Uchaguzi 2025 Rukwa: CV za Wabunge mwaka 2020 - 2025. Mbunge wako ametimiza ahadi zake?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,814
13,580
Wakuu,

1. Deus Clement Sangu – Mbunge wa Kwela

Chama Cha Siasa: Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Matokeo ya Uchaguzi wa 2020: Alishinda kwa kura 48,918, akimshinda Ngogo Naftal Daniel kutoka CHADEMA ambaye alipata kura 23,542.

Teuzi ya Serikali: Aliteuliwa kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (Julai 2024).

Elimu

Shahada ya Uzamili (Master’s) katika Procurement and Supply Chain Management kutoka Mzumbe University (2013–2015).

Shahada ya Bachelor katika Management Science kutoka University of Dar es Salaam (2007–2010).

Uzoefu wa Kazi:

Senior Manager Procurement, TPB Bank PLC (2018–2020).
Head of Procurement na Procurement Officer, Twiga Bancorp Ltd.
Bank Operations Officer, Twiga Bancorp Ltd na Barclays Bank T Ltd.

Mchango katika Siasa:

Katibu wa tawi la CCM katika UDSM (2007–2010).
Mwanachama wa Kamati ya Utekelezaji ya Wazazi (2011–2015).


2. Aida Joseph Khenan – Mbunge wa Nkasi Kaskazini

Chama Cha Siasa: Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

Matokeo ya Uchaguzi wa 2020: Alishinda kwa kura 21,226, akimshinda Ali Mohamed Keissy kutoka CCM ambaye alipata kura 19,972.

Elimu

Shule ya Msingi ya Kantalamba (CSEE, 2006–2009).
Diploma katika DASCO (2009–2012).


Mchango katika Siasa:

Mwenyekiti wa Kanda wa BAVICHA (2009–2014).
Mwenyekiti wa Wilaya wa BAWACHA (2014).

Mchango Bungeni:

Mbunge wa Tanzania (2015–2020) na tena kuchaguliwa kwa kipindi cha 2020–2025.
Mwanachama wa Kamati ya Hesabu za Umma (2021–2023).
Mwanachama wa Kamati ya Sheria na Mambo ya Katiba (2015–2018).


3. Aeshi Khalfan Hilaly – Mbunge wa Sumbawanga Mjini

Chama Cha Siasa: Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Matokeo ya Uchaguzi wa 2020: Alishinda kwa kura 36,807, akimshinda Ikuwo Sadrick Malila kutoka CHADEMA ambaye alipata kura 17,829.

Elimu

Shule ya Msingi Jangwani (1980–1987).
Shule ya Sekondari Mazwi (1988–1992), alihitimu kwa cheti cha CSEE.
Diploma katika Taasisi ya Mafunzo ya Serikali za Mitaa, Hombolo, Dodoma (2019), akijikita katika usimamizi na utawala.


Mchango Bungeni:

Alitoa michango 20 na maswali moja la nyongeza katika bunge.


Kazi Upande wa Siasa
Kamati ya Nishati na Madini (2010–2013).
Kamati ya Mambo ya Kiuchumi, Viwanda na Biashara (2013–2015).
Naibu Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Umma (2015–2020).
Mwanachama wa Kamati ya Maendeleo ya Miundombinu (2021–2023).


4. Vincent Paul Mbogo – Mbunge wa Nkasi Kusini

Chama Cha Siasa: Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Matokeo ya Uchaguzi wa 2020: Alishinda kwa kura 20,934, akimshinda SotokA Alfred Daniel kutoka CHADEMA ambaye alipata kura 8,783.
 
Back
Top Bottom