitu gani?
Hata ukiangalia baraza la mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi wilayani, wakurugenzi mikoani, wenyeviti wa bodi za mashirika ya umma, mabalozi, Kwa nini waislamu ni wachache sana?. Je waislamu hawana vigezo vya kutosha?, Je waislamu hawasomi shule hizihizi wanazosoma wengine?
Hoja ya kusoma siyo hoja tena maana waislamu wenye elimu ya kutosha wapo wengi sana na hii ni kwa mujibu wa rekodi. Sheikh Khalifa alitoa orodha ya Ma Dr wanaofika 100 waislamu kuonyesha kuwa hoja ya elimu siyo hoja ya msingi!
Magufuli kuwa karibu na BAKWATA na kusaidia kujenga msikiti au kuwasaidia masheikh rafiki zake mambo yao siyo hoja ya msingi kuonyesha kuwa utawala wake umekuwa positive na kutenda haki ipasavyo kwa jamii ya waislamu.
Waislamu hawana shida ya majengo makubwa ili kuwa misikiti waislamu wana shida ya kutendewa haki katika nchi yao, wawe treated fairly kwenye kuijenga nchi na kugawana keki ya Taifa. Kama ni misikiti wanaweza kujenga wao wenyewe!. Magufuli na wasaidizi wake lazima watambue kuwa hili linawakwaza sana waislamu, linawauma sana, hawalipendi na wataliaddress mbele yake muda muafaka ukifika lakini salamu zimfikie aelewe kuwa waislamu wanataka kuona uwakilishi unaolingana na proportion yao nchini katika ajira, utumishi wa umma na serikalini.
3. Utawala wa Magufuli haujali maslahi ya Mfanyakazi
Magufuli aliingia madarakani kwa kuahidi kuboresha maslahi ya mfanyakazi, lakini mpaka leo hii hakuna nyongeza za mishahara zilizopo kwa mujibu wa mikataba yao ya ajira na sheria, Kumekuwepo na manung'uniko mengi katika hili suala, Katika hili suala, Magufuli ana kazi ngumu ya kuwashawishi wafanyakazi wa umma wamuone kama mtu anayestahili kuongezewa muda
4. Kumekuwepo na propaganda kubwa kuliko ukweli na hali halisi
Tukiangalia hali ya nchi ambayo vijana wanamaliza vyuo, elimu za sekondari na shule za msingi wanazidi kujazana mitaani. Uwezo wa serikali kutoa ajira na kutengeneza ajira mpya ukiwa ni. mdogo, unajiuliza je Magufuli ana sababu gani za kuaminiwa kupewa tena miaka mitano mingine. Juzi hapa wakati akilihutubia bunge alisema ametengeneza ajira milioni 6!!!. Hii ni namba ya kubumba, ni propaganda iliyowazi!. Kwanza takwimu yake hiyo inatofautiana na takwimu aliyotoa waziri mkuu, lakini pia takwimu zinaonyesha kupungua kwa ajira zinazotolewa na serikali (permanent and pensionable), hizo figure za ajira milioni 6, Magufuli alizipata wapi, zaidi ya kuwa hizo figure zimetiwa chumvi?.
Mtindo huu wa propaganda za kuzidi kiasi ndiyo maana leo hata TV ya Taifa TBC kazi yao ni kuimba mapambio tu kuanzia asubuhi hadi usiku. Jamani Chema chajiuza kibaya chajitembeza. Acheni kupiga mayowe, tuachieni wananchi tuone sisi wenyewe!
5. Kuliweka bunge mfukoni na kuliondolea mamlaka yake
Katika kipindi cha utawala wake, Magufuli kafanikiwa kuliweka bunge mfukoni na kulivuka kwa kufanya mambo ambayo kikawaida ni lazima yafanyike kwa ridhaa ya bunge. Kwa mfano manunuzi ya ndege za awali kabisa hayakuzingatia matakwa haya. Bunge ndiyo mamlaka inayopaswa kuidhinisha malipo makubwa kabisa kama yale ya manunuzi ya ndege hizo. Lakini serikali ya Rais Magufuli ilienda yenyewe kama yenyewe kununua hizo ndege bila kupitishwa na bunge, Katika nchi yenye kuheshimu checks and balances hilo ni kosa kubwa sana, ni kosa la kikatiba lakini pia ni matumizi mabaya ya madaraka.
Kwa bahati mbaya sana katika bunge lililopita tulikuwa na Spika ambaye hakutambua ipasavyo nafasi yake kama mkuu wa mhimili mmoja wa dola wenye nguvu sana, akaamua kuwa mtumishi mwaminifu wa mhimili wa serikali ndiyo maana akafikia hatua ya kumfanyia mtu kampeni bungeni aendelee kutawala kinyume cha utamaduni wetu wa vipindi viwiliviwili vilivyoheshimiwa na maraisi wetu waliopita. Unfortunately speaker wetu huyu alishiriki kikamilifu kwenye kutunga sheria ambazo zinazidi kuuongezea nguvu mhimili wa serikali kujichimbia chini zaidi kwa kunyang'anya uhuru na haki kidogo ambazo wananchi na taasisi za kiraia walikuwa wakizienjoy sana kwa miaka takriban 30 iliyopita!
6. Uchumi wa makaratisini
Utawala wa JPM umeendelea kudai kuwa uchumi umekua, lakini hali halisi ya hiyo kauli ni tofauti huku mtaani. Huku mtaani sekta binafsi iko hoi, biashara zinasuasua sana, Wakulima wana hali ngumu, Hata bajeti ya kilimo haijawahi kupelekwa kufika hata 30% tangu utawala huu uingie madarakani.
Vyuma mtaani bado vimekaza kwelikweli. Ukizingatia hali ngumu ya biashara na kusuasua kwa sekta binafsi, ni vigumu sana kuwaconvince watu juu ya performance ya utawala huu.
7. Kukua na kuongezeka sana kwa deni la Taifa
Raisi Magufuli anasema tunajenga miradi kwa fedha zetu za ndani, sawa, maana hata tukikopa tutalipa, lakini tunakopa baadhi ya mikopo kwa interest kubwa sana, tumeona mikopo ya SGR kupitua Standard chattered bank, ni mikopo ambayo riba yake siyo rafiki. Lakini ukiacha mbali na hilo, deni la Taifa kwa ajili ya kufinance hiyo miradi linakua kwa kasi kubwa mno, Ndani ya miaka hii michache ya Magufuli tumeshakopa pesa nyingi kuliko tulizokopa katika kipindi chote cha utawala wa awamu ya nne!.
Sasa tuoo katika hii hali lakini bado miradi haijakamilika, Je ikikamilika hali ya deni la Taifa itakuwaje?. Kibaya zaidi pesa nyingi tunazokopa zinarudi nje ya nchi. Kama ni ujenzi wa SGR, chuma tunachotumia tunakitoa nje, hii maana yake dola nyingi sana tunazokopa zinarudi nje badala ya kutumika humu humu nchini.
8. Tumepoteza ushawishi wa kidiplomasia ndani ya Afrika
Ndani ya utawala huu tumeona namna ambavyo nchi yetu imekua ikipoteza mahusiano mazuri ya kidiplomasia na nchi nyingine, ikifikia hatua hadi ya kufungiana mipaka.
Tumeona raisi wa South Africa akilalamika kuwa Mwenyekiti wa SADC ambaye ni rais Magufuli hachukui initiative ya kuitisha vikao vya kikanda kujadili suala la COVID-19,Tumeona rais tangu aingie madarakani hajawahi kusafiri nje ya ukanda wa kusini mwa Equotor, hadi vikao vya waafrika wenzetu vya AU hajawahi kwenda hata mara moja. Katika mazingira hayo ni dhahiri kuwa ushawishi na diplomasia yetu iko chini. Kuna mikutano inahitaji mkuu wa nchi awepo, hata kama akituma muwakilishi, hiyo inakuwa haitoshi maana uzito wa vikao husika ili viweze kuwa na tija inabidi awepo mkuu wa nchi mwenyewe. Lakini pia tukiachilia mbali hilo, Mkuu wa nchi akikutana na wawekezaji wakubwa ambao wako huko anaweza kwa urahisi kuwashawishi kuwekeza nchini kuliko kama wakikutana na wawakilishi wake.
9. Watu kupotea na Wasiojulikana kuendelea kutojulikana
Jukumu la awali kabisa la serikali yoyote ni kulinda uhai wa raia wake, na kuhakikisha usalama wao.
hadi leo tunapoongea serikali ya awamu ya Tano haijafanya uchunguzi wa nani alimpiga Tundu risasi, hatujui wapi alipo Azory Gwanda, Ben Saanane na hakuna taarifa za uchunguzi wowote wa matukio hayo. Hilo linatosha kuuhoji utawala huu ili utupe majibu, kulikoni haujishughulishi kuhusiana na masuala hayo?. Je si ni jukumu la serikali kufuatilia jinai na kuhakikisha haki inatendeka?, kwa nini utawala huu hauna interest na raia wake hawa.
Kwa hiyo tunapata wasiwasi kuwa kama serikali haina interest ya kufuatilia usalama wa watu hawa. Je ni. kipi kitatuhskikishia kuwa kama ukipewa muda mwingine haya yaliyotokea ya watu wasiojulikana hayatatokea tena?, Na kama yakitokea tena, itakuwa ni kwa scale ipi?, Je yatazidi au yatapungua.
Nadhani tunahitaji mgombea atakayekuwa mkali kwelikweli na asiye na mchezo kwenye kulinda na kutetea usalama wa wananchi wa Tanzania
10. Kupambana na Ufisadi imekuwa very selective
Mpaka sasa wanaokamatwa kwenye ufisadi ni wakwepa kodi, watu wadogowadogo wanaopewa kesi za uhujumu uchumi, Hatujaona Kigogo yeyote wa chama na serikali aliyefikishwa mahakamani kwa ufisadi, tena kuna wengine wanasamehewa kwa kauli ya raisi mwenyewe.
Mara Kibao Magufuli anazungumzia uwepo wa mijizi kwenye chama chake lakini hajawahi kuyapekeka mahakamani. Sasa katika hali kama hiyo, je kweli tunapambana na ufisadi au tunaleta usanii? Hata tukija kwenye suala la ufisadi wa elimu kupitia vyeti feki, Magufuli hakugusa wateule wake wala watu wa vyombo vya dola, Hii maana yake ni kwamba yuko selective kwenye kupitisha mkasi wake, yaani anadeal na soft targets, ila zile ngumu ngumu anazikwepa.
Tunataka mtu ambaye akisema anapambana na ufisadi basi apambane nao kweli kweli, siyo maneno maneno tu.