RIWAYA: Black star

THE SPIRIT THINKER

JF-Expert Member
Sep 9, 2019
417
651
Black Star 01
Mtunzi: Tariq H Haji
Mawasiliano: 0624065911

Watu waliendelea kushangilia kwa nguvu baada vishindo kadhaa kusikika. "Mshkaji hajui kupiga kidogo, anabutuwa kisawasawa" alisikika mtu mmoja akiongea.

Watu wawili kati ya watatu waliokuwa wakipambana na kijana huyo walikuwa chini bila fahamu. "Dogo unajifanya Vam Dame, nitakuonyesha" aliongea huku akihema kama kibonge alietembea safari ndefu.

Mtu huyo akakusanya nguvu zake zote na kumvaa kijana aliekuwa makini. Kijana akamkwepa ila macho yake yakabakia mwili mwa mtu hiyo.

Pasi na mtu yeyote kutambuwa, kijana huyo akageuka kwa kasi na kuzamishia ngumi nzito iliyoingia mbavuni mwa mpinzani.

Ukwenzi mkali ukamtoka mtu huyo na kuanguka huku akishika upande wa mbavu ambao ngumi ilituwa.

Baada ya kummaliza na huyo, akaokota mfuko wake na kuondoka. Hakujali watu aliopambana nao walikuwa katika hali gani.

Taratibu akajichanganya na kundi la watu na kutokomea.

Hakuonekana kama mtu mwenye maisha mazuri, nguo zake zilikuwa zimechakaa kupita maelezo. Alionekana kama mtu ambae hakuoga kwa siku nyingi.

Baada ya mwendo wa dakika kama kumi hivi, akasimama na kugeuka nyuma. Alihisi kama kuna mtu anamfatilia.

"Labda ni mawazo yangu tu" alijisemea na kuendelea na safari yake. "Hisia zangu hazijawahi kuniangusha" alijisemea tena na kusimama.

Akaweka mfuko wake chini na kuvua ndala, eneo alilokuwepo hakukuwa na watu kwa wakati huwo. Akaangaza kulia na kushoto. "Jitokeze kabla mambo hayajaharibika" aliongea.

Katika pembe ya jengo bovu akaitokeza mtu aliekuwa na suti. "Kwanini unanifatilia" aliongea kwa hasira, "tajiri wangu anataka kukuona" aliongea mtu huyo kwa sauti iliyotulia. Hakuonesha wasi wasi wowote ule. "Sina haja ya kuonana na mtu mimi, tena naomba uache kunifata" akageuka na kuvaa ndala zake kisha akabeba mfuko wake na kutaka kuondoka.

Kabla hajafanya hivyo, machale yakamcheza akageuka nyuma kwa kasi. Na bila kukusudia akabonyea chinu, konde zito likapita juu. Akarudi nyuma huku mapigo ya moyo yakimuenda mbio. Mwili wake wote ulikuwa ukitetemeka lakini ajabu alikuwa akitabasamu.

Mtu yule aliemshambulia akageuka kwa kasi na kufanya shambulio jingine. Kijana huyo akalikwepa huku macho yake yakiwa yamesalia mwili mwa mtu huyo.

Viini vyake vya macho vilicheza haraka na ndani ya sekunde moja tu akamsogelea mtu huyo na kuvurumisha konde kali sana. Alikusudia litue kifuani, ila safari hii mpinzani wake alikuwa gwiji.

Akalipangua konde hilo na kurudi nyuma, "inatosha" Ikasikika sauti nyingine. "Kijana, samahani kwa usumbufu ila kwa kipaji chako unaweza kutengeza pesa nyingi sana na ukasahau maisha ya dhiki. Ukiwa tayari nitafute japo sina zaidi ya wiki moja katika nchi hii" aliongea mtu huyo mwingine na kumkabidhi kadi yake ya biashara. Akampa ishara yule mtu wake, wakaondoka.
*****

Usiku wa siku hiyo hakupata usingizi kabisa, "isije ikawa ndio ile biashara ya kunyofolewa figo na viungo vingine" alijisemea akigaragara katika kitanda chake cha kamba. "Potelea mbali, maisha yenyewe magumu kinoma. Kama mbwai na iwe mbwai tu.".

Asubuhi mapema akajiandaa na kuweka vocha kweye simu yake. Akaitoa ile kadi ya yule mfanya biashara, akaingiza namba na kupiga. "Mimi ni yule kijana ulienipa kadi jana, sawa" akakata simu na kuirudisha mfukoni.

Akakwea daladala na kuelekea mpaka maeneo alipoambiwa ashuke. "Nifuate" kulikuwa na mtu mwenye suti akimsubiri kituoni. Walitembea kwa dakika tatu, safari yao ikakomea mbele ya nyumba ya kisasa.

Geti likafunguliwa, wakaingia na moja kwa moja mpaka katika mlango wa kuingilia ndani.

"Kijana karibu sana" alipokewa na yule mzee aliempa ile kadi. Alikuwa sebuleni akisoma gazeti, "asante na samahani kwa tabaia nilionesha jana" aliitika na kuomba msamaha. "Usijali, katika hali kama ile hata mimi ningefanya kama vile" alijibu yule nzee huku akitabasamu. Akamuonesha mkono katika kochi.

"Jambo la kwanza ni kujitambulisha, inawezekana umeona jina langu kwenye kadi niliyokupa lakini ni vyema nikajitambulisha rasmi, mimi Don Pizallo Pizillo Pazlo. Wewe unaitwa nani?"

"Fahad Abedi" alijibu
"Fahad, unajuwa una kitu ambacho ni asilimia chache sana ya binaadamu wamejaaliwa kuwa nacho" aliongea Don Pizallo.
"Sijakufahamu hapo".

Don Pizallo akasimama na kutembea umbali wa wa mita kama mbili kutoka alipo Fahad. Mkononi alikuwa na kitu kama kibira. Akageuka kwa kasi na kukirusha kuelekea kwa Fahad.

Mwili wa Fahad pasi na kusubiri amri kutoka ubongoni kwake, ukasogea pembeni huku macho yake yakiwa katika kipira kilichokuwa kikija upande wake.

Bila mategemeo akakidaka na katika hali iso kawaida akazunguka na kukirudisha kilipotoka mara mbili ya kasi kilichokuja nayo.

Don Pizallo akakikwepa, "hicho ndicho nilichokuwa nakwambia" kisha akaongea.
"Unawezaje kufanya hivyo" aliuliza.

"Hata mimi sijui, mara zote ninapokuwa katika uso wa hatari. Mwili hufanya maamuzi wenyewe pasi na mimi kufikiri kurudisha majibu mara mbili ya jambo lilnalotokea" alijibu Fahad.

"Huwo ulokuwa nao ni ugonjwa katika tekinolojia ya sasa lakini hapo kale ilikuwa ni zawadi.

Iliitwa 'nguvu ya macho', ama kwa kiingereza wanaita visual prowse. Katika hatari macho yako na ubongo vinafanga kazi mara dufu kuliko kawaida. Chochote kinachotokea, katika macho yako ni kama kinakwenda katika kasi ndogo sana 'slow motion'. Hivyo inaipa akili yako uwezo wa kupambanuwa njia ya kukwepa hatari hiyo".

Bado Fahad alikuwa njia panda, asielewe ni jambo gani hasa alilomaanisha mtu huyo.

"Najuwa utakuwa na maswali mengi, ukidhani kwamba mambo kama hayo hayawezekani lakini kijana katika hii dunia kuna mambo mengi sana ambayo hayana majibu.

Na kama ilivyoada kwa binadamu, jambo lolote ambalo halielewi aidha anasema ni janga, ugonjwa au ana kanusha kabisa" aliendelea kuelezea.

"Umenambia kipaji changu kinaweza kunipa utajiri kama sikosei, kivipi?" aliuliza Fahad.
"Ukinitumikia mimi, nitakikuza kipaji chako"
"Kukutumikia kivipi?"

"Utaniwakilisha mimi ulingoni, utapigana kwa ajili yangu. Mimi nitakulipa, kila pambano moja utachukuwa robo ya faida yote.

Ulingo utakaopambana si wa kawaida. Utakutana na watu wenye vipaji kama chako na visivyo kawaida kabisa".

"Tunapoongelea mapato, tunaongelea kiasi gani kwa mfano"
"Kwa mtu kama wewe ambae utaanza daraja la chini, kila mechi utakayoshinda. Mapato yake hayatakuwa chini milioni mia moja.

Ikiwa tutashinda milioni mia moja wewe utachukuwa milioni ishirini na tano. Hiyo itakuwa yako tu, kuhusu malazi na kuishi kwa jumla yote hayo yatakuwa juu yangu kama mdhamini wako"

Fahad akameza funda kubwa la mate, tayari alishaona utajiri mbele ya macho. Taswira ya wazazi wake wanavyo hangaika ikajirudi akilini kwake. "Kama ilivyo kwa faida, katika mapambano hayo kufa ni jambo la kawaida.

Kitendo cha kuingia ulingoni kwa mara ya kwanza, huenda ikawa ndio mara ya mwisho pia" alikatishwa mawazo yake na maneno hayo.

Fahad akameza funda kubwa la mate, tayari alishaona utajiri mbele ya macho. Taswira ya wazazi wake wanavyo hangaika ikajirudi akilini kwake. "Kama ilivyo kwa faida, katika mapambano hayo kufa ni jambo la kawaida. Kitendo cha kuingia ulingoni kwa mara ya kwanza, huenda ikawa ndio mara ya mwisho pia" alikatishwa mawazo yake na maneno hayo.

Endelea nayo..

Fahad akakaa kimya kidogo, alionekana kutafakari mambo mengi sana. "Kweli kuingia ulingoni ni sawa na kuuza roho ila ikiwa kuuza kwangu roho kutaisaidia familia yangu kutoka katika dimbwi la fedheha" maneno hayo yalipita kichwani mwake. Akashusha pumzi ndefu kisha akainuwa kichwa kumuangalia kumuangalia Don Pizallo. Don Pizallo akatabasamu na kuinuwa mkono wake juu kisha akasema "niletee mkataba".

Hakutaka hata kusubiri jibu kutoka kwa Fahad, macho tu yalitosha kujieleza kama alikuwa tayari kuuvaa ulimwengu huwo wenye kunukia harufu ya damu. Mlinzi mmoja akaleta bahasha kubwa ya A4 na kumkabidhi bosi wake. Akaifunguwa na kutoa mkataba ulioandikwa lugha nne, Kizungu, Kifaransa, Kichina na Kiswahili. Akamkabidhi Fahad, akausoma kwa lugha anazoelewa.

" Naomba kalamu" aliongea, "kijana mkataba huwo hausainiwi kwa kalamau" alijibu Don Pizallo kisha akatoa kisu kidogo kwenye ile bahasha na kumkabidhi. "Kata kidole gumba na weka saini ya damu" aliongea, Fahad akakata kidole alichoambiwa na kuweka saini.

Don Pizallo akatoa simu kwenye bahasha hiyo hiyo na kuiwasha. "Kuanzia leo utakuwa chini ya himaya yangu, mimi nitakuwa mlezi wako. Jambo la kwanza unalotakiwa kufanya ni kukata mawasiliano na watu wote ambao hujahusiana nao kwa damu. Hatuwa ya pili ni kuhama unapokaa sasa na kuhamia katika nyumba nitakayokupa mimi lakini huyu hutakaa na wazazi wako".

" Sasa wao watakaa wapi"
"Usijali kuhusu hilo, tokea siku ya kwanza nilipokuona nilikuwa najiandaa kwa siku ya leo. Hivyo kila kitu kimeandaliwa, kete ya mwisho ilikuwa ni wewe tu.

Madhali wewe ushaicheza, sasa bao limekamilika. Karibu katika ulimwengu mzuri na mchungu"
Fahad hakuwa na la kusema zaidi tayari maji alishayavulia nguo na hakuwa na budi kuyaoga.

"Wazazi wako tushawaandalia sehemu ya kukaa na mipango yote ya wadogo zako kuhamishwa shule iko tayari" Kwa Fahad, nafasi hiyo ilikuwa ni kama kuzaliwa upya. Katika maisha yake hakuwahi kufikiria kama itatokea siku ataondoka kwao masikini na ndani ya saa chache atarudi akiwa tajiri.

"Shika hii kadi ya benki, password iko nyuma. Katika akaunti hiyo kuna bilioni moja. Hiyo ni zawadi ya kujiunga na taasisi yangu. Tumia hiyo kubadilisha maisha yako, Mimi nitakutafuta baada ya miezi sita kwa ajili ya kuendelea na mambo mengine" aliongea na kumkabidhi kadi hiyo.

Baada ya mazungumzo hayo wakaagana na kuondoka wakiahidiana kuonana baada ya siku tatu kwa ajili ya kuhama. Fahad akatoka katika nyumba yatu huyo akiwa bado haamini kama maisha yake yamebadilika tayari.

Akasindikizwa mpaka kituoni na kupanda daladala ya kurudi nyumbani.

Aliposhuka tu akaingia ATM na kutoa laki nne kisha akapita mgahawani na kununua chakula kwa ajili ya nyumbani. Alitamani afike haraka nyumbani ili angalau wazee wake wale chakula kizuri ambacho hawakukila kwa muda mrefu sana.

*********
"Shikamoo mama" alipoingia ndani na kumkuta mama ake akiwa jikoni. "Marahaba mwanangu, afadhali umekuja baba. Hali nyumbani si nzuri, tokea kulipokucha hakuna alietia chakula mdomoni. Wadogo zako wameemda shule bila chochote" aliongea mama ake huku akilengwa na machozi.

Japo Fahad alitambulika mtaani kwa uwezo wake kupigana, mbele ya familia yake alikuwa mwepesi sana.

Ulifika wakati alilala njaa siku mbili bila kula, kwa sababu tu chakula alichokuja kuja nacho hakikutosha kwa watu wote nyumbani.

"Usijali mama, nimekuja na chakula. Twende ndani tukamuamshe baba halafu tule" aliongea huku moyo wake ukimuuma sana. Hakutaka kulaumu mtu kwa sababu maisha yalikuwa magumu.

Wakaingia ndani, mama ake akaishia sebleni na yeye akaenda kumuamsha baba ake. Mzee huyo alikuwa amekonda kupita maelezo.

Kwa haraka haraka alionekana kati ya miaka hamsini na tano na sitini na tano. Lakini kiuhalisia alikuwa na miaka arobaini na tano tu.

Fahad akamsaidia mzee huyo mpaka sebleni, kumuweka kitako. Akaenda kuchukuwa maji na kuwanawisha wazazi wake.

Akafungua mfuko alokuja na nao na kutoa paseli za chakula. Akakiweka kwenye sahani. Ama njaa haina mzee, kijana wala mtoto, wazazi wake walivyokiona tu walifakamia. Fahad akakaa pembeni akiwaangalia huku machozi yakimtoka. "Maisha haya mwisho leo, hata ikibidi nipambane na dunia nzima sitaruhusu murudi huku" alijisemea kisha akaungana nao na kupata chakula.

Wadogo zake nao waliporudi walikula mpaka wakasaza, siku hiyo ilikuwa ni sherehe kwao. Maana chakula kilikuwemo ndani na kila aliejisikia kula alikula.

Usiku wa siku hiyo baada ya wadogo zake kulala, Fahad akawaita wazazi wake. "Kuna nini Fahad baba" aliuliza baba ake.
"Kuna jambo nataka niwaeleze, na naombeni mnibariki maana sina njiaa nyingine ya kujikomboa katika maisha haya. Nitawaeleza kila kitu kwa sababu kuwaficha haliyakuwa jambo la busara"

"Sema tu baba" aliongea mama ake. Fahad akawaeleza kila kitu pasi na kuficha jambo lolote lile. Wazee wake walimsikiliza kwa makini, mama ake alionekana kutokubaliana nae mwanzo lakini baada ushawishi kutoka kwa mumewe hatimae akakubali.

"Fahad baba, wewe sasa ni mkubwa. Mimi nina heshimu maamuzi yako, nafahamu kama sehemu ya maamuzi yako ni kutokana na mimi kushindwa kufanya majukumu yangu kama baba wa familia hii hivyo mzigo kukuangukia wewe. Naomba unisamehe mwanangu" aliongea mzee huyo.

"Hapana baba, mimi nakumbuka sana maisha kabla ya haya, hatukuwa hivi sisi na ulijitahidi kadiri ya uwezo wako kuhakikisha familia inabakia moja. Mimi sitachukuwa jukumu lako la kuishughulikia, kichwa wa familia utabaki kuwa wewe tu".

Baada ya mazungumzo wakaagana na kila mmoja akaelekea chumbani kwake kwa ajili ya kupitisha usiku. Siku ya pili asubuhi mapema sana, Fahad akatoka kuelekea kufanya mambo yake na maandalizi mengine kabla ya kuhama.

Safari hiyo iliishia nje ya mlango wa mpenzi wake wa muda mrefu, mwanamke ambae alitokea kuuteka moyo wa kijana huyo. Siku hiyo alikuwa amependeza sana, na alifika kwa lengo la kumpa taarifa nzuri mwanamke huyo lakini moyo wake ulikuwa ukimuenda mbiyo. Alihisi kama hakuhitaji kuwepo eneo hilo.

Baada kujishauri hatimae akagonga mlango, kimya!. Akajaribu tena mara ya pili, kimya!. "Nina uhakika niliisikia sauti yake nilipofika kwanini hataki kufunguwa" alijiuliza swali lilikosa jibu, akagonga mara ya tatu. Safari hii aligonga kwa nguvu kiasi kama angepita mtu angejuwa mlango unataka kuvunjwa. Baada ya sekunde chache mlango ukafunguliwa kwa kishindo.

Akatoka mwanaume mwenye mwili mkubwa uliojaa, alikuwa amevaa kaptula na alionekana akitoka jasho kama mtu aliekuwa akifanya kazi ngumu.

"Wewe nani na kwanini unasumbuwa watu wakiwa wamempumzika" alifoka mwanaume huyo. Fahad hakujibu kitu, aling'ata meno kwa nguvu ili kudhibiti hasira zake.

"Baby, nyani gani hiyo anaesumbuwa watu mchana wote" sauti ya kike ikitokea nyuma ya mtu hiyo ikasikika.

Fahad alaitamani sauti isiwe ya mtu aliempenda zaidi kutoka katika mtima wa moyo wake.

Ana kwa ana na mpenzi wake akiwa kajifunga kanga ya kifua. "Fey!" aliita Fahad akiangusha mfuko aliokuwa ameubeba.

Mwanamke huyo alirudi ndani kwa kasi kama mtu alieona kiumbe cha ajabu. "Oya, unamjuaje demu wangu" aliuliza yule mwanaume mwengine. Fahad hakujibu kitu, akageuka na kuanza kuondoka.

"Dogo acha dharau" aluongea yule mwanaume na kuingia. Akavaa flana na kutoka kwa ajili ya kumfuata Fahad. "Pati sikia, muache aende usitafute matatizo" Fey alikuwa nyuma ya mwanaume huyo huku akimsihi kutomfata Fahad. "Mtu yeyote anaekata starehe yangu lazima alipe" aliongea Pati na kujifanya ana hasira mno.

Fahad alitembea taratibu kuelekea kituo cha daladala, furaha yake yote ilitoweka. Alihisi kufanyiwa dhuluma ya hali ya juu kuliko kitu chochote. Akiwa katika dimbwi la mawazo akatahamaki amepigwa kikumbo kizito. Akaweweseka na kuanguka chini.

"We boya mi nimekuuliza umemjuwaje demu, unajifanya husikii siyo" aluongea Pati akiwa kafura kwa hasira.

"Mimi sina ugomvi na wewe, na kama ni huyo mwanamke mimi nakuachia wewe. Naomba niende zangu, kuhusu nimemjuaje muulize yeye mwenyewe.

Mimi sina huwo muda" alijibu Fahad, alikuwa akitokota rohoni. Hata hivyo hakutaka kufanya vurugu, alijisafisha mavumbi na kuanza kuondoka.

Pati kuona hivyo, akamfata kwa kasi akiwa na lengo la kumtia kabari. Fahad akamkwepa na kurudi nyuma. "Umeomba mwenyewe, kitakachokukuta umekitafuta mwenyewe" aliongea kwa hasira na kumuangalia Pati aliekuwa akitabasamu mbele yake kisha akaendelea "au ndio umezoea ule msemo, unachukuwa mali ya mtu na unampiga mwenye mali. Si ndio".

Pati akajitutumua na kutaka kumvaa Fahad tena, Fahad akamkwepa tena. Ila wakati Pati anageuka, Fahad nae akazunguka kwa kasi na kuachia teke zito. Kutokana na kugeuka kwa mpinzani wake kulikuwa kwa kasi.

Hatari ya teke lake iliongezeka mara mbili na lilipotuwa kifuani kwa Pati lilikuwa na nguvu mithili ya risasi ya shot gun.

Akarudishwa nyuma mita kadhaa, Fahad hakuishia hapo, mguu wake ulipotuwa tu akamsogelea kwa kasi na kuruka huku akizunguka na kufyetua teke jingine "Teke la punda" lilituwa kifuani na kumtupa huko kama mzigo.

Watu waloshuhudia pigo hilo walidhani wamemuona Jin Claude Van Dame akiwa kazini kumbe ni mswahili mwenzao. Pati akajaribu kuinuka lakini mwili wake ukagoma kutoa ushirikiano na kujikuta akirudi chini huku fahamu zikimtupa mkono. "Fey, mimi na wewe tumeishi vizuri kwa muda mrefu na sikuwahi kabisa kufikiria suala la kusaliti penzi letu.

Nashukuru kwa muda wako na msaada wako mkubwa katika maisha yangu ila mara hii ndio itakuwa mwisho mimi na wewe. Najuwa kama kunisaliti hujaanza leo, lakini kwa vile sikuwahi kukuona sikutaka kukushutumu kutokana na ushahidi mchache wa sms. Ila leo ndio itakuwa mwisho kuniona".

Akafunguwa begi lake na kutoa bahasha ndogo, akamkabidhi mschana huyo. " Chukulia hiyo kama zawadi ya uliokuwa upendo wangu kwako".

Bila kumuangalia usoni akageuka na kuondoka. Fey akaifunguwa bahasha hiyo, macho yalimtoka na mapigo ya moyo yakamuenda kasi. Bila hata kuangalia hali ya Pati akageuka na kutimuwa kama mwenda wa zimu.

*******

Siku ya tatu, Fahad akapokea simu kutoka kwa bosi wake iliyomueleza ajiandae. Wakachukuwa vitu vichache tu vya muhimu. Mchana ikafika gari nyeusi kubwa aina ya range rover na kuwachukuwa.

Na safari mpya ya maisha yao ikaanza. Walifikishwa kwanza familia yake katika nyumba yao na baada mambo kukaa sawa, Fahad akapelekwa katika nyumba ambayo angeishi yeye.

Baada ya kukamilisha kila kitu kwa siku, akaupitishwa usiku uliojaa upweke huku mawazo ya kusalitiwa yakitabda kichwa mwake. Asubuhi iliyoufuata akaenda kwa wazazi wake kwa ajili ya kwenda nao madukani. Siku walifanya manunuzi ya nguo na vitu vingine vingi tu, jioni wakarudi nyumbani na kula chakula cha pamoja.

Kwa wazazi wake siku hiyo ilikuwa ni moja kati siku za furaha zaidi lakini kwa Fahad siku hiyo ilikuwa ya mwisho ndani ya miezi sita ijayo kula na wazazi wake.

Wakiwa nje na Mzee Abedi.
"Mimi nikiondoka leo, tutaonana baada ya miezi sita. Kutokana na asili ya kazi yangu, mimi ndio nitawatafuta. Ile nyumba kule tulipokuwa tunakaaa mwanzo iuze na uongezee pesa utakayoipata na hii ufungue tena biashara yako, najuwa bado hujazeeka sana kushindwa kufanya kazi" aliongea Fahad na kumkabidhi mzee wake begi ndogo yenye pesa ndani.

"Mungu akutangulie katika mapambano yako, kumbuka kumuweka yeye mbele" aliongea Mzee Abedi na kumkumbatia mwanae.

Baada ya mazungumzo marefu wakaagana, Fahad akaondoka na kuelekea katika maisha yake mapya ambayo yaliambatana na misukosuko mingi sana.
******

"Jina langu ni Mr Kim, mimi nitakuwa mshauri wako" alijitambulishwa mwanaume mmoja mwenye asili ya kikorea. "Kuanzia leo, ratiba zako zote nitazipanga mimi. Utakula nini, utavaa nini, utalala saa ngapi, utaamka saa ngapi, yote hayo nitapanga mimi. Kazi yako wewe itakuwa ni kufuata tu. Kuanzia leo, uhakika tutakuwa na miezi kumi na miwili mpaka mzunguko wa kwanza wa mtoana.

Katika miezi hiyo kumi na miwili, tutatumia miezi sita kukujenga kiakili, kimwili, kifikra na kitaswira kama mpiganaji pro "Pro Fighter". Kutakuwa na kikosi maalum kitakachohakikisha yote hayo niliokuambia" aliongea Kim.

Dakika chache wakiwa katika mazungumzo wakaingia watu wengine kadhaa katika ukumbi huwo. "Huyo hapo ni Miss Pei Pei, pamoja na timu yake watahusika na afya ya mwili wako".

"Anaefuata ni Dr Xie, bingwa wa dawa na tiba asili za kichina, pamoja na timu yake watahusika na afya yako"
"Anaefuata ni Mark Phil, pamoja na timh yake watahusika mafunzo yako ya kujenga mwili".
"Ndani ya miezi sita, utakuwa mtu mwengine kabisa" aliongea Kim na kuweka miwani yake sawa, Fahad akameza funda kubwa la mate.

Miezi sita baadae.
"Anaendeleaje?" aliongea Don Pizallo akiwa katika kikao na Mr Kim. "Naweza sema umeokota almasi kwenye rundo la mawe, anashika mambo mapema sana. Ukikutana nae sasa hivi, unaweza hata usimtambue" alifafanuwa Mr Kim. "Nipe taarifa zake zote"

"Urefu wake ni mita mia na thamanini na tatu, uzito ni kilogramu sabini na tano. Kiwango cha mafuta mwilini ni sifuri pointi tano. Mwili ni ule wa mwana mazoezi wa kati, hana shida yeyote ya kiafya. Gurupu lake la damu ni O+ na mwisho uwezo wa akili ndio shida, maana ni ule wa mtu wa kawaida tu"

"Ahsante baada ya hili mpe likizo ya wiki moja aende akaonane na familia yake na kuwaaga kabisa. Wakati akiwa huko chukuwa tokeni ya silver nenda ubalozi wa China. Kutana na Xie Fey, muoneshe hiyo tokean na kila kitu kitakuwa vizuri" aliongea Don Pizallo na kumkabidhi Mr Kim tokeni ya silver. Baada ha mazungumzo ya muda mrefu wakaagana na Mr Kim akaondoka.

Nyumbani kwa mzee Abedi.
Audie coupe yenye rangi ya almasi, ilisimama nje ya geti la nyumba ya mzee huyo. Honi kadhaa zikapigwa, mlinzi akafunguwa mlango mdogo na kutoka nje. "Samahani mkuu, naweza onana na baba mwenye nyumba" aliongea Fahad kwa upole sana. "Sawa, ngoja nimepelekee taarifa" aliongea mlinzi huyo na kurudi ndani kisha akafunga geti.

Akaingia ndani ya kibanda chake na kunyanyua mkonga wa simu kisha akabonyeza namba kadhaa. "Mkuu, kuna kijana anataka kukuona. Yupo nje ya geti hapa" aliongea na baada ya kujibiwa akakata simu.
Akabonyeza kitufe na geti kubwa linaloendeshwa kwa umeme likafunguka.

Taratibu Fahad akaingiza gari na kwenda sehemu ya maegesho. Kulikuwa na magari mingine matatu ya kisasa zaidi aina ya land cruise amazon V8. Fahad akaegesha gari yake pembeni kwenye eneo ambalo halikuwa na gari. Akazima na kushuka, "kijana habari yako" akasikia sauti nzito ikitokea nyuma yake.

Moja kwa aliitambuwa kuwa ni ya babaake tena ya kipindi ambacho alikuwa na maisha mazuri.

Akageuka na kumuangalia asiamini macho yake, "Fahad" aliita baba ake. "We mwana kasoro nikusahau" aliongea mzee huyo na kufunguwa mikono. Fahad akaingia kwenye mikono hiyo ambayo kwa kipindi kirefu ilipoteza umoto wake.

"Kijana wangu sasa umekuwa mtu mzima, Gentleman. Twende ndani, nina uhakika kuna mengi sana tunataka kuongea" aliongea mzee huyo baada kuachiana na mwanae. "Mzee unaonekana umekuwa kijana sana" aliongea Fahad akiwa na tabasamu usoni.

Wakaingia ndani na kuketi kwenye makochi, mzee Abed akainuka na kuelekea chumbani kwake. Baada kama dakika chache akarudi akiwa kamshika mkewe mkono. "Mke wangu, ndio kwanza ina miezi sita. Unajifanya kama ina miezi nane" aliongea kwa utani. "Najifanya! Kama unaona rahisi twende nikakupe wewe hili tumbo" alijibu mkewe kwa kudeka. "Basi mama watoto, nitakununulia chakula ukipendacho leo".

Fahad aliekuwa sebleni alisikia maneno yote, bila matarajio yake machozi yakatengeza njia na kububujika mashavuni mwake. " Hatimaye furaha imerejea katika mioyo yao" alijisemea mwenyewe. "We Fahad mbona umepumbazika hapoa" aliisikia sauti iliyokua kwa ukali. "Ah! Mama nilidhani na wewe umenisahau, maana mzee hapo alikuwa kanisahau".

"Yaani nikubebe tumboni miezi tisa, nikunyonyeshe miaka miwili na kubadilisha nepu zako mpaka uwezo wa kunusa umekufa. Leo nikusahau kwa sababu umeongezeka kidogo tu" aliongea mama ake huku akitabasamu. "Hilo ndio tabasamu nilikumbukalo kutoka kwa mama yangu kipenzi" maneno hayo yalipita kichwani mwake. Akainuka kutoka kwenye kiti na kwenda kumkumbatia.

"Nimewakumbuka sana wazazi wangu" aliongea wakiwa wameketi sebleni wakisindikizwa na sharubati ya baridi. "Tumekukumbuka pia sema ndio hivyo tulikuwa na makubaliano. Na mimi naheshimu sana makubaliano" aliongea babaake. "Yah! Akili ya mfanya biashara kwa damu" aliongea Fahad na kutabasamu.

