RPC, Wakili Kibatala walivyochuana kesi mjane wa Bilionea Msuya

Oldmantz

JF-Expert Member
Jan 24, 2023
704
1,456
1686934190843.png

Dar es Salaam. Wakili wa utetezi, Peter Kibatala katika kesi ya mauaji ya Aneth aliyekuwa dada wa mfanyabiashara wa madini Mirerani mkoani Manyara, marehemu Erasto Msuya (Bilionea Msuya), amechuana vikali na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Richard Mchomvu.

Hayo yalitokea jana Juni 15 baada ya kesi hiyo kuendelea kusikilizwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Aneth aliuawa kinyama Mei 25, 2016 kwa kuchinjwa kama mnyama nyumbani kwake Kibada, Kigamboni wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam, na mwili wake ukaachwa ukiwa utupu, bila nguo yoyote mwilini.

Kufuatia mauaji hayo watu wawili walitiwa mbaroni na hatimaye kufunguliwa mashtaka ya mauaji hayo ambao ni Miriam Mrita, na mwenzake Revocatus Muyella, maarufu kama Ray.

Miriam ambaye ni mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo namba 103 ya mwaka 2018, ni wifi wa marehemu Aneth, kutokana na kuwa ni mjane wa Bilionea Msuya aliyeuawa kwa kupigwa risasi eneo la Mijohoroni, wilayani Hai mkoani Kilimanjaro Agosti 7, 2013.

Akiwa ni shahidi wa 10 wa upande wa mashtaka kati ya mashahidi 45 wanaotarajiwa kutoa ushahidi katika kesi hiyo, Kamishna Mchomvu amehitimisha ushahidi wake baada ya kusimama kizimbani kwa siku tatu.

Pamoja na mambo mengine, wakati akihojiwa na Wakili wa utetezi, Peter Kibatala, shahidi huyo alikiri kuandika maelezo kuhusiana na mauaji hayo, lakini Wakili Kibatala alipomuuliza kama angependa kuyatoa maelezo yake hayo yapokewe mahakamani kama kielelezo cha ushahidi wa upande wa utetezi, alikataa.

Kabla ya shahidi huyo kukataa, yaliibuka malumbano ya hoja baina ya Wakili Kibatala na Wakili wa Serikali, Yasinta, baada ya Wakili Kibatala kumshtaki Wakili Yasinta kwa Jaji kuwa anamfundisha shahidi majibu.

Ushahidi wa msingi wa ACP Mchomvu
Katika ushahidi wake akiongozwa na mwendesha mashtaka, wakili wa Serikali Mwandamizi, Yasinta Peter, ACP Mchomvu, ambaye wakati wa mauaji hayo alikuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa (RCO) wa Kipolisi Temeke, akiwa na cheo cha Mrakibu Mwandamizi wa Polisu (SSP), alieleza kama ifuatavyo:

ACP Mchomvu: Mei 26, 2016, asubuhi saa 12:30 nilipokea simu kutoka kwa mwananchi kuwa Kigamboni Kibada kuna mtu ameuawa. Nilimtafuta, OC-CID (Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya) sikumpata.

Baadaye (OC-CID) akanipigia akanieleza kuwa yuko Kibada kwenye tukio la mauaji kuna dada mmoja ameuawa ndani ya nyumba yake, akanitaka niende tusaidiane.

Nilimchukua Sajenti John ambaye alikuwa mtaalamu wa forensic tukaenda mpaka pale Kibada tukamkuta OC-CID.

Alinionesha kuwa hiyo nyumba alikuwa anaishi dada anaitwa Aneth Msuya na mtoto wake mdogo wa kiume pamoja na binti wa kazi. Tulimkuta mtoto lakini dada wa kazi hakuwepo.

Alisema mlango wa nyumba wa chuma na wa mbao ilikuwa umevunjwa kwa tofali na alionesha chumba ambacho marehemu alikuwa amelala.

Niliingia ndani ya chumba nikiwa na Sajenti John tukakuta mwili wa mwanamke umelala kifudifudi (hata hivyo alimaanisha chali kwani alifafanua kuwa alikuwa amelalia mgongo) na ulikuwa umechinjwa kwa kitu chenye ncha kali na damu ilikuwa imetapakaa chumbani.

