PakiJinja
JF-Expert Member
- Jan 16, 2012
- 10,772
- 23,718
Ghafla bin Vuuu... watu wanashuhudia Helikopter ya Jeshi la Urusi aina ya Mi-8 inaingia kwenye kituo cha anga cha Poltava nchini Ukraine. Hilo halikua shambulizi bali ni tukio la Mwanajeshi huyo kutorokea Ukraine
Rubani huyo aliwasili na helikopta ya Urusi aina ya Mi-8 AMTSh kwenye kituo hicho cha kijeshi cha anga huko Kharkiv siku ya Jumatano, tukio lililowashangaza wafanyakazi wa kituo hicho.
Andriy Yusov, msemaji wa idara ya ujasusi ya kijeshi ya Ukraine, aliviambia vyombo vya habari vya eneo hilo kwamba tukio hilo lilikuwa linahitimisha mkakati wa siri uliokua ukitekelezwa hatuaka hatua kwa muda wa miezi sita.
Walianza kwa kuihamisha Familia ya rubani huyo na kuipeleka nchini Ukraine kutokea Urusi.
Wanajeshi wengine wawili waliokuwemo kwenye Helicopter hiyo hawakuujua mpango huo. Idara ya ujasusi ya kijeshi ya Ukraine imesema kuwa wanajeshi hao wawili hawakua tayari kusalimu amri hivyo walilazimika kuwa "terminate".