"Wadogo zako watarudi muda si mrefu" aliongea mama ake. "Mi sina haraka, nitakuwepo hapa kwa wiki nzima. Ni matumaini yangu tu chumba changu hakijawa cha kuhifadhia vitu" aliongea na kutania. Wote wakacheka, wakaendelea kuongea bila kuwa makini na muda. Walishtuliwa na mlango ukifunguliwa. Walikuwa wadogo zake wawili, wote wa kike. Walivyomuona tu, wakamkimbilia na kumkumbatia. "Naona mumekuwa sana" aliongea akiwa na furaha sana.

"Mimi ndio nimekuwa, Salha yupo vile vile" aliongea mmoja kati yao. "Hapana, mimi ndio nimekuwa Salma ndiyo bado yuko vile vile" mwingine nae akaongea. "Nyie mtapishana vimo tu, si mnajuwa kama nyie ni mapacha" aliongea akiwagusa vichwani, wakiwa wamekaa katika mapaja yake. "Kama sisi mapacha mbona hatufanani" aliuliza Salha. "Kwani kila mapacha lazima wafanane?", "ndio" alijibu Salma.

"Hilo si kweli, mapacha wengine wala hawafanani"
"Sasa kati yetu nani kulwa nani doto" aliuliza Salha.
"Hilo hata mimi sijui, muulizeni mama"
"Nyie vichwa, nendeni mukabadilishe nguo, muda wa kula umekaribia" aliongea mama yao. Wote wawili wakashuka kitoka mapajani mwa kaka yao na kuelekea chumbani kwao.

*******
"Kaka unaondoka leo" aliuliza Salha, "hapana, nitakuwepo kwa wiki moja" alijibu. Maongezi hayo yalifanyika wakati wa kula. Baada ya kupata chakula wakajumuika pamoja sebleni na kuongea na kufurahia. Kwa Fahad siku hizo ndani ya wiki hiyo zilikuwa na maana kubwa sana.

Kwa vile siku ya pili ilikuwa weekend walitoka na kufanya matembezi maeneo mbali mbali. Kila mmoja ndaji ya familia alifurahi sana.
"Baba, mimi kesho naondoka" aliongea Fahad akiwa nje na mzee Abedi.
"Tutakuona lini tena?"
"Sijui ila huenda nikawa mbali kwa zaidi ya mwaka na nusu"
"Mwaka na nusu ni kipindi kirefu sana, kuwa makini sana mwanangu. Popote utakapokuwa tambuwa kuwa ikiwa utakosa sehemu ya kutoa mawazo yako. Njoo nyumbani mimi nitakusikiliza"
"Kuna kitu nahitaji kukusitiza baba"
"Kitu gani"
"Najuwa ipo siku watakuja, unaweza kuwasemehe lakini usije ukawaleta katika maisha yetu.

Unawafahamu vizuri ni watu wa aina gani" sauti yake ilionesha wazi kuwachukia aliokuwa amewakusudia katika sentensi yake.
"Usijali, hilo halitatokea" alijibu mzee Abedi na kumshika mwanae begani kama ishara ya kumhakikishia alichokisema. Wakaendelea na maongezi mpaka usiku ulivyokuwa mkubwa, wakaagana na kila mtu akaenda chumbani kwake kwa ajili ya kupimzika.

Siku ya pili asubuhi, Fahad akaaga familia yake na kuondoka. Alipofika tu nyumbani kwake alipokelewa na Mr Kim aliekuwa getini akimsubiri. "On time" aliongea mkorea huyo. "Mipango imekaaje" aliuliza Fahad baada salamu. "Kila kitu kipo sawa, kesho usiku tutaruka kuelekea China" alijibu.

"Sawa hakuna shida" alijibu na sura yake ikabadilika kabisa. Tabasamu jepesi likajichora usoni mwake, kwa mtu wa kawaida angedhani labda amefurahishwa na kitu lakini kwa Mr Kim tabasamu hilo lilionesha wazi taswira halisi ya Fahad. Alikuwa akitazamia maisha yake mapya ulingoni, japo hakuelewa ulikuwa ulingo wa aina gani. Damu yake haikuacha kuchemka kila alipofikiria matumaini ya kuingia na kutoka katika ulingo ambao ungekuwa ndio mwisho wa maisha yake.

Beijing international airport, China.
Ndege ya shirika la Emirates ilkanyaga ardhi ya China saa kumi na moja alfajiri. Baada ya safari ndefu takriban saa kumi nane, kwa mara ya kwanza Fahad anakanyaga ardhi ambayo si ya nchi yake. Akiwa ameongozana na kikosi chake, wakaelekea mpaka sehemu ya kukaguliwa mizigo. Walipofika hapo, Mr Kim akatoa ile tokeni ya silver. Wakaelekezwa sehemu ya kusubiri.

Dakika tano baada akafika mtu akiwa mavazi rasmi ya taifa hilo na kuwapa ishara ya kumfata. Wakainuka na kufanya kama walivyoambiwa. Wakapita mlango maalum wa VIP na kuongozwa hadi nje ambako kulikuwa na gari ikiwasubiri. Wakaingia na safari ya kuelekea katika hoteli ambayo walipangiwa kufika.

"Karibuni Beijing" Kwa mara ya kwanza aliongea yule aliewafuata kule ndani. "Mutapumzika kwa leo, kesho nitawapeleka maeneo mbali mbali kwa ajili ya utalii" aliendelea kuongea huku akiwaelekeza mambo mbali mbali kuhusu jamii ya watu wa hao. Baada ya safari ya dakika kama kumi na tano hivi wakawasili katika sehemu ambayo wangepumzika kwa siku hiyo.

Haikuwa hoteli kama walivyotegemea, ilikuwa ni nyumba ya chini iliojengwa kimila zaidi. Wakakaribishwa na wenyeji wa eneo hilo na kila mmoja akaoneshwa chumba ambacho angelala. Baada ya hapo wakatembezwa maeneo mengine ya nyumba hiyo na walipomaliza ziara hiyo ndogo kila mmoja akarudi chumbani kwake kwa ajili ya kupumzika. Kutokana na uchovu safari, Fahad alipojiweka tu kitandani usingizi mzito ukamchukuwa.

Alikuja kushtuka baada ya baridi kuwa kali sana, akashuka kitandani na kufunguwa begi lake. Akatoa koti kubwa na kuvaa kisha akakaa kitandani, baada mwili wake kupata joto la kutosha. Akabadili nguo na kuvaa taula kubwa kisha akaingia bafuni na kufanya usafi wa mwili.

*********
Siku ya pili asubuhi baada ya kupata kifunguwa kinywa, Fahad na kamati yake wakatoka na kuelekea ziarani. Walitembea maeneo mbalimbali katika mji huwi. Jioni wakarudi walipofikia kwa ajili ya kupumzika. Wakiwa wanapata chakula cha usiku, simu ya Mr Kim ikaita.

"Habari yako mkuu" aliipokea na kuongea, "sawa, hakuna shida. Niko nae na hapa" aimalizia na kumkabidhi simu Fahad. "Fahad kijana wangu, habari za siku" aliongea Don Pizallo. Alionekana kuwa na furaha sana, "nzuri mkuu sijui upande wako" alijibu Fahad. Wakaongea mawili matatu kisha akairudisha simu kwa Mr Kim. Na baada ya maongezi ya muda mrefu, Mr Kim akakata simu na kushusha pumzi ndefu.

"Inaonekana likizo inakwisha leo, mkuu anakuja kesho na kesho hiyo hiyo tutakwenda kwenye majaribio kwa ajili ya kutafuta mwalimu wa kukufundisha kwa kipindi ambacho tutakuwa tunasubiri mzunguko wa mtoano" aliongea.

Fahad akatabasamu kidogo kisha akarudi katika hali yake ya kawaida. "Atatua saa nne, tutakutana nae muda huwo na kuelekea huko kwa walimu" alimalizia kisha akaendelea kupata chakula cha usiku. Baada ya chakula hicho wakaagana na kuelekea vyumbani mwao.

Akiwa huko Fahad akavua nguo na kubakiwa na kaptula, akaanza kupiga push up kama sehemu ya kuukumbusha mwili wake kama hakuja katika nchi hiyo kutalii. Hakuishia hapo aliendelea kufanya mazoezi mbalimbali mpaka akariwa jasho japo kulikuwa na baridi. Akaingia bafuni na kujisafisha kisha akarudi chumbani na kuupitisha usiku.

Saa nne na nusu asubuhi nje ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Beijing. Don Pizallo alikuwa nje ya uwanja huwo akisalimiana na kukosi cha Fahad. "Pole kwa safari" alionfea Fahad na kumpa mkono.
"Ahsante" aliitika akiupokea mkono, kitendo kilifanya damu yake iende mbio. "Kweli ni Fahad ninaye mjuwa mimi huyu au" alijuliza lakini hakutaka kuonesha wasiwasi wake. Wakaingia kwenye gari na safari ya kuelekea katika majaribio ikaanza.

"Fahad, huko tunapokwenda hatutakuwa peke etu, kutakuwa na wapiganaji wengine pamoja na mabosi zao. Usijali hakutakuwa na kupigana, ila kutakuwa na mashine ambayo utatakiwa upige ngumi. Mashine hiyo itakuzawadia tarakimu kuanzia moja mpaka mia. Ni mashine ambayo itapima uzito wa ngumi yako, kiwango cha chini ili walimu wakuchague unafakiwa ufikishe hamsini" alifafanuwa Don Pizallo.

"Lakini mimi sijui hata uzito wa ngumi yangu, sijawahi kujaribu kuupima hata siku moja" "Katika mapambano yako yote, si umewahi kupiga mtu ngumi ya mbavu ukahisi umemvunja mbavu"
"Ndio ila mara nyingi ni kwasababu, mtu huyo anakuwa katika mwendo, mwili wake na ngumi yangu vinapo kutana madhara ndio huwa hivyo"

"Usijali sana kuhusu hilo, wewe jitahidi kupiga kadri ya uwezo wako unavyokuruhusu. Hata hivyo uzito utakuwa ni kwa mikono yote miwili, hata ikiwa iwa mmoja utapata ishirini na mwingine ukapata thalathini inatosha"

Maongezi hayo yaliifanya safari hiyo ndefu kuwa fupi, hatimae gari ikawasili nje ya jengo kubwa. Lilikuwa kama ngome kwa nje. Wakashuka na kuelekea ndani ya jengo hilo, "hili ni jengo la biashara lakini sisi ndio tunajuwa hasa maana ya jengo hili" aliongea Don Pizallo. Walipofika ndani wakapanda lifti lakini hawakubonyeza vitufe vya kawaida. Don Pizallo akatoa kadi fulani ya dhahabu na kuigusha katika ukuta wa nyuma wa lifti hiyo.

"Karibu mshiriki" sauti ilisikikam kisha lifti hiyo ikafubguka nyuma, wakatoka. Kulikuwa na watu wengi waliokuwepo eneo hilo kwa ajili ya majaribio. Fahad alipigwa na bumbuwazi, tayari alishaweka akilini mwake kuwa yeye ndio atakuwa kivutio katika macho ya wengi. Lakini alichokutana nacho humi kilikuwa ni kinyume na matarajio yake.

Hao wahusika wengie walikuwa ni watu aina yao peke yao. Walikuwa wamejazia kisawasawa, walikuwa wanatisha hata kuwaangalia. "Oh! Pizallo naona umetuletea mtoto wa kike katika majaribio ya kiume" aliongea mtu mmoja, alikuwa na kofia ya cowboy kichwani na sigara nene mdomoni. "Naona hujabadilika, Han Panzo. Mpaka leo unadhani kuwa na mwili mkubwa ndio kuwa na nguvu nyingi" aliongea Don Pizallo akijitahidi kuficha hasira zake.

"Hahaha, Pizallo wewe ni mtoto wa juzi tu. Huyajui haya mambo, unadhani kuna mwalimu atakaechukuwa kimbuzi kilichokonda namna hiyo"
"Kwanini tusiweke hakiba ya maneno mpaka baada ya majaribio" alijibu Don Pizallo na kumpa ishara Fahad waondoke. "Fahad ukiwa huku usitumie jina lako halisi, hawa washenzi wakishajuwa jina halafu wakahisi unatishia biashara na wapiganaji wao watatafuta mbinu ya kukudhibiti" aliongea Don Pizallo.
"Sawa"

"Sasa umefikiria jina lolote utakalotumia" aliuliza Don Pizallo.
Fahad akakaa kimya kwa dakika kama moja hivi akijaribu kutafuta jina ambalo halitakuwa gumu lakini litakuwa na maana nzito. Akatabasamu na kumuangalia Don Pizallo.
Jina ni "BLACK STAR".

"Habari, mabibi na mabwana. Tumemaliza mchakato wa kwanza wa kuwaandikisha majina wale vijana ambao wataziwakilisha kampuni zetu katika mashindano ya Indra na Ashra. Muda si mrefu tutawatambulisha walimu ambao wamejitolea kuwepo hapa kwa ajili ya kuchukuwa wanafunzi. Ikumbukwe kila mwalimu ataruhusiwa kuchukuwa wanafunzi watatu tu, hakuna zaidi" aliongea MC wa shughuli hiyo.

"Bila kuchelewa naomba kuwaleta kwenu walimu kumi na moja ambao watachugulia vijana watakaovutiwa nao kwa ajili ya kuwapa mafunzo kabla ya mzunguko wa mtoano".
Akawatambulisha walimu wote, walikuwa ni watu wa mataifa mbali ila nusu yao walikuwa ni wa asili ya kichina. "Natumai mumewaona, nisiibe mwanga zaidi.

Acha niwakaribishe washiriki wote ulingoni kwa ajili ya kupima uzito wa ngumi zao. Ikumbukwe kuwa yeyote chini ya hamsini atakosa haki ya kuchaguliwa wala kushiriki katika mzunguko wa mtoano" aluongea huku akitoka uwanjanj hapo.

"Watu zaidi ya mia ila wanatakiwa kwa wingi wao basi si zaidi ya thalathini na tatu. Kwelu dunia haina usawa" aliongea Han Panzo akimwangalia Don Pizallo kisha akaendelea "ila waki atakuwa mtu wa thalathini na nne, na unajuwa maana ya kuwa yuko. Hatochaguliwa hahaha" alicheka huku akiwa kakunja sura kama mtu alieyalamba kipande cha ndimu chachu.

Don Pizallo hakumjibu kitu, macho yote yalikuwa kwa Fahad ambae alikuwa ametulia. Hakuonesha dalili yeyote ya kuwa na wasiwasi. "Mshiriki wa kwanza ni kutoka kwa kampuni ya Han Panzo, Machikoz Elotente ni mwamba ulioshindikana huko Mexiko. Ana uzito wa kilo mia na tano, mpaka sasa anashikilia ushindi wa mapambano kumi mkononi mwake" aliongea MC.

Machikoz Elotente akapita mbele huku akiwa ametunisha misuli yake mikubwa. "Jamaa ana kifua kikubwa kama kalio" aliongea mmoja kati ya washiriki. Machikoz akafika mpaka karibu na mashine hiyo, akakunja ngumi mpaka mighipa ya damu iliokuwa ikisafiri juu ya ngozi ikaonekana.

Akajitutumua na kufyetua ngumi kali sana ya mkono wa kulia. Baada ya sekunde kadhaa mashine hiyo ikaonesha namba sabini. Wengi wakashangaa, ikiwa mtu mwenye misuli iliyoshiba kiasi kile amepata sabini tu. Je vimbao vitafikisha hata hamsini.

Naam! Baada ya hapo karibu nusu nzima hawakufika hata hamsini. "Ndugu watazamaji mpaka sasa wameshaenda washiriki sitini na saba lakini walofanikiwa kufika zaidi ya hamsini ni saba tu na aliepata namba ya juu zaidi ni Machikoz peke yake" aliongea MC na kuendelea "sasa acha tufanye mambo yazidi kunoga, kwa anaedhani kuwa hakuna atakaezidi namba ya Machikoz aweke pesa mezani.

Mchezo utakuwa hivi, kila atakaeweka kisu mezani, atapata mara mbili ya alichoweka ikiwa matokeo yataendelea kuwa hivi na kiwango kitatolew na nyumba yetu hii".
Wengi wakaweka hivyo hasa wale ambao washiriki wao waliokuwa wameshashindwa. Mpaka anafiki mshiriki wa tisini nane hakuna aliefanikiwa kufika namba ya Machikoz. "Inaonekana nyumba yetu itajinyakulia kitita kizito leo" aliongea MC akimkaribisha mshiriki anaefuata, nae pua hakufika pia.

"Mabibi na mabwana sasa tunamkaribisha mshiriki wetu wa mwisho, anaitwa Black Star kutoka nyumba ya Don Pizallo. Hana ushindi wote mkononi na inasemekana alikuwa panya wa mtani tu. Uzito wake ni kilo tisini na tano tu, hatujui ametuandalia nini ila acha tuone kama atatufurahisha.

Fahad akamuangalia Don Pizallo na kutikisa kichwa, Don akatabasamu na kugonga mezani kwa nguvu kisha akabonyeza sehemu na kuanza kuongea "huyo ni mpiganaji wangu, mimi naweka kadi yangu dhahabu mezani, nina uhakika ataivunja rikodi ya Elotente. Haijalishi, yeyote anaeamini vingine na aweke kitu mezani. Chochote tu kitafaa, sina haja kadi ya dhahabu ya mtu mwengine".

Uwanja mzima ukaingia ubaridi, " Pfff, hahahaha" Han Panzo akaanguwa kicheko. "Unaamini yule kimburu anaweza kupita namba ya mwamba wangu" aliongea. "Han Panzo, hatuongei kwa maneno hapa unaweka nini mezani" aliongea Pizallo na hakuonesha kama alikuwa akitania hata kidogo. "Owwww! Sawa, mi naweka ndege yangu pamoja na boti zangu mbili.

Zote mpya, hazijafikisha hata mwezi" aliongea Han Panzo kwa kujiamini. "Hii ni kati yangu mimi na Pizallo, sitaki mtu mwengine aweke chochote" aliongea. "Mabibi na mabwana inaonekana tuna watu wawili ambao wana ugomvi, sisi kwenye nyumba hii tunasema tuwaachie wao tu au mnasemaje" aliongea MC. "Ndio" sauti zikasikika.

Fahad akasogea mpaka kwenye mashine hiyo na kuigusa kisha akashusha pumzi. Akatanuwa miguu na kuvuta pumzi nyingi sana ndani, kifua chakie kikapanda ikiashiria kuwa mapafu yake yalishajaa upepo wa kutosha. Akazungusha mguu wake kuingia ndani, likafata paja lake la mguu wa kulia. Misuli yake ya paja ikakaza kisawasawa, akakunja ngumi na kuikaza kisha akaivurumisha kwa nguvu zake kadiri misuli yake ilivyomruhusu.

Ni katika wakat huwo, Fahad akahisi damu yake ikisafiri kwa kasi na kuijaza misuli yake ya mkono wa kulia. Misuli hiyo ikakamaa mithili ya chuma, na ilipoachia tu ngumi yake ikatuwa kwenye uso wa mashine hiyo. Sauti kama ya mzinga ikasikika, Fahad akaachia pumzi na kurudi nyuma, mkono wa kulia ulikuwa umekufa ganzi na ulikuwa ukitetemeka. Akahisi maumuzi makali sana begani kama vile bega limefyetuka na kurudi sehemu yake ndani ya sekunde chache.

Kwa sekunde kadhaa mashine haikuonesha kitu, ghafla ikaonesha mia na baada ya sekunde tano ikaonesha alama za kuuliza (??). "Nini kimetokea, nimeona mia ama ni macho yangu tu" alijisemea mtu mmoja. "Sio peke yako, wengi tumeona mia ila imetoweka na zimetokea zile alama za kuuliza. Fahad akiwa katika ya maumivu akiwa kashika mkono wake wa kulia ambao tayari ulishaanza kukolea rangi ya brown. Akashtuka akiguswa, akageuka na kukutana kibabu kikongwe. "Kijana usupofanya kitu utaupoteza huwo mkono" aliongea kwa sauti ya chini.

Akatoa kipochi kidogo mfukoni na kuchomoa sindano kubwa, "ngoja nikusaidie" aliongea na kuushika kisha akautoga maeneo kadhaa, damu nyingi ikaanza kutoka tena ilikuwa nyeusi ti. Fahad akakunja sura, wimbi la maumivu makali sana likasafiri mpaka kwenye ubongo wake, karibu machozi yamtoke. Yule mzee akamchoma pini chini ya kwapa na ndipo akapata nafuu.

"Vipi unataka kuwa mwanafunzi wangu" alimuuliza akirudisha pini yake katika pochi. "Sikulazimishi lakini hutaweza kujifunza aina nyingine yeyote ya kupambana isipokuwa nitakayokufundisha mimi. Mwili wake uliumbwa kwa ajili ya kurithi aina yangu mimi ya kupambana. Fikiria na wala usikurupuke kunijibu. Tuna siku nzima baada ya hapa" akarudisha pochi yake mfukoni na kurudi walipokuwa walimu wengine na kukaa.

Spectacular aliongea mmoja kati ya watu waliokuwa kwenye kikao maakum wakifuatilia majaribio hayo. Harnandez, inaonekana tuna mnyama mpya katika ulimwengu wetu, kama katika jamii ya paka bado yule ni paka wa nyumbani, bado hajafika daraja la kutembea na kina simba na jamii nyingine ya paka wakubwa.

Ila kumbe hata paka wa nyumbani ukimbananisha ukutani atapigana tu hata kama atakuwa anafahamu huenda akapoteza maisha. Ricky, Harnandez tulieni kwanza. Yule kijana bado mbichi sana na itamchukuwa zaidi ya miaka mitano kufika super league. Kwa hiyo tulizeni majini, hakikisheni hamumfati chini. Raha ya tunda liliwe likiwa limeiva aliongea mtu mwengine aliokuwa amekaa na katika sofa kubwa peke, mkononi mwake walikuwa na gilasi kubwa sana ya mvinyo. Akapiga funda moja kunbwa kisha akatabasamu na akasimama na kuondoka.

What a monster aliongea Harnandez, mwili wake ulikuwa ukitetemeka. Hakuwa akifahamu kama kutetemeka kulikuwa ni kwasababu ya kumuogopa au ya kumheshimu. Harnandez, katika maisha yangu siombi hata siku moja Automata inipangie mechi na huyo jamaa. Na ikitokea, nitanyanuwa mikono kabla hata ya mechi haijaanza. Ikiwa itabidi nichague kupambana ulingoni nae au kujiondoa katika ulimwengu huu. Basi ni bora nijiondoe tu. Siwezi uza maisha yangu kwa vijipesa kidogo tu. Maisha matamu bwana aliongea Ricky kijasho chembamba kikimtoka.

*******
Han Panzo nina imani tuna makubaliano aliongea Don Pizallo akiinuka, Ndio! Usijali kuhusu hilo lakini usijipe matumaini sana. Katika mtoano hatotoboa kijana wako, omba Mungu tu angalau abaki na uhai wake laa sii hivyo ndio itakuwa mwisho wa maisha yake aliongea Han Panzo akionekana kuwa na hasira sana. Mbwa mkongwe kazi yake kubweka tu, hana hata meno ya kungatia aliongea na kuondoka.

Moja kwa moja mpaka katika chumba alichokuwa Fahad, Unaendeleaje alimuuliza baada ya kuingia. Nashukuru Mungu, kama sio yule mzee nahisi saa hivi ningekuwa sina mkono alijibu Fahad akitabasamu. Ila ulichokionesha kimepitiliza mpaka mategemeo yangu aliongea akionekana wazi kuwa na mshangao. Hata mimi sifahamu nguvu kiasi kile nimetoa wapi, nilipokuja kuzinduka nilikuwa nahisi kama mkono wangu ulikuwa umefungwa mashine nyuma aliongea Fahad na kucheka kidogo.

Yule mzee amekwambia nini aliliuliza Don Pizallo, amenambia kama nitakuwa tayari anichukue kama mwanafunzi wake. Wewe mwenyewe unaonaje, mimi siwezi kukuchangulia mwalimu kwasababu ulingoni utapanda wewe na sio mimi. Mimi ni mdhamini wako tu, nitabaki kuwa hivyo na wala sitakuingilia katika maamuzi yako hata kidogo labda liwe linanihusu mimi moja kwa moja.

Amenambia yeye ndie mwalimu pekee ambae ataweza kukilea kipaji changu kinawiri katika ubora wake kabisa. Nahisi pia si jambo baya kuwa chini yake, mkataba si wa miezi sita tu. Baada ya hapo naweza kuamuwa kuendelea nae ama laa aliongea Fahad. Kijana umeanza kuwa mfanya biashara sasa.

Inaonekana ushafanya maamuzi. Baada ya kutoka humu chumbani, mimi na wewe tutaonana baada ya miezi sita katika mzunguko wa mtoano. Nikitoka hapa nitakwenda kuonana na yule mzee, wewe ukitoka hapa utaungana nae na kwenda mafunzoni. Mimi nakutakia mafunzo mema alimaliza kuongea, wakapeana mikono kisha Don akatoka chumbani humo.

Mwalimu habari yako na nashukuru kwa kumsaidia kijana wangu aliongea Don Pizallo akikaa pembeni ya mzee huyo. Ohoo! Pizallo, unaonekana umekuwa sasa aliongea mzee huyo na kupeleka mawimbi ya shoti katika ubongo wa Pizallo. Master Ge, ni wewe kweli aliongea Pizallo na kusimama kisha akarudi nyuma na kupiga magoti.

Naomba unisamehe kijana wako, maana nimepewa macho ila nimeshindwa kuona aliongea huku mwili wake mzima ukitetemeka kama mtu aliemwagiwa maji ya baridi. Kaa vizuri kijana wangu, ni miaka mingi sana imepita siwezi kukulaumu kwa kutonikumbuka ila ile dhahabu umeokota wapi? aliongea na kutupa swali.

*******************
“Karibu nyumbani Fahad aliongea Master Ge, ahsante alijibu akiangalia nyumba ndogo iliyojengwa katika mfumo wa asili wa kichina. Hapa tulikuiwa tunaishi wawili ila kuanzia leo tutakuwa watatu aliendelea kuongea Master Ge.

Karibu nyumbani, baba sauti laini ya kike ilisikika ikitokea ndani ya nyumba hiyo, masikio ya Fahad yakasimama kama mbwa aliepata harufu ya kitoeo. Oh Eunice, nilijuwa umeenda kuchota maji aliongea mzee huyo huku akimuangalia Fahad kwa wizi. Hapana, nisharudi. Nimetoka asubuhi sana leoalijibu huku akitoka nje ya nyumba hiyo.

Macho ya Fahad yakatuwa katika uso wa binti mzuri, mapigo yake ya moyo yakaanza kuenda kasi. Damu kasafiri kwa kasi zaidi mwilini mwake. Japo msichana huyo alikuwa akitembea kwa mwendo wa haraka lakini machoni mwa Fahad alikuwa akitembea taratibu sana. Bila kutegemea, mwili wake ukasogea kwa kasi na wakati huwo huwo Eunice akajikwa na kuanguka. Hakufika chini kama ilivyo mawazo ya mengi, aliangukia mikononi mwa Fahad.

Hata master Ge mwenyewe hakutegemea hilo, alibaki ametoa machoa. Ahsante, unaweza kuniachia sasa aliongea Eunice huku mashavu yake yakiwa na wekundu. Fahad akazinduka sasa na kugunduwa kuwa japo alikuwa amemdaka lakini mkono wake mmoja umetuwa sehemu sio na kufanya tukio zima la usaidiaji kuwa kama tukio la kujichulia faida kutoka msichana alietaka kuanguka.

Samahani akamuachia na kusimama kisha akarudi nyuma, Eunice nenda ndani, mimi naenda kumuonesha mgeni chumba chake aliongea Master Ge. Akamgeukia Fahad na kumpa ishara, japo macho yake yakuwa kwa Master lakini akili yake bado ilikuwa inatafsiri tukio lilitokea hapo nyuma. Humu ndimo utakapokuwa unalala, na sheria za nyumba hii ni mbili. Unaamka kabla mimi na unalala baada mimi. Na sheria nyingine makhususi kwa ajili yako, kaa mbali na mwanangu aliongea mzee huyo na kuondoka bila kumuangalia Fahad.

Fahad umefanya nini, siku yako ya kwanza tu umeshaharibu alijisemea na kukaa kitandani, Whatever, mtoto kama kashushwa kutoka mbinguni. Lakini ndio hivyo sio kila kizuri kinafikika, vingine unatakiwa uviangalie kwa mbali aliendelea kuongea mwenyewe huku akili yake bado ikiwa inairudiarudia picha ya Eunice kichwani mwake.

Siku iliofata mapema Fahad aliamka na kutoka nje, kulikuwa na baridi wastani katika hicho hivyo alitoka na nguo nyepesi. Akiwa nje akapasha mwili kidogo na kkukimbia mizunguko kadhaa. Mwili wako umeujenga vizuri Master Ge aliongea, Fahad akaacha kupiga push na kusimama, akamsabahi habari ya asubuhi mwalimu.

Nzuri, umepumzika vizuri
Ndio
Vizuri, leo nitakutembeza maeneo mbalimbali ya sehemu hii. Kesho tutaanza mazoezi rasmi, nikuonye tu ukifanya mzaha utakufa huku kabla hujafika mzunguko wa mtoano. Nitakusukuma kuelekea katika mwili wa mpiganaji hata ikibidi nikuvunje kabla ya kukutengeneza aliongea Master Ge, hakuonesha masihara hata kidogo.

Nimeelewa mwalimu, nitajitahidi niishi katika mfumo unaokupendeza zaidi alijibu Fahad na kutabasamu. Safari yake ndio ilikuwa imeannza rasmi.

"Vua fulana" aliongea Master Ge, Fahad akafanyw kama alivyoambiwa. Master Ge akaanza kumkaguwa, "umeitengeza misuli yako vizuri" aliongea huku akitabasamu. "Lakini kuna misuli hujaifanyia kazi vizuri na hiyo inaeleza kwanini mkono wako uliathirika na msukumo baada ya ngumi kutuwa" aliongea huku akimgusa misuli ya mgongoni.