Pia niliona kisu pembeni karibu na mwili wa marehemu na Sajenti John akafanya upekuzi kuona kama kuna vitu ambavyo vinaweza kuwa vielelezo vya ushahidi.

Mbali na kisu pia alipata filimbi na chupi ambavyo vilikuwa kando kidogo ya mwili kuelekea uvunguni.
Sajenti John alivifunga vile vitu na akavichukua kama vielelezo, nikamuelekeza OC-CID auchukue mwili aupeleke mochwari.

Kwa hiyo tulijiuliza nani kaua na dada wa kazi yuko wapi? Tulifanikiwa kupata namba ya simu ya mama mzazi wa marehemu, nikafanya mawasiliano naye, baada ya kupokea nikamuuliza kama ana mtoto wake Kigamboni akasema ndio nikamuuliza kama anajua kuwa amepata tatizo akasema kuwa ameuawa.

Nikamwambia sasa huyu dada (wa kazi) hayupo nasi tunaendelea kumtafuta. Namba yake ilikuwa haipatikani.

Jina lake anaitwa Getrude. Tuliendelea kimtafuta na Julai 20,2016 mama wa marehemu alinipigia akanieleza kuwa amefanya uchunguzi amegundua yule binti Getrude yuko nyumbani kwao Moshi kwa wazazi wake, na kwamba yuko tayari kueleza Polisi kilichotokea.

Alisema anaweza kwenda kwa RPC. Hivyo Julai 22, 2016 nikatuma askari wawili Sajenti Jumanne na Koplo Lenada kwenda Moshi kwa RCO na niliwaeleza kilichotokea.

Julai 24 askari wale walirudi na yule binti Getrude, wakaja naye ofisini kwangu, muda wa saa 1 au 2 hivi usiku, nikaongea naye akasema yuko tayari kueleza kilichotokea maana kinamuuma sana.

Alinieleza kuwa pale nyumbani siku ya tukio walifika watu wawili mmoja mwanaume na mwingine mwanamke.

Alieleza kwamba yule mwanamke anamfahamu kwa sababu alishawahi kumuona kule Moshi, alishatambulishwa na mama wa marehemu kuwa ni mke wa kaka wa marehemu lakini mwanaume alikuwa hamfahamu kwa sababu alikuwa hajawahi kumuona.

Alisema yule mwanamke alimwambia kuwa asilale pale na akampa na pesa.

Julai 25, 2016 nilimkabidhi kwa maafisa wawili, ASP Jumanne na ASP David kutoka ofisi ya DCI (Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai), kwa mahojiano zaidi.

Walinipa maelezo kuwa walipata picha halisi ya huyo mwanamke aliyekwenda na kwamba yuko Arusha na namna ambavyo wanaweza kumpata.

Agosti 5, 2016 hao maafisa wawili walinijulisha kuwa wamempata yule mwanamke kule Arusha na kwamba wamemleta yuko kituo cha Polisi Kilwa Road na kwamba jina lake ni Mariamu (Miriam).

Baada ya kunijulisha kuwa wamekuja naye nikaamua kwenda kuonana naye tukasalimiana nikamuuliza kama yeye ni mke wa marehemu Msuya aliyeuawa kule Moshi, akasema ndio.

Agosti 7, 2016 nilitoa maelekezo kuwa yule binti (Getrude) aletwe kwa ajili ya gwaride la utambulisho kwa mtuhumiwa aliyekuwapo Kilwa Road, Mariam.

Gwaride lilifanyika na wale wapelelezi waliniambia kuwa yule binti alifanikiwa kumtambua mtuhumiwa na kwamba wanataka wafanye naye mahojiano ili kujua yule mwanume aliyekwenda naye (kwa marehemu) ni nani.

Walipofanya naye mahojiano mtuhumiwa alimtaja mtuhumiwa mwanaume na kwamba yuko Arusha.
Walikwenda Arusha wakarudi Agosti 21 wakaniambia kuwa wamempata yule mtuhumiwa wa kiume na nilielekeza naye afanyiwe gwaride la utambuzi.

Agosti 28, niliamua kupata sampuli kuhusianisha na vielelezo tulivyovipata chumbani kwa marehemu, pamoja na mtuhumiwa.

Nilimjulisha mtuhumiwa wa pili Revocatus kuwa tunataka kufanya DNA na kwamba sisi pale hatuna wataalamu hivyo tukaenda Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.

Alisema hana pingamizi wala shida, hivyo nikaelekeza apelekwe Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, akapelekwa na mimi nikaenda huko.

Nilimpa fomu naye akasaini kuonesha kwamba alikubali kuchukuliwa sampuli na nilimfahamisha haki zake na kumhakikishia kuwa hazitatumika kwa matumizi mengine bali kwa uchunguzi huo tu.

Kisheria hata kama mtuhumiwa amegoma (kuridhia) lazima hizo sampuli zichukuliwe ili haki itendeke.

Hivyo tulikwenda Polisi Makao Makuu kupata hizo sampuli ili kulinganisha na vile vielelezo tulivyovipata na alipelekwa na WP Elitruda.

Sampuli zilichukuliwa zikafungwa kwenye bahasha na kupelekwa kwenye maabara pamoja na vielelezo vile.

Pingamizi
Baada ya maelezo hayo, Wakili Yasinta alimuuliza shahidi huyo kama angependa fomu hiyo ipokewe mahakamani kama kielelezo cha ushahidi upande wa mashtaka, naye akakubali, lakini wakili Kibatala aliweka pingamizi akiiomba mahakama hiyo isiipokee fomu hiyo.

Pamoja na mambo mengine wakili Kibatala alidai kuwa shahidi huyo hana mamlaka ya kutoa fomu hiyo kwani Sheria ya Vinasaba vya Binadamu inaelekeza kuwa mwenye mamlaka ya kutoa fomu hiyo ni ofisa mchukua sampuli na si mamlaka ya kuomba sampuli hizo, ambazo ni pamoja na askari Polisi.

"Kwa hiyo fomu hii imekiuka masharti ya lazima ya Sheria ya DNA," alidai wakili Kibatala.

Pia alidai kuwa hata kama wakiiona kuwa fomu hiyo ni halali kutolewa na shahidi huyo, lakini imefanyiwa marekebisho kwa kuongezewa taarifa nyingine ambazo hazimo katika fomu ya msingi na hawakusaini kuonesha kuthibitisha marekebisho hayo.

Akijibu hoja hizo, Wakili wa Serikali, Yasinta alipinga hoja za wakili Kibata pamoja na mambo mengine akidai kuwa shahidi huyo ana mamlaka ya kutoa fomu hiyo huku akirejea uamuzi wa Mahakama ya Rufani kuwa imeweka vigezo vya shahidi anayestahili kuwasilisha kielelezo mahakamani.

Alivitaja vigezo hivyo kuwa ni pamoja na kuwa mwandaaji wa kielelezo hicho, kuwa amekitunza au mwenye ufahamu nacho na kwamba shahidi huyo amekidhi vigezo hivyo kwani ndiye aliyeiandaa.

Hata hivyo alisema mtuhumiwa angeweza kuchukuliwa tu sampuli hizo hata bila kuwepo kwa fomu hiyo ya ridhaa kwani Sheria ya Vinasaba inaeleza kuwa katika uchunguzi wa kijinai sampuli zinaweza kuchukuliwa kwa mtu bila hata kupata ridhaa yake.

Hivyo Wakili Yasinta aliiomba Mahakama ilitupilie mbali pingamizi hilo na iipokee iwe kielelezo cha ushahidi wa upande wa mashtaka.

Uamuzi wa Mahakama
Hata hivyo Katika uamuzi wake jana, Jaji Edwin Kakolaki anayesikiliza kesi hiyo alikataa pingamizi hilo la upande wa utetezi akisema kuwa halina mashiko.

Jaji Kakolaki alisema kuwa Mahakama hii inaona kwamba utaratibu uliotumika kuchukua sampuli kwa mtuhumiwa haukumdhuru na upande wa utetezi haujasema kama ulikuwa na madhara yoyote.

