Kuna scenario kama tatu nimekutana nazo.
1. Mtu kufoji cheti cha kuzaliwa, kila kitu kinaonekana kimetoka RITA, akashinda kesi.
2. RITA kutoa vyeti viwili au vitatu vya kifo kwa marehemu mmoja. Mama mjane anakuja anapewa cheti chake, kaka wa marehemu amepewa cheti chake, na mtoto wa marehemu amekuja amepewa cheti chake. vyeti vyote vinaonekana vimetolewa na RITA (pia through ofisi ya usajili vizazi na vifo Wilaya), na inaleta mgogoro mkubwa sana.
3. Kuna mjane nimekutana naye juzi, alikuwa na cheti cha mazishi alichotumia kuchukua cheti cha kifo, amechukua cheti cha kifo cha mme wake....akakaa miezi kadhaa, akastuka ofisi ileile ya wilaya imetoa cheti kingine cha kifo cha marehemu mke wake, na wanabunya mali, mahakama imeshamteua mtu kuwa msimamizi against his interests kwenye mali zake.
NAOMBA KUULIZA: Hivi, inawezekana ofisi moja, iwe ya RITA au pale kwa Mkuu wa Wilaya, vikatoka vyeti viwili au vitatu vya marehemu mmoja? suala hili limetokea mwaka 2016 hata sio zamani. RITA wewe msajili mkuu wa vizazi na vifo, ndoa etc, hauna data base ambayo kama kifo kilishasajiliwa na kutolewa cheti, hakuna mtu mwingine atakuja kupata cheti cha kifo au ndoa kwa jina hilo? mbona mnachanganya watu, mnafanya nini huko maofisini kama kazi zenu ni kama za watu wasiosoma namna hii?
NATAKA MAJIBU TOKA KWA MTU WA RITA kama yupo hapa. Kwanini haman database kuweza kubaini maombi ya cheti kilichokwisha sajiliwa? Wajane wengi wanakosa haki kwasababu yenu, hivi bado mpo analogy? Hizo computer tunazoziona hapo ni za nini?
Kuna mteja wetu mmoja the same story imetokea huko MAKETE, ofisi ya mkuu wa wilaya Makete wanatoa vyeti vya vifo mara mbilimbili, kuna mjane mmoja wa kikinga amehangaika hadi tumetuma wakili wetu aende kuangalia makete, mbona wazembe sana ninyi? Mkuu wa Wilaya ya Makete upo? unafanya kazi gani hapo?
Ninyi si ndio wawakilishi wa RITA ndio maana mnafungisha hadi ndoa na kutoa vyeti, sasa, mbona mnatoa vyeti vya kifo mara mbilimbili? Mnafanya kazi kienyeji? RITA mnafaida gani sasa kama mnafanya kazi namna hiyo? watu wangapi wamekosa haki kwa kuchanganywa na ofisi yenu?