"Sijakufahamu, miminilikuwa nafuata utaratibu nilioekewa" aliongea Fahad. "Ndio, umefuata utaratibu lakini hawajakupangia ratiba ya kutengeza misuli yako ya mgongo" alifafanuwa. "Hivyo kuanzia leo na kwa mwezi mmoja mzima tutakuwa tunaifanyia kazi misuli yako ya mgongo. Baada ya mwezi mmoja ndio nitakwambia faida ya kufanya hivi".
"Nimeelewa mwalimu" alijibu Fahad.

"Zoezi lako kubwa litakuwa na kupasuwa vigogo vya mti, kwa maneno mingine utakuwa unachanja kuni". Mshangao mkubwa ukamvaa Fahad, lakini hakutaka kuuliza chochote. " Kwa siku unatakiwa kupasua vigogo mia tano na utafanya hivyo kwa siku kisha vitaongezeka idadi kwa yenye kufanana na idadi ya mwanzo" aliendelea kuongea mwalimu wake.

"Sawa, nitajitahidi nifikishe idadi hiyo kwa siku"
"Shoka utakazotumia si shoka zinazotumika na watu wa kawaida. Shoka hizi zina mpini wa chuma na zipo katika uzito wa tofauti. Zipo za kuanzia kilo kumi mpaka hamsini. Chaguwa kilo unayotaka ila kwa kukushauri tu ni bora uanze na kilo kumi".

Baada ya maelezo hayo, Fahad akafuatana na master Ge mpaka sehemu zilipo shoka. Akachuka shoka ya kilo kumi kama alivyoshauriwa. " Kumbuka jitahidi utumie misuli ya mgongo" master Ge aliongea wakati Fahad akitoka. Fahad akatikisa kichwa na kuelekea vilipo vigogo.

Kazi haikuwa rahisi kama alivyofikiria, kutokabasubuhi mpaka inafika saa kumi jioni alikuwa amepasuwa vigogo mia mbili tu. Mwili wake mzima ulikuwa unauma kama kidonda. Misuli ilikuwa imekakamaa na haikumruhusu kufanya kazi yeyote. Kifua kilikuwa kimekaza na kizito hata pumzi alikuwa hapati vizuri. Akaweka shoka pembeni na kukaa chini akijaribu kutafuta upepo.

"Naona umejitahidi sana" sauti ya master Ge ilisikika ikitokea nyuma. "Ah wapi, sijafika hata nusu na siku inaenda kuisha" alijibu akionekana kukwazika na kushindwa kwake. "Somo la kwanza, mpiganaji harushi tu ngumi hovyo. Kila ngumi inayotoka, inatakiwa ifike inayokusudiwa" aliongea.
"Sijakufahamu" alohiji Fahad.

"Katika kigogo kuna sehemu ngumu na laini. Sehemu ngumu ni sehemu ya nje ya kigogo na laini ni sehemu ya kati. Unatakiwa kwa kuangalia mara moja tu ujue wapi shoka yako itatua" alifafanuwa mwalimu huyo.

Akachukuwa shoka na kuweka kigogo kimoja katika sehemu ya kuchanjia. Akanyanyua mkono na kuusha kwa kasi, akakipasua kigogo hicho katikati. Macho yakamtoka Fahad, yeye alihangaika sana mpaka kufanikiwa kupasua baadhi ya vigogo. "Mwanzo ni mgumu lakini jitihada zitazaa matunda.

*****
Tanzania
*Abedi, tunajuwa kama tumekukosea na familia yako. Ila sisi ni ndugu zako na huwezi kutufanyia hivi". "Siwezi kuwafanyia hivi, kwani mimi nimwafanyia nini hasa watu nyie mliokosa shukrani" alijibu huku akiwa amekunja uso. "Tena naomba msije tena ofisini kwangu, mimi na nyinyi udugu wetu ulishakufa kitambo sana. Hatudaiani kitu chochote. Mulichukuwa kila kitu mkaniacha nahaingika na maisha. Leo nimepata kidogo mnaleta pua zenu, niacheni na familia yangu. Ondokeni" alifoka mzee Abedi.

Wakainuka na kutoka nje, "huyu jamaa kisa katoka kimaisha ndio anajiona namna gani vipi". "Sisi ndio wazee wa figisu, kama tuliweza kucchukuwa mali yote iliyo katika jina lake mara ya kwanza na wakati huu pia tutabeba". " Ommy, we tulia tu. Na mara hii tunamuua kabisa, hawezi kutuzidi sisi huyu bwege. Sisi ni kaka zake asijione kwasababu tu ana pesa ndio ajikute mkubwa" aliongea Bahati.

Baada ya ndugu zake kuondoka, mzee Abedi akashusha pumzi ndefu sana. Aliwatambuwa vizuri watu hao ni watu wa aina gani. "Mara hii tutakula sahani moja, damu weka pembeni" alijisemea na kutoa simu kisha akaingiza tarakimu kadhaa na kupiga.

"Umepotea njia leo" aliongea aliepokea upande wa pili.
"Hujabadilika" alipmgea mzee Abedi kwa sauti kavu.
"Mpaka leo umenitafuta ni wazi kwamba kuna kazi unataka kunipa" aliongea mtu wa upande wa pili.
"Kesho una nafasi, nataka tufanye biashara"
"Kwa wewe, hata kama ingekuwa haipo ningelazimisha iwepo"
"Sawa, nitakutumia eneo ambalo tutaonana" alimaliza kuongea na kukata simu. "Nilikuwa sitaki kurudi kule lakini mumenisukuma. Sawa nitacheza lakini kwa sheria zangi safari hii".

*********
Ilikuwa jumamosi, Fahad aliamka asubuhi mapema na kutoka nje. Tofauti na siku nyingine, siku hiyo hakukuta mzigo wa kuni. Akakimbia mizunguko kadhaa na kunyoosha viungo kisha akakaa kitako na kufumba macho. "Leo ni siku ya mapumziko, Eunice atakupeleka kwenye chem chem ya maji ya vugu. Yatakusaidia kutoa uchovu wa siku zote za nyuma. Lakini mukiwa munaelekea huko, kuna mzigo nitakupa uupitishe kwa Master Pong. Yeye atakupa tokeni ya kuingilia katika chem chem" akiwa katika hali hiyo ya kufumba macho, alimsikia mwalimu wake akiongea.

"Sawa mwalimu" alijibu na kufumbuwa macho, "nenda kajiandae Eunice atatoka sasa hivi". Fahad akainuka na kuingia ndani, akabadilisha nguo na kutoka. Akamkuta Eunice akiwa anamsubiri, "mzigo ule pale" aliongea akinyoosha kidole kwenye kikapu.

Fahad akakibeba mgongoni, kilikuwa kizito kupita maelezo lakini hakutaka kuangalia ndani kuna nini. Eunice akatangulia na kuongoza njia. Walitembea kwa muda mrefu pasi na kuongea jambo lolote. Pamoja na uzito wa kikapu hicho, Fahad hakuonekana kupata shida kabisa kwenye kukibeba.

"Eunice! Wewe sio mchina" swali hilo lilitoka mdomoni mwa Fahad pasi na kukubaliana na akili yake. "Kwanini?" alijibu Eunice bila kugeuka.
"Sijui niliwekeje hili lakini hufanani na wachina kabisa" alishindwa kutoa sababu iliyonyooka.
"Kwani wachina wanafananaje" hapo Fahad akajikuta akiwekwa kwenye kipembe asione pa kutokea. "Kama mbwai na iwe mbwai tu, mimi tokea lini nikawa na aibu" alijisemea na kuongeza mwendo mpaka alipofika pembeni ya Eunice.

"Hivi umewahi kusimama mbele ya kioo na kujiangalia?" alitupa swali. Eunice akasimama na kumuangalia Fahad akiwa na mshangao. "Kabisa unauliza swali hilo" akakwepa kujibu swali hilo. "Usikwepe swali, nijibu" Fahad akakaza sura na kumuangalia usoni bidada huyo. Eunice akajikuta akishindwa kukutanisha macho na mwamba huwo wa kiafrika.

"Afadhali tumemaliza pori sasa" alionhea Eunice na kukazana, Fahad hakuona haja ya kuendelea kulazimisha jibu. Wakaendelea na safari h uku kk imya kikitawala kati yao, taratibu wakaanza kuonana na watu wengine njiani. Na baada ya mwendo wa dakika kama tano hivi, wakakutana na mji mkubwa tu. Shughuli za hapa na pale zilikuwa zikiendelea.

"Sikujuwa kama kuna mji mkubwa kama hivi" Fahad akavunja ukimya. "Hiki ni kiji cha Naxi, ni kijiji cha kale sana. Si kukubwa sana lakini wakazi wa huku wameamuwa kuishi kivyao bila kujichanganya na ulimwengu. Huku hutaona gari, pikipiki wala baiskeli. Huku watu wanatumia usafiri wa miguu na wanyama tu" alifafanuwa Eunice.

"Duh! Kweli wameamuwa. Duniani huko watu wanapambana usiku na mchana kukimbizana na tekinolojia lakini wao hata habari hawana" aliongea Fahad.
"Ah! Kwa master Pong ni pale. Twende tukamkabidhi mzigo wake kisha nitakupeleka huko kwenye chemchem ya maji ya vuguvugu" aliongea Eunice.

Wakatembea kwa mwendo wa kukazana mpaka katika nyumba hiyo. Eunice akagonga, kibabu kikongwe sana kikafunguwa mlango. "Oh! Eunice, Master Ge amenambia utaniletea mzigo wangu lakini sikutegemea kama ingekuwa mapema kiasi hiki" aliongea kwa sauti ya kukwaruza.

"Yote ni kwasababu huyu mwanafunzi wa baba hajapumzika safaro nzima" aliongea Eunice na kusogea pembeni. "Heshima kwako Master Pong" aliongea Fahad na kukutanisha viganja vyake kisha akainama kidogo. "Kijana una heshima sana, siku hizi hata wanafunzi wetu hawatusalimii hivyo" aliongea kikongwe huyo. Fahad akaachia tabasamu jepesi.

"Huwo mzigo uweke hapo", Fahad akautuwa mzigo huwo kwa makini. Hakujuwa ndani kuna nini na alihofia kukiharibu. Baada ya hapo wakaagana na kuondoka. Master Pong akaunyanyua mzigo huwo kwa mkono na kuingia nao ndani.

"Unamuonaje" sauti nzito ikasikika alipofunga tu mlango.
"Umejiokotea dhahabu kwenye rundo la mawe"
"Hahaha"

"Lakini ule mgongo si wa wiki moja, nianbie tu ukweli mzee mwenzangu. Huyu mwanafunzi umeanza kumfundisha kabla ya kuja nae huku. Maana kwa wiki moja tu, mtu kufikia mgongo wenye nguvu kiasi kile si jambo la kawaida".

"Sina cha kukuficha, hayo ni matunda ya wiki moja tu. Muwahi mapema kabla hajapotea. Si unakumbuka kilichotokea mara ya mwisho"
"Njia mtu anachaguwa mwenyewe, hata umuelekeze vipi kama akili yake haitaweza kuhimili mhemko wa mtiririko wa DOQI, kitamkuta kama kilivyomkuta mwanafunzi wangu aliepita"
"Sawa, ila kumbuka ukifa wewe kila kitu tulichopigania kitakuwa kimefika mwisho. Jitahidi sana upate mrithi kabla muda haujakutupa mkono".

***************
Baada ya mwendo wa dakika kama ishirini hivi, wakawasili katika chemchem. "Wanaume ni upande huwo huko" aliongea Eunice. Wakaagana na Fahad akaelekea upande ambao ameelekezwa. Alipofika eneo la kubadili nguo, akabadili na kujifunga taulo kisha akaelekea katika chemchem. Maji yalikuwa yakitoka mosho lakini hayakuwa ya moto sana. Akaingia kwenye maji na kujiroweka, alihisi uchovu wote ukiacha mwili wake.

Akiwa ndani ya maji hayo, akili yake ikaanza kuwa nyeupe. Akajikuta anakosa uwezo kufikiri vizuri, ni kama mtu ambae hakuwa amelala kwa muda mrefu na sasa usingizi mzito ulikuwa unamchukuwa.
Alikuja kufumbuwa macho akiwa katika eneo ambalo limesambaa mpaka mwisho wa upeo wa macho yake. Mita chache kutoka alipokaa kulikuwa na mtu mzee sana.

"Habari yako mkubwa wangu, samahani naomba kuuliza hapa ni wapi. Nahisi nimepotea" aliongea Fahad kwa sauti ya chini. Yule mzee akainuwa macho juu kisha akatabasamu. Akamuonesha ishara akae.
Fahad akakaa, "karibu chai" aliongea akimsogezea kikombe.

"Ahsante" akakipokea na kushukuru, "hujapotea hapa umekuja bila wewe kukusudia" aliongea. Fahad akashusha kikombe taratibu na kukiweka kwenye kisahani. "Samahani umesema" aliuliza.
"Nakwambia hapa hujapotea, umekuja mwenyewe ila bila kukusudia" aliongea. Fahad akabaki kimya asijue nini la kuongea, "hapa ni wapi" alijikuta akiuliza.

"Hapa ni katika kitako cha mlima Sumeru, yote yalipoanzia. Asili ya ugomvi kati jamii ya Asura na Indra" aliposema maneno hayo tu Fahad akaanza kusikia mlio wa ngoma kubwa. Ililia kwa nguvu mithili ya ngurumo, "muda wako wa kuwa hapa umeisha, nina imani tutaonana tena".

Fahad akazinduka kutoka usingizini, akaangalia kushoto na kulia ili kujithibitishia kama hakuwa sehemu ambayo aliiota. Ajabu hakuna mtu aliekuwa na habari nae. Akachukuwa taulo yake na kujifunga kisha akatoka na kuelekea bafuni. Akajimwagia maji na kutoka nje kabisa. Baada ya nusu saa Eunice akatoka. "Umekaa muda mrefu sana" aliuliza.

"Hapana, nimetoka muda si mrefu" alijibu na kutabasamu. "Oh! Sawa tuondoke" aliongea bi dada huyo na kuongoza njia. Fahad alikuwa nyuma akitembea taratibu, macho yake yaliganda chini ya kiuno kilichobeba mzigo wa nyama wa wastani wa bidada huyo. "Ukiendelea kunianfalia hivyo nitakunyofoa macho" aliongea Eunice akionekana kukereka. "Kama itakuwa kitu cha mwisho kuona ni wewe, yanyofoe tu" alijibu pasi na kutegemea.

Eunuce akageuka mbele na kutabsamu, Fahad akakaza mwendo mpaka pembeni ya bi dada huyo. "Unajuwa hujanijibu swali langu nlokuuliza kabla kufikisha mzigo" aliongea.

"Nitajibu maswali matatu yeyote utakapofanikiwa kuingia mzunguko wa pili wa mashindano ya Indra na Asura" aliongea. "Umeweka ahadi mwenyewe, jiandae kujibu maswali yangu tu. Hakuna namna ambayo nitashindwa kupita mzunguko wa kwanza" aliongea Fahad na kutabasamu. "Ni ahadi" alimalizia Eunice.

Safari ikaendelea na ukimya ukatawala, baada ya safari ndefu hatimae wakawasili nyumbani. Wakaagana na kila mmoja akaelekea eneo analokaa. Akiwa chumbani akakaa chini na kukunja miguu na kufunga macho. Amezoea kufanya hivyo kama sehemu yake ya kusafisha mawazo kichwani. Akiwa katika hali hiyo akaanza kuzisikia zile ngoma, safari hii ziliongezeka sauti kadei muda ulivyokwenda. Akasimama na kutoka nje, akawa kama mtu anaetafuta kitu.

"Fahad unatafuta nini" aliuliza mwalimu wake lakini Fahad hakujibu kitu. Aliendelea kuangalia na kule, ghafla akageuka na kumsogeza mwalimu pembeni kwa nguvu. Akarudisha mguu mmoja nyuma na kubonyea. Akakaza misuli yake yote ya mwili na kuvuta pumzi ndefu. Mishipa yake inayosafirisha damu miguu ikavimba na kusafirisha damu nyingi zaidi.

Ng'ombe mkubwa mithili ya nyati aliekuwa amemponyoka mchungaji alitokea kwenye pori kwa kasi kubwa. Ngoma ikakata ghafla na ng'ombe huyo tayari alikuwa mbele ya Fahad. Akaachia pumzi, misuli yake mikubwa ilionekana kama kupumuwa na kusafirisha damu kwa kasi zaidi. Akamshika mapembe na kuzidi kukaza miguu na misuli yake ya mgongo. Akaburuzika kama mita moja kutoka alipokuwa amesimama na kumzuia ng'ombe huyo kabisa. Akamuachia na misuli yake ikalegea, akaanguka na kupoteza fahamu.

"Sikutegemea kama tutaonana tena mapema kiasi hiki" alisikia sauti alioitambuwa. Akafumbuwaa macho na kujikuta akiwa amekaa chini na kikombe cha chai. "Nimefikaje hapa" aliuliza, "kama mwanzo tu".
"Samahani mkubwa wangu, huyu kijana bado hajalitambuwa jina lako" aliongea Fahad."Oh ziko wapi heshima zangu" aliongea mzee huyo na kuchezea ndevu zake nyingi, ndefu na nyeupe. "Karakantha" alijitambulisha.

"Kijana kama hutojali tembea na mimi, utajifunza kitu" aliongea na kusimama. Fahad nae akasimama, hakutaka kuuliza mambo mengi. Kwa wakati huwo alikuwa na lengo moja tu, kuelekea kwanini amefika hapa. "Mara ya kwanza ulipokuja huku, ulisikia ngoma si ndio" aliuliza mzee Karakantha.
"Ndio"

"Hiyo ngoma inaitwa Alambara, na ikilia huwa inatoa sauti kali inayofanana ngurumo za radi. Ngoma hiyo inatambulika kama ngoma ya vita, inaposikika ni kwamba tunajiandaa na vita" aliongea naa kuafafanuwa.
"Sasa kwanini mimi nimeisikia"

"Mpaka sasa unadhani wewe ni mtu wa kawaida. Sivyo! Baada ya leo maisha yako yatabadilika kabisa. Kuna jambo kubwa sana linakusubiri mbeleni huko. Umeingia katika ulimwengu ambao binadamu wa kawaida hawezi kuamini kama upo".
" Ndiyo ulimwengu gani huwo"
"Ulimwengu wa MARTIAL ARTS, na siyo ile uloizoea. Kuna mambo mengi utajifunza baada ya leo. Na pia utaweza kufahamu kwa undani zaidi mimi ni nani"

Fahad akataka kuuliza swali jingine lakini akakatizwa na mlio mkali sana wa ngoma. Alambara ilianza kulia. "Tutaonana tena mara nyingine, muda wako wa kuwa hapa umeisha" aliongea mzee huyo. Fahad akapepesa macho na kutahamaki alikuwa kabakia peke yake.

Akafumbuwa macho na kuangaza huku na kule, pembeni yake upande wa kulia alikuwa Eunice. Alikuwa amepitiwa na usingizi, akatabasamu na kushusha pumzi kidogo. Eunice akafumbuwa macho na kumkuta kijana huyo akitabasamu. "Ushaamka" akauliza.

"Hapana, unaota" alijibu Fahad kwa utani, wakiwa katika hali hiyo ya utani mlango ukafunguliwa. Master Ge akaingia akifuatana na Master Pong.
"Unajisikiaje" aliuliza Master Ge.
"Sijawahi kujsikia vizuri kama ninavyojisikia sasa hivi" alijibu Fahad.
Master Pong akapita mbele na kuanza kumkaguwa, ukaguzi huwo ulikamilika baada dakika tano. Akageuka na kumuangalia Master Ge kisha akatikisa kichwa.

"Fahad tufuate" aliongea Master Ge. Fahad akajinyanyua na kujishoosha, viungo vyake vilitoa mlio kudata ikiashariaa kama alikuwa amelala kwa muda mrefu. "Kwani nimelala kwa muda gani" ilibidi aulize.
"Siku kumi" alijibu Eunice, "eti nini" aliuliza kwa mshangao. "Unashangaa nini, umelala kwa siku kumi" alikazia Eunice. Alikuwa na maswali mengi lakini alihisi huwo si muda wake. Akateremka kitandani na kutoka nje, akafinya macho kutokana na kuwepo kwa miale mikali ya juwa.

"Tunaenda wapi?" aliuliza Fahad, "tunaenda kwenye hekalu la Martial Dao" alijibu Eunice. Wakakfika sehemu kuna mlango mkubwa, "Eunice, tufungulie mlango" aliongea Master Ge.

Eunice akapita mbele na kufunguwa kitambaa kilichokuwa kimeshika nywele zake. "Dance of the sky: basic stance" akanena maneno hayo na kuanza kucheza. Nywele zake ndefu zikaanza kuinuka na kuelea, katikati baina nyusi zake kukatokea vidoti vitatu. Majani yaliokuwa karibu yake na yakaanza kuelekea huku yalifuata mtiririko wa jinsi anavyocheza.

Akafika mpaka karibu na jiwe kubwa, akakusanya nguvu katika mkono wake wa kulia na kwa kutumia kiganja akalipiga jiwe hilo. Mlio mkali sana ukasikika, masikioni mwa Fahad haukuwa mgeni mlio huwo.
Ghafla tetemeko likaanza kusikika, mlango mkubwa wa jiwe ukafunguka chini. Kulikuwa na ngazi nyingi zilizopotelea gizani kuelekea chini. Master Ge akamgeukia Fahad na kumpa ishara. Akazinduka kutoka kwenye mshangao wake na kuamfata.

Wakashuka mpaka chini kabisa ya ngazi hizo, mlango mwengine ukafunguka. Mbele yao kulikuwa na ukumbi mkubwa sana. Kulikuwa na watu wengine, hakuna alieshughulika nao kila mmoja aliendelea na mambo yake.

"Achana nao" aliongea Eunice, alionekana kuchoka sana. Jasho jingi lilikuwa likimtoka, "Master Ge kwanini tusipumzike kidogo ili tumpe Eunice angalau dakika kidogo apumzike" aliongea Fahad kwa sauti kidogo. Eneo zima likazizima, kila mtu akaacha kazi na kuwaangalia wanne hao.

"Nimesikia jina la Eunice"
"Hata mimi pia"
"Mna uhakika kama mumesikia sahihi au masikio yenu yanawadanganya" aliuliza mtu mzima aliekuwa pembeni yao.

Hali ya hewa ndani ya ukumni huwo ikaanza kuwa nzito, "Master Ge, endelea na safari hawa niachie mimi" aliongea akikunja mikono ya nguo yake. "Hapana, kwa afya yako hutaweza kufanya kitu" alijibu Master Ge.
Wakati wao wakiongea Fahad alikuwa katulia tuli, alikuwa aksikia sauti kali sana ya ngoma ya Alambara. Damu ikaanza kumuenda mbio, hisia zake zikakuwa mpaka katika ubora wake kabisa. Alisikia kila kitu ndani ya ukumbi huwo. Hata sisimizi waliokuwa wakitembea aliwasikia pia.

Akarudisha mguu wake mmoja nyuma na kukutanisha viganya vyake kama vile mtu aneyeomba msamaha. Lakini kwake haikuwa hivyo, mwili wake ukaanza kutoa harufu ya damu ikiyokuwa inaunguwa. "Yeyote anaetaka kuyatupa maisha yake amsogelee Huyu mwanamke" aliongea kwa kunguruma.
"Haha anadhani anatutisha" alisikika mtu mmoja akiongea na kupiga hatuwa moja mbele. Lahaula! Hakujuwa ninikimemkuta lakini mwili wake ulishindwa kutoa ushiriakiano kabisa. Pumzi ikamuwia ngumu kuivuta, jasho jingi likaanza kumtoka.

"Black Star, utamuuwa" Eunice aliongea kwa tabu na kumgusa Fahad mgongoni. Akazinduka na kuangalia sehemu aliokuwa amesimama. Ilikuwa imechimbika na baraza ilikuwa imepasuka. "Nini kimetokea" akamuuliza, kabla Eunice hajajibu kitu akaishiwa nguvu na kutaka kuanguka. Fahad akamuwahi na kumbeba, Master Ge akamfanyia ishara wawahi.

Wakaelekea kwenye mlango mwengine, "tusubiri mpaka Eunice aamke. Yeye peke yake ndie mwenye uwezo wa kuufunguwa mlango huu" aliongea Master Ge. Fahad akamshusha na kumlaza sehemu kisha akakaa pembeni yake.

Baada ya masaa mawili Eunice akaamka, akasimama na kusogea mpaka kwenye kitasa cha mlango akakishika na kukifunguwa. Moshi mwingi sana ukatoka punde tu mlango huwo ulipoanza kufunguka. Akawapa ishara wamfuate, wote wakaingia na mlango huwo ukajifunga.
_cbea0a0f-39f8-4d58-bb62-0bfb9f9573eb.jpeg

"Nahisi sasa ni muda muafaka wa kumueleza Fahad lengo la kumleta huku. Ila kabla hatujafanya hivyo, inabidi atueleze kilichotokea muda mchache uliopita" aliongea Eunice. Alikuwa kabadilika kabisa, alionekana kama kiongozi kwa wakati huwo.

SEHEMU YA PILI
SEHEMU INAYOFUATA
SEHEMU INAYOENDELEA
SEHEMU INAYOFUATA
SEHEMU INAYOENDELEA
SEHEMU INAYOENDELEA
SEHEMU INAYOFUATA
SEHEMU INAYOENDELEA
SEHEMU INAYOFUATA
SEHEMU INAYOFUATA
SEHEMU INAYOENDELEA
SEHEMU INAYOFUATA
SEHEMU INAYOENDELEA
SEHEMU INAYOFUATA
SEHEMU INAYOENDELEA
SEHEMU INAYOFUATA
SEHEMU INAYOFUATA
SEHEMU INAYOENDELEA
SEHEMU INAYOENDELEA
SEHEMU INAYOFUATA
SEHEMU INAYOENDELEA
SEHEMU INAYOENDELEA
SEHEMU INAYOENDELEA
SEHEMU INAYOFUATA
SEHEMU INAYOFUATA
SEHEMU INAYOFUATA
SEHEMU INAYOENDELEA
SEHEMU INAYOENDELEA
SEHEMU INAYOFUATA
SEHEMU INAYOENDELEA
 
BLACK STAR

SEHEMU YA PILI

_19a2d3d6-8b5e-475b-a7f8-38ece6023221.jpeg

Eunuce akageuka mbele na kutabsamu, Fahad akakaza mwendo mpaka pembeni ya bi dada huyo. "Unajuwa hujanijibu swali langu nlokuuliza kabla kufikisha mzigo" aliongea.

"Nitajibu maswali matatu yeyote utakapofanikiwa kuingia mzunguko wa pili wa mashindano ya Indra na Asura" aliongea. "Umeweka ahadi mwenyewe, jiandae kujibu maswali yangu tu. Hakuna namna ambayo nitashindwa kupita mzunguko wa kwanza" aliongea Fahad na kutabasamu. "Ni ahadi" alimalizia Eunice.
Safari ikaendelea na ukimya ukatawala, baada ya safari ndefu hatimae wakawasili nyumbani.

Wakaagana na kila mmoja akaelekea eneo analokaa. Akiwa chumbani akakaa chini na kukunja miguu na kufunga macho. Amezoea kufanya hivyo kama sehemu yake ya kusafisha mawazo kichwani. Akiwa katika hali hiyo akaanza kuzisikia zile ngoma, safari hii ziliongezeka sauti kadei muda ulivyokwenda. Akasimama na kutoka nje, akawa kama mtu anaetafuta kitu.

"Fahad unatafuta nini" aliuliza mwalimu wake lakini Fahad hakujibu kitu. Aliendelea kuangalia na kule, ghafla akageuka na kumsogeza mwalimu pembeni kwa nguvu. Akarudisha mguu mmoja nyuma na kubonyea. Akakaza misuli yake yote ya mwili na kuvuta pumzi ndefu. Mishipa yake inayosafirisha damu miguu ikavimba na kusafirisha damu nyingi zaidi.

Ng'ombe mkubwa mithili ya nyati aliekuwa amemponyoka mchungaji alitokea kwenye pori kwa kasi kubwa. Ngoma ikakata ghafla na ng'ombe huyo tayari alikuwa mbele ya Fahad. Akaachia pumzi, misuli yake mikubwa ilionekana kama kupumuwa na kusafirisha damu kwa kasi zaidi.

Akamshika mapembe na kuzidi kukaza miguu na misuli yake ya mgongo. Akaburuzika kama mita moja kutoka alipokuwa amesimama na kumzuia ng'ombe huyo kabisa. Akamuachia na misuli yake ikalegea, akaanguka na kupoteza fahamu.

"Sikutegemea kama tutaonana tena mapema kiasi hiki" alisikia sauti alioitambuwa. Akafumbuwaa macho na kujikuta akiwa amekaa chini na kikombe cha chai. "Nimefikaje hapa" aliuliza, "kama mwanzo tu".
"Samahani mkubwa wangu, huyu kijana bado hajalitambuwa jina lako" aliongea Fahad."Oh ziko wapi heshima zangu" aliongea mzee huyo na kuchezea ndevu zake nyingi, ndefu na nyeupe. "Karakantha" alijitambulisha.

"Kijana kama hutojali tembea na mimi, utajifunza kitu" aliongea na kusimama. Fahad nae akasimama, hakutaka kuuliza mambo mengi. Kwa wakati huwo alikuwa na lengo moja tu, kuelekea kwanini amefika hapa. "Mara ya kwanza ulipokuja huku, ulisikia ngoma si ndio" aliuliza mzee Karakantha.
"Ndio"

"Hiyo ngoma inaitwa Alambara, na ikilia huwa inatoa sauti kali inayofanana ngurumo za radi. Ngoma hiyo inatambulika kama ngoma ya vita, inaposikika ni kwamba tunajiandaa na vita" aliongea naa kuafafanuwa.

"Sasa kwanini mimi nimeisikia"
"Mpaka sasa unadhani wewe ni mtu wa kawaida. Sivyo! Baada ya leo maisha yako yatabadilika kabisa. Kuna jambo kubwa sana linakusubiri mbeleni huko. Umeingia katika ulimwengu ambao binadamu wa kawaida hawezi kuamini kama upo".

" Ndiyo ulimwengu gani huwo"
"Ulimwengu wa MARTIAL ARTS, na siyo ile uloizoea. Kuna mambo mengi utajifunza baada ya leo. Na pia utaweza kufahamu kwa undani zaidi mimi ni nani"

Fahad akataka kuuliza swali jingine lakini akakatizwa na mlio mkali sana wa ngoma. Alambara ilianza kulia. "Tutaonana tena mara nyingine, muda wako wa kuwa hapa umeisha" aliongea mzee huyo. Fahad akapepesa macho na kutahamaki alikuwa kabakia peke yake.