Pia alisema kuwa mahakama inaona kwamba fomu hiyo haina tofauti sana na jinsi inavyoonekana katika jedwali la Sheria ya Vinasaba vya Binadamu na kwamba hata marekebisho yaliyodaiwa kufanya kwenye fomu hiyo hayana athari.

Vilevile Jaji Kakolaki alisema kuwa, shahidi huyo ana mamlaka ya kuwasilisha fomu hiyo kwani amekidhi vigezo kwa kuwa, kama Afisa wa Polisi ndiye aliyeomba kuchukuliwa Vinasaba, na ndiye aliyekuwa akimiliki (kuitunza) na pia kuna saini yake.

"Hivyo Mahakama inaona kwamba hapakuwa na madhara. Kwa sababu hizo masharti yote matatu ya upokeaji kielelezo yamekidhi na Mahakama inaona mapingamizi ya upande wa utetezi hayana mashiko na inaelekeza kwamba kielelezo hicho kinapaswa kupokelewa," alisema Jaji Kakolaki.

Baada ya uamuzi huo ACP Mchomvu aliendelea na ushahidi wake akiongozwa na wakili Yasinta.

Baada ya kumaliza kumsomea haki zake nilimkabidhi kwa mtaalamu kwa ajili ya kumchukua sampuli ambayo aliifunga kwenye bahasha akaweka na lakiri akanikabidhi nikaziunganisha na vielelezo vilivyopatikana eneo la tukio.

Alisema Agosti 29, 2016 aliwaelekeza Sajenti John kupeleka vielelezo hivyo makao makuu na kuomba ridhaa kwa ajili ya kuvipeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali.

“Machi 2017 nilipata taarifa kuwa viko tayari kwa mkemia nikamtuma Sajenti John avifuate nikavitunza ofisini kwangu,” alisema.

Maswali ya dodoso
Baada ya ACP Mchomvu kumaliza ushahidi wake akiongozwa na mwendesha mashtaka, aliulizwa maswali ya dodoso na Wakili Kibatala pamoja na mambo mengine alimuuliza shahidi huyo kama aliwahi kuandika maelezo yake kuhusiana na kesi hiyo na shahidi huyo akakubali.

Kisha Wakili Kibatala alimuuliza shahidi huyo kama angependa kuyatoa maelezo yake hayo yapokewe mahakamani kama kielelezo cha ushahidi wa upande wa utetezi.

Hata hivyo, kabla shahidi huyo hajatoa jibu kukubali au kukata, Wakili Kibatala aliibua madai dhidi ya Wakili Yasinta kuwa alikuwa alimwelekeza shahidi jibu la kukataa kwa kumfanyia ishara ya kutikisa kichwa madai ambayo yalipingwa vikali na Wakili Yasinta.

Hivyo Wakili Kibatala aliiomba mahakama hiyo hoja madai yake hayo yaingizwe kwenye kumbukumbu za mwenendo wa kesi hiyo.

Baada ya Wakili Kibatala kusisitiza madai yake hayo, Jaji Kakolaki alitoa nafasi kuwasikiliza mawakili wa pande zote akianza Kibatala, ambaye alisema, wakati anamhoji PW10 (shahidi wa 10 upande wa mashtaka) kuhusiana na maelezo yake aliyoyarekodi Oktoba 25, 2017 alimuomba iwapo ana pingamizi kwa ajili ya kutenda haki.

“Wakati shahidi anajiandaa kujibu nilimuona kwa macho yangu Wakili wa Serikali Yasinta Peter akimuonesha kwa ishara ya kichwa shahidi kwamba akatae ombi hilo na kweli kabisa shahidi akaanza kukataa kama ambavyo alioneshwa.

“Mheshimiwa Jaji bila kumdodosa shahidi haiwezekani kupima strong (uimara) yake, maana yake ni kwamba ninanyimwa haki yangu ya kufanya kazi na faida ya ushahidi ambayo nilipaswa kuipata haipo tena na sina namna ambayo naweza kufidiwa kuhusu hiyo statement."

