Ruto athibitisha kuwa Kenya imelipa Kshs Milioni 500 kwa waandaaji wa Grammys ili tuzo zifanyike nchini humo

Mindyou

JF-Expert Member
Sep 2, 2024
1,151
3,089
Wakuu,

Hivi karibuni Rais William Ruto amedokeza kuwa kuwa serikali ya Kenya tayari imelipa Tshs Milioni 500 Kenya iweze kuwa mwenyeji wa tuzo za Grammys mwaka 2027.

Akizungumza wakati wa mkutano wa Townhall Jumatatu usiku, Ruto alisema kuwa hili linaweza kuthibitishwa na wawakilishi wa Grammys waliokuwepo kwenye hafla hiyo.

"Pesa za Grammys tayari tumezilipa. Tumeshalipa Shilingi milioni 500 na nina uhakika mwakilishi kutoka Grammys anaweza kuthibitisha kuwa huo hiyo ndio hatua inayofuata" alisema.

Kupitia mitandao ya kijamii, Wakenya wamehoji maswali mengi ikiwemo ni venue gani hasa tuzo hizo zitafanyika na iwapo pesa hizo zitarudi kwa serikali ya Kenya.

 
Back
Top Bottom