Akafumbuwa macho na kuangaza huku na kule, pembeni yake upande wa kulia alikuwa Eunice. Alikuwa amepitiwa na usingizi, akatabasamu na kushusha pumzi kidogo. Eunice akafumbuwa macho na kumkuta kijana huyo akitabasamu. "Ushaamka" akauliza.

"Hapana, unaota" alijibu Fahad kwa utani, wakiwa katika hali hiyo ya utani mlango ukafunguliwa. Master Ge akaingia akifuatana na Master Pong.
"Unajisikiaje" aliuliza Master Ge.
"Sijawahi kujsikia vizuri kama ninavyojisikia sasa hivi" alijibu Fahad.

Master Pong akapita mbele na kuanza kumkaguwa, ukaguzi huwo ulikamilika baada dakika tano. Akageuka na kumuangalia Master Ge kisha akatikisa kichwa.

"Fahad tufuate" aliongea Master Ge. Fahad akajinyanyua na kujishoosha, viungo vyake vilitoa mlio kudata ikiashariaa kama alikuwa amelala kwa muda mrefu. "Kwani nimelala kwa muda gani" ilibidi aulize.

"Siku kumi" alijibu Eunice, "eti nini" aliuliza kwa mshangao. "Unashangaa nini, umelala kwa siku kumi" alikazia Eunice. Alikuwa na maswali mengi lakini alihisi huwo si muda wake. Akateremka kitandani na kutoka nje, akafinya macho kutokana na kuwepo kwa miale mikali ya juwa.

"Tunaenda wapi?" aliuliza Fahad, "tunaenda kwenye hekalu la Martial Dao" alijibu Eunice. Wakakfika sehemu kuna mlango mkubwa, "Eunice, tufungulie mlango" aliongea Master Ge.

Eunice akapita mbele na kufunguwa kitambaa kilichokuwa kimeshika nywele zake. "Dance of the sky: basic stance" akanena maneno hayo na kuanza kucheza. Nywele zake ndefu zikaanza kuinuka na kuelea, katikati baina nyusi zake kukatokea vidoti vitatu.

Majani yaliokuwa karibu yake na yakaanza kuelekea huku yalifuata mtiririko wa jinsi anavyocheza. Akafika mpaka karibu na jiwe kubwa, akakusanya nguvu katika mkono wake wa kulia na kwa kutumia kiganja akalipiga jiwe hilo. Mlio mkali sana ukasikika, masikioni mwa Fahad haukuwa mgeni mlio huwo.

Ghafla tetemeko likaanza kusikika, mlango mkubwa wa jiwe ukafunguka chini. Kulikuwa na ngazi nyingi zilizopotelea gizani kuelekea chini. Master Ge akamgeukia Fahad na kumpa ishara. Akazinduka kutoka kwenye mshangao wake na kuamfata.

Wakashuka mpaka chini kabisa ya ngazi hizo, mlango mwengine ukafunguka. Mbele yao kulikuwa na ukumbi mkubwa sana. Kulikuwa na watu wengine, hakuna alieshughulika nao kila mmoja aliendelea na mambo yake.

"Achana nao" aliongea Eunice, alionekana kuchoka sana. Jasho jingi lilikuwa likimtoka, "Master Ge kwanini tusipumzike kidogo ili tumpe Eunice angalau dakika kidogo apumzike" aliongea Fahad kwa sauti kidogo. Eneo zima likazizima, kila mtu akaacha kazi na kuwaangalia wanne hao.

"Nimesikia jina la Eunice"
"Hata mimi pia"
"Mna uhakika kama mumesikia sahihi au masikio yenu yanawadanganya" aliuliza mtu mzima aliekuwa pembeni yao.

Hali ya hewa ndani ya ukumni huwo ikaanza kuwa nzito, "Master Ge, endelea na safari hawa niachie mimi" aliongea akikunja mikono ya nguo yake. "Hapana, kwa afya yako hutaweza kufanya kitu" alijibu Master Ge.
Wakati wao wakiongea Fahad alikuwa katulia tuli, alikuwa aksikia sauti kali sana ya ngoma ya Alambara. Damu ikaanza kumuenda mbio, hisia zake zikakuwa mpaka katika ubora wake kabisa. Alisikia kila kitu ndani ya ukumbi huwo. Hata sisimizi waliokuwa wakitembea aliwasikia pia.

Akarudisha mguu wake mmoja nyuma na kukutanisha viganya vyake kama vile mtu aneyeomba msamaha. Lakini kwake haikuwa hivyo, mwili wake ukaanza kutoa harufu ya damu ikiyokuwa inaunguwa. "Yeyote anaetaka kuyatupa maisha yake amsogelee Huyu mwanamke" aliongea kwa kunguruma.
"Haha anadhani anatutisha" alisikika mtu mmoja akiongea na kupiga hatuwa moja mbele. Lahaula! Hakujuwa ninikimemkuta lakini mwili wake ulishindwa kutoa ushiriakiano kabisa. Pumzi ikamuwia ngumu kuivuta, jasho jingi likaanza kumtoka.

"Black Star, utamuuwa" Eunice aliongea kwa tabu na kumgusa Fahad mgongoni. Akazinduka na kuangalia sehemu aliokuwa amesimama. Ilikuwa imechimbika na baraza ilikuwa imepasuka. "Nini kimetokea" akamuuliza, kabla Eunice hajajibu kitu akaishiwa nguvu na kutaka kuanguka. Fahad akamuwahi na kumbeba, Master Ge akamfanyia ishara wawahi.

Wakaelekea kwenye mlango mwengine, "tusubiri mpaka Eunice aamke. Yeye peke yake ndie mwenye uwezo wa kuufunguwa mlango huu" aliongea Master Ge. Fahad akamshusha na kumlaza sehemu kisha akakaa pembeni yake.

Baada ya masaa mawili Eunice akaamka, akasimama na kusogea mpaka kwenye kitasa cha mlango akakishika na kukifunguwa. Moshi mwingi sana ukatoka punde tu mlango huwo ulipoanza kufunguka. Akawapa ishara wamfuate, wote wakaingia na mlango huwo ukajifunga.

"Nahisi sasa ni muda muafaka wa kumueleza Fahad lengo la kumleta huku. Ila kabla hatujafanya hivyo, inabidi atueleze kilichotokea muda mchache uliopita" aliongea Eunice. Alikuwa kabadilika kabisa, alionekana kama kiongozi kwa wakati huwo.

Wote wakamgeukia Fahad na kumuangalia, "baada ya kulitaja jina lako" alianza kueleza. "Nikaanza kuhisi macho ya watu yakikuangalia katika hali isiyo ya kawaida. Bila mategemeo yangu hasira ikaanza kunipanda. Sijui nielezeje lakini ni kama vile mtu kutaka kuchukuwa kitu changu mbele ya macho yangu. Kitu cha mwisho ninachokumbuka ni kuhisi damu yangu ikimchemka na mapigo ya moyo kuongeza kasi".
Eunice akatabasamu kidogo kisha akamuuliza "hakuna jingine unalotaka kutuambia". "Hapana ni hilo tu" alijibu.

"Kwasasa nahisi imetosha, sasa nitakueleza lengo la wewe kuletwa huku huku" aliongea na kukaa kitako.
"Jambo moja utambue kwanza kwamba hatutarudi tulipotoka mpaka utakapo maliza mafunzo yako. Huku tulipo binadamu wa kawaida hawezi kufika, uliowaona kule katika ukumbi ni watu wanaoishi katika ulimwengu huu. Kazi yao kubwa ni kujifunza MARTIAL ART tu. Ulimwengu ni mwingine kabisa, unafanya kazi tofauti na tulipotoka. Unatakiwa ujifunze kwa muda miezi sita, hiyo ingekuwa ni kule tulipotoka. Lakini miezi ya kule ni sawa na miaka sita huku".

"Hivyo utakaa huku kwa miaka sita kabla ya kurudi katika ulimwengu wako wa kawaida. Kabla hatujatoka katika eneo hili kuelekea katika ulimwengu wa Dao, itabidi uchaguwe aina ya martial art utakayojifunza".
"Kwanini usinichagulie yeyote tu"

"Hapana, inasemekana kuwa mtu hachagui aina ya Martial art anayotaka kujifunza bali inamchaguwa yenyewe. Katika eneo hili kuna vitabau vitatu, kimoja kati ya hivyo ndiyo kitakuwa kitabu chako" alifafanuwa Eunice.

"Sasa kitabu kinanichaguaje?" aliuliza Fahad kama mtu alieona utani vile.
"Usijali na pia hakuna anaejuwa jibu hilo. Sisi tumekuta hivyo pia"

Akamaliza kumuelezea kisha akafungua kabati kubwa lililokuwa pembeni yake. Akampa ishara Fahad asimame mbele ya kabati hilo nae akafanya hivyo. Ghafla moyo wake ukaanza kumuenda kasi, hatuwa kwa hatuwa mpaka karibu kabisa na kabati hilo. Akaingiza mkono na kutoa kitabu kilichokuwa kimejaa vumbi. Baada ya kukitoa tu kabati likajifunga.

"Kitabu gani" akauliza Master Ge.
"Hutaamini, kitabu hiki tokea alivyokufa mtumiaji wake wa kwanza. Hakikumchagua mtu mwengine mpaka leo hii" alijibu Master Pong huku macho yakiwa yamemtoka.
"THE IRON FORTRESS" alitamka jina hilo, "hatimae mrithi wa NGOME YA CHUMA amepatikana" aliongea Master Ge huku machozi yakitengeza njia katika mashavu yake.

*****************
Katika hoteli moja kubwa jijini Dar-es-salaam, watu wawili walikuwa wamekaa kwenye meza ndogo katika chumba maalum cha VIP.
"Nikuite kwa jina lako halisi au jina lako la kazi" aliongea mzee Abedi. "Tuko hapa kwa ajili ya kujadili kazi na siyo kirafiki" alijibu mtu huyo. "Sawa, Victor Smith" alitabasamu mzee Abedi. "Sawa, niambie unataka jambo gani kutoka kwangu" aliongea Victor.

"Nahitaji ulinzi wa familia yangu, kuna kunguni wanataka kuniuma korodani" aliongea mzee Abedi. Sauti yake nzito ilitisha. Alionekana kama mtu mwengine kabisa. "Ulinzi tu na si mambo mengine" aliuliza Victor.

"Ndio, kwasababu ni jambo la kifamilia. Mimi nataka ulinzi kwa familia yangu tu. Mambo mengine nitayashughulikia mwenyewe" alijibu.

"Ila unafahamu huduma zetu ni ghali sana ukizitaka kamili ila bei inazungumzika ukitaka nusu".
Mzee Abedi akaingiza mkono mfukoni na kutoa cheki, akamsogezea. Victor akainyanyua na kuiangalia, akameza funda kubwa la mate. "Nafurahi kufanya kazi na wewe" akampa mkono. Mzee Abedi akatabasamu na kuupokea mkono huwo. "Kumbuka kazi zote zifanyike gizani isipokuwa pale kwenye ulazima tu" alisisitiza.

"Hiyo ndio protokali ya kazi yetu, hawatajuwa kabisa. Mkataba nitakuletea kesho" aliongea na kumalizia kinywaji chake kisha akafunika glasi na kuondoka. Hiyo ilikuwa ishara ya niachie mimi na uwe na amani.
Mzee Abedi akamalizia kinywaji na kutoa pesa, akaiweka mezani na kuondoka. Alipofika nje akatoa simu yake na kuandika ujumbe mfupi. Akautuma na kuingia kwenye gari yake na kuondoka eneo hilo.

Victor akiwa njiani akaupokea ujumbe uliotumwa na mzee Abedi. "Mwamba" ujumbe ulisomeka hivyo, akatabasamu. Akaingiza tarakimu kadhaa, "Mwamba yupo kazini, amerudi rasmi. Kikosi chake kijiandae, muda wowote atawahitaji" aliongea punde baada simu kupokewa kisha akakata.

*********
"Unajisikiaje kuwa katika ulimwengu wa Dao" aliongea Master Ge wakiwa wanatoka ndani ya pango kubwa. "Hewa ya huku ni tamu mno" alijibu Fahad akivuta pumzi ndefu. Ardhi ya Dao ilipambwa na milio mbali mbali ya ndege pamoja na kijani iliyosambaa mpaja mwisho wa upeo wa jicho.

"Katika ulimwengu huu kuna tawala kumi na mbili kubwa, nane ndogo na moja iliyokufa. Sisi tunaelekea katika eneo la mbali mbali kabisa la ulimwengu huu. Itatuchukuwa karibu siku saba mpaka kufika tunapoelekea" aliongea Master Ge.

Safari ya watu wanne ikaanza, haikuwa rahisi kwa Fahad ambae maisha yake yote amezoea kupanda usafiri katika safari zake. Kadri siku zilivyokatika ndivyo hali ya hewa ilivyobadilika, miti ilianza kupunguwa na wanyama vivyo hivyo pia.

"Karibu katika mji uliokufa" aliongea Master Ge, mbele yao kulikuwa na ardhi kubwa iliokuwa uchi. Haikuwa na nyasi hata moja, kulionekana kama ardhi hiyo ilikaushwa na chanzo chenye joto sana na kuuwa mpaka rutuba ya ardhi hiyo. Harufu kali sana ya damu ilisafiri mpaka ndani ya pua za Fahad. Akakunja sura na kuangalia kushoto na kulia.

"Tumezungukwa na watu wenye silaha" aliongea, "usijali hao ni watu wetu" alijibu Eunice na kutoa kitambaa cha zambarau akanyoosha mkono juu. Papo hapo ile haeufu ya damu ikakatika. Wakajitokeza watu waliokuwa na silaha tofauti tofauti. Akafika mtu mmoja na kupiga goti mbele ya Eunice. "Karibu nyumbani Malkia" aliongea na kuinamisha kichwa.

"Ma..ma... Malkia" Fahad alijikuta akipata kigugumizi cha ghafla. "Sasa unafahamu kwanini ulipolitaja jina lake tu, watu wote kule pangoni walikuwa vile" aliongea Master Pong na kupiga goti pia. Master Ge akapita mbele na kusuuza koo kisha akaongea "Malkia amerejea nyumbani, toeni heshima zenu".

Watu wote waliokuwa eneo hilo wakapiga goti na na kuinamisha vichwa vyao chini. Kwa pamoja wakaongea "karibu nyumbani Malkia na pole kwa uchovu wa safari ndefu". Eunice akatembea hatu kadhaa mbele na kuinuwa mkono wake juu. "Nimerudi salama na nawashukuru kwa kuacha kazi zenu kuja kunipokea" aliongea na kutabasamu.

Muda wote huwo Fahad alikuwa amesimama, "nafasi na kumiliki jiko hiyoo inapepea, lakini hata kama malkia kwani sio mwanamke. Nitattema tu madini, akinikubali si nitakuwa mfalme" alikuwa akijiwazia mwenyewe na kutabasamu.

_19a2d3d6-8b5e-475b-a7f8-38ece6023221.jpeg
 
"Nahitaji kumuona mfalme" alifika mtu mmoja nje ya jengo kubwa na kupiga magoti kisha akaomba kuonana na mfalme. "Mfalme sasa hivi yupo katika faragha na watumwa wake" alijibu mmoja kati ya walinzi waliokuwa wanalinda lango na kuingilia ndani humo. "Mimi ni waziri wa mji wa maji, nina taarifa muhimu sana, tena ni muhimu kuliko unavyofikria" aliendelea kusisitiza mtu huyo.

Wakiwa katika katika malumbano hayo, mlango ukafunguliwa. Akatoka mtu mmoja alievalia kofia nyeusi na gagulo la zambarau. "Kuna nini mbona munataka kumsumbuwa mfalme usiku wote huu" aliuliza kwa hasira.

"Huyu anasema eti ana taarifa muhimu anataka kuifikisha kwa mtukufu mfalme" alijibu mlinzi. "Mimi ni waziri kutoka mji wa maji, nina taarifa muhimu sana kwa mfalme. Nataka imfikie kabla haijafika kwa wafalme wengine" aliongea yule mtu. "Unaitwa nani" aliuliza yule mtu, "Fukulo, mheshimiwa" alijibu yule mtu, "Fukulo, mimi ni mshauri wa mkono wa kulia wa mfalme, naitwa Ganji. Kama hutojali tembea na mimi unieleze kilichokuleta umbali wote huu tena katika giza totoro" aliongea na kujitambulisha.

Fuluko akasimama na kuungana na Ganji, "malkia Eunice amerudi kutoka upande wa pili" alimnong'oneza.
"Una uhakika na unachokisema"
"Ndio, nimemshuhudia kwa macho yangu nilopokuwa kwenye hekalu la Martial Dao. Alikuwa pamoja na washauri wake wote wawili, Ge na Pong. Pia kulikuwa na mtu mwengine, nina uhakika ni mtu wa upande wa pili. Na pia amevunja sheria na kuonesha kiu ya damu ndani ya hekalu" alijibu na kufafanuwa.

"Kabisa! Hizo ni habari nzuri na ni vyema zimfikie mfalme sasa hivi" aliongea Ganji na kukuna ndevu zakw nyingi. "Nifuate" akampa ishara na kuelekea ndani ya jengo hilo la mfalme. "Mtaarishieni mgeni chumba cha kupumzika" aliongea. Waschana wawili wakatikisa vichwa na kumfanyia ishara Fuluko wamfuate.

*****************
Asubuhi mapema Fahad anatoka katika chumba alicholala. Nje hata miale ya juwa haikuwa ikionekana vizuri. Alipofika nje, akatabasamu kidogo baada ya kuona kuna vigogo vingi vya kupasuwa. Akapasha misuli kidogo kisha akaangalia kushoto na kulia. Alipoona alichokuwa anakutafuta akatabasamu na kuelekea kilipo.

Aliinyanyua shoka kubwa yenye mpini wa chuma. Akatafuta sehemu nzuri na kuanza kupasuwa vigogo hivyo. Kadri muda ulivyokwenda ndivyo misuli yake mikubwa ilivyojaa. Taratibu miale ya juwa ikaanaa kumgusa mgongoni. "Muda umekwenda sana" alijesemea na kuiweka shoka chini.

Alipogeuka akakutana na macho ya watu, walikuwa wakimuangalia kwa mshangao. Wengi wao walikuwa wanawake, yeye hakufahamu kwanini wanamshangaa. "Black Star, vaa fulana yako" aliisikia sauti aluyoifahamu. Hapo ndipo akagunduwa kama alikuwa kifua wazi. Akageuka na kuanza kuitafuta.

Akaivaa, alipogeuka akakutana tena na macho ya watu. "Nani alokwambia utumie shoka yangu" alisikia sauti nzito. "Samahani sikujuwa kama kila mtu ana miliki shoka yake" aliongea na kuinamisha kichwa. Eunice alipoona hivyo akataka kuingilia lakini master Ge akamzuia. "Unataka kujuwa uwezo wa Fahad endelea kuangalia tu" aliongea.

Fahad akainyanyua ile shoka na kumkabidhi, "wuuuuu" watu wote wakamaka.
"Oi, ile shoka ni nzito balaa"
"Ila jamaa kaibeba kama sio kitu vile"
"Hivi ina kilo ngapi ile shoka"
"Kama sijasahau ina kilo arobaini"

Baadhi ya watu wakawa wananong'ona, "unanidharau siyo" aliongea mtu huyo mkubwa aliejazia.
"Hapana, ila ni njia yangu ya kuonesha samahani yangu" alijibu Fahad.
"Sawa, iweke chini" Fahad akaiweka chini bila kujuwa maana ya kufanya hiviyo.
"Black Star umekubali pambano dhidi Decath" aliongea Master Pong.

"Pambano, kivipi?" aliuliza akiwa na sintofahamu.
"Ndivyo sheria za huku zilivyo, kuweka shoka mbele ya mtu ni kunadi pambano dhidi yake katika kuchanja kuni" alielezwa.

"Sikuwa nikifahamu hilo lakini hakuna shida, bado misuli yangu haijatosheka" alijibu na kutabasamu. "Decath umekubali pambano kutoka kwa Black Star" aliuliza Master Pong.
Decath akatikisa kichwa na kunyanyua shoka yake. "Nataka nimpe nafasi mpinzani wangu ya kuchagua shoka atakayotumia" aliongea.

"Mpelekeni kwenye sehemu ya kuhifadhia shoka" alitpa amri Master Pong. Fahad akachukuliwa mpaka kwenye jengo maalum. Ndani humi kulikuwa na shoka nyingi na za kila aina. "Utachagua yeyote humu ndani" aliongea aliyempeleka.

Fahad akaangaza pande mbali mbali mpaka macho yalipotuwa kwenye shoka yenye mpini wa silva. Akaelekea ilipo shoka hiyo, "hii ina kilo ngapi" akamuuliza aliempeleka.

"Nakusihi uchague shoka nyingine, shoka hiyo watu wote tumeikuta hapo na hakuna aliefanikiwa kuinyanyua" aliongea mtu huyo. Fahad wala hakumsikiliza, akaushika mpini na kuinyanyua. Haikuinuka! Akavuta pumzi ndefu na kujaribu tena.

Majibu yakawa hasi, "hii ni shoka na mimi ni binadamu. Itanyanyuka ikataka isitake" alijisemea na kukaza misuli yake ya mgongo, akaishika kwa mikono miwili na kuanza kuinyanyua.

Misuli ya Fahad ilianza kulia kutokana na kulazimishwa kufanya kazi ngumu kuliko uwezo wake. "Nyanyuka, nyanyuka, nyanyuka" alijisemea. Misuli yake ya paja nayo ikavimba, mishipa ya damu ikatanuka na kuanza kusafirisha damu nyingi zaidi.

Mara mgongo wake ukatanuka zaidi, kifua chake kikatanuka nacho. Mishipa yote ya mwili mzima ikatanuka mpaka mishipa midogo iliyopita machoni ikaonekana kujaa damu.

Akang'ata meno kwa nguvu, akatanuwa miguu na kubonyea zaidi. "Sitanyanyua mikono mpaka utakapoinuika" aliiambia shoka hiyo kama mtu vile. "Wewe ni shoka tu, huna budi kutii amri ya atakae kutumia" aliendelea kuongea nayo. Yule aliempeleka kuchukuwa shoka, akakimbia na kwenda kuwaita viongozi wa tawala hiyo.

Eunice na kikosi chake wakafika kushuhudia nini kinaenda kutokea. Harufu ya damu kuunguwa ikaanza kusikika kutoka mwilini mwake. Iliambatana na harufu chuma kulichokuwa na kutu. "Nyanyuka" aliongea kwa nguvu na kukaza zaidi misuli yake ya mwili.

Akiwa katika hiyo akaanza kuisikia ngoma ya vita ikilia. "Nipe nguvu zaidi hata kama zitauvunja mwili wangu. Naahidi sitaiacgia hii shoka mpaka niweze kuiinuwa" alisema kwa nguvu. Kila aliekuwa hapo alishangaa kusikia maneno hayo. Kadri muda ulivyokwenda ndivyo sauto ya ngoma ya vita Alambara ilizidi kusikika katika ngome zake za masikio yake.

"Uko tayari kuyapokea majukumu yako" ghafla ngoma ikazima, akaisikia sauti ya mzee Karakantha. "Ndio" alijibu, "uko tayari kubeba jukumu zito litakalokupotezea amani katika maisha yako".
"Ndio, niko tayari"

"Uko tayari kuwa katika uadui na miungu wanayoamini watu wa ulimwengu wa Dao".
"Mimi naami katika Mungu mmoja tu, kama kuna mwingine huyo si mungu ni binaadamu tu mwenye uwezo kidogo zaidi ya binadamu wengine. Ikiwa watasimama katika njia yangu, nitakuwa ASURA muuaji wa miungu bandia. Natamani kuisikia Alambara ikiendelea kupiga. Sauto ya ngoma hiyo ndio sauti niipendayo zaidi. Iache iliye mpaka nizibuke masikio lakini sitaiachia hii shoka mpaka niinue".

"Karibu ASURA Fahad, binaadamu unaekwenda kuwa muuaji wa miungu bandia" sauti ya Mzee Karakantha ikapotea na milio mikali ya Alambara ikarudi masikioni mwake. Ngoma hiyo ya vita ikazidi kulia kwa nguvu na kusababisha damu nyepesi kuanza kutoka masikioni mwake.

Katika kilele cha mlima Sumeru, katika kiti cha mfalme INDRA. Mfalme huyo aliekuwa amesinzia kwenye kiti chake, alishtuka kutoka katika kusinzia huko na kutoa macho. "Alambara inalia" akaongea kwa nguvu, watu waliokuwa pembeni wote wakodoe macho.

"Mtukufu mfalme wa Miungu Indra, umesema unaisikia Alambara" aliongea Sun Wukong (monkey king). "Ndio kuna kiumbe anajaribu kuinyanyua shoka ya Asura na ni kiumbe kutoka upande wa pili".
"Inakuaje kiumbe kutoka upande wa pili ajaribu kuinyanyoa shoka iliowashinda mpaka miungu" aliongea Esus Westas, anaijitambulisha kama mungu wa upepo wa magharibi.

"Ni mpumbavu ambae amechoka kuishi" aliongea Ezy Estas, anaejitambulisha kama mungu wa upepo wa maashariki.
"Kimya" alifoka Indra na kuendelea "yeyote atakaekuwa huyo kiumbe inabidi atafutwe na auwawe haraka iwezekanavyo. Kwasababu amefanikiwa kuiinuwa shoka ya Karakantha, na mnafahamu vita kati yetu na huyo mjinga. Sitaki kilichotokea miaka hiyo kijirudia".

***************
Fahad alikuwa akihema kwa nguvu huku shoka ikiwa mkononi mwake. Alikuwa akitokwa damu masikioni, puani na mdomoni. "Sasa twenda tukachanje kuni" aliongea na kugeuka. Alishangaa kuwakuta watu kadhaa wakiwa wamesujudu. Mbele ya watu hao alikuwa Eunice, "Eunice, unafanya nini?" aliuliza akijaribu kumuinuwa.

"Mtukufu Asura Fahad, ni matumaini yangu utapokea heshima hii ya mtumwa wako"
"Mbona sikuelewi, simama" aliongea kwa hasira, Eunice akasimama huku akitetemeka. "Samahani sijjakusudia kukufokea" aliongea kwa upole na kumshika begani.

Akaiweka shoka yake begani, na kutoka nje. "Hii miti imeota lini, si muda mchache tu kulikuwa hakuna kitu" aliongea akistaajabu. Wote waliokuwepo hapo wakaangaliana, kulikuwa na jambo walitamani kumueleza lakini hakuna aliethubutu kuinuwa mdomo.

"Halafu Master Pong na Decath siwaoni hapa" aliendelea kuongea. Eunice akamfata kwa nyuma na kumshika bega. Alipogeuka akampa ishara ya kumfuata. Wakafika sehemu kuna mawe mawili, jiwe moja lilisomeka Master Pong na jingine lilisomeka Decath. "Usiniambie haya ni makaburi" aliongea.

"Ndio, ni makaburi hayo"
"Lakini haiwezekani, nimewaacha muda si mrefu kwenda kuchukuwa shoka. Wamekufaje?" alihoji.
"Kwanza kabla ya yote, unahitaji kwenda kumuona Master Ge na yeye hali yake si nzuri" aliongea Eunice. Mambo yote yalimuacha Fahad njia panda, kila kitu kilikuwa sivyo alivyokiacha. Ila aliamini kwenda kumuona Master Ge ndiko atakapopata majibu anayoyahitaji.

Chumbani kwa Master Ge.
"Kijana wangu umeamka hatimae" aliongea Master Ge akijitahidi kukaa. Shuka alilokuwa amejifunika, likaanguka na kuonesha baka kubwa jeusi. "Mwalimu nini kimetokea, naomba unielezw kila kitu maana hakuna kinachonipa maana niitakayo" aliongea Fahad.

Alianza Mastet Ge "Fahad hujakaa ndani ya lile jengo kwa muda mfupi kama unavyofikiria. Ilikuchukuwa wiki nzima mpaka kuweza kuiinuwa hiyo shoka. Lakini punde baada ya kufanya hivyo ukapoteza fahamu. Kutokana na uzito wako kutokuwa wa kawaida hakuna alieweza kukuinua, hivyo tukakuacha pale pale. Kiufupi ulikuwa katika usingizi mzito kwa muda wa miaka mitano".

"Ikiwa ni miaka mitatu tangu uingie katika usingizi wako. Ulizuka ugomvi mkubwa, Eunice alichukuliwa na mfalme wa ya URUI. Walitoa maagizo kwamba ikiwa tutahitaji kumrudisha ilikuwa ni kupitia vita tu. Kweli tulijipanga na kuingia vitani. Tulishinda lakini ushindi huwo ulikuja na majeraha sana.

Katika vita hiyo tu lipoteza wapanaji wengi na Master Pong na Decath ni miongoni mwa hao. Na mimi ndio nimebaki na jeraha hili ambalo linafanya nikose uwezo wa kucheza martial art tena. Naomba unisamehe sitaweza kukufundisha kama nilivyo ahidi".

Aliongea huku machozi yakimtoka, Fahad akamsogelea na kumshika mkono. "Wewe kuwa hai inatosha kwangu, usijali huhitaji kunifundisha chochote. Nimefundishwa kila kitu na muasisi wa ngome ya chuma, Grand Master Karakantha. Kwa jinsi ninavyoliona jeraha lako, ni kwamba wameharibu DANTIAN ya kifua chako. Hivyo kuharibu pia MERIDIAN zinazosafirisha QI katika mwili wako".

"Unachktakiwa kufanya ni kutuliza akili yako na kufuta majonzi kisha tumia DOQI kuijenga upya DANTIAN ya kifua chako. Kutokana na umri wako itakuchukuwa takriban miezi sita kuijenda DANTIAN ya kifua chako na mwaka mmoja kurekebisha mishipa yako ya MERIDIAN ili iweze kusafirisha QI sawa sawa."

"Lakini kutokana na hali halisi ilivyo, hutaweza kufika hata miezi sita. Hivyo basi, nitakugaia sehemu ndogo ya Dantian yangu ambayo itakuponya kabisa mpaka meridian zako kwa muda wa wiki moja tu. Ila itabidi uvumilie, maumivu utakayokuwa unayasikia hujawahi kuyasikia tokea kuzaliwa kwako."

