DOKEZO Rushwa katika mchakato wa mikopo ya 10% ya halmashauri mkoani Mbeya

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Kumekuwa na vitendo vya kudai rushwa kunakofanywa na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya ili waweze kupitisha vikundi vya vijana kupata mkopo wa 10% Inayotolewa na halmashauri.

Hili jambo lipo katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya hapa mji mdogo wa Mbalizi.

Maafisa maendeleo katika kata kama Nsalala wanadai rushwa ili waweze kupitisha vikundi vya vijana katika mchakato mzima wa kupata hiyo mikopo.

Waziri Tamisemi na TAKUKURU wafuatilie hili jambo hasa katika halmshauri ya wilaya ya Mbeya mji mdogo wa Mbalizi.
 
Back
Top Bottom