Wakuu,
Niliposikia tu kuwa Rais atapokea ripoti ya mchanga wa dhahabu na itarushwa "live" nilijua kuwa ni wazi Ile ripoti ilikuwa na vitu ambavyo yeye (Rais) alitaka kuvisikia. Ni dhahiri alishapewa akaisoma akaona ni bora "auzie sura" ili aonekane anapigania rasilimali zetu ili aurudishe ule "umagufuli" wa miezi mitatu ya mwanzo wa utawala wake.
Sasa nakumbuka hizi kamati zilipishana wiki moja katika kuundwa kwao. Lakini katika nyuzi zangu kuhusu sakata hili nimekuwa nikisisitiza tufuatilie hili suala mpaka mwisho bila kupepesuka maana ndio tutajifunzia hapa.
Sasa tunataka tujue kamati ya wanasheria na wachumi italeta ripoti yake lini? Imefikia wapi? Ni kweli wanakamati wanaendelea na utafiti au wamesharudi mtaani kuendelea na majukumu Yao?
Ninachoomba ni taarifa tu, watuambie kuwa itachukua hata miaka mitatu, tutasubiri tu ila kikubwa ni taarifa tu(kuwa bado ipo na inaendelea na kazi).
Kwa akili za kawaida tu ni kuwa baada ya ripoti ya profesa Mruma, kamati ingeanzia pale pale (kama ACACIA wamedanganya basi huo ni wizi na ni kinyume cha mkataba). Sisi ndio tungeanza kufungua kesi sio ACACIA.
Nahisi tu kuwa ripoti ipo tayari ila haina kile ambacho Bwana Mkubwa anataka kukisikia.
Naruhusu kukosolewa.