RITA wanalipisha kupata verification code, kwanini wasitengeneze vyeti kama NECTA then wakaweka zile code kama namba ya cheti kama ilivyo namba NECTA

GOSSO MZEKEZEKE

Senior Member
Dec 13, 2013
172
195
Habari WanaJF

Nimekuwa nikijiuliza maswali kwanini kuna zoezi zima la verification codes wakati wa zoezi la ujazaji form za mikopo ya elimu ya juu kulipia?, Kwanini wasitengeze vyeti vya kuzaliwa na kuviingiza kwenye mfumo na ku-print ikiwa na namba zake(namba ambazo zinazotumwa kama verification codes ambazo hutumika kuingiza kwenye mfumo wa bodi ya mikopo).

Hii iwe kama NECTA kwamba ukiingiza hizo namba hizo basi ikuletee infomation zote kama vile unapoomba vyuo ukiingiza namba ya NECTA inavyokuletea matokeo yako, Hiki kitendo cha kulipia kila unapoomba mkopo na kuverify kila mwaka au kila unapohitaji uhakiki ni mimi binafsi naona kama ni njia ya upigaji tu.

Leo ukitaka kuomba mkopo, ukikosa mwaka huu eti mwakani unahitaji kuomba verification tena,. Ushauri wangu ni kwamba vyeti vya kuzaliwa vitengenezwe na kuwa printed na hizo verification codes, halafu RITA waonganishe mfumo wao na mifumo mingine ya taasisi zingine ili kama ikitokea wanataka cheti cha kuzaliwa basi waingize taarifa kwenye mfumo wao iwape maajibu.
 
Sasa
Ni chanzo cha mapato kwa serikali iliyojikita zaidi kwenye tozo zisizo na mpangilio.
Sasa huoni kama inaongeza gharama kwa mwananchi? Lengo la serikali ni kupunguza gharama kwa mwananchi, hii ya kulipa kila mwaka na mbaya zaidi gharama zinaongezeka. Mwaka jana 3000 mwaka huu 6000. Huu ulipaji wa kila mwaka ni kama tozo zilizohalalishwa.
 
ni upigaji uliohalalishwa kama ule wa ku-certify vyeti kwa mwanasheria
 
Sasa

Sasa huoni kama inaongeza gharama kwa mwananchi? Lengo la serikali ni kupunguza gharama kwa mwananchi, hii ya kulipa kila mwaka na mbaya zaidi gharama zinaongezeka. Mwaka jana 3000 mwaka huu 6000. Huu ulipaji wa kila mwaka ni kama tozo zilizohalalishwa.
Ni mzigo kwa mwananchi. Lakini ni nani atatusikiliza wakati wao wamejikita zaidi kwenye ukusanyaji wa kodi pasipo kujali mwananchi anaumiaje?
 
Back
Top Bottom