Akamsogelea na kumshika kifua kwa dakika kama tatu hivi. Master Ge akakohoa damu nyeusi kisha akaanza kukunja sura. "Nitamsubiri mwalimu mpaka apone, kisha tutaenda kupeleka majibu" aliongea na kumuachia.

"Unakusudia kufanya nini" aliuliza Eunice akionesha kuwa na wasiwasi. "Nini kingine, nyumbani kwetu tuna msemo unaosema UKIMWAGA MBOGA SISI TUNAMWAGA UGALI. Wataonja kidogo tu chumvi ya chakula chao walichokipika" aliongea. Macho yake yalikuwa makavu. Yalikusudia alichokisema, "lakini huu ugomvi ni wa kwetu sisi" aliongea Eunice.

"Nifuate" aliongea na kutoka chumbani kwa mwalimuwa wake moja kwa moja chumba anacholala Eunice. "Unataka kufanya nini chumbani kwangu" alihoji Eunice.
"Ingia ndani" alitoa amri, Eunice akasita lakini hakuwa na namna. Mtu aliesimama mbele yake, alikuwa hatanii hata kidogo. "Asije mtu kugonga" aliwageukia walinzi na kuongea. Waktikisa vichwa na kuondoka.
"Nambie unataka nini" aliongea Eunice.

"Vua nguo zako, vaa nguo nyepesi"
"Siwezi kufanya hivyo, huna haki ya kuuona mwili wangu kwasasa"
"Hujasikia nilichokisema au vipi. Unataka nikuvue mimi" alikazia. Eunice kuona hakuna njia ya kujitetea, akaingia katika chumba kidogo cha kubadilishia nguo na kufanya kama alivyoambiwa.

Alipotoka Fahad alikuwa amekaa kitandani, alimuangalia kwa makini. "Nini kilitokea ulipokamatwa" aliuliza. Swali hilo likaufanya moyo wa Eunice uende mbio. "Hakujatokea jambo" alijibu huku akijishika bega la upande wa kushoto. Hiyo ilikuwa ni kawaida ya kila alipojaribu kusema uongo.

Fahad akainuka kutoka alipokuwa amekaa na kumsogelea. Akamzunguka na kusimama nyuma yake. Akauzungusha mkono wake katika kiuno cha mwanamke huyo na kumvuta kwake zaidi mpaka mgongo wa Eunice ukagusana na kifua chake.
 
Attachments

  • _41ccc8ab-b1d6-4bc8-b3ef-ff3807ad0f4d.jpeg
    _41ccc8ab-b1d6-4bc8-b3ef-ff3807ad0f4d.jpeg
    243.4 KB · Views: 30
"Nahitaji kumuona mfalme" alifika mtu mmoja nje ya jengo kubwa na kupiga magoti kisha akaomba kuonana na mfalme. "Mfalme sasa hivi yupo katika faragha na watumwa wake" alijibu mmoja kati ya walinzi waliokuwa wanalinda lango na kuingilia ndani humo. "Mimi ni waziri wa mji wa maji, nina taarifa muhimu sana, tena ni muhimu kuliko unavyofikria" aliendelea kusisitiza mtu huyo.
Wakiwa katika katika malumbano hayo, mlango ukafunguliwa. Akatoka mtu mmoja alievalia kofia nyeusi na gagulo la zambarau. "Kuna nini mbona munataka kumsumbuwa mfalme usiku wote huu" aliuliza kwa hasira.
"Huyu anasema eti ana taarifa muhimu anataka kuifikisha kwa mtukufu mfalme" alijibu mlinzi. "Mimi ni waziri kutoka mji wa maji, nina taarifa muhimu sana kwa mfalme. Nataka imfikie kabla haijafika kwa wafalme wengine" aliongea yule mtu. "Unaitwa nani" aliuliza yule mtu, "Fukulo, mheshimiwa" alijibu yule mtu, "Fukulo, mimi ni mshauri wa mkono wa kulia wa mfalme, naitwa Ganji. Kama hutojali tembea na mimi unieleze kilichokuleta umbali wote huu tena katika giza totoro" aliongea na kujitambulisha.
Fuluko akasimama na kuungana na Ganji, "malkia Eunice amerudi kutoka upande wa pili" alimnong'oneza.
"Una uhakika na unachokisema"
"Ndio, nimemshuhudia kwa macho yangu nilopokuwa kwenye hekalu la Martial Dao. Alikuwa pamoja na washauri wake wote wawili, Ge na Pong. Pia kulikuwa na mtu mwengine, nina uhakika ni mtu wa upande wa pili. Na pia amevunja sheria na kuonesha kiu ya damu ndani ya hekalu" alijibu na kufafanuwa.
"Kabisa! Hizo ni habari nzuri na ni vyema zimfikie mfalme sasa hivi" aliongea Ganji na kukuna ndevu zakw nyingi. "Nifuate" akampa ishara na kuelekea ndani ya jengo hilo la mfalme. "Mtaarishieni mgeni chumba cha kupumzika" aliongea. Waschana wawili wakatikisa vichwa na kumfanyia ishara Fuluko wamfuate.
*****************
Asubuhi mapema Fahad anatoka katika chumba alicholala. Nje hata miale ya juwa haikuwa ikionekana vizuri. Alipofika nje, akatabasamu kidogo baada ya kuona kuna vigogo vingi vya kupasuwa. Akapasha misuli kidogo kisha akaangalia kushoto na kulia. Alipoona alichokuwa anakutafuta akatabasamu na kuelekea kilipo.
Aliinyanyua shoka kubwa yenye mpini wa chuma. Akatafuta sehemu nzuri na kuanza kupasuwa vigogo hivyo. Kadri muda ulivyokwenda ndivyo misuli yake mikubwa ilivyojaa. Taratibu miale ya juwa ikaanaa kumgusa mgongoni. "Muda umekwenda sana" alijesemea na kuiweka shoka chini.
Alipogeuka akakutana na macho ya watu, walikuwa wakimuangalia kwa mshangao. Wengi wao walikuwa wanawake, yeye hakufahamu kwanini wanamshangaa. "Black Star, vaa fulana yako" aliisikia sauti aluyoifahamu. Hapo ndipo akagunduwa kama alikuwa kifua wazi. Akageuka na kuanza kuitafuta.
Akaivaa, alipogeuka akakutana tena na macho ya watu. "Nani alokwambia utumie shoka yangu" alisikia sauti nzito. "Samahani sikujuwa kama kila mtu ana miliki shoka yake" aliongea na kuinamisha kichwa. Eunice alipoona hivyo akataka kuingilia lakini master Ge akamzuia. "Unataka kujuwa uwezo wa Fahad endelea kuangalia tu" aliongea.
Fahad akainyanyua ile shoka na kumkabidhi, "wuuuuu" watu wote wakamaka.
"Oi, ile shoka ni nzito balaa"
"Ila jamaa kaibeba kama sio kitu vile"
"Hivi ina kilo ngapi ile shoka"
"Kama sijasahau ina kilo arobaini"
Baadhi ya watu wakawa wananong'ona, "unanidharau siyo" aliongea mtu huyo mkubwa aliejazia.
"Hapana, ila ni njia yangu ya kuonesha samahani yangu" alijibu Fahad.
"Sawa, iweke chini" Fahad akaiweka chini bila kujuwa maana ya kufanya hiviyo.
"Black Star umekubali pambano dhidi Decath" aliongea Master Pong.
"Pambano, kivipi?" aliuliza akiwa na sintofahamu.
"Ndivyo sheria za huku zilivyo, kuweka shoka mbele ya mtu ni kunadi pambano dhidi yake katika kuchanja kuni" alielezwa.
"Sikuwa nikifahamu hilo lakini hakuna shida, bado misuli yangu haijatosheka" alijibu na kutabasamu. "Decath umekubali pambano kutoka kwa Black Star" aliuliza Master Pong.
Decath akatikisa kichwa na kunyanyua shoka yake. "Nataka nimpe nafasi mpinzani wangu ya kuchagua shoka atakayotumia" aliongea.
"Mpelekeni kwenye sehemu ya kuhifadhia shoka" alitpa amri Master Pong. Fahad akachukuliwa mpaka kwenye jengo maalum. Ndani humi kulikuwa na shoka nyingi na za kila aina. "Utachagua yeyote humu ndani" aliongea aliyempeleka.
Fahad akaangaza pande mbali mbali mpaka macho yalipotuwa kwenye shoka yenye mpini wa silva. Akaelekea ilipo shoka hiyo, "hii ina kilo ngapi" akamuuliza aliempeleka.
"Nakusihi uchague shoka nyingine, shoka hiyo watu wote tumeikuta hapo na hakuna aliefanikiwa kuinyanyua" aliongea mtu huyo. Fahad wala hakumsikiliza, akaushika mpini na kuinyanyua. Haikuinuka! Akavuta pumzi ndefu na kujaribu tena.
Majibu yakawa hasi, "hii ni shoka na mimi ni binadamu. Itanyanyuka ikataka isitake" alijisemea na kukaza misuli yake ya mgongo, akaishika kwa mikono miwili na kuanza kuinyanyua.
Misuli ya Fahad ilianza kulia kutokana na kulazimishwa kufanya kazi ngumu kuliko uwezo wake. "Nyanyuka, nyanyuka, nyanyuka" alijisemea. Misuli yake ya paja nayo ikavimba, mishipa ya damu ikatanuka na kuanza kusafirisha damu nyingi zaidi.
Mara mgongo wake ukatanuka zaidi, kifua chake kikatanuka nacho. Mishipa yote ya mwili mzima ikatanuka mpaka mishipa midogo iliyopita machoni ikaonekana kujaa damu.
Akang'ata meno kwa nguvu, akatanuwa miguu na kubonyea zaidi. "Sitanyanyua mikono mpaka utakapoinuika" aliiambia shoka hiyo kama mtu vile. "Wewe ni shoka tu, huna budi kutii amri ya atakae kutumia" aliendelea kuongea nayo. Yule aliempeleka kuchukuwa shoka, akakimbia na kwenda kuwaita viongozi wa tawala hiyo.
Eunice na kikosi chake wakafika kushuhudia nini kinaenda kutokea. Harufu ya damu kuunguwa ikaanza kusikika kutoka mwilini mwake. Iliambatana na harufu chuma kulichokuwa na kutu. "Nyanyuka" aliongea kwa nguvu na kukaza zaidi misuli yake ya mwili.
Akiwa katika hiyo akaanza kuisikia ngoma ya vita ikilia. "Nipe nguvu zaidi hata kama zitauvunja mwili wangu. Naahidi sitaiacgia hii shoka mpaka niweze kuiinuwa" alisema kwa nguvu. Kila aliekuwa hapo alishangaa kusikia maneno hayo. Kadri muda ulivyokwenda ndivyo sauto ya ngoma ya vita Alambara ilizidi kusikika katika ngome zake za masikio yake.
"Uko tayari kuyapokea majukumu yako" ghafla ngoma ikazima, akaisikia sauti ya mzee Karakantha. "Ndio" alijibu, "uko tayari kubeba jukumu zito litakalokupotezea amani katika maisha yako".
"Ndio, niko tayari"
"Uko tayari kuwa katika uadui na miungu wanayoamini watu wa ulimwengu wa Dao".
"Mimi naami katika Mungu mmoja tu, kama kuna mwingine huyo si mungu ni binaadamu tu mwenye uwezo kidogo zaidi ya binadamu wengine. Ikiwa watasimama katika njia yangu, nitakuwa ASURA muuaji wa miungu bandia. Natamani kuisikia Alambara ikiendelea kupiga. Sauto ya ngoma hiyo ndio sauti niipendayo zaidi. Iache iliye mpaka nizibuke masikio lakini sitaiachia hii shoka mpaka niinue".
"Karibu ASURA Fahad, binaadamu unaekwenda kuwa muuaji wa miungu bandia" sauti ya Mzee Karakantha ikapotea na milio mikali ya Alambara ikarudi masikioni mwake. Ngoma hiyo ya vita ikazidi kulia kwa nguvu na kusababisha damu nyepesi kuanza kutoka masikioni mwake.

Katika kilele cha mlima Sumeru, katika kiti cha mfalme INDRA. Mfalme huyo aliekuwa amesinzia kwenye kiti chake, alishtuka kutoka katika kusinzia huko na kutoa macho. "Alambara inalia" akaongea kwa nguvu, watu waliokuwa pembeni wote wakodoe macho.
"Mtukufu mfalme wa Miungu Indra, umesema unaisikia Alambara" aliongea Sun Wukong (monkey king). "Ndio kuna kiumbe anajaribu kuinyanyua shoka ya Asura na ni kiumbe kutoka upande wa pili".
"Inakuaje kiumbe kutoka upande wa pili ajaribu kuinyanyoa shoka iliowashinda mpaka miungu" aliongea Esus Westas, anaijitambulisha kama mungu wa upepo wa magharibi.
"Ni mpumbavu ambae amechoka kuishi" aliongea Ezy Estas, anaejitambulisha kama mungu wa upepo wa maashariki.
"Kimya" alifoka Indra na kuendelea "yeyote atakaekuwa huyo kiumbe inabidi atafutwe na auwawe haraka iwezekanavyo. Kwasababu amefanikiwa kuiinuwa shoka ya Karakantha, na mnafahamu vita kati yetu na huyo mjinga. Sitaki kilichotokea miaka hiyo kijirudia".
***************
Fahad alikuwa akihema kwa nguvu huku shoka ikiwa mkononi mwake. Alikuwa akitokwa damu masikioni, puani na mdomoni. "Sasa twenda tukachanje kuni" aliongea na kugeuka. Alishangaa kuwakuta watu kadhaa wakiwa wamesujudu. Mbele ya watu hao alikuwa Eunice, "Eunice, unafanya nini?" aliuliza akijaribu kumuinuwa.
"Mtukufu Asura Fahad, ni matumaini yangu utapokea heshima hii ya mtumwa wako"
"Mbona sikuelewi, simama" aliongea kwa hasira, Eunice akasimama huku akitetemeka. "Samahani sijjakusudia kukufokea" aliongea kwa upole na kumshika begani.
Akaiweka shoka yake begani, na kutoka nje. "Hii miti imeota lini, si muda mchache tu kulikuwa hakuna kitu" aliongea akistaajabu. Wote waliokuwepo hapo wakaangaliana, kulikuwa na jambo walitamani kumueleza lakini hakuna aliethubutu kuinuwa mdomo.
"Halafu Master Pong na Decath siwaoni hapa" aliendelea kuongea. Eunice akamfata kwa nyuma na kumshika bega. Alipogeuka akampa ishara ya kumfuata. Wakafika sehemu kuna mawe mawili, jiwe moja lilisomeka Master Pong na jingine lilisomeka Decath. "Usiniambie haya ni makaburi" aliongea.
"Ndio, ni makaburi hayo"
"Lakini haiwezekani, nimewaacha muda si mrefu kwenda kuchukuwa shoka. Wamekufaje?" alihoji.
"Kwanza kabla ya yote, unahitaji kwenda kumuona Master Ge na yeye hali yake si nzuri" aliongea Eunice. Mambo yote yalimuacha Fahad njia panda, kila kitu kilikuwa sivyo alivyokiacha. Ila aliamini kwenda kumuona Master Ge ndiko atakapopata majibu anayoyahitaji.
Chumbani kwa Master Ge.
"Kijana wangu umeamka hatimae" aliongea Master Ge akijitahidi kukaa. Shuka alilokuwa amejifunika, likaanguka na kuonesha baka kubwa jeusi. "Mwalimu nini kimetokea, naomba unielezw kila kitu maana hakuna kinachonipa maana niitakayo" aliongea Fahad.
Alianza Mastet Ge "Fahad hujakaa ndani ya lile jengo kwa muda mfupi kama unavyofikiria. Ilikuchukuwa wiki nzima mpaka kuweza kuiinuwa hiyo shoka. Lakini punde baada ya kufanya hivyo ukapoteza fahamu. Kutokana na uzito wako kutokuwa wa kawaida hakuna alieweza kukuinua, hivyo tukakuacha pale pale. Kiufupi ulikuwa katika usingizi mzito kwa muda wa miaka mitano".
"Ikiwa ni miaka mitatu tangu uingie katika usingizi wako. Ulizuka ugomvi mkubwa, Eunice alichukuliwa na mfalme wa ya URUI. Walitoa maagizo kwamba ikiwa tutahitaji kumrudisha ilikuwa ni kupitia vita tu. Kweli tulijipanga na kuingia vitani. Tulishinda lakini ushindi huwo ulikuja na majeraha sana. Katika vita hiyo tu lipoteza wapanaji wengi na Master Pong na Decath ni miongoni mwa hao. Na mimi ndio nimebaki na jeraha hili ambalo linafanya nikose uwezo wa kucheza martial art tena. Naomba unisamehe sitaweza kukufundisha kama nilivyo ahidi".
Aliongea huku machozi yakimtoka, Fahad akamsogelea na kumshika mkono. "Wewe kuwa hai inatosha kwangu, usijali huhitaji kunifundisha chochote. Nimefundishwa kila kitu na muasisi wa ngome ya chuma, Grand Master Karakantha. Kwa jinsi ninavyoliona jeraha lako, ni kwamba wameharibu DANTIAN ya kifua chako. Hivyo kuharibu pia MERIDIAN zinazosafirisha QI katika mwili wako".
"Unachktakiwa kufanya ni kutuliza akili yako na kufuta majonzi kisha tumia DOQI kuijenga upya DANTIAN ya kifua chako. Kutokana na umri wako itakuchukuwa takriban miezi sita kuijenda DANTIAN ya kifua chako na mwaka mmoja kurekebisha mishipa yako ya MERIDIAN ili iweze kusafirisha QI sawa sawa.".
"Lakini kutokana na hali halisi ilivyo, hutaweza kufika hata miezi sita. Hivyo basi, nitakugaia sehemu ndogo ya Dantian yangu ambayo itakuponya kabisa mpaka meridian zako kwa muda wa wiki moja tu. Ila itabidi uvumilie, maumivu utakayokuwa unayasikia hujawahi kuyasikia tokea kuzaliwa kwako"
Akamsogelea na kumshika kifua kwa dakika kama tatu hivi. Master Ge akakohoa damu nyeusi kisha akaanza kukunja sura. "Nitamsubiri mwalimu mpaka apone, kisha tutaenda kupeleka majibu" aliongea na kumuachia.
"Unakusudia kufanya nini" aliuliza Eunice akionesha kuwa na wasiwasi. "Nini kingine, nyumbani kwetu tuna msemo unaosema UKIMWAGA MBOGA SISI TUNAMWAGA UGALI. Wataonja kidogo tu chumvi ya chakula chao walichokipika" aliongea. Macho yake yalikuwa makavu. Yalikusudia alichokisema, "lakini huu ugomvi ni wa kwetu sisi" aliongea Eunice.
"Nifuate" aliongea na kutoka chumbani kwa mwalimuwa wake moja kwa moja chumba anacholala Eunice. "Unataka kufanya nini chumbani kwangu" alihoji Eunice.
"Ingia ndani" alitoa amri, Eunice akasita lakini hakuwa na namna. Mtu aliesimama mbele yake, alikuwa hatanii hata kidogo. "Asije mtu kugonga" aliwageukia walinzi na kuongea. Waktikisa vichwa na kuondoka.
"Nambie unataka nini" aliongea Eunice.
"Vua nguo zako, vaa nguo nyepesi"
"Siwezi kufanya hivyo, huna haki ya kuuona mwili wangu kwasasa"
"Hujasikia nilichokisema au vipi. Unataka nikuvue mimi" alikazia. Eunice kuona hakuna njia ya kujitetea, akaingia katika chumba kidogo cha kubadilishia nguo na kufanya kama alivyoambiwa.
Alipotoka Fahad alikuwa amekaa kitandani, alimuangalia kwa makini. "Nini kilitokea ulipokamatwa" aliuliza. Swali hilo likaufanya moyo wa Eunice uende mbio. "Hakujatokea jambo" alijibu huku akijishika bega la upande wa kushoto. Hiyo ilikuwa ni kawaida ya kila alipojaribu kusema uongo.
Fahad akainuka kutoka alipokuwa amekaa na kumsogelea. Akamzunguka na kusimama nyuma yake. Akauzungusha mkono wake katika kiuno cha mwanamke huyo na kumvuta kwake zaidi mpaka mgongo wa Eunice ukagusana na kifua chake.
Mkuu kazi safi sana, ije kwawingi itupunguze hii hangover nimeanza kuwa naota matukio yake usiku kama naangalia video
 
BLACK STAR
NA
TARIQ HAJJ

"Nambie ukweli" alimnong'oneza sikioni, ujasiri wote wa Eunice ukavuka. Macho yake yakajaa machozi. Akamgeukia Fahad na kumkumbatia kwa nguvu. Akaangusha kilio kizito, Fahad kumuona Eunice katika hali hiyo moyo wake ukaanza kufukuta. Hasira ikaanza kumpanda, "wamenidhalilisha" aliongea Eunice kwa sauti ya kilio na kwikwi juu. "Wamenitesa sana na mfalme wao ametaka kuniingilia kwa nguvu" aliendelea kumwaga kilio.

"Lia, usizuie machozi. Sura yako haifai kuwa na huzuni" aliongea Fahad. "Unaweza ukawa malkia mbele ya macho yao lakini kwangu wewe ni mwanamke tu. Na ulisema huu ugomvu haunihusu, ila kosa walilofanya ni kumdhalilisha mwanamke nimpendae. Na hilo litawagharimu tawala yao nzima.

Eunice alilia kifuani kwa Fahad mpaka usingizi ukamchukuwa. Akamlaza kitandani na yeye akajilaza pembeni. Usingizi mzito ukamchukuwa kutokana kuchoka maana alitumia uwezo wake wote katika kudhidhibiti hasira zake.

Alikuja kushtuka baada ya miale kumpiga usoni, alihisi kifua chake kizito. Akainuwa kichwa na kuangalia nini kinasababisha uzito. Akamuona Eunice akiwa amelala fofofo, "ama uliumbwa uje kuukamata moyo wangu" alijisemea na kurudisha kichwa chini.

Hakutaka kumuamsha, aliamini kabisa mwanamke huyo hakuweza kulala vizuri baada ya mambo yote kutokea. Baada takriban saa nzima Eunice akaamka.

"Umelalaje" aliuliza Fahad, Eunice akamuangalia usoni kwa aibu kisha akashuka kitandani kukimbilia katika chumba cha kubadilishia nguo. Fahad akateremka na kutoka chumbani humo. Akasimama nje na kushusha pumzi, baada ya nusu saa Eunice akatoka.

"Ahsante, nimelala vizuri" alijibu.
"Nafurahi kusikia hivyo"

Wakaelekea kumuona Master Ge ambae alikuwa yupo katika safari yake kuponya jeraha. "Unaendeleaje" aliuliza Fahad. "Naendelea vizuri, Dantian yangu ya kifua imepona kabisa" alijibu. "Endelea kutuliza akili, hakikisha Qi inatembea vizuri. Usijaribu kunyonya DOQi kutoka katika mazingira mpaka utakapopona kabisa" aliongea Fahad.

"Malkia, naona umerudi katika hali yako ya kawaida. Ulikuwa unanipa wasiwasi sana" aliongea Master Ge. "Fanya haraka upone kuna mambo mawili makubwa nahitaji tujadili" aliongea Fahad. Wakamuacha Master Ge aendelee kupumzika, wao wakatoka nje.

Eunice alikuwa akitembea nyuma ya Fahad, kila walipopita watu walishangaa. Fahad wala hakuelewa walikuwa wakishangaa nini. "Eunice unaweza kunitembeza" alimgeukia na kuongea. "Hakuna shida" alijibu.
Waliitumia siku hiyo kuzunguka maeneo tofauti ya ngome hiyp iliyochakaa. Maeneo mengi ya eneo hilo yalikuwa hayaoti hata majani. Ardhi ilikuwa imekufa kabisa.

"Hali ikiendelea hivi, baada ya muda itabidi muihame ngome na kuitelekeza" aliongea Fahad wakiwa njiani kurudi katika mji mkuu wa ngome hiyo. "Hatuna jinsi, na hata tukitoka hapa. Hatuna pa kwenda, hakuna ngome itakayokubali wananchi wa ngome ya ASURA".

"Kwani ilikuwaje mpaka hali ikawa hivi" aliuliza.
"Ni hadithi ndefu nitakuhadithia tukifika nyumbani". Safari ikaendelea kwa ukimya huku mara chache Fahad akiuliza maswali ya hapa na pale.

Walifika mji mkuu tayari kiza kilishaanza kuingia. "Karibu nyumbani" aliongea mlinzi na kuinamisha kichwa. "Ahsante" alijibu Eunice na kutangulia.
Chakula kilikuwa tayari mezani, "kwanini unakula umejifungia ndani" aliuliza Fahad. "Ni mila zetu ndio ziko hivi, mtawala lazima ale peke yake au na watu wenye vyeo katika nchi".

"Katika hali ya sasa, unatakiwa ule na watu wako ndio utapata kuwajuwa vizuri. Utapata kufahamu hali zao vizuri" aliongea Fahad. "Hilo litakuwa ni jambo jipya na sidhani kama watu watakubali".
"Niamini utashangaa kitakachotokea", wakaendelea kula. Baada ya chakula, Fahad akamsindikiza Eunice chumbani kwake. "Leo hulali huku" aliuliza Eunice.

"Unataka nilale"
"Ndio, naogopa kulala peke yangu. Zile ndoto mbaya mara zitanirudia".
" Ukiiweka hivyo, siwezi kukuacha peke yako" akafunga mlango na kuingia ndani. Akakaa kitandani, Eunice akaelekea chumba cha kubadilisha nguo. Aliporudi tayari usingizi ulishamchukuwa Fahad. Akapanda kitandani na kujilaza pembeni yake.

**************
"Fahad ulinambia kuna mambo mawili muhimu unataka tuongee pindi nitakapopona tu" aliongea Master Ge akijiweka vizuri kitandani.

"Ndio, mwalimu lakini si mawili tena, ni matatu sasa". Eunice alikuwa pembeni akiwaangalia wawili hao wakiongea hata yeye mwenyewe alikuwa na shauku ya kutaka kujuwa mambo aliyotaka kuongea Fahad.
"Haya nakupa masikio yangu yote mawili" aliongea Master Ge.

"La kwanza, najuwa huku munategemea sana martial art katika kila kitu na muna imani pia kwamba kila kitu kinahitahi nishati fulani ya asili ili kukuwe. Ardhi yenu haina rutuba, ni kweli kabisa inaonekana haina uhai. Ila tunaweza kuirutubisha tena ikaweza kuzalisha chakula kitakachowasukuma katika kipindi hiki kigumu mpaka pale mtakpoweza kurudisha uhai katika ardhi hii" aliongea Fahad. Kisha akawaelekeza jinsi ya kutengeza mbolea kupitia vitu vya kawaida kabisa.

"Enhe jambo la pili" aliongea Master aliongea Master Ge.
"La pili, ni kubwa zaidi ya la kwanza na ndio la muhimu zaidi. Linamuhusu malkia wenu, Eunice kuanzia sasa ni malkia wangu" aliongea kwa kuficha kidogo.

"Lakini mtu yeyote anaeingia katika ngome hii, humfanya Eunice kuwa malkia wake kisheria" aliongea Master Ge.
"Sijamaanisha hivyo, ngoja ninyooshe. Eunice ni mwanamke wangu" aliongea macho makavu.
"Eti nini, Fahad kuna mipaka huwezi kuvuka" aliongea Master Ge akionekana kukereka na maneno ya Fahad.

"Narudia tena, sijali kama mi malkia, au tunatoka limwengu mbili tofauti. Eunice ni mwanamke wangu na nina uhakika hana pingamizi juu ya hilo" aliongea na kunyoosha mkono wake upande alio Eunice. Bila hata kufikiria afanye nini, Eunice akainuka na kuingia kwapani kwa Fahad kama kifaranga cha kuku kinachotaka joto kutoka kwa mama ake.

Master Ge hakuwa na la kusema tena, majibu alishayapata. Akatabasamu kidogo na kuongea "inaonekana alishasalimu amri kitambo". "Enhe la tatu ni lipi".
"Malipo" alibadilika ghafla.
"Unakusudia nini"

"Kifo cha Master Pong na Decath hakitaenda bila kulipwa. Kila ninapo kaa nazisikia roho zao zinavyosononeka. Lakini kubwa zaidi inabidi mfalme wao atambuwe kama kumgusa tu mwanamke wangu basi ni sawa na kuposa kifo. Atalipa vilivyo, na neno litafika ulimwenguni kote kuwa, yeyote atakaesogelea ngome Asura ataangamia mikononi mwangu. Mimi sikopeshi, tunamalizana hapo hapo na hiyo ndio mila yangu" alifafanuwa.

"Hapana Fahad hata kama umepokea baraka zote kutoka Asura wa kwanza, hutaweza kupambana na ngome nzima peke yako" aliongea Master Ge. Akaendelea "isitoshe ngome zote huku kusini zipo chini ya usumamizi wa mungu gharika, Mtukufu Masiyo".

"Master Ge, subiri nikwambie kitu. Najuwa nyinyi mnaamini katika miungu tofauti. Na mnaamini pia binaadamu wa kawaida anaweza kupanda mpaka kuwa mungu. Kwangu mimi hilo halipo, naamini katika huu ulimwengu mungu mmoja tu na siwalazimishi nyinyi kuamini hivyo. Ila hao mnaowaita miungu ni wanafiki tu, si chochote bali ni binadamu tu waliokuwa na uwezo kidogo zaidi ya binadamu wengine" alijibu Fahad.

"Sawa kila mtu anaamini katika kile anachoamini lakini huku hao watu ni miungu. Na kupambana nao ni sawa na kututoa kafara sote" alisisitiza Master Ge na kuendelea "kilichotokea hapa ni matokeo ya mtu mmoja tu, alikwenda kinyume na miungu.

Matokeo eneo lote hili likapata maafa, mpaka alipokuja mungu Asura akaliweka eneo hili chini yake ndio uhai ukarudi. Hata hivyo miungu hawakulitaka hilo wakaungama, kupambana na Asura. Baada ya vita hiyo alipotea na damu yake ndio angalau inaipa uhai ardhi hii".

"Huwo ni uwongo uliotungwa na kusambazwa na hao wanaojiita miungu ili musiujue ukweli halisi" aliongea Fahad kwa jazaba kidogo. "Una maanisha nini kusema hivyo, huko ni kuchupa mipaka yako kijana" master Ge alionekana kukereka na kauli hiyo.

