Royal Tour ni kichocheo tu, mamlaka zisijisahau

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
299,512
751,975
Ni mwezi wa royal tour (jina haliakisi Utanzania)

Bado tuna safari ndefu kujinasua kwenye makucha ya mabeberu, lakini hili si hoja yangu kwa leo.

Wabongo tuna tatizo sugu na lazima tuliseme hapa wazi na hili ni tatizo mpaka kwenye mamlaka zetu Rasilimali watu hatuipi kipeumbele hata siku moja mbinu za kibiashara na huduma bora nalo ni tatizo kubwa sana.

Tunaamini katika majengo na vitu vya kuonekana kwa macho.
Tunaamini katika kununua madege mengi kisha tunaishia hapo mengine yataji sort yenyewe
Tunaamini katika takwimu za kujenga madarasa mengi bila kusema chochote kwa walimu na vifaa vya kufundishia
Tunaamini katika takwimu za kujenga vituo vya afya vingi lakini bila watalam wa kuvisimamia na vifaa tiba..

Hili tatizo naona nalo linajitokeza kwenye royal tour. Wachambuzi kila kona wanaongea siasa na vitu vya kufikirika. Wanaongea kuhusu watalii milioni 2.5 warakaokuja kwa sababu tu wameona filamu ya Royal Tour.

Sijaona hata mmoja akizungumzia sasa maandalizi muhimu ya kuwapokea kuwahudumia tangu wanapoingia mpaka wanapoondoka ili yasitokee mashetani yakaharibu nia njema.

Hawazungumzii hotel nzuri na za bei stahimilivu
Hawazungumzii changamoto na uswahili wa airport zetu
Hawazungumzii ubabaishaji kwenye huduma mbali mbali kuanzia usafiri wa ndani wawapo nchini, usafiri wa ndege zetu, huduma za vyakula, vinywaji na malazi
Hawazungumzii tatizo la rushwa kwenye mamlaka zetu na hata watu wa kawaida
Hawazungumzii customer care ya viwango vya wageni nknk

Kinachoendelea mitandaoni ni majisifu, kusifiasifia tu na siasa nyingi as if hiyo filamu itafanya yote hayo in automation mode. Maandalizi yasipokuwa mazuri watalii watakaokuja mwaka huu baada ya kuona filamu ya royal tour Wa naweza kuwa wa mwisho.

Tusiwaige hawa wafanyabiashara wetu wanajenga bar nzuri, ama hotel nzuri ama sehemu ya vyakula nzuri kabisa. Lakini anakuja kuajiri cheap labour isiyofahamu chochote kuhusu customer care. Yaani badala ya kumuona mteja ni mfalme yeye ndio anataka kuonwa ni malkia

Kuna vita ya kibiashara hapo hasa na majirani zetu. Je, tumejipangaje kwa hilo? Lazima kuna wachafuzi watataka kuharibu.. Je tuna maandalizi yoyote? Tuache siasa tufanye kazi

La mwisho ni hili la tetesi zisizothibitishwa kwamba mfadhili wa royal tour hawekwi wazi. Ni kwanini inakuwa hivyo? Maana kila kiongozi anaongea lake. Tusianze kuharibu mapema. Hii ikiingia kwenye hisia za kashfa. Tutaharibu mengi. Tutaharibu mapema

Viva tour du royale!
 
Ipo siku huyo mfadhili wa Royal Tour atafahamika tu pamoja naalengo yake.

Wataendelea kutuficha laki watanzania tutajua tu.

Mpaka sasa bado hatujapewa taarifa ni watu wangapi wamefuatilia uzinduzi huo online.

Watu wangapi wamenunua filamu Amazon.

Ni watu wangapi mpaka sasa wamefanya booking ya kuja kutembelea.

Tuambiwe hayo tukilinganisha na figures za miaka iliyopita.

Kinachoendelea ni kusifiana tu kutuambia hiyo movie imetupa faida gani mpaka sasa.
 
Tanzania pia inahitaji filamu nyingine nyeti kabisa inayohusu #FURSA zilizopo Tanzania,maeneo ya kilimo, madini yalipo,aina za madini zilizopo,ya metali na Vito uvuvi na nk.

Kwa ukubwa wa bahari tuliyonayo kitoweo cha Samaki kilipaswa kuwa kingi kwa bei ndogo kabisa.
 
Tanzania bado tupo kwenye kundi la nchi yenye hatari ya ugaidi. Ilipaswa pia kuongea vizuri na US ili warekebishe travel advisory yao kuhusu Tanzania.

Unajiuliza baada ya kuangalia royal tour hao watu usalama wao ukoje wakija ikiwa Kuna ugaidi nchini? Nchi za amerika ya kusini zina vivutio vizuri sana vya utalii Ila moja ya sababu inayofanya watu wasiende san ni usalama

Screenshot_20220428-100029_1.jpg
 
Kuna jambo linafikirisha;hivi hiyo siñema ya Loyal tour ilipokuwa inaandaliwa mulienda sehemu muhimu za kihistoria katika hii nchi ambazo ni Kilwa Yetu na Bagamoyo ili dunia ijue! nimetazama kipande cha hiyo sinema sijaona hizi sehemu nyeti kama zimejumuishwa.

#matoyangu
Angalia yote Kwanza then ulete mrejesho
 
Kuna jambo linafikirisha;hivi hiyo siñema ya Loyal tour ilipokuwa inaandaliwa mulienda sehemu muhimu za kihistoria katika hii nchi ambazo ni Kilwa Yetu na Bagamoyo ili dunia ijue! nimetazama kipande cha hiyo sinema sijaona hizi sehemu nyeti kama zimejumuishwa.

#matoyangu
Bagamoyo alienda, na kilwa pia alifika
 
Mshana Jr niambie upo upande gani? Mi najua wewe ni mmoja wa Watanzania mliokuwa mnataka Dkt Magufuli afe ili aje rais mwingine. Ila hoja unayo tena kubwa sana. Nenda kwenye hizo shule au vituo vya afya, nenda huko vyuoni wanakofundishwa hao ma tabibu au waalimu, yaani ni ovyo mno. Nadhani taifa hili kwa sehemu kubwa viongozi wake wamejaa ubinafsi sana hawajali wala kuona mambo muhimu. Uarabuni walichotushinda ni uamuzi wao wa kuimarisha rasilimali watu.
 
Tanzania pia inahitaji filamu nyingine nyeti kabisa inayohusu #FURSA zilizopo Tanzania,maeneo ya kilimo, madini yalipo,aina za madini zilizopo,ya metali na Vito uvuvi na nk.
Kwa ukubwa wa bahari tuliyonayo kitoweo cha Samaki kilipaswa kuwa kingi kwa bei ndogo kabisa.
Naam tubadilike tu na kuwa Taifa la Wasanii na Waigizaji..., nadhani kuhangaika na basics.., kama kilimo (kulima) madini (kuchimba) Uvuvi (kutunza mazingira na vizazi vya samaki) kunatuchelewesha sana...
 
Mshana Jr niambie upo upande gani? Mi najua wewe ni mmoja wa Watanzania mliokuwa mnataka Dkt Magufuli afe ili aje rais mwingine. Ila hoja unayo tena kubwa sana. Nenda kwenye hizo shule au vituo vya afya, nenda huko vyuoni wanakofundishwa hao ma tabibu au waalimu, yaani ni ovyo mno. Nadhani taifa hili kwa sehemu kubwa viongozi wake wamejaa ubinafsi sana hawajali wala kuona mambo muhimu. Uarabuni walichotushinda ni uamuzi wao wa kuimarisha rasilimali watu.
Kuja raisi mwingjne haimaanishi akikosea watu wasiseme.

Mmekua na akili za aina gani? Kwa kuwa tulikua hatumtaki Magufuli basi tafsiri yake raisi yoyote akija hata akikosea iwe sawa tu?
 
Back
Top Bottom