Rushwa ni donda ndugu ndani ya CCM

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Taarifa za habari katika vyombo mbalimbali vimenukuliwa vikisema kwamba kuna wanachama wa chama cha mapinduzi CCM ambao walikuwa wamejitosa katika kinyang'anyiro cha kuwapata wagombea nafasi za Ubunge wa Afrika mashariki (EALA) kwamba walitoa Rushwa ili wapitishwe na ngazi za maamuzi za chama cha mapinduzi CCM.

Amenukuliwa Msemaji wa chama hicho Ndugu Humphrey Polepole kwamba wanachama hao wa CCM watapewa adhabu, au kuwajibishwa na kamati ya maadili ya chama hicho; Kwa tafsiri nyingine, Bwn. Polepole amekubaliana na ukweli kwamba wapo wanachama waliotoa Rushwa.

Sote tunafahamu kwamba Rushwa sio suala la upande mmoja, bali pande mbili, mtoaji na mpokeaji, na hili liliwekewa mkazo hata muasisi wa Taifa letu hayati Mwl. Nyerere kwamba mtoaji na mpokeaji wa Rushwa wote wana hatia.

Maana yake ni kwamba, wanachama hao wanalo kosa la jinai la kutoa Rushwa, lakini pia viongozi waandamizi wa CCM pia wanalo kosa la Jinai la kupokea Rushwa, maana yake wote hawa wametenda makosa ya jinai, na wanapaswa kuwajibishwa mbele ya macho ya sheria za nchi yetu.

Chama cha mapinduzi CCM kimekuwa ni kichaka cha kuwafichia watoaji na wapokeaji wa Rushwa, Kwa kisingizio kwamba watawajibishwa na kamati za chama hicho za maadili, huu ni zaidi ya uhalifu, kwanini Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ndiyo isiingie kuchunguza na kuwakamata wahusika wote kisha kuwafikisha mahakamani na sheria ichukue mkondo wake? Inamaana hata Chama hicho kikibaini wanachama wake wanajihusisha na Madawa ya kulevya, Ujangili, Ufisadi, n.k. kitawawajibisha kwenye kamati za chama na kuzuia mamlaka husika za nchi kuwawajibisha Kwa mujibu wa sheria?

Hii haikubaliki, na watanzania wanapaswa kufahamu kwamba nchi yetu inashindwa kuvishinda vita hivi dhidi ya Rushwa na Ufisadi, Kwa sababu Chama kilichounda serikali ndiyo wadau wa kubwa wa jinai hizo, na wanalindana vikali.

Wenu katika demokrasia na maendeleo
 
Amani iwe nanyi, inashangaza serikali inayojinasibu kupambana na rushwa na ufisadi kuendelea kutuhumiwa kuwa kunara wa kutoa rushwa.

Tulianza kusikia wabunge wote wa ccm walihongwa mil 10 kila mmoja ili kupitisha madudu bungeni, watu walipaza sauti kukemea na kuhoji swala hili lakini serikali sikivu ya awamu ya tano ikaziba masikio yake.

Nakumbuka kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni mh freeman mbowe alimuuliza waziri mkuu live bungeni ili watanzania tujue, lakini kwa dharau kubwa naibu spika alimkingia kifua waziri mkuu asijibu swali hili akisema sio la kisera.

Hivi karibuni tumesikia kauli kutoka kwa wabunge lema na nasari wakikituhumu chama cha mapinduzi kuwa kimekua kikimtumia mkuu wa mkoa wa arusha bwana gambo kununua madiwani mbalimbali jijini arusha ili kuidhoofisha chadema, cjasikia kauli ya takukuru wala mkuu wa kaya kuzungumzia hili.

Kwa uzoefu wangu ukiona ccm wanatuhumiwa kuhusu jambo fulani na wakanyamaza basi mara zote tuhuma hizo zinakuwa ni kweli tupu. Sasa hapa tujiulize hivi ccm kweli wanasimamia wanayotamka? Mtu unasema unachukia rushwa asubuhi ikifika jioni unatoa rushwa hii imekaaje?

Hivi ni kweli imefika pahala ccm mmelewa madaraka kiasi mnaona watanzania wote ni mazuzu? Maana siku hizi mmenda mbali mnatutukana hadharani mara wapumbafu mara malofa, hapa najiuliza kati ya wananchi na nyinyi nani lofa kuliko mwengine?

Mwisho nimeamini ccm ndo mwalimu wa kutoa na kupokea rushwa hawa watanzania mnaotuita wapumbavu tunaendelea kuwalaani ili ifike siku tuwaonyeshe upumbavu na ulofa wetu.

Mungu ibariki tanzania.
 
 
Hakuna rushwa hapo Cdm wanacheza na hakiri za watu mkuu mh lema na nassari wanaitisha press kudai madiwani kuongwa kisha ushaidi utaletwa baadae ni mtoto tu ndio anaweza kuamini haya maigizo
 
hahaha mkuu me nakupinga cz binafsi nikiumwa uji kwangu ni adui labda unegesema sisiemu na grand corruption ni kama uhai na mwili
 
Navyoelewa CHADOMO ingekuwa wanao ushaidi hiyo Video ya Madiwani wakipokea Rushwa tungekuwa tulishaiona lakini hawana ushaidi wowote Mbwembwe tupu
 
Ccm ni mawakala wa mafisadi na mabepari.....wameshauza nchi kwa wawekezaji kwa maslahi ya matimbo yao....kazi yao miaka 50 ni kuwatengenezea watz matatizo alafu kuja kujifanya wanayatatua......mbwa kabisa ccm
 
Hakuna rushwa hapo Cdm wanacheza na hakiri za watu mkuu mh lema na nassari wanaitisha press kudai madiwani kuongwa kisha ushaidi utaletwa baadae ni mtoto tu ndio anaweza kuamini haya maigizo
Na wale watu Gambo aloambiwa awaite walipewa nini? Ccm ni chaka la uchafu wote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…