"Hiyo ni hadithi ndefu na inahitaji kikao kirefu ili muielewe vizuri. Lakini fahamuni tu kwamba mnachokijuwa sicho cha kweli" alijibu Fahad na kusimama.

"Unaenda wapi" aliuliza master Ge, "nina ahadi na baadhi ya watu na huu ni muda tuliopanga kuonana" alojibu. "Sawa, wewe nenda. Mimi nataka kujadili mambo kadhaa na Eunice kisha nitakuja huko nje". Fahad akatikisa kichwa na kutoka.

"Eunice, nini msimamo wako"
"Kuhusiana na Fahad, mimi sina la kusema. Amejihakikisha kuwa anaweza kuwa mume na pia kiongozi bora kwa watu wangu" alijibu bidada huyo.

"Na vipi kuhusiana na kisasi chake, uhafahamu kabisa kufanya ni kukaribisha mauti kwa watu wetu" alionesha wasiwasi wake Master Ge.
"Kuhusiana na hilo itabidi tusubiri tuone mwisho wake" alijibu Eunice. Alionesha kuwa na imani na maamuzi ya Fahad kwa asilimia mia moja.

*********
"Hakikisha unavuta pumzi nyingi, usiiachie mpaka uhisi mapigo ya moyo yanapiga masikioni" alitoa maelekezo Fahad akiwa mbele. "Sawa" wakaitika kwa pamoja na kufanya kama walivyoambiwa.
Master Ge alipotoka akakutana na umati wa watu wakipata mafunzo kutoka kwa Fahad. "Nini kinaendelea" aliuliza akiwa na sintofahamu.

"Fahad ameamuwa kuwafundisha wote wanaotaka hatuwa ya kwanza ya ngome ya chuma" alijibu Eunice aliekuwa pembeni akiaangalia mazoezi hayo.

"Fanya mazoezi ili siku nyingine akichukuliwa mtu wako wa karibu usitegee mtu mwingine akufanyie kazi yako" aliongea Fahad kwa nguvu. Motisha ya watu waliokuwa nyuma yake ikapanda, wakaongeza juhudi. Mazoezi yalikuwa makali lakini hakuna alielalamika hata mmoja.

Baada takriban saa mbili hivi, mazoezi ya siku hiyo yakafikia tamati. Fahad akawaruhusu waende kupumzika na kuendelea na majukumu mengine.
"Fahad, njoo tuongee" alisikia sauti ya Master Ge. Wakaondoka eneo hilo na kwenda pembeni wawili peke yao, hata Eunice aliambiwa asubiri.

"Nimefikiria sana, najuwa kufanya hili nitakuwa nakiuka mila na desturi zetu lakini hii ngome kwasasa inahitaji mtu roho ya chuma ili isimame tena. Eunice peke yake hatoweza kufanya hivyo, hivyo basi wiki moja kutoka sasa utafunga ndoa na Eunice.

Katika wiki moja hii ya kusubiri, itabidi usome taratibu na mila za kifalme. Kumbuka huku hakuna demokrasia, kauli ya mfalme ndio kauli ya mwisho" aliongea Master Ge.
"Nafirahi kusikia hivyo, na nakuahidi sitakuangusha. Sijui ngome hii huko nyuma ilikuwaje lakini historia itaandikwa upya" alijibu Fahad. Macho yake yalionyesha kusudio lake.

"Na jambo jingine, ukiwa mfalme itabidi utambulishwe kwa jina lako. Jambo ambalo litakuwa ni hatari kwako na familia yako upande wa pili. Hivyo basi na kupa nafasi uchague jina lolote ambalo litakuwa jina lako ukiwa huku. Achana na Black Star, jina lako la ulingoni. Huku unahitaji jina jipya kabisa lenye kufanana na majina ya huku".

"Fey Ge, ndio jina nitakalotumia huku", jibu hilo likamshtuwa sana Master Ge. "Kwanini umeamuwa jina hilo".
"Kila mtu anahitaji mtu wa kumshauri na kumuongoza. Nimekuchaguwa wewe uwe baba yangu nikiwa huku."

Machozi yakatengeza michirizi mashavuni mwa Master Ge. Hayakuwa ya hizuni bali ya furaha. "Ahsante Fahad, sikutegemea hata mara moja katika maisha yangu nitapewa thamani ya kuitwa baba. Hiyo kwangu ni heshima kubwa kuliko hata kuitwa master" aliongea akionesha wazi furaha yake.

*****
_19a2d3d6-8b5e-475b-a7f8-38ece6023221.jpeg
 
Wiki moja baadae.
"Kupitia mamlaka niliokabidhiwa na waandamizi wa ngome, namtawadha Fey Ge kuwa mfalme wa tatu wa tawala hii. Anamchukuwa Malkia Eunice kama mtawala msaidizi na malkia wake. Kuanzia sasa nawatangaza wawili hawa kuwa mume na mke" aliongea Master Ge katika sherehe maalumu ilioandaliwa siku hiyo.

Wakiwa katika sherehe hiyo, alifika mtu mmoja kutoka umoja wa ngome zinazoongozwa na miungu kumi na moja. Alifika akiwa na barua iliaondikwa kutoka huko huko, mfalme Fey akaipokea na kumkabidhi mshauri wake mkuu ambae ni master Ge. Akaifunguwa na kuanza kuisoma.

"Hongera kwa mfalme mpya, ni wajibu wetu kukutakia majukumu mema na kukuhabarisha kuwa utapewa miaka kumi ya kujenga ngome yako. Pia utapewa nafasi tatu za upendeleo kuchaguwa unachotaka" barua ikaishia hapo.

Fahad akasimama na kumuangalia yule mjumbe alieleta barua hiyo. "Nenda kawaambia, nahitaji watu wangu wote waliokamatwa na kutumikishwa pasi na kutaka kwao. Hata kama wamekufa, waniletee vitu vyao. Hilo moja la pili, peleka taarifa kwa yule mpuuzi aliemdhalilisha mke wangu, najuwa unamfahamu. Mwambie ajiandae siku tatu kutoka leo nakuja kumuangamiza.

Na la tatu miaka yangu kumi ikiisha waambie waongoze kumi mingine. Na yeyote atakaethubutu kunigusa katika kipindi hicho. Mungu awe na huruma nae, kitakachomkuta atakisimulia popote atakapo kuwa" alimaliza kuongea na kurudi kwenye kiti chake.

Master Ge aliandika mambo yote hayo yaliyosemwa kisha akamkabidhi yule mjumbe. Akapokea na kuondoka, "ahsante mfalme kwa kuwaweka ndugu zetu mbele" wananchi waliokuwa hapo wakapiga magoti huku baadhi machozi yakiwatoka.

"Anadhani yeye ni nani mpaka kuongea kama hivi" aliongea mtu mmoja. "Punguza jazba, haya ni mambo madogo tu. Ila kuhusu wewe itabidi ujipange tu. Unajuwa kabisa kama wakuu, hawatataka kuhusishwa. Wewe jipange kesho kutwa atakuja. Sidhani kama ana uwezo wa kukuzidi" aliongea mtu mwengine.
Mfalme wa kumi na sita, Mfalme Damesh alijulikana kwa kiu yake ya wanawake.

Alitaka kila mwanamke aliemzuri awe wake. Alifikia hadi kuwaua waume za wanawake aliowapenda kisha kuwamiliki wanawake hao. Mfalme huyu aliongoza ngoke ya Urui, iliyokuwa chini ya uamgalizi wa wa mungu Masiyo.

"Ganji, andaa wapambanaji wetu mashuhuri zaidi. Nataka tumuoneshe huyu bwana mdogo kama mimi si saizi yake" aliongea mfalme Damesh. Ganji akatikisa kichwa, baada ya majadiliano ya muda mrefu, hatimae wakafikia makubaliano kuwa kila ngome itaachia raia nusu wa ngome ya Asura. Kufanya kuna hakikisha kuwa wana jambo la kumzuia mfalme huyo mpya asifanye kama anavyotaka.

Miongoni mwa watu watakaoachiwa walikubaliana pia wawemo wapelelezi kutoka ngome hizo. Baada ya kikao hicho, wakaandika barua na kutumwa kwa ngome ya Asura. Fahad alipoisoma barua hiyo akatabasamu kidogo. "Sio mwanzo mbaya, lakini msitegemee kama mtakuwa mumenifunga kamba za mikono".

Akatoka katika chumba hekalu lake na kuita watu wake wote. "Hapa nina habari nzuri na mbaya. Nitaanza na mbaya kisha itafuata nzuri. Mbaya ni kwamba wamekubali kuwaachia nusu ya ndugu zetu, nzuri ya kwanza ni kwamba wamekubali kuongeza miaka kumi katika ile kumi ya mwanzo. Na hivyo kutupa miaka ishirini ya kujiandaa. Na nzuri ya mwisho ni kwamba mfalme wa Urui amejipanga kunikabili".

Kwa taarifa hizo hawakujuwa washangilie au wahuzunike, kila mmoja alionesha furaha kivyake.
Siku tatu baadae, Fahad aliondoka nankikundi kidogo cha watu akiwemo Eunice na master Ge na wengine kumi.

Jumla ukawa msafara wa watu kumi na watatu. Walisafiri kwa farasi kwa takriban saa kumi na sita mpaka kumaliza ardhi ya Asura. Wakasafiri kwa siku tatu mpaka kufika ngome ya Urui. Master Ge akatangulia kutoa taarifa ujio wa mfalme kutoka Asura. Wakapokelewa na mshauri mkuu wa ngome hiyo, bwana Ganji.

"Samahani Master Ge, hapa mbona simuoni mfalme" aliongea Ganji. Kauli hiyo ikawaudhi sana wengine mpaka Eunice. Master Ge yeye ndo alikuwa kafura vibaya sana. "Baba, achana nae huyo mpuuzi anatujaribu" aliongea Fahad akiinuwa mkono kama ishara ya kuwatuliza.

Ganji akawaongoza mpaka katika uwanja wa mapambano. "King Fey Ge amewasili" Ganji akatangaza na watu wote waliokuwepo hapo wakaanza kuzomea. "Tulieni hivyo hivyi, wamepanga kutuchachafya, wanataka wapate sababu ya kuanzisha vita nyingine" aliongea Fahad akitabasamu.

Upande mmoja wa ulingo huwo alikuwepo mfalme wa taifa hilo, mfalme Damesh na upande mwingine ndio alikuwa Fahad na kikosi chake. "Kwasababu hili pambano linapiganwa nyumbani kwety, basi tutatumia sheria za kwetu" aliongea Ganji akiwa katikati ya uwanja huwo. "Ni matumaini yangu mfalme Fey utakubaliana na hilo" aliendelea kuongea na kumuangalia Fahad.

Fahad akatikisa kichwa kuashiria kukubaliana nae. Ganji akaachia tabasamu la kinafiki "umeingia katika mtego wangu" alijisemea mwenyewe.

Mfalme Damesh akapanda ulingoni, "mimi ninachotaka kwa ushindi na malkia wako, uko tayari kumtoa" aliongea kwa nguvu. "Unajuwa thamani ya malkia wangu na uko tayari kutoa jambo lenye thamani kama yeye japo nafahamu hakuna kitu kama hicho" aliongea Fahad na kusimama.
"Hahahah!! Sema unachotaka"

"Ngome yako iwe mtumwa wa ngome yangu. Kila mwezi utalipa ada kwa muda wa miaka ishirini" aliongea Fahad.
"Hilo haliwezekani, sema jingine"
"Kama hilo haliwezekani na wewe huna haki hata ya kumwangalia malkia wangu. Sio tu malkia wangu bali huna haki ya kuwa na mwanamke yeyote yule"

"Unajuwa ngome yangu ina watu wako wanaofanya kazi kama watumwa zaidi ya laki tano. Ukishinda nitawaachia watu wako wote" aliongea mfalme Damesh. Alijulikana kwa kufanya jambo lolote lile ili kumpata mwanamke amtakae.

Fahad akamgeukia Eunice, "nitakubali adhabu yeyote tukirudi nyumbani. Naomba nikuweke rehani ili tuondoke na watu wetu" aliongea Fahad. Eunice akatikisa kichwa, Fahad akageuka mbele na kuongea "hakikisha unawakusanya wote, ikiwa watanambia kuna hata mmoja anakosekana. Hii ndio itakuwa siku yako mwisho kuiona ngome yako nzuri" aliongea Fahad.

Mfalme Damesh akaramba midomo yake kumuangalia Eunice aliekuwa nyuma ya Fahad. "Sasa tunakuja kwenye sheria ya pili,"

"Kabla hatujaendelea, ili tusipoteze muda zaidi" Aliongea Fahad na kusimama, akavua joho lake na kumkabidhi master Ge. Akapanda katoka ulingo, "chagua wapambanaji watano mashuhuri, akiwemo mfalme wako. Wote hao nitapambana nao mimi. Nasisitiza usiniletee wadudu hapa uwanjani" aliongea kwa kujiamini.

"Mfalme Fey una uhakika na ulichokisema. Kwa jinsi ninavyokuona, ndio kwanza uko DAN ya kwanza. Wapiganaji wetu wa juu zaidi wako DAN ya nne na mfalme wetu yupo LIN DAN ya kwanza" aliongea Ganji.
"Kwangu hilo halina maana, leta hizo kafara hapa juu" aliongea Fahad kwa nguvu kiasi cha kufanya uwanja mzima usikie alichokiongea.

Ganji akatabasamu na kuinuwa mkono juu, wakapanda watu wa nne ulingoni. Wote walikuwa majenerali katika ngome hiyo.

"Mtakuja mmoja mmoja au munataka muje wote kwa wakati mmoja" aliongea Fahad.
Wakaangaliana kisha mmoja wao akasogea mbele, "mimi naitwa jenerali Fu Shu, Dan ya nne. Nitakuwa mpinzani wako katika mzunguko wa kwanza" aliongea.

"Nafurahi kukujuwa, jina langu unalifahamu na wala sijui niko Dan ya ngapi kwasababu hina maana kwangu. Unaonekana mtu mzuri sana, tungekutana katika mazingira mengine labda tungekuwa marafiki" aliongea Fahad.

"Kabla ya kuendelea ningependa kujuwa kama unatumia silaha yeyote" aliongea jenerali Fu Shu. "Nina shoka, sijisikii kuitumia. Lakini wewe unaruhusiwa kutumia silaha unayojisikia huenda ukanifanya nitake kutumia shoka yangu" alijibu.

Jenerali Fu Shu akaonesha alama ya kushukuru kisha akainyanyua silaha yake. Ulikuwa mkuki mrefu wenye zaidi ya mita moja na nusu. Juu ulikuwa na kichwa chenye ncha kali kilichokuwa na rangi ya dhahabu na shingoni ulifungwa kitambaa chekundu. Akauzungusha mara kadhaa kisha akautoga chini na kusababisha shimo dogo. "Nitapambana kwa uwezo wangu wote, na naomba na wewe ufanye hivyo" aliongea. "Nitfanya hivyo" alijibu Fahad.

Fu Shu aliuzungusha mkuki wake kwa kasi kiasi cha kufanya uonekane kama duara tu. Hauonekani mwanzo wala mwisho, bila hata taarifa akamvaa Fahad kwa kasi. Fahad akakwepa shambulio hilo, Fu Shu aliendelea kufanya mashambulizi ya kasi. Na Fahad aliendelea kuyakwepa pasi na kuonesha tabu yeyote ile.

"Nilikuwa na dukuduku ila sasa nimethibitisha" aliongea Fahad akiangalia nguo yake ya juu. Ilikuwa imechanika lakini wala hakuguswa na mkuki huwo. "Sijui unamaanisha nini" alionge Fu Shu. "Unatumia silaha ya hatari sana ila hujui kuitumia ipasavyo. Ikiwa uko tayari kuwa mfuasi wangu, nitakuonyesha njia sahihi ya kuutumia huwo mkuki" aliongea Fahad.

"Nashukuru kwa ofa yako ila hapana, katika ngome hii mimi ndio mtu pekee mwenye wa uwezo wa juu zaidi katika kutumia mkuki".
"Shujaa wa kweli, ila bado nahitaji uwe mfuasi wangu. Kwasasa pambano hili limeisha na nitaazima mkuki wako kwa ajili ya mapambano yanayofuata".

Fu Shu kwa kasi akamfata tena mpinzani wake, safari hii Fahad alikusudia kweli kulimaliza mapambano hilo. Akamkwepa na kwa kutumia mkono wake wa kushoto akaudaka mkono wenye mkuki. Akaburuza mkono wake mpaka kifuani. Kwa kutumia sehemu yake ya mbele ya kiganja na kutumia nguvu kidogo akamchapa kibao kikali sana.

Nguvu ya kibao kikamrudisha Fu Shu mita kadhaa kutoka aliposimama. Alipojiangalia mikononi hakuuona mkuki wake. Hakupata hata muda wa kufikiri akajikuta akitupwa nje ya uwanja huwo kutoka katika nguvu ya teke kali sana lilituwa kifuani.

Master Ge akasogea na kuzuia kisha akamlaza mbele ya Eunice, Eunice akamgusa baadhi ya maeneo na kumfanya acheuke damu. "Pumzika" akaongea na kurudi kwenye kiti chake.
"Naomba niazime mkuki wako" aliongea Fahad na kuuzungusha mara kadha.

"Wamekuonea sana, mimi siyo bwana wako ila nitakuamsha" aliongea akiuwangalia mkuki huwo kisha akachana kile kitambaa chekundu kilichofungwa karibu na ncha. Kwenye shingo ya kichwa cha mkuki huwo kulikuwa na vishimo viwili. "Amka Behemoth" aliongea maneno hayo na kuanza kuuzungusha kwa kasi sana.

Msuguano kati ya kichwa cha mkuki huwo na upepo ulisababisha uonekana kama unatoa moto. Fahad akaugonga chini kwa nguvu katika kitako chako na kisababisha tetemeko dogo la ardhi.
Kichwa kilikuwa kama kipande cha mkaa kilichoshika moto kweli kweli. "Njooni nyote sina muda wa kupoteza" aliongea na kuwanyooshe mkuki.

Wale majenerali watatu waliobaki wakamzunguka na kuanza kufanya mashambulizi ya kasi lakini hayakuzaa matunda. Ni kama alikuwa akijuwa kabisa watafanya nini. Baada ya dakika tano wote wakatupwa nje ya uwanja wakiwa na majeraha makubwa sana.

"Damesh nakusubiri hapa nimeshamaliza maandilizi" aliongea na kugeuka. Akaenda mpaka katika kingo za uwanja huwo na kumrushia Fu Shu mkuki wake. "Unatumia silaha nzuri lakini huitendei haki", Jenerali Fu Shu akaudaka kisha akainamisha kichwa kuasheria heshima.

Fahad akarudi katikati ya ulingo na kusimama, mfalme Damesh akavua joho lake na kupanda uwanjani taratibu. "Nioneshe mpambano mzuri" aliongea na kukutanisha mikono yake. "Usijali na baada ya leo hutawezaa tena kupambana" Alijibu na kupeleka mkono wake nyuma, akaishila shoka yake na kuichomoa katika pochi.

"Kama unadhani alivyokuwa akipigana na wewe alikuwa akitumia uwezo wake wote, angalia kwa makini utafahamu kama usingeweza kusimama hata sekunde kumi kama angefanya hivyo" aliongea Master Ge akimuangalia jenerali Fu Shu.

Mfalme Damesh akachomoa visu viwili vyenye urefu wa sentimita kana arobaini hivi. Katika mipini ya visu hivyo kulikuwa na vito vilivyokuwa vinang'aa.

Fahad akavuta pumzi ndefu na kuvua nguo yake ya juu, alihisi inambana sana. Akafunga macho yake kwa sekunde kadhaa. Alipoyafunguwa mboni zake zilikuwa zinezungukwa na maduara mawili nje yakisindikizwa na vidoti kadha. Akatabasamu, mwili wake ukaanza kutoa harufu ya damu. "Natamani sana kukuuwa lakini kwa leo nitakukata mikono na kukutofoa macho" aliongea na kufyetuka kwa kasi ya ajabu, mfalme Damesh alikuta katika wakati mgumu mno.

Kasi ya Fahad ilikuwa kubwa kiasi cha kumfanya atambue shambulio linakuja wapi. Alipokuja kushoto, alishambulia kutoka kulia na alipokuja kulia alishambulia kutoka kushoto. Mapigo yake hayakuwa na ramani maalum, Mfalme Damesho alopotegemea linakuja shambulio, lilikuja kinyume na matarajio yake. Kwa dakika mfalme akawa katika ulinzi tu pasi na kufanya mashambulizi.

Fahad akaacha kushambulia na kurudi nyuma kidogo, akatanuwa miguu na kubonyea. "Njoo" akaongea kwa nguvu, mfalme Damesh akachukuwa nafasi kurudisha mashambulizi. Mfalme Damesh alijitahidi kufanya mashambulizi ya kasi na yenye nguvu lakini hayakuzaa matunda. Fahad hakusogea hata hatuwa moja kutoka aliposimama, mishipa yale ya damu ilivimba na kuonekana vilivyo. Ilisafirisha damu kwa kasi sana, ilionekana ikitweta mithili ya mapigo ya moyo.

Mfalme Damesh baada kufanya mashambuliz kwa muda mrefu akarudi nyuma ili avute pumzi. Aliposimama tu akahisi kitu kikali kikipita begani kwake, kikifuatiwa na kitu cha moto. "Kosa ulilofanya ni kumuangalia kwa uchu mke wangu, hilo ni kwanza. Kosa la pili ni kumgusa na mikono yako michafu" alisikia sauti ya Fahad ikitokea nyuma yake.

Akageuka kwa kasi kumuangalia, "unaangalia wapi" Akasikia tena sauti, na wakati huwo huwo akahisi tena kitu kikali kikipita katika mkono wake ulobaki. Kikafuatiwa na umaji maji wa moto. Baada ga Fahad akarudi nyuma, macho yalikuwa mekundu huku michirizi ya damu ikitengeza njia mashavuni.

Akarudisha shoka yake kwenye pochi, na kusimama. "Angalia ngome yako kwa mara ya mwisho" aliongea huku akimsogelea. "Nimekubali ku.." hakumaliza kuongea akapiga kelele kutokana na maumivu aliyoyapata baada vidole vya Fahad kuzama machoni mwake.

Kisha akawageukia wanancho wa ngome hiyo na kuacha tabasamu, halikuwa la furaha bali lilionesha kiu ya damu "hivi ndivyo nitamfanya mtu yeyote yule atakaecheza na kilicho changu. Najuwa hapa kuna wajumbe wa ngome nyingine, pelekeni taarifa kwa mabwana zenu. Kugusa ngone yangu ni mwiko, na sio tu nyinyi hata hao mnaowaabudu, wakinigusa watahisi hasira yangu".

Akashuka uwanjani hapo, Master Ge akamfika na kumivika joho lake pamoja na taji la kifalme. "Ganji, sina mud wa kupoteza. Nipatie watu wangu niondoke" aliongea akimuangalia. "Hayo ndiyo yalikuwa makubaliano yetu, wati wako wote wako nje ya ngome hii.

Utawakuta hapo na ni matumaini yangu, hakutakuwa na ugomvi kati yetu huko mbeleni" aliongea kwa sauti ndogo. Fahad akamuangalia kisha akamsogelea na kumnong'oneza "siku jingine utafute mtu mwenye akili ili ajifanye mfalme, mfalme Damesh. Siyo yule mpuuzi, hili litabaki kati yetu", kisha akaondoka.
 
Attachments

  • _cbea0a0f-39f8-4d58-bb62-0bfb9f9573eb.jpeg
    _cbea0a0f-39f8-4d58-bb62-0bfb9f9573eb.jpeg
    266 KB · Views: 42
"Nambie ukweli" alimnong'oneza sikioni, ujasiri wote wa Eunice ukavuka. Macho yake yakajaa machozi. Akamgeukia Fahad na kumkumbatia kwa nguvu. Akaangusha kilio kizito, Fahad kumuona Eunice katika hali hiyo moyo wake ukaanza kufukuta. Hasira ikaanza kumpanda, "wamenidhalilisha" aliongea Eunice kwa sauti ya kilio na kwikwi juu. "Wamenitesa sana na mfalme wao ametaka kuniingilia kwa nguvu" aliendelea kumwaga kilio.

"Lia, usizuie machozi. Sura yako haifai kuwa na huzuni" aliongea Fahad. "Unaweza ukawa malkia mbele ya macho yao lakini kwangu wewe ni mwanamke tu. Na ulisema huu ugomvu haunihusu, ila kosa walilofanya ni kumdhalilisha mwanamke nimpendae. Na hilo litawagharimu tawala yao nzima.

Eunice alilia kifuani kwa Fahad mpaka usingizi ukamchukuwa. Akamlaza kitandani na yeye akajilaza pembeni. Usingizi mzito ukamchukuwa kutokana kuchoka maana alitumia uwezo wake wote katika kudhidhibiti hasira zake.

Alikuja kushtuka baada ya miale kumpiga usoni, alihisi kifua chake kizito. Akainuwa kichwa na kuangalia nini kinasababisha uzito. Akamuona Eunice akiwa amelala fofofo, "ama uliumbwa uje kuukamata moyo wangu" alijisemea na kurudisha kichwa chini.

Hakutaka kumuamsha, aliamini kabisa mwanamke huyo hakuweza kulala vizuri baada ya mambo yote kutokea. Baada takriban saa nzima Eunice akaamka.

"Umelalaje" aliuliza Fahad, Eunice akamuangalia usoni kwa aibu kisha akashuka kitandani kukimbilia katika chumba cha kubadilishia nguo. Fahad akateremka na kutoka chumbani humo. Akasimama nje na kushusha pumzi, baada ya nusu saa Eunice akatoka.

"Ahsante, nimelala vizuri" alijibu.
"Nafurahi kusikia hivyo"

Wakaelekea kumuona Master Ge ambae alikuwa yupo katika safari yake kuponya jeraha. "Unaendeleaje" aliuliza Fahad. "Naendelea vizuri, Dantian yangu ya kifua imepona kabisa" alijibu. "Endelea kutuliza akili, hakikisha Qi inatembea vizuri. Usijaribu kunyonya DOQi kutoka katika mazingira mpaka utakapopona kabisa" aliongea Fahad.

"Malkia, naona umerudi katika hali yako ya kawaida. Ulikuwa unanipa wasiwasi sana" aliongea Master Ge. "Fanya haraka upone kuna mambo mawili makubwa nahitaji tujadili" aliongea Fahad. Wakamuacha Master Ge aendelee kupumzika, wao wakatoka nje.

Eunice alikuwa akitembea nyuma ya Fahad, kila walipopita watu walishangaa. Fahad wala hakuelewa walikuwa wakishangaa nini. "Eunice unaweza kunitembeza" alimgeukia na kuongea. "Hakuna shida" alijibu.
Waliitumia siku hiyo kuzunguka maeneo tofauti ya ngome hiyp iliyochakaa. Maeneo mengi ya eneo hilo yalikuwa hayaoti hata majani. Ardhi ilikuwa imekufa kabisa.

"Hali ikiendelea hivi, baada ya muda itabidi muihame ngome na kuitelekeza" aliongea Fahad wakiwa njiani kurudi katika mji mkuu wa ngome hiyo. "Hatuna jinsi, na hata tukitoka hapa. Hatuna pa kwenda, hakuna ngome itakayokubali wananchi wa ngome ya ASURA".

"Kwani ilikuwaje mpaka hali ikawa hivi" aliuliza.
"Ni hadithi ndefu nitakuhadithia tukifika nyumbani". Safari ikaendelea kwa ukimya huku mara chache Fahad akiuliza maswali ya hapa na pale.

Walifika mji mkuu tayari kiza kilishaanza kuingia. "Karibu nyumbani" aliongea mlinzi na kuinamisha kichwa. "Ahsante" alijibu Eunice na kutangulia.
Chakula kilikuwa tayari mezani, "kwanini unakula umejifungia ndani" aliuliza Fahad. "Ni mila zetu ndio ziko hivi, mtawala lazima ale peke yake au na watu wenye vyeo katika nchi".

"Katika hali ya sasa, unatakiwa ule na watu wako ndio utapata kuwajuwa vizuri. Utapata kufahamu hali zao vizuri" aliongea Fahad. "Hilo litakuwa ni jambo jipya na sidhani kama watu watakubali".
"Niamini utashangaa kitakachotokea", wakaendelea kula. Baada ya chakula, Fahad akamsindikiza Eunice chumbani kwake. "Leo hulali huku" aliuliza Eunice.

"Unataka nilale"
"Ndio, naogopa kulala peke yangu. Zile ndoto mbaya mara zitanirudia".

" Ukiiweka hivyo, siwezi kukuacha peke yako" akafunga mlango na kuingia ndani. Akakaa kitandani, Eunice akaelekea chumba cha kubadilisha nguo. Aliporudi tayari usingizi ulishamchukuwa Fahad. Akapanda kitandani na kujilaza pembeni yake.
**************
 
"Nambie ukweli" alimnong'oneza sikioni, ujasiri wote wa Eunice ukavuka. Macho yake yakajaa machozi. Akamgeukia Fahad na kumkumbatia kwa nguvu. Akaangusha kilio kizito, Fahad kumuona Eunice katika hali hiyo moyo wake ukaanza kufukuta. Hasira ikaanza kumpanda, "wamenidhalilisha" aliongea Eunice kwa sauti ya kilio na kwikwi juu. "Wamenitesa sana na mfalme wao ametaka kuniingilia kwa nguvu" aliendelea kumwaga kilio.

"Lia, usizuie machozi. Sura yako haifai kuwa na huzuni" aliongea Fahad. "Unaweza ukawa malkia mbele ya macho yao lakini kwangu wewe ni mwanamke tu. Na ulisema huu ugomvu haunihusu, ila kosa walilofanya ni kumdhalilisha mwanamke nimpendae. Na hilo litawagharimu tawala yao nzima.

Eunice alilia kifuani kwa Fahad mpaka usingizi ukamchukuwa. Akamlaza kitandani na yeye akajilaza pembeni. Usingizi mzito ukamchukuwa kutokana kuchoka maana alitumia uwezo wake wote katika kudhidhibiti hasira zake.

Alikuja kushtuka baada ya miale kumpiga usoni, alihisi kifua chake kizito. Akainuwa kichwa na kuangalia nini kinasababisha uzito. Akamuona Eunice akiwa amelala fofofo, "ama uliumbwa uje kuukamata moyo wangu" alijisemea na kurudisha kichwa chini.

Hakutaka kumuamsha, aliamini kabisa mwanamke huyo hakuweza kulala vizuri baada ya mambo yote kutokea. Baada takriban saa nzima Eunice akaamka.

