KERO  RITA badilikeni, toeni majibu ya uhakiki wa vyeti kwa wakati

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Jantisa

Member
Feb 13, 2023
51
47
Habari wadau poleni na utekelezaji wa majukumu ya Kila siku katika harakati za kulijenga taifa

Kero yangu ya leo inatoka kwa mamlaka inayohusika na usajili wa vizazi na vifo Tanzania RITA
RITA wamekuwa Wana makosa yake Yale Kila mwaka yanayojirudia na hivyo kukwamisha baadhi ya watu kupata Haki zao

Mfano suala la kuomba vyeti vya kuzaliwa kwa njia ya mtandao mfumo huwa unafunguka vizuri mteja anajaza Kila kitu mpaka control namba anagenerate na kulipia baada ya hapo anaanza kusubilia kwa muda usiojulikana huduma yake kukamilika naomba kuuliza kama imewezekana kufanya malipo papo kwa hapo inashindikana vipi kupata huduma papo kwa hapo hususani kipindi hichi ambacho serikali inasisitiza matumizi ya tehama katika ofisi za umma.

Kuna mdau mmoja analalamika ameshafanya process zote za kufanya certification ya vyeti RITA kwa ajili ya huduma za kuomba mkopo ila toka alipie ni wiki ya Tatu sasa bado hajapokea majibu yoyote yale na hajui kama cheti kitahakikiwa au la

Naomba mamlaka zinazohusika hususani idara ya tehama wabadilike wafanye Kazi kwa weledi kama inawezekana kupata control Namba za malipo kwa siku moja inashindikana vipi kupata huduma uliyolipia kwa siku hiyo hiyo.

Pia soma
=====

UPDATES; Aug 1, 2024

=====

Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) watolea ufafanuzi madai haya.

Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) umepokea jumla ya maombi uhakiki 143,157 ambapo kati ya hayo, maombi 87,665 sawa na asilimia 61.2 yameshafanyiwa kazi na majibu kutumwa kwa wahusika.

Zaidi, soma;

Madai ya kuchelewesha Vyeti, RITA yasema imepokea maombi 143,157, yaliyofanyiwa kazi ni 61.2%
 
Pesaa kaka pesa jiongeze

Ooooh kaulize kule kwenye I'd zingine
 
Pole mleta mada kama unasubiri majibu ya sms hakuna kama umeshalipia cheti chako angalia kwenye profile utakuta comments pale,approved,pending ama rejected.

Kama ni approved nenda ofisi za rita ulikoomba kuchukulia cheti ukachukue cheti chako.

Cheti kinaprintiwa ndani ya siku moja
 
Kuna Changamoto nyingine ya mfumo wa ku apply mkopo unadai arrangements ya DOD haijakaa sawa so haikupelek next step na cheti kimekua verified na Rita Sasa wao wanataka kikaaje au watu waedit vipi?
Screenshot_20240731-124846~2.jpg
 
Mwisho wa kujaza form za mkopo ni tarehe ngapi?
 
Tunaomba mtupazie sauti , Rita imekua shida tumetuma kuhakiki vyeti vya kuzaliwa na tunaoatiwa control number ya kulipia shiling elfu sita, kama gharama tuanalipa.

Huduma yao imekua haueleweki inachukua wiki mpaka nne hatupati majibu.

Kudhibitisha hili tembelea account yao ya Instagram watu wanalalamika sana wanaomba watumiwe control number walizo fanyia malipo( tembelea account yao post wanayo elekeza namna ya kuomba namba ya verification uone malalamiko almost 1000+ complain).

Tunaomba Mamlaka husika ziingilie jambo hili ukizingatia dirisha la maombi ya mkopo litafungwa tarehe 31 kwa wanafunzi wa vyuo vikuu je Rita wamefanya mawasiliano na bodi ya mikopo kueleza mrundikano wa maombi ya verification ya vyeti?? Au lengo lao ni lipi Rita kua watu wakose mikopo?

