benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,517
3,174
Tumeona taarifa kwenye vyombo vya habari yenye kichwa cha habari kinachosema, "RPC; ANAYEDAIWA KUBAKWA NA KULAWITIWA ALIKUWA KAMA ANAJIUZA", kauli inayodaiwa kutolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma. Hayo yametokana na mazungumzo kwa njia ya simu na Mwandishi wa gazeti la Mwananchi ambaye miongoni mwa maswali aliyomuuliza kamanda (mwandishi huyo), Je upelelezi wa kesi umekamilika? na swali lingine alilomuuliza inadaiwa alikuwa anajiuza? Majibu ya kamanda aliyomjibu mwandishi huyo ni kwamba hata kama ni hivyo hangestahili kutendewa hivyo.

Pia soma>> Polisi: Wanaotuhumiwa kubaka na kulawiti ni kama wavuta bangi, hawakutumwa na Afande, yule dada alikuwa kama anajiuza

Jeshi la Polisi lingependa kutoa taarifa kuwa kauli hiyo kama inavyoonekana kwenye hicho kichwa cha habari siyo msimamo wa Jeshi la Polisi kauli sahihi ni kama zilivyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi kwa umma Agosti 4,6 na 9,2024. Vilevile tungependa kujulisha kuwa watuhumiwa watafikishwa mahakamani leo Agosti 19,2024.

Jeshi la Polisi lingependa kuomba radhi kwa kila mmoja aliyeguswa na kuchukizwa na kauli hiyo inayosambaa kwenye vyombo vya habari wakati ufuatiliaji ukifanyika kupata usahihi wake. Aidha wakati uchunguzi huo wa kupata usahihi wa kauli hizo, Mkuu wa Jeshi la Polisi amefanya mabadiliko madogo kwa kumhamisha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP Theopista Mallya kwenda Makao Makuu ya Polisi Dodoma na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP George Katabazi.

 
Namna hiyo, no time for jokes
 
Weka link ya hiyo akaunti ya Polisi iliyopo Instagram
 
Safi kabisa,alitakiwa kutumbuliwa kabisa ,huu ni upuuzi πŸ‘‡πŸ‘‡

View: https://www.instagram.com/p/C-2H0mKtrXj/?igsh=YnB0Z2Rud3hhNDAy
 
Safi sana. Yule mama hana akili.

Hata kama mtu anajiuza ndio abakwe hadharani na kulawitiwa na kisha kusambazwa mitandaoni?

Sheria ya cyber crime inasemaje, inakataza kusambaza maudhui ya ngono. Sheria za Tanzania zinakataza kulawiti, kufira na kusambaza maudhui ya ngono.

Yule mama hata huo u rpc aliupataje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…