"Umelalaje" aliuliza Fahad, Eunice akamuangalia usoni kwa aibu kisha akashuka kitandani kukimbilia katika chumba cha kubadilishia nguo. Fahad akateremka na kutoka chumbani humo. Akasimama nje na kushusha pumzi, baada ya nusu saa Eunice akatoka.

"Ahsante, nimelala vizuri" alijibu.
"Nafurahi kusikia hivyo"

Wakaelekea kumuona Master Ge ambae alikuwa yupo katika safari yake kuponya jeraha. "Unaendeleaje" aliuliza Fahad. "Naendelea vizuri, Dantian yangu ya kifua imepona kabisa" alijibu. "Endelea kutuliza akili, hakikisha Qi inatembea vizuri. Usijaribu kunyonya DOQi kutoka katika mazingira mpaka utakapopona kabisa" aliongea Fahad.

"Malkia, naona umerudi katika hali yako ya kawaida. Ulikuwa unanipa wasiwasi sana" aliongea Master Ge. "Fanya haraka upone kuna mambo mawili makubwa nahitaji tujadili" aliongea Fahad. Wakamuacha Master Ge aendelee kupumzika, wao wakatoka nje.

Eunice alikuwa akitembea nyuma ya Fahad, kila walipopita watu walishangaa. Fahad wala hakuelewa walikuwa wakishangaa nini. "Eunice unaweza kunitembeza" alimgeukia na kuongea. "Hakuna shida" alijibu.
Waliitumia siku hiyo kuzunguka maeneo tofauti ya ngome hiyp iliyochakaa. Maeneo mengi ya eneo hilo yalikuwa hayaoti hata majani. Ardhi ilikuwa imekufa kabisa.

"Hali ikiendelea hivi, baada ya muda itabidi muihame ngome na kuitelekeza" aliongea Fahad wakiwa njiani kurudi katika mji mkuu wa ngome hiyo. "Hatuna jinsi, na hata tukitoka hapa. Hatuna pa kwenda, hakuna ngome itakayokubali wananchi wa ngome ya ASURA".

"Kwani ilikuwaje mpaka hali ikawa hivi" aliuliza.
"Ni hadithi ndefu nitakuhadithia tukifika nyumbani". Safari ikaendelea kwa ukimya huku mara chache Fahad akiuliza maswali ya hapa na pale.

Walifika mji mkuu tayari kiza kilishaanza kuingia. "Karibu nyumbani" aliongea mlinzi na kuinamisha kichwa. "Ahsante" alijibu Eunice na kutangulia.

Chakula kilikuwa tayari mezani, "kwanini unakula umejifungia ndani" aliuliza Fahad. "Ni mila zetu ndio ziko hivi, mtawala lazima ale peke yake au na watu wenye vyeo katika nchi".

"Katika hali ya sasa, unatakiwa ule na watu wako ndio utapata kuwajuwa vizuri. Utapata kufahamu hali zao vizuri" aliongea Fahad. "Hilo litakuwa ni jambo jipya na sidhani kama watu watakubali".
"Niamini utashangaa kitakachotokea", wakaendelea kula. Baada ya chakula, Fahad akamsindikiza Eunice chumbani kwake. "Leo hulali huku" aliuliza Eunice.

"Unataka nilale"
"Ndio, naogopa kulala peke yangu. Zile ndoto mbaya mara zitanirudia".

" Ukiiweka hivyo, siwezi kukuacha peke yako" akafunga mlango na kuingia ndani. Akakaa kitandani, Eunice akaelekea chumba cha kubadilisha nguo. Aliporudi tayari usingizi ulishamchukuwa Fahad. Akapanda kitandani na kujilaza pembeni yake.
**************
 
"Fahad ulinambia kuna mambo mawili muhimu unataka tuongee pindi nitakapopona tu" aliongea Master Ge akijiweka vizuri kitandani.
"Ndio, mwalimu lakini si mawili tena, ni matatu sasa". Eunice alikuwa pembeni akiwaangalia wawili hao wakiongea hata yeye mwenyewe alikuwa na shauku ya kutaka kujuwa mambo aliyotaka kuongea Fahad.
"Haya nakupa masikio yangu yote mawili" aliongea Master Ge.

"La kwanza, najuwa huku munategemea sana martial art katika kila kitu na muna imani pia kwamba kila kitu kinahitahi nishati fulani ya asili ili kukuwe. Ardhi yenu haina rutuba, ni kweli kabisa inaonekana haina uhai. Ila tunaweza kuirutubisha tena ikaweza kuzalisha chakula kitakachowasukuma katika kipindi hiki kigumu mpaka pale mtakpoweza kurudisha uhai katika ardhi hii" aliongea Fahad. Kisha akawaelekeza jinsi ya kutengeza mbolea kupitia vitu vya kawaida kabisa.

"Enhe jambo la pili" aliongea Master aliongea Master Ge.
"La pili, ni kubwa zaidi ya la kwanza na ndio la muhimu zaidi. Linamuhusu malkia wenu, Eunice kuanzia sasa ni malkia wangu" aliongea kwa kuficha kidogo.
"Lakini mtu yeyote anaeingia katika ngome hii, humfanya Eunice kuwa malkia wake kisheria" aliongea Master Ge.

"Sijamaanisha hivyo, ngoja ninyooshe. Eunice ni mwanamke wangu" aliongea macho makavu.
"Eti nini, Fahad kuna mipaka huwezi kuvuka" aliongea Master Ge akionekana kukereka na maneno ya Fahad.

"Narudia tena, sijali kama mi malkia, au tunatoka limwengu mbili tofauti. Eunice ni mwanamke wangu na nina uhakika hana pingamizi juu ya hilo" aliongea na kunyoosha mkono wake upande alio Eunice. Bila hata kufikiria afanye nini, Eunice akainuka na kuingia kwapani kwa Fahad kama kifaranga cha kuku kinachotaka joto kutoka kwa mama ake.

Master Ge hakuwa na la kusema tena, majibu alishayapata. Akatabasamu kidogo na kuongea "inaonekana alishasalimu amri kitambo". "Enhe la tatu ni lipi".
"Malipo" alibadilika ghafla.
"Unakusudia nini"

"Kifo cha Master Pong na Decath hakitaenda bila kulipwa. Kila ninapo kaa nazisikia roho zao zinavyosononeka. Lakini kubwa zaidi inabidi mfalme wao atambuwe kama kumgusa tu mwanamke wangu basi ni sawa na kuposa kifo. Atalipa vilivyo, na neno litafika ulimwenguni kote kuwa, yeyote atakaesogelea ngome Asura ataangamia mikononi mwangu. Mimi sikopeshi, tunamalizana hapo hapo na hiyo ndio mila yangu" alifafanuwa.

"Hapana Fahad hata kama umepokea baraka zote kutoka Asura wa kwanza, hutaweza kupambana na ngome nzima peke yako" aliongea Master Ge. Akaendelea "isitoshe ngome zote huku kusini zipo chini ya usumamizi wa mungu gharika, Mtukufu Masiyo".

"Master Ge, subiri nikwambie kitu. Najuwa nyinyi mnaamini katika miungu tofauti. Na mnaamini pia binaadamu wa kawaida anaweza kupanda mpaka kuwa mungu. Kwangu mimi hilo halipo, naamini katika huu ulimwengu mungu mmoja tu na siwalazimishi nyinyi kuamini hivyo. Ila hao mnaowaita miungu ni wanafiki tu, si chochote bali ni binadamu tu waliokuwa na uwezo kidogo zaidi ya binadamu wengine" alijibu Fahad.

"Sawa kila mtu anaamini katika kile anachoamini lakini huku hao watu ni miungu. Na kupambana nao ni sawa na kututoa kafara sote" alisisitiza Master Ge na kuendelea "kilichotokea hapa ni matokeo ya mtu mmoja tu, alikwenda kinyume na miungu. Matokeo eneo lote hili likapata maafa, mpaka alipokuja mungu Asura akaliweka eneo hili chini yake ndio uhai ukarudi. Hata hivyo miungu hawakulitaka hilo wakaungama, kupambana na Asura. Baada ya vita hiyo alipotea na damu yake ndio angalau inaipa uhai ardhi hii".

"Huwo ni uwongo uliotungwa na kusambazwa na hao wanaojiita miungu ili musiujue ukweli halisi" aliongea Fahad kwa jazaba kidogo. "Una maanisha nini kusema hivyo, huko ni kuchupa mipaka yako kijana" master Ge alionekana kukereka na kauli hiyo.

"Hiyo ni hadithi ndefu na inahitaji kikao kirefu ili muielewe vizuri. Lakini fahamuni tu kwamba mnachokijuwa sicho cha kweli" alijibu Fahad na kusimama.
"Unaenda wapi" aliuliza master Ge, "nina ahadi na baadhi ya watu na huu ni muda tuliopanga kuonana" alojibu. "Sawa, wewe nenda. Mimi nataka kujadili mambo kadhaa na Eunice kisha nitakuja huko nje". Fahad akatikisa kichwa na kutoka.

"Eunice, nini msimamo wako"
"Kuhusiana na Fahad, mimi sina la kusema. Amejihakikisha kuwa anaweza kuwa mume na pia kiongozi bora kwa watu wangu" alijibu bidada huyo.

"Na vipi kuhusiana na kisasi chake, uhafahamu kabisa kufanya ni kukaribisha mauti kwa watu wetu" alionesha wasiwasi wake Master Ge.

"Kuhusiana na hilo itabidi tusubiri tuone mwisho wake" alijibu Eunice. Alionesha kuwa na imani na maamuzi ya Fahad kwa asilimia mia moja.

*********
"Hakikisha unavuta pumzi nyingi, usiiachie mpaka uhisi mapigo ya moyo yanapiga masikioni" alitoa maelekezo Fahad akiwa mbele. "Sawa" wakaitika kwa pamoja na kufanya kama walivyoambiwa.
Master Ge alipotoka akakutana na umati wa watu wakipata mafunzo kutoka kwa Fahad. "Nini kinaendelea" aliuliza akiwa na sintofahamu. "Fahad ameamuwa kuwafundisha wote wanaotaka hatuwa ya kwanza ya ngome ya chuma" alijibu Eunice aliekuwa pembeni akiaangalia mazoezi hayo.

"Fanya mazoezi ili siku nyingine akichukuliwa mtu wako wa karibu usitegee mtu mwingine akufanyie kazi yako" aliongea Fahad kwa nguvu. Motisha ya watu waliokuwa nyuma yake ikapanda, wakaongeza juhudi. Mazoezi yalikuwa makali lakini hakuna alielalamika hata mmoja.

Baada takriban saa mbili hivi, mazoezi ya siku hiyo yakafikia tamati. Fahad akawaruhusu waende kupumzika na kuendelea na majukumu mengine.

"Fahad, njoo tuongee" alisikia sauti ya Master Ge. Wakaondoka eneo hilo na kwenda pembeni wawili peke yao, hata Eunice aliambiwa asubiri.

"Nimefikiria sana, najuwa kufanya hili nitakuwa nakiuka mila na desturi zetu lakini hii ngome kwasasa inahitaji mtu roho ya chuma ili isimame tena. Eunice peke yake hatoweza kufanya hivyo, hivyo basi wiki moja kutoka sasa utafunga ndoa na Eunice. Katika wiki moja hii ya kusubiri, itabidi usome taratibu na mila za kifalme. Kumbuka huku hakuna demokrasia, kauli ya mfalme ndio kauli ya mwisho" aliongea Master Ge.
"Nafirahi kusikia hivyo, na nakuahidi sitakuangusha. Sijui ngome hii huko nyuma ilikuwaje lakini historia itaandikwa upya" alijibu Fahad. Macho yake yalionyesha kusudio lake.

"Na jambo jingine, ukiwa mfalme itabidi utambulishwe kwa jina lako. Jambo ambalo litakuwa ni hatari kwako na familia yako upande wa pili. Hivyo basi na kupa nafasi uchague jina lolote ambalo litakuwa jina lako ukiwa huku. Achana na Black Star, jina lako la ulingoni. Huku unahitaji jina jipya kabisa lenye kufanana na majina ya huku".

"Fey Ge, ndio jina nitakalotumia huku", jibu hilo likamshtuwa sana Master Ge. "Kwanini umeamuwa jina hilo".
"Kila mtu anahitaji mtu wa kumshauri na kumuongoza. Nimekuchaguwa wewe uwe baba yangu nikiwa huku."

Machozi yakatengeza michirizi mashavuni mwa Master Ge. Hayakuwa ya hizuni bali ya furaha. "Ahsante Fahad, sikutegemea hata mara moja katika maisha yangu nitapewa thamani ya kuitwa baba. Hiyo kwangu ni heshima kubwa kuliko hata kuitwa master" aliongea akionesha wazi furaha yake.
*****
 
Wiki moja baadae.
"Kupitia mamlaka niliokabidhiwa na waandamizi wa ngome, namtawadha Fey Ge kuwa mfalme wa tatu wa tawala hii. Anamchukuwa Malkia Eunice kama mtawala msaidizi na malkia wake. Kuanzia sasa nawatangaza wawili hawa kuwa mume na mke" aliongea Master Ge katika sherehe maalumu ilioandaliwa siku hiyo.

Wakiwa katika sherehe hiyo, alifika mtu mmoja kutoka umoja wa ngome zinazoongozwa na miungu kumi na moja. Alifika akiwa na barua iliaondikwa kutoka huko huko, mfalme Fey akaipokea na kumkabidhi mshauri wake mkuu ambae ni master Ge. Akaifunguwa na kuanza kuisoma.

"Hongera kwa mfalme mpya, ni wajibu wetu kukutakia majukumu mema na kukuhabarisha kuwa utapewa miaka kumi ya kujenga ngome yako. Pia utapewa nafasi tatu za upendeleo kuchaguwa unachotaka" barua ikaishia hapo.

Fahad akasimama na kumuangalia yule mjumbe alieleta barua hiyo. "Nenda kawaambia, nahitaji watu wangu wote waliokamatwa na kutumikishwa pasi na kutaka kwao. Hata kama wamekufa, waniletee vitu vyao.

Hilo moja la pili, peleka taarifa kwa yule mpuuzi aliemdhalilisha mke wangu, najuwa unamfahamu. Mwambie ajiandae siku tatu kutoka leo nakuja kumuangamiza.Na la tatu miaka yangu kumi ikiisha waambie waongoze kumi mingine. Na yeyote atakaethubutu kunigusa katika kipindi hicho. Mungu awe na huruma nae, kitakachomkuta atakisimulia popote atakapo kuwa" alimaliza kuongea na kurudi kwenye kiti chake.

Master Ge aliandika mambo yote hayo yaliyosemwa kisha akamkabidhi yule mjumbe. Akapokea na kuondoka, "ahsante mfalme kwa kuwaweka ndugu zetu mbele" wananchi waliokuwa hapo wakapiga magoti huku baadhi machozi yakiwatoka.

"Anadhani yeye ni nani mpaka kuongea kama hivi" aliongea mtu mmoja. "Punguza jazba, haya ni mambo madogo tu. Ila kuhusu wewe itabidi ujipange tu. Unajuwa kabisa kama wakuu, hawatataka kuhusishwa. Wewe jipange kesho kutwa atakuja. Sidhani kama ana uwezo wa kukuzidi" aliongea mtu mwengine.
Mfalme wa kumi na sita, Mfalme Damesh alijulikana kwa kiu yake ya wanawake.

"Ganji, andaa wapambanaji wetu mashuhuri zaidi. Nataka tumuoneshe huyu bwana mdogo kama mimi si saizi yake" aliongea mfalme Damesh. Ganji akatikisa kichwa, baada ya majadiliano ya muda mrefu, hatimae wakafikia makubaliano kuwa kila ngome itaachia raia nusu wa ngome ya Asura. Kufanya kuna hakikisha kuwa wana jambo la kumzuia mfalme huyo mpya asifanye kama anavyotaka.

Miongoni mwa watu watakaoachiwa walikubaliana pia wawemo wapelelezi kutoka ngome hizo. Baada ya kikao hicho, wakaandika barua na kutumwa kwa ngome ya Asura. Fahad alipoisoma barua hiyo akatabasamu kidogo. "Sio mwanzo mbaya, lakini msitegemee kama mtakuwa mumenifunga kamba za mikono".

Akatoka katika chumba hekalu lake na kuita watu wake wote. "Hapa nina habari nzuri na mbaya. Nitaanza na mbaya kisha itafuata nzuri. Mbaya ni kwamba wamekubali kuwaachia nusu ya ndugu zetu, nzuri ya kwanza ni kwamba wamekubali kuongeza miaka kumi katika ile kumi ya mwanzo. Na hivyo kutupa miaka ishirini ya kujiandaa. Na nzuri ya mwisho ni kwamba mfalme wa Urui amejipanga kunikabili".

Kwa taarifa hizo hawakujuwa washangilie au wahuzunike, kila mmoja alionesha furaha kivyake.
Siku tatu baadae, Fahad aliondoka nankikundi kidogo cha watu akiwemo Eunice na master Ge na wengine kumi. Jumla ukawa msafara wa watu kumi na watatu. Walisafiri kwa farasi kwa takriban saa kumi na sita mpaka kumaliza ardhi ya Asura.

Wakasafiri kwa siku tatu mpaka kufika ngome ya Urui. Master Ge akatangulia kutoa taarifa ujio wa mfalme kutoka Asura. Wakapokelewa na mshauri mkuu wa ngome hiyo, bwana Ganji.

"Samahani Master Ge, hapa mbona simuoni mfalme" aliongea Ganji. Kauli hiyo ikawaudhi sana wengine mpaka Eunice. Master Ge yeye ndo alikuwa kafura vibaya sana. "Baba, achana nae huyo mpuuzi anatujaribu" aliongea Fahad akiinuwa mkono kama ishara ya kuwatuliza.

Ganji akawaongoza mpaka katika uwanja wa mapambano. "King Fey Ge amewasili" Ganji akatangaza na watu wote waliokuwepo hapo wakaanza kuzomea. "Tulieni hivyo hivyi, wamepanga kutuchachafya, wanataka wapate sababu ya kuanzisha vita nyingine" aliongea Fahad akitabasamu.

Upande mmoja wa ulingo huwo alikuwepo mfalme wa taifa hilo, mfalme Damesh na upande mwingine ndio alikuwa Fahad na kikosi chake. "Kwasababu hili pambano linapiganwa nyumbani kwety, basi tutatumia sheria za kwetu" aliongea Ganji akiwa katikati ya uwanja huwo. "Ni matumaini yangu mfalme Fey utakubaliana na hilo" aliendelea kuongea na kumuangalia Fahad.

Fahad akatikisa kichwa kuashiria kukubaliana nae. Ganji akaachia tabasamu la kinafiki "umeingia katika mtego wangu" alijisemea mwenyewe.

Mfalme Damesh akapanda ulingoni, "mimi ninachotaka kwa ushindi na malkia wako, uko tayari kumtoa" aliongea kwa nguvu. "Unajuwa thamani ya malkia wangu na uko tayari kutoa jambo lenye thamani kama yeye japo nafahamu hakuna kitu kama hicho" aliongea Fahad na kusimama.

"Hahahah!! Sema unachotaka"
"Ngome yako iwe mtumwa wa ngome yangu. Kila mwezi utalipa ada kwa muda wa miaka ishirini" aliongea Fahad.
"Hilo haliwezekani, sema jingine"

"Kama hilo haliwezekani na wewe huna haki hata ya kumwangalia malkia wangu. Sio tu malkia wangu bali huna haki ya kuwa na mwanamke yeyote yule"

"Unajuwa ngome yangu ina watu wako wanaofanya kazi kama watumwa zaidi ya laki tano. Ukishinda nitawaachia watu wako wote" aliongea mfalme Damesh. Alijulikana kwa kufanya jambo lolote lile ili kumpata mwanamke amtakae.

Fahad akamgeukia Eunice, "nitakubali adhabu yeyote tukirudi nyumbani. Naomba nikuweke rehani ili tuondoke na watu wetu" aliongea Fahad. Eunice akatikisa kichwa, Fahad akageuka mbele na kuongea "hakikisha unawakusanya wote, ikiwa watanambia kuna hata mmoja anakosekana. Hii ndio itakuwa siku yako mwisho kuiona ngome yako nzuri" aliongea Fahad.

Mfalme Damesh akaramba midomo yake kumuangalia Eunice aliekuwa nyuma ya Fahad. "Sasa tunakuja kwenye sheria ya pili, "

"Kabla hatujaendelea, ili tusipoteze muda zaidi" Aliongea Fahad na kusimama, akavua joho lake na kumkabidhi master Ge. Akapanda katoka ulingo, "chagua wapambanaji watano mashuhuri, akiwemo mfalme wako. Wote hao nitapambana nao mimi. Nasisitiza usiniletee wadudu hapa uwanjani" aliongea kwa kujiamini.

"Mfalme Fey una uhakika na ulichokisema. Kwa jinsi ninavyokuona, ndio kwanza uko DAN ya kwanza. Wapiganaji wetu wa juu zaidi wako DAN ya nne na mfalme wetu yupo LIN DAN ya kwanza" aliongea Ganji.
"Kwangu hilo halina maana, leta hizo kafara hapa juu" aliongea Fahad kwa nguvu kiasi cha kufanya uwanja mzima usikie alichokiongea.

Ganji akatabasamu na kuinuwa mkono juu, wakapanda watu wa nne ulingoni. Wote walikuwa majenerali katika ngome hiyo.

"Mtakuja mmoja mmoja au munataka muje wote kwa wakati mmoja" aliongea Fahad.
Wakaangaliana kisha mmoja wao akasogea mbele, "mimi naitwa jenerali Fu Shu, Dan ya nne. Nitakuwa mpinzani wako katika mzunguko wa kwanza" aliongea.

"Nafurahi kukujuwa, jina langu unalifahamu na wala sijui niko Dan ya ngapi kwasababu hina maana kwangu. Unaonekana mtu mzuri sana, tungekutana katika mazingira mengine labda tungekuwa marafiki" aliongea Fahad.

"Kabla ya kuendelea ningependa kujuwa kama unatumia silaha yeyote" aliongea jenerali Fu Shu. "Nina shoka, sijisikii kuitumia. Lakini wewe unaruhusiwa kutumia silaha unayojisikia huenda ukanifanya nitake kutumia shoka yangu" alijibu.

Jenerali Fu Shu akaonesha alama ya kushukuru kisha akainyanyua silaha yake. Ulikuwa mkuki mrefu wenye zaidi ya mita moja na nusu. Juu ulikuwa na kichwa chenye ncha kali kilichokuwa na rangi ya dhahabu na shingoni ulifungwa kitambaa chekundu.

Akauzungusha mara kadhaa kisha akautoga chini na kusababisha shimo dogo. "Nitapambana kwa uwezo wangu wote, na naomba na wewe ufanye hivyo" aliongea. "Nitafanya hivyo" alijibu Fahad.

Fu Shu aliuzungusha mkuki wake kwa kasi kiasi cha kufanya uonekane kama duara tu. Hauonekani mwanzo wala mwisho, bila hata taarifa akamvaa Fahad kwa kasi. Fahad akakwepa shambulio hilo, Fu Shu aliendelea kufanya mashambulizi ya kasi. Na Fahad aliendelea kuyakwepa pasi na kuonesha tabu yeyote ile.

"Nilikuwa na dukuduku ila sasa nimethibitisha" aliongea Fahad akiangalia nguo yake ya juu. Ilikuwa imechanika lakini wala hakuguswa na mkuki huwo. "Sijui unamaanisha nini" alionge Fu Shu. "Unatumia silaha ya hatari sana ila hujui kuitumia ipasavyo. Ikiwa uko tayari kuwa mfuasi wangu, nitakuonyesha njia sahihi ya kuutumia huwo mkuki" aliongea Fahad.

"Nashukuru kwa ofa yako ila hapana, katika ngome hii mimi ndio mtu pekee mwenye wa uwezo wa juu zaidi katika kutumia mkuki".
"Shujaa wa kweli, ila bado nahitaji uwe mfuasi wangu. Kwasasa pambano hili limeisha na nitaazima mkuki wako kwa ajili ya mapambano yanayofuata".

Fu Shu kwa kasi akamfata tena mpinzani wake, safari hii Fahad alikusudia kweli kulimaliza mapambano hilo. Akamkwepa na kwa kutumia mkono wake wa kushoto akaudaka mkono wenye mkuki. Akaburuza mkono wake mpaka kifuani. Kwa kutumia sehemu yake ya mbele ya kiganja na kutumia nguvu kidogo akamchapa kibao kikali sana.

Nguvu ya kibao kikamrudisha Fu Shu mita kadhaa kutoka aliposimama. Alipojiangalia mikononi hakuuona mkuki wake. Hakupata hata muda wa kufikiri akajikuta akitupwa nje ya uwanja huwo kutoka katika nguvu ya teke kali sana lilituwa kifuani.

Master Ge akasogea na kuzuia kisha akamlaza mbele ya Eunice, Eunice akamgusa baadhi ya maeneo na kumfanya acheuke damu. "Pumzika" akaongea na kurudi kwenye kiti chake.

"Naomba niazime mkuki wako" aliongea Fahad na kuuzungusha mara kadha.

"Wamekuonea sana, mimi siyo bwana wako ila nitakuamsha" aliongea akiuwangalia mkuki huwo kisha akachana kile kitambaa chekundu kilichofungwa karibu na ncha. Kwenye shingo ya kichwa cha mkuki huwo kulikuwa na vishimo viwili.

"Amka Behemoth" aliongea maneno hayo na kuanza kuuzungusha kwa kasi sana. Msuguano kati ya kichwa cha mkuki huwo na upepo ulisababisha uonekana kama unatoa moto. Fahad akaugonga chini kwa nguvu katika kitako chako na kisababisha tetemeko dogo la ardhi.

Kichwa kilikuwa kama kipande cha mkaa kilichoshika moto kweli kweli. "Njooni nyote sina muda wa kupoteza" aliongea na kuwanyooshe mkuki. Wale majenerali watatu waliobaki wakamzunguka na kuanza kufanya mashambulizi ya kasi lakini hayakuzaa matunda.

Ni kama alikuwa akijuwa kabisa watafanya nini. Baada ya dakika tano wote wakatupwa nje ya uwanja wakiwa na majeraha makubwa sana.

"Damesh nakusubiri hapa nimeshamaliza maandilizi" aliongea na kugeuka. Akaenda mpaka katika kingo za uwanja huwo na kumrushia Fu Shu mkuki wake. "Unatumia silaha nzuri lakini huitendei haki", Jenerali Fu Shu akaudaka kisha akainamisha kichwa kuasheria heshima.

Fahad akarudi katikati ya ulingo na kusimama, mfalme Damesh akavua joho lake na kupanda uwanjani taratibu. "Nioneshe mpambano mzuri" aliongea na kukutanisha mikono yake. "Usijali na baada ya leo hutawezaa tena kupambana" Alijibu na kupeleka mkono wake nyuma, akaishila shoka yake na kuichomoa katika pochi.

"Kama unadhani alivyokuwa akipigana na wewe alikuwa akitumia uwezo wake wote, angalia kwa makini utafahamu kama usingeweza kusimama hata sekunde kumi kama angefanya hivyo" aliongea Master Ge akimuangalia jenerali Fu Shu.

Mfalme Damesh akachomoa visu viwili vyenye urefu wa sentimita kana arobaini hivi. Katika mipini ya visu hivyo kulikuwa na vito vilivyokuwa vinang'aa.

Fahad akavuta pumzi ndefu na kuvua nguo yake ya juu, alihisi inambana sana. Akafunga macho yake kwa sekunde kadhaa. Alipoyafunguwa mboni zake zilikuwa zinezungukwa na maduara mawili nje yakisindikizwa na vidoti kadha. Akatabasamu, mwili wake ukaanza kutoa harufu ya damu. "Natamani sana kukuuwa lakini kwa leo nitakukata mikono na kukutofoa macho" aliongea na kufyetuka kwa kasi ya ajabu, mfalme Damesh alikuta katika wakati mgumu mno.

Kasi ya Fahad ilikuwa kubwa kiasi cha kumfanya atambue shambulio linakuja wapi. Alipokuja kushoto, alishambulia kutoka kulia na alipokuja kulia alishambulia kutoka kushoto. Mapigo yake hayakuwa na ramani maalum, Mfalme Damesho alopotegemea linakuja shambulio, lilikuja kinyume na matarajio yake. Kwa dakika mfalme akawa katika ulinzi tu pasi na kufanya mashambulizi.

Fahad akaacha kushambulia na kurudi nyuma kidogo, akatanuwa miguu na kubonyea. "Njoo" akaongea kwa nguvu, mfalme Damesh akachukuwa nafasi kurudisha mashambulizi. Mfalme Damesh alijitahidi kufanya mashambulizi ya kasi na yenye nguvu lakini hayakuzaa matunda. Fahad hakusogea hata hatuwa moja kutoka aliposimama, mishipa yale ya damu ilivimba na kuonekana vilivyo. Ilisafirisha damu kwa kasi sana, ilionekana ikitweta mithili ya mapigo ya moyo.

Mfalme Damesh baada kufanya mashambuliz kwa muda mrefu akarudi nyuma ili avute pumzi. Aliposimama tu akahisi kitu kikali kikipita begani kwake, kikifuatiwa na kitu cha moto. "Kosa ulilofanya ni kumuangalia kwa uchu mke wangu, hilo ni kwanza. Kosa la pili ni kumgusa na mikono yako michafu" alisikia sauti ya Fahad ikitokea nyuma yake.

Akageuka kwa kasi kumuangalia, "unaangalia wapi" Akasikia tena sauti, na wakati huwo huwo akahisi tena kitu kikali kikipita katika mkono wake ulobaki. Kikafuatiwa na umaji maji wa moto. Baada ga Fahad akarudi nyuma, macho yalikuwa mekundu huku michirizi ya damu ikitengeza njia mashavuni. Akarudisha shoka yake kwenye pochi, na kusimama.

"Angalia ngome yako kwa mara ya mwisho" aliongea huku akimsogelea. "Nimekubali ku.." hakumaliza kuongea akapiga kelele kutokana na maumivu aliyoyapata baada vidole vya Fahad kuzama machoni mwake.

Kisha akawageukia wanancho wa ngome hiyo na kuacha tabasamu, halikuwa la furaha bali lilionesha kiu ya damu "hivi ndivyo nitamfanya mtu yeyote yule atakaecheza na kilicho changu. Najuwa hapa kuna wajumbe wa ngome nyingine, pelekeni taarifa kwa mabwana zenu. Kugusa ngone yangu ni mwiko, na sio tu nyinyi hata hao mnaowaabudu, wakinigusa watahisi hasira yangu"

Akashuka uwanjani hapo, Master Ge akamfika na kumivika joho lake pamoja na taji la kifalme. "Ganji, sina mud wa kupoteza. Nipatie watu wangu niondoke" aliongea akimuangalia. "Hayo ndiyo yalikuwa makubaliano yetu, wati wako wote wako nje ya ngome hii.

Utawakuta hapo na ni matumaini yangu, hakutakuwa na ugomvi kati yetu huko mbeleni" aliongea kwa sauti ndogo. Fahad akamuangalia kisha akamsogelea na kumnong'oneza "siku jingine utafute mtu mwenye akili ili ajifanye mfalme, mfalme Damesh. Siyo yule mpuuzi, hili litabaki kati yetu", kisha akaondoka.
 
Alipogeuka akakutana jenerali Fu Shu akiwa amepiga goti moja mkuki wake ukiwa mkononi. "Liege, naomba niwe miongoni mwa wafuasi wako" aliongea. "Mfalme, mpaka amekuita hivyo ana maana atakufuata hata katika kifo" aliongea Master Ge.

Fahad akatabasamu na kumuinua, "kuanzia sasa sisi ni ndugu, au kuna shida yeyote Ganji" aliongea na kumgeukia. "Chukulia huyo kama kombe la ushindi wako" alijibu akikunja sura.

"Baba, muache apande farasi wangu. Amechoka sana hataweza kutembea."

"Sawa mfalme" alijibu master Ge.

Wakatoka nje, "asante mfalme wetu, tunapiga magoti mbele yako. Tunaahidi hatutakusaliti, hasa ukituambia tuingie ndani ya shimo la moto tutaingia" wote waliokuwepo nje walipiga magoti na kuongea. Fahad kuwaona jinsi walivyochoka, moyo wake uliuma sana.

"Kuanzia leo muko huru, twendeni nyumbani familia zenu zina wasubiri" aliongea na kupita mbele, akaanza kuongoza njia. Kutokana na watu hao kuchoka sana, na miili yao dhoofu. Safari ya kurudi ilichukuwa wiki tatu mpaka kufika katika ngome yao.

Watu walipopokea taarifa ya mfalme wao kurudi walikusanyika nje ya ngome. "Kama nilivyoahidi, nimerudi nyumbani na wapendwa wetu. Kwa wale ambao wapendwa wao hawatakuwa miongoni mwa hawa. Nawaomba muwe na subiria, hawa ni kutoka ngome moja tu. Kuna wengine tutawapokea kadiri siku zinavyokwenda" aaliongea.

"Ahsante mfalme" walijibu kwa pamoja kisha wakainakisha vichwa, baada ya hapo kila mtu akaanza kutafuta ndugu, jamaa na rafiki katika kundi hilo kubwa la watu laki tano. "Umefanya vyema mume wangu, twende ukapumzike.

Muachie master Ge atashughulika nao kwa sasa" aliongea Eunice akimuangalia Fahad usoni kwa huruma. Kwa wengine alionekana hana shida yeyote lakini ukweli ni kwamba alikuwa akijitahidi tu.

Mwili wake aliuhisi kama jiwe, alikuwa akipata maumivu makali sana. Maumivu hayo yalikuwa katika kila kona ya mwili wake. "Baba nakuachia wewe hapa mimi naenda kupumzika, mtafutie Fu Shu sehemu ya kupumzika kwa usiku huu. Kesho nitaongea nae vizuri" aliongea huku akihisi mwili ukitaka kumsaliti.

Master Ge akaitikia, hata yeye alifahamu hali aliyokuwa nayo kwa wakati huwo ilikuwa si nzuri. Alihitaji muda wa kutosha wankupumzika pamoja kuijaza tena DOQI katika mwili wake. Akawaaga wananchi wake na kuelekea chumbani kwake. Alipoingia tu ndani akaanguka chini na kukohoa damu. "Ngoja nikamwite master Ge" aliongea Eunice na kutaka kutoka lakini akamshika mkono.

"Usiende, kwasasa wanahitaji mfalme asiyeonesha ulegevu hata kidogo. Hii ni hatuwa ya kwanza katika kuijenga tena ngome hii. Wanahitaji kufikiri mfalme wao ni mti mwenye nguvu sana. Wanahitaji kuamini kuwa hata ikitokea hao miungu wakataka kuvamia basi nitawalinda. Kwasasa hawamuhitaji Fahad bali wanamuhitaji mfalme Fey, mtu mwenye nguvu kuliko yeyote yule katika ulimwengu huu" aliongea na kusimama. Akavua nguo zake na kukaa kitandani.

Eunice akamletea shuka na kumfunika kisha akaelekea kumuandalia mazingira ya kuoga. Aliporudi Fahad alikuwa kalegea kabisa. Alikuwa akitokwa na damu masikioni na puani. Akamsaidia mpka kwenye bwawa la maji ya vuguvugu na kumuingiza. Fahad akazinduka, "samahani kwa usumbufu" aliongea na kutabasamu. Aliona kwa jinsi mwanamke huyo alivyokuwa na wasiwasi.

Baada kuoga, akamrudisha chumbani na kumlaza kitandani. Akamfunika shuka, wala haikumchukuwa muda usingizi mzito ukamchukuwa. Eunice akafuta zile damu na kusafisha nguo zote. Kwa Eunice hakutaka mumewe ashughulikiwe na mtu mwengine yeyote isipokuwa yeye wakiwa chumbani. Walikubaliana kuwa atachukuwa majukumu ya mke na si kama malkia.

**********
Miale ya juwa ndio nlosababisha Fahad kufumbuwa macho yake. Akayafikicha kiasi kisha akajikokota na kuinuka. Akakaa kitako na kujinyoosha kidogo, mwili wake ulidata kama kuni zilizokuwa kwenye moto. Akateremka kitandani na kuvaa nguo zilizokuwa zinaning'inia katika sehemu maalum ya kuning'inizia nguo.

Baada ya maandalizi ya kutosha, akatoka nje. "Mfalme ameamka" mtu mmoja akapiga kelele kwa nguvu na kuacha kazi aliyokuwa anafanya. Taarifa hiyo ikasambaa kama moto wa porini. Kila mtu akaacha kazi aliyokuwa anafanya na kukimbilia ilipo chemba ya mfalme. Fahad hata hakujuwa kwanini walikuwa na furaha kiasi hicho. Kama kuonana walionana siku ya nyuma tu.

"Usishangae, umelala kwa siku tatu mfululizo" alisikia sauti ya Eunice ikitokea pembeni yake. "Eti nini, siku tatu mi sijafika muda huwo kwa kulalal" aliongea akiwa kakodoa macho.

Ndani ya dakika chache kundi kubwa la watu lilikuwa limekusanyika mbele yake. Wote kwa pamoja wakapiga goti moja kuinamisha vichwa "uhali gani mfalme" waliongea.

Fahad akainuwa mkono mmoja juu, akawapa ishara ya kusimama. "Asante kwa kunihofia, nafurahi sana" aliongea. Wote waliokuwepo hapo wakatabasamu na kuinuka.

"Unajiskiaje mtukufu mfalme" aliongea Fu Shu akipita mbele ya umati huwo.

"Sasa hivi niko vyema" alijibu na kutabasamu.

"Ukishamaliza kuongea na watu, uje ofisini kwako. Kuna mambo kadhaa inabidi uyajue kabla ya kuendelea na mambo mingine" aliongea Master Ge.

Baada ya kuongea wanangome wake, Fahad akaelekea katika chemba ambayo ndio ofisi yake. Huku aliwakuta mkewa pamoja na master Ge wakimsubiri.

"Kuna jambo gani" aliuliza akikaa katika kiti chake.

"Kuna mambo matatu kwa sasa ambayo yanahitaji masikio yako yote mawili" aliongea Master Ge. Akaendelea "moja unatakiwa uchonge muhuri wako pamoja na kuichora bendera yako. La pili muda wako wa kuwa huku umeisha. Umebakisha siku kumi tu, na la mwisho kabla hujaondoka unatakiwa utimize wajibu wako kama mfalme na mume kwa mkeo. Unatakiwa uache alama ya uwepo wako ilo heshima ya watu isishuke kipindi ambacho hutakuwepo".

"La kwanza na la pili halina shida, hilo la tatu" akamgeuka Eunice. Macho yalipokutana, bidada huyo akageuza macho pembeni.

"Ndani ya hizi siku kumi, nitahakikisha na ratibu muhuri pamoja na bendera. Lakini pua kuna jambo nataka nilifanye, ili nikirudi nisiwe na wananchi wa kawaida. Nitakwenda kufunguwa hekalu la mababu na kila mwananchi atakuwa na haki ya kujifunza martial art. Tutakuwa na ngome yenye wananchi ambao ni wapambanaji".

"Unajuwa ili kuufunguwa mlango, inabidi uweze kupoga ngoma maalum. Mpaka sasa hakuna aliyeweza kuipiga baada ya mfalme wa kwanza" aliongea Master Ge. "Usijali, siku ya kesho, mpaka kilele cha mlima Sumeru kitatikisika kwa sauti ya ngoma ya vita, Alambara" alijibu na kutabsamu.
 
Black Star
*******

Nawahitaji hawa wawili aliongea mtu mmoja akikbabidhi picha yenye watoto wawili wa kike. Nipe taarifa zao zaidi, picha tu haitoshi aliongea alieipokea picha hiyo. Kadiri unavyojuwa taarifa zao finyu ni heri kwako, maana nikikupa nyingi zitahatarisha maisha yako.

Wewe jua tu ukifanikiwa utaachana na umasikini moja kwa mbili. Nitakupa milioni tatu kama ujira wa kazi yako, moja na nusu saa hivi na iliyobaki utakapokamilisha kazi yangu.

Hakuna shida, nipe siku tatu tu kazi yako itakuwa imekamilika alijibu mtu huyo akipokea bahasha
iliokuwa na pesa ndani na kuiweka katika begi lake la mgongoni kisha akaondoka. Tuone sasa utafanyaje, Abedi.

Bosi katika siku mbili hizi kuna mtu amekuwa akiwafuatilia watoto wa Mwamba aliingia ndani mtu mmoja na kutoa taarfa kwa Victor Smith. Wameanza, endelea kumchunguza tu na wewe. Usije ukafanya chochote kitakacho hatarisha maisha ya watoto wale.

Mwamba si mtu wa kawaida, jambo lolote likitokea kwa watoto wake basi utakiona kiama aliongea Victor na kumruhusu aondoke.

Alipotoka mtu huyo, Victor akatoa simu yake na kuingiza tarakimu kadhaa kisha akapiga na kuweka
sikioni. Habari ya wakati huu Mwamba, wameanza kuwafuatilia watoto wako wale mapacha aliongea baada ya simu hiyo kupokewa.

Ndio, hakuna shida akaitika na kukata simu, sijui unakusudia kufanya nini safari hii lakini nanusa harufu ya kifo alijisemea na kuirudisha simu yake katika mtoto wa meza.

Mzee Abedi a.k.a Mwamba, baada ya kukata simu akairudisha katika mfuko wake wa koti na kushusha pumzi ndefu sana. Ommy, Bahati, safari hii nitakula sahani moja na nyinyi. Mara ya kwanza damu ilikuwa nzito. Wakati huu kama mbwai na iwe mbwai tu hata kama mzee atanilaani huko alipo alijesemea na kurudi ndani kwenye kikao.

************************
 
Fahad alikuwa kasimama mbele ya ngoma kubwa, vigongo vya kupigia ngoma hiyo vilitengezwa kwa mti chuma maalum na kuvifanya viwe vizito kuliko vinavyoonekana. Alambara,ngoma ya vita. Nitakupiga kwa nguvu mpaka ardhi itatikisika.

Watalala walioamka na kuwashtuwa waliojisahau aliongea na kuvishikia vigongo hivyo. Akavuta pumzi nyingi na kukaza misuli, mgongo wake ukazidi kuwa mkubwa na misuli yake ya mwili mzima ikatanuka na kuruhusu damu nyingi isafiri kupita katika mishipa minene iliyotanukwa.

Akaipiga mara ya kwanza, mara ya pili, ya tatu kisha akaanza kuchanganya kuipiga. Aliipiga kwa
nguvu na kasi iliongezeka kadiri muda ulivyokwenda. Wingu zito likatanda, upepo mkali ukaanza kuvuma na ardhi ikaanza kutikisika.

Mvua kali ikaanza kunyesha ikiambatana na radi na ngurumo kali sana. Hilo wala halikumshtuwa Fahad, aliendelea kuiadhibu ngoma hiyo kadiri misuli yake ilivyomruhusu, aliipiga kwa masaa mawili mfululizo bila kupumzika.

Indra akiwa katika kiti chake, alihisi damu kumuenda mbio. Mshenzi mkubwa, amethubutu kuipiga Alambara alijisemea na kukunja ngumi. Heraki, peleka ujumbe kwa miungu yote wakubwa kwa wadogo. Waambie mwezi ukipinduka mara mbili (miezi miwili) tutakuwa na kikao.

Pia tuma wajumbe wetu waende upande wa pili wakawaandae vijana wetu, na peleka ujumbe kwa mlinzi wa bahari saba, Pasyet. Mwamba nyota nyeusi imetujia aliongea kwa hasira. Heraki ambae ni mtu wa mkono wa kulia wa Indra akaitika amri hiyo na kuondoka.

Siamini kama binadamu wa kawaida ameweza kuiadhibu Alambara, ngoma ambayo hata mimi
mwenyewe nimeshindwa kuifanya hivyo aliongea na kusimama. Ndevu zake ndefu zilifika mpaka katikati ya kifua chake.

Kwa kawaida alionekana kama mtu mwenye umri kati ya miaka sabini na thamanini lakini ukweli alikuwa na zaidi ya miaka elfu moja. Hilo pia limewafanya miungu wengine kumheshimu na kumuogopa maana hakuna aliekuwa anajuwa uwezo halisi wa mtu huyo.

Baada ya masaa mawili, Fahad akaacha kupiga ngoma hiyo na kuweka vigongo chini, mwili wake mkubwa ulitoa harufu ya utawala. Kila aliekuwa nyuma yake alilazimika kupiga goti ili kujikabidhi kiakili na kimwili kwa mtu huyo. Akashuka katika mnara uliokuwa umebeba ngoma hiyo na kuelekea katika hekalu la mababu.

Alipokaribia tu mlango ukafunguka, Watu wangu kuanzia kila mtu anaruhusiwa kujifunza martial art. Katika utawala wangu, mwenye atakuwa yule tu ambae atakuwa na uwezo wa kusimama na mimi katika uwanja wa vita.

Si hilo tu, kwa wale ambao hawatakuwa na uwezo wa kujifunza martial art kwa ajili ya kupanda. Kuna aina za martial art zilizobobea katika siasa, tiba, kilimo na mambo mengine ambayo hayahitaji nguvu nyingi bali akili.

Hivyo basi kila mtu atakuwa na uwezo wa kujifunza jambo moja au jingine. Pia ndani ya hekalu hili kuna mto mkubwa unaosafirisha nguvu ya asili. Kama ilivyo mishipa katika mwili wa binadamu, ili kujifunza na kupata mwili na akili nzuri, mtaingia kwa zamu kwa ajili ya kunyonya nguvu hiyo katika miili yenu. Hamtakiwi muwe na haraka, miaka ishirini ya amani ni mingi sana kwa kujiandaa hivyo kila mtu afanye jambo kutokana na uwezo wake na si kuiga kwa mtu mwingine.

Pia kuna wengine ambaoa hawatafanyia mazoezi yao humu, watafanya katika msitu wenye
mtiririko wa Qi chafu. Kazi yao itakuwa ni kunyonya Qi hiyo, na kuisafisha katika miili yao. Na hao watakuwa watu maalum ambao nitawachaguwa mimi na watakuwa chini ya usimamizi wangu binafsi alimaliza kufafanuwa na kuwaruhusu watu waingie. Kila aliingia na kuchaguwa kitabu chenye aina ya martial art yenye kumfaa na wala hawakugombaniana kwa sababu vitabu hivyo viliwachaguwa wao.

Wakati watu wakiendelea na zoezi hilo, Fahad akatoka pamoja na Master Ge, Malkia Eunice na Fu Shu. Baba kuna majina kumi na mbili nitakupa, watu hawa watakwenda katika msitu wenye Qi chafu na kufanyia mazoezi yao huko. Watakuwa huko mpaka pale nitakaporejea kutoka upande wa
pili. Ndani ya miaka miwli wote watajifunza hatuwa ya kwanza na ya pili ya ngome ya chuma.

Baada ya hapo kila mmoja nitamkabidhi kitabu ambacho kitakuwa na martial art atakayojifunza. Watu hawa kumi na mbili watakuwa walinzi wangu binafsi aliongea na kutabasamu. Master Ge akapokea maelezo hayo na kuelekea ofisini kwake. Fu Shu wewe ni miongoni mwa watu hao kumi na mbili, utaanza upya katika safari yako kama mpiganaji aliongea na kumuangalia. Nimesikia na nitatii Fu Shu akaongea na kuinamisha kichwa.

Siku kumi zilikatika kama mchezo, hatimae siku ya kundoka Fahad ikawadia. Mke wangu, mimi naondoka. Sitachukuwa chini ya miaka miwili mpaka kurejea kwangu. Naondoka nikijuwa ngome yangu iko chini ya mikono salama. Kila kitu kitakwenda vyema ikiwa utafata maelekezo niliyokuachia.

Natumai nikirudi maisha ya watu wangu yatakuwa bora kuliko ninavyo yaacha aliongea Fahad akiwa chumbani na Eunice. Usijali kila kitu kitakwenda kama ulivyopanga, nenda kawaoneshe nani mfalme alijibu Malkia eunice na kumkumbatia kwa nguvu. Baada ya kumbatio hilo Fahad akabadili nguo na kuvaa nguo za kawaida.

Akatika chumbani kwake na kuwakuta watu wake wakimsubiri, mpaka wakati huwo wengi hawakufahamu kabisa asili ya mfalme wao. Wengi waliamini anakwenda katika safari ya upweke kwa ajili ya kujiufunza na kuimarisha uwezo wake wa kupambana. Hiyo ilikuwa ni jambo la kawaida kwa watu wengi katika ulimwengu wa Dao.

Wengi walipofikia kiwango fulani cha uwezo waliaga nakuondoka kwa miaka mingi kwa ajili ya kunoa uwezo. Na hivyo ndivyo walivyoambiwa kuwa mfalme wao anakwenda katika safari ya mafunzo ya kiakili na kimwili pamoja na kuimarisha uwezo wake kwa ujumla. Na atachukuwa zaidi ya miaka miwli au mitatu mpaka kukamilisha safari yake.

Aliwaaga na kupanda Farasi wake, watu wake wakamsindikiza kwa macho mpaka alipopotea kabisa
katika upeo wa macho kisha lango kuu la ngome hiyo likafungwa na kutiwa loki kabisa. Katika kipindi chote ambacho hatokuwepo aliagiza mlango huwo ufungwe na usifunguliwe mpaka atakaporudi.

Alitembea kwa farasi kwa muda masaa zaidi ya nane, kisha akamuacha na kumuamuru aende porini. Kuanzia hapo akakimbia, katika kichwa chake ni kama kulikuwa na ramani ya alipotakiwa kuenda ambako kulikuwa na mlango wa siri ulounganisha ulimwengu wa Dao na Dunia. Alipofika tu eneo hilo mwanga mkali ukammeza, mwanga huwo ulisababisha mpaka kuona akawa haoni vizuri.
 
Mwanga ulipopotea tu akakijikuta yupo katikati ya watu wengi, akatulia kwa makini ili kujuwa wapi alipo. Alikuwa pembeni kidogo ya kijiji Naxi katika mji wa mawe wa Baoshanm nchini Uchina. Moja kwa moja akaelekea mpaka katika nyumba aliokuwa anakaa Master Ge na kuchukuwa begi lake, akalifunguwa na kutoa simu kisha akaiwasha. Sekunde chache tu baada ya kuwaka simu yake ikaita.

Don Pizallo akapokea na kuongea, On time, nimetuma vijana wangu wako njiani wanakuja kukuchukuwa. Tunahitaji kufanya maandalizi ya mwisho kabla kushiriki mzunguko wa mtoano utakaofanyika wiki ijayo aliongea. Sawa hakuna shida, watanikuta nawasubiri Beijing alijibu. Waliendelea na mazungumzo kwa dakika kama tano kisha akakata simu na kuirudisha katika begi.

Akabadili nguo na kuvaa nguo za kawaida kisha akaondoka kuelekea Beijing ambako ndipo vijana wa
Don Pizallo watakampokuta.

********************
Salha na Salma walikuwa nje ya geti la shule wakisubiri gari yao ya nyumbani ije kuwachukuwa, dakika tano baadae gari ikafika, wakapanda na kuondoka. Oya, kama hutojali unaweza kutufuata
aliongea mtu mmoja aliekuwa amevaa kapelo kumwambia mtu aliekuwa anasoma gazeti pembeni ya mapacha walioondoka muda si mrefu.

Kwani nyi ni akina nani, achaneni na mimi aliongea akitaka kuondoka, utatufuata au hutufuati alirudia tena. Safari hii alisogeza koti pembeni na kuonesha mdomo wa bastola. Sawa, hakuna shida alipoona kuwa hana ujanja wa kuwachomoka akakubali kufuatana nao huku kichwani akipanga mipango ya kuwachomoka.

Wakati akiwa katika kufikiri huko, akaihisi kitu chenye ncha kali kikizama shingoni, baada ya sekunde chache akapoteza fahamu. Ikafika gari, wakamuingiza na kuondoka nae.

Alikuja kufmbuwa macho akiwa kafungwa kwenye kiti, karibu tena duniani aliongea Victor akikaa kwenye kiti mbele ya mtu huyo. Hapa ni wapi na wewe ni nani aliuliza mtu huyo, tulia kijana, hapa huenda ndio sehemu utakayokufa ukileta ubwege aliongea Victor na kutoa kisu kilichongaa.

Bro, sikia mimi sijawafanyia kosa lolote kwanini mnataka kunifanyia hivyo alilalamika, unajuwa kuongea sana au sio. Ukiendelea kuongea utumbo nitakukuta midomo alifoka Victor. Yule mtu akakaa kimya, maana alipoona macho ya Victor yalikuwa yana kiu ya kuchukuwa roho ya mtu.

Vizuri sasa, tunaweza kuanza. Hapa utatoka sala endapo utanambia nani amekupa kazi aliongea akimuangalia kwa macho yenye uchu wa wa damu. mimi sijui unasema nini, mimi kazi yangu ni kusambaza magazeti na vitu vidogo vidog alijitetea. Nahisi hujanipata vizuri aliongea na kasi akamtoga kisu pajani kisha akakichezesha kama mtu anetia kwenye gari iliyofeli clachi.

Usijali, sijaumiza mshipa wowote mkubwa wa damu, hivyo hutakufa. Ah! Utakufa lakini sio saa hivi aliongea na kurudi kwenye kiti chake. Narudia, nani alokupa kazi ya kuwafuatilia wale watoto, bro mi nasema kweli tena, mimi mbona pale ndio eneo langu la kufanyia kazi.

Sio kama nilikuwa namfuatilia mtu aliongea huku akikunja ndita kutokana na maumivu ya kisu alichochomwa pajani. Victor akatabsamu na kusimama tena, akaingiza vidole pale kwenye jeraha na kuanza kuchokonoa kama vile mtu anaetanuwa mpira. Yule jamaa akapiga kelele kali sana mpaka akapoteza fahamu.

Tutaendelea ukiamka akainuka na kuondoka, moja kwa moja mpaka ofisini kwake. Akakaa kwenye kiti na kutoa simu. Akaingiza tarakimu na kupiga Habari ya saa hizi Mwamba, tunae mkononu lakini anagoma kusema aliemtuma. Hakuna shida, namalizia kikao hapa. Nikitoka nitakuja huko alijibu mzee Abedi na kukata simu. Inaonekana nitaenda kuoga damu akajisemea na kurudi kwenye kikao.

Nusu saa baadae kikao kikafikia mwisho, Mzee Abedi akamuaachia maagizo mkurugenzi wake na kuondoka. Safari yake ilikomea njie ya nyuma nzuri iliyojengwa kisasa. Geti likafunguliwa akaingiza gari ndani na kuiacha sehemu.

Akamkabidhi funguo mlinzi aipeleke kwenye maegesho. Sura yake tu ilionesha kama alikuwa kavurugwa, na alikuwa eneo hilo kishari shari tu. Karibu aliongea Victor, ahsante, nipeleke alipo sina muda wa kupoteza aliongea. Victor akaongoza njia mpaka katika chumba alichokuwa amefungwa yule jamaa.

Kijana sikia, mimi sina muda wa kupoteza. Naomba unambie tu nani amekutuma, japo mimi namfahamu lakini napenda nisikie kutoka katika kinywa chako aliongea mzee Abedi akifunguwa vifungo vya mikononi vya sha lake na kulikunja mpaka kwenye kiwiko.

Mi nimesema sijui mnachotaka kujuwa na wala sijatumwa na mtu. Victor nenda nje na vijana wako, mi napenda sana watoto watundu kama hawa, wanaifanya damu yangu ichemke aliongea. Victor akakusanya vijana wake na kutoka, kitakachotokea saa hivi ni bora msikishuhudie, huyo ndio Mwamba. Walipofika tu nje zikasikika kelele kali sana huku mtu akiomba msamaha.

Baada ya dakika kumi mzee Abedi akatoka akiwa karowa damu mikononi, alikuwa na kifuko kidogo
kilichokuwa na vidole viwili pamoja na meno kadhaa. Akamkabidhi Victor Viweke vizuri hivi, kesho
nitakutumia ujumbe utakaombatana na vidole hivyo kwenda katika anuwani nitakayokupa aliongea. Akasogea kwenye sinki na kunawa mikono kisha akaagana na Victor, akaondoka kama alivyokuja.

Beijing, Uchina
Fahad anashuka kutoka kwenye treni na kupandisha mpaka nje ya kituo, akiwa hapo simu yake inaingia ujume. Akausoma na kuangaza huku na kule mpaka alipoona alichokuwa anatafuta. Kwa mwendo wa taratibu akatembea mpaka ilipo gari nyeusi. Akapokewa begi na kufunguliwa mlango.

Bosi anakusubiri aliongea aliefunguwa mlango. Fahad akatikisa kichwa na kuingia ndani, safari ya
lkuelekea alipo Don Pizallo ikaanza.

Safari haikuwa ndefu sana, baada ya dakika kumi waliwasili nje ya hoteli kubwa ya kisasa zaidi. Gari ikaelekea sehemu ya maegesho na kusimama. Wakashuka na mtu aliekuwa dereva wa gari hiyo akaongoza njia mpaka ndani ya jengo hilo kubwa.

Apofika mapokezi akaonesha kadi ya dhahabu na kupita bila kukaguliwa wala kuulizwa jambo. Waliingia kwenye lift, ikaanza kupanda. Baada ya muda kidogo ikasimama na mlango ukafunguka.
Yule mtu akaongoza njia mpaka kwenye lifti nyingine, akatumia ile kadi ya dhahabu na kuipitisha katika kifaa maalum cha lifti hiyo.

Mlango ukafunguka, wakaingia na kuzidi kupanda juu. Mpaka wakati huwo hakuna jambo lililomshangaza Fahad. Alifahamu kabisa kuwa watu walikuwa na utahiri mkubwa sana. Baada ya dakika mbili, lifti ikasimama na mlango ukafunguka.

Ghorofa hiyo ilikuwa na vyumba vinne tu, kila upande kulikuwa na chumba kimoja. Wakatembea mpaka kwenye mlango wa chumba kimoja. Yule mtu akagonga mlango na kukaa pembeni, Mlango ukafunguliwa na mwanamke mzungu mwenye asili ya kitaliano. Karibu aliongea akisogea pembeni, Fahad akapita ndani na kusimama. Yule bidada akampokea begi na kumuelekeza eneo alilopo Don mwenyewe.

Ahsante alijibu Fahad na kuelekea varanda, ambayo ilitenganishwa na chumba hicho kwa mlango
lwa kioo. Akausukuma na kupita, karibu sauti nzito yenye mikwaruzo ilisikika. Ahsante alijibu Fahad na kuurudisha mlango. Don Pizallo alikuwa amekaa kwenye kiti, mkononi alikuwa siga iliyokuwa ishateketea nusu. Vipi hali yako aliongea Fahad na kukaa kwenye kiti cha pembeni.

Nzuri tu, vipi Master Ge anaendeleaje aliongea Don Pizallo.

Anaendelea Vyema

Nafurahi kusikia hivyo alijibu na kupiga pafu kubwa la sigara kisha akaaendelea kuongea ni
lmatumaini yangu umejiandaa vya kutosha, nikuthadharishe tu kuwa watu utakaokutana nao
lulingoni hawafanani kabisa na watu uliokuwa ukiwanyoosha mitaani. Wengi ni binadamu kwa
lmaumbile tu lakini ni wanyama hatari sana kuliko unavyofikria.

Itakuwa haina raha kama hawatakuwa tofauti na watu wa mtaani, natazamia kubadilishana nao
lufundi alijibu Fahad huku akitabasamu. Tabasamu hilo likapeleka shoti kusafiri katika uti wa
lmgongo wa Don Pizallo.

Alinusa kabisa harufu ya damu kutoka kwa mtu huyo, wamekupa mafunzo gani huko, umekuwa kama mnyama unaesaka damu alijisemea kichwani mwake. Nafarijika kuwa una motisha nzuri kiasi hicho. Na mimi natazamia mapambano mazuri ulingoni, nina imani hutaniangusha aliongea na kupiga pafu nyingine kisha akacheka kidogo.

Kwa Fahad ulingoni kulikuwa ni sehemu ya kunoa uwezo wake wa kupambana ila kwa Don Pizallo ulingo ulikuwa ni sehemu ya kukuza utajiri wake. Kila mmoja alikuwa na lengo lake kichwani, mkataba wa Fahad ulimfunga chini ya mtu huyo kwa miaka mitano.

Baada ya miaka mitano nitakuwa huru kabisa alijisemea Fahad na kushuha pumzi. Sidhani kama utafika miaka mitano, acha nikutumie mpaka pale tamati itakapotukuta alijiwazia Don Pizallo.
*************************
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom