Rose Odinga asipotuomba msamaha, Watanzania tutampa adhabu hii

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,185
18,513
Huyu Rosemery Odinga aliamua kwa makusudi kabisa kudanganya ulimwengu kuwa panapo semekana binadamu wa kwanza aliishi ni kenya wakati eneo lenyewe li ajulikana lipo arusha Tanzania.

Hii tabia ya Wakenya kujigamba kwa vitu vya Tanzania kana kwamba ni vya kwao lazima tupamvane nayo.

Wazo langu ni kuwa huyu dada asipo omba msamaha kwa haya aliyo yafanya basi tutatafuta kitu kibaya au chochote chenye sifa mbaya tutakiita Rosemery Odinga kama kumbukumbu ya mabaya haya aliyo tufanyia.

Sasa hapa tutapiga kura na kujua jina hili litumike kwa kitu gani.


Kuna refa aliwafanyia vibaya wajapan kwenye kombe la dunia wajapan walipo rudi kwao basi jina la yule refa likawa linatumika badala ya neno toilet hadi refa alipo omba msamaha.


Sisemi na sisi tutafanya hivyo ila naamini tutapata kitu cha kukiita Rosemery Odinga


Hilo jina litatumika hadi siku atakapo tuomba msamaha.
 
wajigambe na vya kwao, ka sivyo tutawabomoa
Hawana ndo maana wanajigamba na vya jirani kwa sababu jiran hajitambui na haijulikani lini atajitambua asimamie mali zake, na Huna uwezo wa kuwanya chochote, wamejitangaza kupitia kiswahili umefanya nn? Wanajitangaza kuhusu mlima Kilimanjaro umewanya nini? Upuuzi
 
wajigambe na vya kwao, ka sivyo tutawabomoa
Kuna mtu mmoja ndani ya nchi za afrika masharuki aliyewahi kuwa kiongozi WA nchi alisema watanzania Ni marehemu wanaotembea ila Si mkumbuki kwa hali hii Kama inajirudia vile. Nashindwa kuelewa wanatuchukuliaje sisi watanzania?
 
Kama wazungu wanaamini hilo fuvu lilipatikana huku na bnadamu alikua nyani "KWANINI TUKIENDA KWAO WANATUZOMEA NA WANASEMA SISI NDO NYANI??"
 
Kuna mtu mmoja ndani ya nchi za afrika masharuki aliyewahi kuwa kiongozi WA nchi alisema watanzania Ni marehemu wanaotembea ila Si mkumbuki kwa hali hii Kama inajirudia vile. Nashindwa kuelewa wanatuchukuliaje sisi watanzania?
Mazombie
 
asingeomba msamaha ningependekeza m.a.v.i. yaitwe RO but keshaomba msamaha japo kikejelikejeli.
 
Mwizi ni mwizi tuu. haangalii unaj8tambua kiasi gani hadi siku wamkate mikono.
 
Kama wazungu wanaamini hilo fuvu lilipatikana huku na bnadamu alikua nyani "KWANINI TUKIENDA KWAO WANATUZOMEA NA WANASEMA SISI NDO NYANI??"
Historia ya uwongo iliyo tungwa na wazungu. haaaa
 
Mi sina shida na Rosemary ametumia fursa, amekamata fursa sababu wenye fursa wenyewe hawaitendei haki fursa yao, wako wapi wizara ya maliasili na utalii ambao ndio wanatakiwa kutangaza mambo yote ya kitalii ndani ya nchi hiii, mkilala wenzenu wataawamsha mi naomba tumshukuru Rosemary kwa kutuamsha kwani tulikuwa tumelala.
 
I love jinsi Watanzania tulivyo-react kuhusu hii issue! Lakini kwa upande mwingine najiuliza nini zingekuwa reactions zetu endapo yule dada angekuwa ni Mtanzania lakini akasema "I was taught Lake Turkana is in Tanzania and so and so...!" Or like this "Lamu Island which's found in our country, Tanga... Tanzania...!"

Kwa Watanzania tulivyo, tungeanza kumkashifu Mtanzania mwenzetu kwa kumwita kilaza asiyefahamu Ziwa Turkana au Lamu ipo wapi!!! Lakini kv sio Mtanzania; tunaona yeye hawezi kuwa Kilaza ila tunamuona ni mtu anayependa kuipaisha nchi yake!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…