Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,806
13,574
Mkoa wa Rukwa ulianzishwa mwaka 1974 baada ya kugawanywa kutoka mikoa ya Tabora (Mpanda) na Mbeya (Sumbawanga). Mwezi Julai 2010, Serikali ya Awamu ya Nne iligawa Mkoa wa Rukwa na kuanzisha Mkoa mpya wa Katavi.

Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 yanaonesha kuwa idadi ya watu
katika Mkoa wa Rukwa ni 1,540,519; wanaume 743,119 na wanawake 797,400.

Majimbo ya Uchaguzi

Mkoa wa Rukwa una majimbo ya uchaguzi matano (5) Sumbawanga, Kwela, Kalambo, Nkasi Kusini na Nkasi Kaskazini. Jimbo la Kwela linaongoza kwa kuwa na watu wengi zaidi (494,330), likifuatiwa na Jimbo la Kalambo lenye watu 316,783. Jimbo lenye idadi ndogo ya watu ni Nkasi Kusini ambalo lina watu 178,134
  1. Nkasi Kaskazini - Idadi ya watu: 247,286
  2. Nkasi Kusini - Idadi ya watu: 178,134
  3. Sumbawanga Mjini - Idadi ya watu: 303,986
  4. Kalambo - Idadi ya watu: 316,783
  5. Kwela - Idadi ya watu: 494,330
Soma Pia:
Rukwa.jpg

Hali ya kisiasa

Matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2020 nchini Tanzania yanaonyesha hali ya upekee kwa kila mkoa, huku CCM ikishinda kwa wingi mkubwa wa kura katika nafasi za udiwani, ubunge, na urais. Mkoa wa Rukwa pia haukuwa tofauti, ukionyesha hali zifuatazo:

Nkansi Kusini - Kalambo: Josephat Sinkamba Kandege (CCM) alipita bila kupingwa
Katika jimbo la Nkansi Kaskazini, Aida Khenani wa CHADEMA alishinda kwa kura 21,226 dhidi ya Ally Keissy wa CCM aliyepata kura 19,972. Hili lilikuwa moja ya maeneo machache ambapo upinzani ulifanikiwa kushinda,

Sumbawanga Mjini: Aeshi Khalfan Hilary (CCM) alipata kura 36,807 dhidi ya Sadrick Enock Malila (CHADEMA) aliyepata kura 17,829
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom