Siku ya June 27 2016 huenda ikawa ni siku ambayo mashabiki wa soka wamepata habari ambazo huenda hawakuzitarajia kutokana na matokeo ya mechi zenyewe, tulianza kusikia taarifa za
Lionel Messi,
Aguero na
Javier Mascherano wakitangaza kustaafu kutokana na kupoteza mchezo wao wa fainali ya
Copa America dhidi ya
Chile.
Kama ambavyo
Messi na wenzake wamefanya, kocha wa timu ya taifa ya
England Roy Hogdson ametangaza kujiuzulu kuifundisha timu ya taifa
England, kutokana na kupoteza mchezo wao wa 16 bora dhidi ya Iceland kwa kufungwa goli 2-1,
England walianza kupata goli la uongozi dakika ya 4 kupitia kwa
Wayne Rooney.
Dakika mbili baadae baada ya
England kupata goli la uongozi, Iceland walisawazisha kupitia kwa
Ragnar Sigurdsson dakika ya 6 na
Kolbeinn Sigposson dakika ya 18.
Roy Hodgson ametangaza uamuzi huo wa kujiuzulu kuendelea kuifundisha England, ikiwa ni siku tatu zimebakia mkataba wake umalizike.