Hivyo Wakili Kibatala alihitimisha madai yake kwa kuiomba mahakama itoe amri nafasi yake ya maswali ya dodoso isiingiliwe tena na ielekeze mawakili wa pande zote kwa kuwa wote ni maafisa wa Mahakama wazingatie na kutii kanuni na taratibu.

Akijibu madai hayo, Wakili Yasinta alikana kumfundisha shahidi majibu, akidai kuwa alitikisa kichwa kulingana na swali alikokuwa ameulizwa na Wakili mwenzake.

"Mheshimiwa Jaji, tuko wawili hapa, mimi na mwenzangu na wakati Wakili ameanza kuuliza mwenzangu akaniuliza ni tarehe 26 au 25 (ya shahidi huyo kuandika maelezo yake), mimi nikakataa," alieleza Wakili Yasinta.

Wakili Yasinta alimweleza Mheshimiwa Jaji Kakolaki kuwa kwa kuwa shahidi huyo alikuwa anaangalia upande wake (Jaji) na yeye (Yasinta) yuko pembeni, (ubavuni mwa shahidi), isingewezekana (kumfanyia ishara hiyo isipokuwa tu kama shahidi huyo ana macho kama ya kunguru.

"Lakini Wakili amesema kuwa shahidi ameanza..., hii ni mahakama ya kisheria hatuwezi kwenda kwa (hisia) assumption," alisema Wakili Yasinta.

Jaji Kakolaki baada ya kusikiliza hoja za pande zote alielekeza mawakili wa pande zote kuongozwa na kanuni.

Maswali ya Kibatala
Baada ya maelekezo hayo Wakili Kibatala aliendelea na swali lake hilo pamoja na maswali mengine kama ifuatavyo:

Wakili Kibatala: Haya maelezo uko tayari kuyatoa kama kielelezo?
Shahidi ACP Mchomvu: Siko tayari kwa sababu ni...
Kibatala: Hizo sababu mimi sizihitaji.
Kibatala: Huyu aliyekupigia simu uliwahi kumfahamu ni nani?
ACP Mchomvu: Sikuwahi kufahamu.
Kibatala: Kwa kuwa namba zake ulikuwa nazo uliwahi kuzifuatilia?
ACP Mchomvu: Sikuwahi kuifuatilia wala sikuona haja.
Kibatala: Unamfahamu kama alama za vidole ziliwahi kupimwa kwenye kisu chupi na filimbi?
ACP Mchomvu: Sifahamu.
Kibatala: Ni kweli au si kweli alama za vidole ni namna za kipelelezi kujua mhusika wa tukio?
ACP Mchomvu: Ni mojawapo.
Kibatala: Kibatala: Uliwahi kuona maelezo ya mashahidi kwenye jalada la kesi hii?
ACP Mchomvu: Sijawahi
Kibatala: Yule Binti wa kazi wa marehemu Aneth uliyesema mlimfuata Moshi hajawahi kutuhumiwa kwa mauaji ya Aneth?
ACP Mchomvu: Hajawahi.
Kibatala: Na hajawahi kukamatwa na kuwekwa chini ya kizuizi kama (mtuhumiwa) suspect?
ACP Mchomvu: Najua hivyo
Kibatala: Hili jalada DSM/Temeke/CID/ SR/262/2016, la Mei 26, 2016 unalifahamu?
ACPMchomvu: Hapana silifahamu
Kibatala: SP Richard (aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya) hakuwahi kukupa taarifa za hili jalada?
ACP Mchomvu: Hakuwahi
Kibatala: Kwa hiyo hufahamu kwamba huyu binti Getrude aliwahi kukamtwa yeye na boyfriend wake Sabri Kombo Haji?
ACP Mchomvu: Sifahamu
Kibatala: Pia hufahamu kuwa siku ya Mei 26, 2016 alikamatwa boyfriend wa marehemu Aneth, Wilbard Mathew Kimario, mfanyabiashara?
ACP Mchomvu: Nafahamu, mimi ndiye niliyesema atafutwe ilituongee naye atueleze tujue nini kilichotokea,
Kibatala: Hebu mwambie Mhehimiwa Jaji namba za jalada lililotumika kumkamata na kumhoji Wilbard Mathew Kimario.
ACP Mchomvu: Sizikumbuki.
Kibatala: Unafahamu kuwa wakazi wa Kibada Kigamboni waliandika barua Makao Makuu Polisi kulalamika Getrud Mfuru, Sabri Kombo Haji, Wilbard Mathew Kimario, Twaha Almas na Amir Said kwa nini walikamatwa?
ACP Mchomvu: Sifahamu
Kibatala: Huyu Getrude Mfuru mara ya kwanza unatoa maelekezo kufuatiliwa ilikuwa lini?
ACP Mchomvu: Nilitoa maelekezo kwa Sajenti Juni 22, 2016
Kibatala: Ni kweli kwamba kabla ya ninyi kuzungumza na huyo binti, alikuwa ameshaongea na mama wa marehemu Aneth?
ACP Mchomvu: Ni kweli.
Kibatala: Unafahamu walichozungumza huyo binti na mama wa marehemu?
ACP Mchomvu: Sifahamu kwa sababu…
Kibatala: Mimi sitaki ufafanuzi nijibu ndio au hapana inatosha.
ACP Mchomvu: Mbona wewe ulikuwa unafafanua, ngoja na mimi nifafanue mbona unakuwa mchoyo? Usiwe mchoyo ili Jaji naye aelewe.
Kibatala: Uliwahi kufahamu kulikuwa na mgogoro mkubwa wa mirathi kati ya mshtakiwa wa kwanza (Miriam) na mama (mama wa marehemu Aneth) Ndeshulwa?
ACP Mchomvu: Sifahamu.
Kibatala: Mama Ndeshulwa wakati anakupigia simu kuwa huyu binti yuko huku na yuko tayari kueleza, aliwahi kukwambia kuwa alikuwa na mgogoro na mshtakiwa wa kwanza wa mirathi?
ACP Mchomvu: Hakuwahi kunielezai.
Kibatala: Kama sehemu ya uchunguzi kwa tukio kubwa kama hilo, Jeshi la Polisi lilishachukua hatua ya kuomba kwa kampuni yoyote ya simu kuomba taarifa ya simu za wote waliohusika katika kesi hii?
ACP Mchomvu: Sina hakika kama ziliwahi kuombwa.
Kibatala: Uliwahi kufahamu kama marehemu na mpenzi wake Wilbard Mathew Kimariowalikuwa na ugomvi?
ACP Mchomvu: Sikuwahi kufahamu
Kibatala: Mliwahi kufuatilia rekodi ya mawasiliano ya Getrude?
ACP Mchomvu: Sikushughulika nayo.
Kibatala: Uliwahi kufuatilia mawasiliano ya mshtakiwa wa kwanza?
ACP Mchomvu: Sikushughulika nayo
Kibatala: Uliwahi kufuatilia rekodi za mawasiliano ya mshtakiwa wa pili?
ACP Mchomvu: Sikushughulika nayo.
Kibatala: Uliwahi kufahamu Getrude alikwenda kulala (siku ya tukio kwa mpenzi wake Kombo?
ACP Mchomvu: Silifahamu
Kibatala: Uliwahi kufahamu kuwa Getrude na mpenzi wake waliwahi kushauriana kuhusu hili tukio?
ACP Mchomvu: Sikufahamu
Kibatala: Uliwahi kuhafamu kuwa Kombo mpenzi wa Getrude alimshauri Getrude aitupe simu yake baharini?
ACP Mchomvu: Sikufahamu
Kibatala: Jana nilikuuliza namba hizi hapa za jalada KGB/IR/2849/2016 jibu lako lilikuwa kwamba huzijui
ACP Mchomvu: Sio kwamba sizijui, sizikumbuki
Kibatala: Sawa, kutokujua na kutokukumbuka ni vitu viwili tofauti. Katika maelezo yake aliyoyaandika ‘Detective’ Sajenti Zabron amezitaja hizo namba?
ACP Mchomvu: Sikumbuki
Kibatala: Eneo la tukio ulisema uliona chupi, kisu na filimbi, chupi ilikuwa na rangi gani?
ACP Mchomvu: Pupple rangi ya zambarau
Kibatala: Kisu kilikuwa cha rangi gani?
ACP Mchomvu: Kilikuwa chembamba chenye mpini mweusi.
Kibatala: Hicho kisu kilikuwa na damu?
ACP Mchomvu: Sikumbuki maana ni siku nyingi kwani ni miaka saba Sasa.
Kibatala: Kwa kumbukumbu zako hiyo damu iliyokuwapo iliwahi kufanyiwa genetics?
ACP Mchomvu: Hatukupima.
Kibatala: Baada ya mama wa marehemu Ndeshulwa kukwambia kuwa tayari amempata yule binti na kwamba yuko tayari kuzungumza na Polisi, ulipata ku-verify kuwa alimpata vipi?
ACP Mchomvu: Sina detail zote, hilo anajua mwenyewe huko.

