beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,880
- 6,365
CAG ameonesha mapungufu yafuatayo katika ulipaji wa mishahara kwa watumishi katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa (MSM);
a) MSM 36 kushindwa kulipa madai mbalimbali ya watumishi yenye thamani ya TZS. 27.84 bilioni
b) MSM 46 kushindwa kuwasilisha makato ya kisheria ya mishahara yenye thamani ya TZS. 5.08 bilioni kwenye taasisi husika (TRA TZS 149.9 millioni, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii TZS 3.92 bilioni, Makato mengine TZS 1.01 bilioni)
Mikopo Iliyopindukia kwa Watumishi bila Kudhibitiwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa 35 kupelekea watumishi 3, 038 kupokea chini ya 1/3 ya mishahara yao huku watumishi 8 katika MSM 6 (H/Jiji Arusha, H/W Kiteto, Njombe, Rombo na Same pamoja na H/Manispaa ya Temeke) hawapati kiasi chochote cha mshahara mwisho wa mwezi.
Kwa kiasi kikubwa makato haya ya watumishi yametokana na ulipaji wa deni la Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu.
Athari:
Kasoro zilizobainishwa zimesababisha athari zifuatazo;
1. Upungufu wa watumishi unaathiri utendaji mzima wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa na kusababisha utoaji duni wa huduma za msingi kama vile elimu, afya na maji salama. Mfano, kuendelea kuwepo kwa vifo vya mama na mtoto chini ya umri wa miaka mitano; kutokufikia uwiano wa mwalimu mmoja kwa wanafunzi 45 kwa shule za msingi (1:45) na kutofikia lengo la kumtua mama ndoo kichwani hadi leo
2. Makato ya mishahara ya watumishi zaidi ya kiwango kilichowekwa cha 1/3 ya mshahara inaathiri utendaji kazi wa watumishi hao ikiwa ni pamoja na kujiingiza kwenye vishawishi na vitendo vya rushwa na ubadhirifu wa rasilimali za umma.
3, Kutokuwasilisha makato ya kisheria ya mishahara ya watumishi katika taasisi husika, ni sawa na kuzikopa fedha hizo ambazo zingetumika kuwekezwa kwa ajili ya mafao ya watumishi. Vilevile, hali hii inawasababishia watumishi usumbufu usio wa lazima unapofika wakati wa kustaafu.
Ushauri:
WAJIBU inashauri yafuatayo yafanyike ili kutatua changamoto zilizooneshwa kwenye ripoti ya CAG;
1. Japokuwa Serikali imeshaanza mchakato wa kutoa ajira kwa mwaka 2020/21, bado kuna uhitaji mkubwa wa kuajiri watumishi hususani kwenye sekta ya afya na elimu. Ofisi ya Rais – TAMISEMI na Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ziendelee kuajiri watumishi wenye sifa ili kujaza nafasi zilizo wazi Serikalini.
2. Halmashauri zilizoshindwa kupeleka makato ya mishahara ya watumishi katika mifuko ya hifadhi za kijamii na TRA, zichukuliwe hatua za kinidhamu kwa mujibu wa Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa 1982 (kama ilivyorekebishwa mwaka 2019) kifungu cha 33 (9)
3. Serikali iendelee kutenga fedha kwa ajili ya kulipa malimbikizo ya madai mbalimbali ya watumishi.
WAJIBU INSTITUTE