RIWAYA: THE REVENGE OF DERRICK (S 01)

Story Za Jay

New Member
Jan 10, 2025
2
0
SIMULIZI:REVENGE OF DERRICK
MTUNZI:WIZZY JOOH

SEHEMU YA KWANZA(1)*

"Walikuwa ni watu wema sana" "Ni kweli bamdogo lakini watu wabaya wamedhurumu nafsi za wazazi wangu na kwa ili bamdogo niahidi kuwa utawakamata hawa wauaji na utawafanya walipie kwa hili" "Nakuahidi Derrick nitawapata hawa watu waliowaua wazazi wako" Alikua ni inspector mbogo akiongea na Derrick mtoto wa marehemu kaka yake huku wakiwa wamesimama mbele ya makabuli matatu ambayo ndani yake wamezikwa wazazi wa Derrick pamoja na mdogo wake wa kike

"Muda umeenda Derrick tunatakiwa turudi nyumbani sasa" "sawa baba" alijibu Derrick kisha taratibu wakaanza kuondoka eneo hilo la makaburini

⭐⭐⭐⭐

"Hongera sana Nzige kwa kumuondoa yule kikaragosi aliyejiingiza kwenye kesi zisizomuhusu" ilikua ni sauti ya mama mtu mzima ambaye alionekana ni mtu mwenye utajiri mkubwa sana kwani alivaa mavazi ya gharama sana huku shingo yake ikipambwa na vito vya thamani sana

"Nashukuru mkuu" ilisikika sauti upande wa pili wa simu "Alafu hakikisha hao watu wako hawajaribu kabisa kufuatilia biashara zangu" "usijali kuhusu hilo mkuu" "Pia malipo yako nakutumia sasa hivi" "nashukuru sana mkuu" mwanamama huyo anakata simu huku uso wake ukiwa umepambwa na tabasamu pana "Binadamu yoyote anayejaribu kwenda kinyume na matakwa yangu ni lazima afee" aliongea kwa dharau mwanamke huyo huku akicheka sana

⭐⭐⭐⭐

Kulikucha asubuhi Derrick anaamka na kutoka nje ya chumba chake kisha anaingia gym iliyokua ndani ya jumba hilo kubwa la Inspector mbogo huko anamkuta baba yake mdogo akiwa tayari ameshaanza kufanya mazoezi nayeye anaamua kuungana naye katika mazoezi hayo

"Derrick baba yako aliniambia kuwa wewe huko nje ulikua ukijifunza karate" aliuliza Inspector mbogo huku akimtazama Derrick "ndio ni kweli bamdogo nilikuwa nikijifunza" "oooh vizuri sana embu njoo tupige sparring kidogo niuone uwezo wako" aliongea Inspector mbogo na kumfanya Derrick atabasamu huku wakisogea sehemu yenye uwazi kisha wakasimama katika style za kimapigano

Mpambano ukaanza huku Derrick akionyesha uwezo mkubwa sana wa kupambana japokuwa Inspector mbogo alijitahidi kumdhibiti Derrick Derrick lakini akajikuta akishindwa kwani Derrick alikua akirusha mateke na ngumi kwa ustadi wa hali ya juu mapigo hayo ya Derrick yakamfanya Inspector mbogo akubari kushindwa na kumfanya Derrick acheke sana kwani baba yake mdogo ajafanikiwa kumgusa na ngumi hata moja

ITAENDELEA

Kwa Story kali na za kusisimua tembelea ukurasa wetu wa Facebook wa story za Jay Ili update kufurahia riwaya kali kama hizi
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…