Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,814
- 13,580
Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma katika kuzuia na kutanzua uhalifu kwa kipindi cha mwezi Januri,2024 tumefanikiwa kuendesha Operesheni, misako na doria mbalimbali maeneo yote ya Mkoa wa Ruvuma ambapo katika misako hiyo tarehe 07.01.2024 katika kijiji cha Nahoro, Kata ya Luegu Wilaya ya Namtumbo tulifanikiwa kumkamata mwanaume mmoja aliyetambulika kwa jina la Dayano Swaum Chowo, (49), Mkazi wa Naholo akiwa na Fuvu lidhaniwalo kuwa la binadamu na vipande vitatu (3) vya ngozi wanyama pori akiwa amevihifadhi ndani ya begi dogo la mgongoni na kuvificha katika nyumba anayoishi.
Pia katika Operesheni hiyo tulizoendesha katika Wilaya ya Namtumbo kwa kushirikiana na Askari wa TAWA Kanda ya Kusini tulifanikiwa kukamata watuhumiwa watatu (3) waliotambulika kwa majina ya Jafari Likwata (41), Mkazi wa Minazini, Nicodemus Pius Ngonyani, (60), Mkazi wa Peramiho – Songea na Jafary George Ngesela wakiwa na Nyara za Serikari ambazo ni Meno ya Tembo mazima 18 na vipande 11 wakiwa wameyahifadhi kwenye mfuko wa Salfeti na kuficha maeneo tofauti tofauti ikiwa kwenye nyumba walizokuwa wananishi.
Issa Wilium (25) na Mohamed Selemeni Omary (37) wote wakazi wa Muhuwesi – Tunduru wakiwa na silaha hizo kinyume cha sheria.
Pia katika Kijiji cha Muhukulu Wilaya Songea tulifanikiwa kuokota Silaha moja aina ya Gobole iliyokutwa imetelekezwana watu wasiofahamika katika Ofisi ya Kitongoji cha Chepukila Kijiji cha Muhukulu.
Msako mkali unaendelea kuwasaka wahusika wa silaha hiyo kwa hatua zaidi.
Sambamba na hilo tulifanikiwa kukamata, jumla ya watuhumiwa 17 wakiwa na Pombe Moshi (Gongo) Lita 20, Pikipiki tatu (3) zenye namba za usajili MC.544 AUA aina ya SANLG rangi nyekundu, MC.955 CDD aina ya Houjue, MC.293 CCN, Engene moja aina ya Houjue, Mifuko minne (4) ya Cement ya Dangote, Marumaru 48PC mali ambazo zidhaniwazo kuwa za wizi pamoja na watuhumiwa 06 wakiwa na bhangi kete 124, Mbegu za bhangi 500gm na Bhangi kavu ikiwa imehifadhiwa ndani ya Salfeti,
Aidha Mkoani Ruvuma kumeanza kujitokeza tabia ya baadhi ya watu wachache wanaojihusisha na matukio ya utapeli kwa kuwadanganya Wananchi kuwa ni watumishi wa Serikali toka idara mbalimbali ikiwa ni kinyume cha sheria za Nchi ambapo Januari 02,2024 majira ya saa tano asubuhi maeneo ya Mgahawa wa Kristapark uliopo Manispaa ya Songea tulifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili waliotambulika kwa majina ya Raymond Francis Maige, (35), Mkurya, Mkazi wa Matarawe na Damiani Everinus Chiwangu, (34), Matengo, Mkazi wa Mji mwema baada ya kumtapeli Henry Mario Msigwa kwa kujifanya Maofisa wa JWTZ wenye cheo cha Kapteni na kuchukuwa kiasi cha pesa za kitanzania Tsh. 500,000/= (Shilingi Laki Tano) ili wamsaidie mdogo wa mfanya biashara huyo kujiunga na Jeshini la Wananchi Tanzania.
Pia katika tukio la pili tarehe 17.01.2024 majira ya saa nne asubuhi maeneo ya njia panda ya Chandamali, Kata ya Seedfarm, Wilaya ya Songea Jeshi la Polisi tulifanikiwa kumkamata Felician Isdol Mgomela, Miaka 40, Mkazi wa Kiji cha Litola – Namtumbo akijifanya Mkuu wa Upelelzi wa Makosa ya Jinai Wilaya ya Namtumbo kwa kumlaghai Father John Otete, (46), Mjaruo raia wa Kenya anayehudumu Parokia ya Ifinga Madaba kuwa anatuhumiwa kujihusisha na biashara haramu ya Nyara za Serikali na kumtaka wakutane nae Mjini ili ampatie kiasi cha pesa kumsaidie juu ya tuhuma hizo.
Baada ya kukamatwa mtuhumiwa huyo Jeshi la Polisi liliendelea na uchunguzi wa kina juu ya mtuhumiwa huyo na kugundua kuwa alishawai kutapeli watu wengine akiwemo Bruda Ponsiam Nduguru wa Lighano Seminary na wanafunzi wa Seminary hiyo 04 kwa kumpa tuhuma kuwa vijana wa utawani hapo kujihusisha na mahusiano ya jinsia moja (ushoga) na kuchukua mali zao ambazo ni simu aina ya Sumsung Garaxy Note 10 moja(1), Tecno POP 3 moja (1), Tecno ya tochi 1, Infinix Hot 10 tisa (9), Itel ya Tochi moja (1),Saa moja ya mkononi, Earphone moja na kiasi cha Tsh.15000 (Shilingi elf kumi na tano) kisha kutokomea nazo kusikojulikana.
Aidha Januari 04,2023 majira ya saa kumi jioni maeneo ya kata ya Mfaranyaki Manispaa ya Songea tulifanikiwa kumkamata Frank Kiluka, Miaka 26, Mkazi wa Matomondo ambae amekuwa akijihusisha na utapeli baada ya kumtapeli Mariam Lazaro kwa Kuchukua kiasi cha Tsh.6,000,000/= (Shilingi milioni sita) ili amletee gari aina ya Brevis toka Dar – es – salaam.
Baada ya kuchukua pesa hizo mtuhumiwa alibadili namba yake ya simu na kutokomea kusikojulikana, Jeshi la Polisi lilianza msako wa mtuhumiwa huyo ambapo Januari 04,2024 tulifanikiwa kumkamata akiwa maeneo ya mfaranyaki – Songea.
Baada ya kukamatwa mtuhumiwa Jeshi la Polisi liliendelea na uchunguzi wa kina na kugundua kuwa huko maeneo ya NMB Tawi la Songea mtuhumiwa huyo alitapeli kiasi cha Tsh.35,265,000/= (Shilingi Milioni Thelathini na Tano, Laki mbili na Sitini na tano elfu) kwa mtumishi wa Benk akimdanganya kumuuzia mahindi kiasi cha gunia 400 ambazo alidai kuwa zipo Halmashauri ya Madaba na baada ya kuchukua pesa hizo alikimbia nazo mpaka tulipofanikiwa kumkamata.
Jeshi la Polisi baada ya upelelezi tumebaini kuwa mtuhumiwa huyo amekuwa na tabia ya kuwatapeli wanawake wafanya biashara na wajane kwa kuwalaghai kufanya nao biashara mbalimbali kisha kuwachukulia pesa na kutokomea kusikojulikana.
Katika Operesheni hizo tulizoendesha tumefanikiwa kukamata jumla ya watuhumiwa 30 na kuwafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi baadha ya upelelezi kukamilika.
Natoa onyo kwa Wananchi wote Mkoani Ruvuma ambao wanajihusisha na vitendo vya kihalifu ikiwa pamoja na utapeli kwa raia wema waache mara moja kwani Mkoa wa Ruvuma sio salama kwao juu ya matukio hayo, badala yake tunawashauri watumie njia halali za kujipatia vipato kuendesha maisha yao kwani Jeshi la Polisi halitafumbia macho vitendo hivyo tutahakikisha tunawasaka mahali popote walipo, tunawakamata na kuwafikisha mahakamani kwa hatua za kisheria.
Pia Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma linatoa wito kwa raia wema kuendelee kushirirkiana na Jeshi la Polisi katika kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili waweze kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria na Mkoa wetu uendelee kuwa salama wakati wote.
IMETOLEWA NA,
MARCO G. CHILYA – ACP
KAMANDA WA POLISI (M) RUVUMA