Tunaomba mamalak husika iingilie kati Rita imekua kero wanakusanya tozo za verification na hawafanyii kazi kwa wakati.

NB: Hivi vyeti tuna pewa na RITA kwanini Tena tufanye verification?

Chati tunalipia kupata then verification tunalipia tunaomba Mamlaka itazame Rita na ichukulie jambo hili kwa udharura na uharaka sana kuokoa wanafunzi na maombi ya mikopo🙏
 
Tunaomba wahusika kuingilia kati. Nilituma cheti cha kuzaliwa kwenye mfumo tarehe 14 Julai ili kigongwe muhuri wa kukithibitisha kama maagizo ya HESLB yanavyoelekeza lakini mpaka Sasa bado sijarejeshewa ili kuendelea na hatua zinazofuata na tarehe 31 mwezi huu ni mwisho ya kutuma maombi ya hayo Bodi ya MIkopo Elimu ya Juu.

Ukipiga namba yao iliyopo kwenye tovuti yao haipokelewi. Nimeenda ofisi zao wilayani nao wanadai Hali ni hiyo hiyo. Internet cafe wanaotoa huduma za kuwasaidia vijana wanaomba huduma hizo nao wanalalamika juu ya kuchelewesha huduma hiyo. Naomba mamlaka husika kuingilia kati.

Kiongozi wa mamlaka husika Kwa nini asiongeze watendaji wa muda kipindi hiki kwani huduma hii wanakusanya pesa sh 6, 000 kuthibitisha cheti kimoja.
 
Internet cafe Kuna foleni za kusubiria verification hizo. Hivi RITA hawana alternative ya kuongeza kasi hii. Au wamejaa watendaji wazee au vijana wazito?
 
Tunaomba wahusika kuingilia kati. Nilituma cheti cha kuzaliwa kwenye mfumo tarehe 14 Julai ili kigongwe muhuri wa kukithibitisha kama maagizo ya HESLB yanavyoelekeza lakini mpaka Sasa bado sijarejeshewa ili kuendelea na hatua zinazofuata na tarehe 31 mwezi huu ni mwisho ya kutuma maombi ya hayo Bodi ya MIkopo Elimu ya Juu.

Ukipiga namba yao iliyopo kwenye tovuti yao haipokelewi. Nimeenda ofisi zao wilayani nao wanadai Hali ni hiyo hiyo. Internet cafe wanaotoa huduma za kuwasaidia vijana wanaomba huduma hizo nao wanalalamika juu ya kuchelewesha huduma hiyo. Naomba mamlaka husika kuingilia kati.

Kiongozi wa mamlaka husika Kwa nini asiongeze watendaji wa muda kipindi hiki kwani huduma hii wanakusanya pesa sh 6, 000 kuthibitisha cheti kimoja.
Msitoe hii ngoja nimalizie usingizi nije kuwachana Hawa RITA.
 
RITA kuna uozo pale RUSHWA
Rafiki yangu alitaka nakala ya cheti cha kuzaliwa. Alipigwa chenga mpaka alipolazimika kutoa kitu kidogo, akakipata mara moja
 
Nje ya mada kidogo.
Na ww umeenda kuombea internet cafe wakati una smartphone. Ni hatari kweli. Yaani pamoja na somo la ICT kuwa la lazima vyuoni lakini wahitimu wake waliowengi hawajui kutumia smartphone kufanya application
 
Acha kuchafua hoja za watu. Hoja hapa ni uzembe wa RITA.
 
Namba yao 0800117482 haipokelewi. Mwenye namba ya Mtendaji Mkuu aiweke hapa tumsumbue labda ataongeza kasi ya kazi.
 
Mimie nimemuombea mdogo wangu certificate verification toka tarehe 6/7/2024 mpaka muda huu sijapata majibu ukisoma status bado inasoma "New"
 
Back
Top Bottom