ngara23
JF-Expert Member
- Aug 31, 2019
- 9,850
- 22,520
Naipongeza Serikali ya Rwanda kuona mbali na kuweka utaratibu mzuri wa makanisa, Misikiti na taasisi za dini
Rwanda imefungia zaidi ya makanisa 600,
Kabla walipiga marufuku matumizi ya azana Kwa Misikiti kuwa unaleta usumbufu Kwa wasio kuwa wa Imani hiyo na kuweka ustaarabu wa kuitana Kwa alarm
Sio alfajiri unapiga ukunga na watu wamepumzika
Taratibu za kufungua kanisa Rwanda
1. Elimu
Lazima mwanzilishi wa Kanisa na wachungaji waandamizi wawe na degree ya teolojia.
Sio kuamka na darasa la 7 yako eti Mungu amekuita uwe nabii na ufungue kanisa
Mwishowe unaanza mahubiri ya Zumaridi, kuuza mafuta na chumvi ya upako au kuamuru waumini kufunga hadi kufa
2. Miundo wa uongozi
Kanisa linatakiwa liwe na mfumo wa uongozi yani liwe taasisi sio mali ya mtu binafsi.
Kwa Hapa nawapongeza wenzetu waislam, hakuna Misikiti unaomilikiwa na shehe Fulani
3 Uungwaji mkono
Mchungaji anayeanzisha kanisa atatakiwa apate idadi ya watu wasiopungua 1000 katika wilaya yake. Sio kanisa Lina la mavazi na maturubai Lina waumini 6 tu huku kwetu
4 Pesa ya kiingilio
Kiingilio au pesa ya kutuma maombi ni takbani million 5 hadi 6, ambayo haitarudishwa kama vigezo vingine havitatimizwa
5 Kuratibu mapato
Serikali itataka kujua mapata ya kanisa na kuyalipia Kodi
Haiwezekani makanisa yakamue Raia masikini wa nchi hiyo huku mchungaji akinunua chopa na magari ya kifahari huku waumini wakitelea yebo
6 Eneo la kujenga kanisa
Serikali ya Rwanda itajiridhisha kuwa kanisa halipo karibu na makazi ya watu, sio kanisa lipo katikati ya makazi ya watu, mikesha kila siku na watu hawalali
Rais Kagame ameonyesha hekima kuu ya utapeli unaojipenyeza katika Imani,
Mwaka Jana maelfu ya watu walikufa huko Kenya msitini Kwa kufuata mafundisho ya uongo
Hapa kwetu makanisa hayalipi Kodi japo wanaingiza mapato makubwa, mizigo bandarini hailpi
Natumai serikali yetu itajipa muda kuinga mfano wa Rwanda