Baada ya Wakili Kibatala kumaliza kumdodosa shahidi huyo, mwendesha mashtaka, Wakili wa Serikali Yasinta alimuuliza tena shahidi huyo maswali ya kumuongoza kusawazisha au kufafanua hoja zilizoibuliwa na Wakili Kibatala kwenye maswali ya dodoso.

Sehemu ya mahojiano hayo ilikuwa kama ifuatavyo:
Yasinta: Shahidi, uliulizwa kuhusu hawa waliokamatwa na wananchi wakaandika barua kuwalalamikia, unaweza kuwazungumziaje kwa kuhusianisha na hawa walioko mahakamani?
ACP Mchomvu: Wanapokamatwa na kuletwa Polisi ni wengi lakini ukirudi kuwafanyia mahojiano unaona kuwa huyu anafaa kuwa shahidi, huyu hana kesi, hivyo sio wote wanaoletwa lazima wafikishwe mahakamani inategemea na mahojiano na upelelezi.

CREDIT: MWANANCHI
 
View attachment 2659907

Vilevile Jaji Kakolaki alisema kuwa, shahidi huyo ana mamlaka ya kuwasilisha fomu hiyo kwani amekidhi vigezo kwa kuwa, kama Afisa wa Polisi ndiye aliyeomba kuchukuliwa Vinasaba, na ndiye aliyekuwa akimiliki (kuitunza) na pia kuna saini yake

Kibatala. Jana nilikuuliza namba hizi hapa za jalada KGB/IR/2849/2016 jibu lako lilikuwa kwamba huzijui

Huyo Miriam alishakiri kuwa alimuua wifi yake Aneth. Kwa hiyo hapo hakuna kesi, kitanzi kinamsubiri tuu!
 
Hata sikumbuki hii case iliishaje maana ni muda mrefu sana. Ni miongoni mwa case zilizotingisha sana Arusha na Dar es Salaam. Je mjane alikutwa na hatia?
Hii kesi nimefuatilia hadi jana hadi nimechoka sasa..but najitahidi tu niwe naendelea kufuatilia ili nielewe kiundani ila hadi saivi mambo mengi yameshakua kua wazi kiasi chake.

Nimemkumbuka Chusa kipindi kile, sijui yuko wapi siku hizi?
 
Uwakili si kazi ambayo ningeweza kufanya, yani kwa namna yule Mama aliuwawa na ushahidi, na taarifa, nisingeweza kutetea regardless amount nitakayolipwa
 
Kwahiyo Kibatala ameamua kumtetea huyo Mama aliyekiri kumuua wifi yake kwa sababu ya kulipwa pesa nzuri. Huyu ndiye tunaambiwa mpigania haki akiwatetea Chadema? Mim kila siku nasema nchi hii kila mtu anatetea tumbo lake na familia yake ila watu hawaelewi.
Yaani
 
Aachiwe tu akalee familia, ata akifungwa uhai uliopotea hauwezi kurudi; cha kujifunza, tujihami sana na vitu vinavyoweza kupoteza uhai wetu, kwa sababu uhai ukitoka haurudi, ata kama aliyekosa atafungwa miaka 200.
 
Back
Top Bottom