RIPOTI: Idadi ya Watu wanaozaliwa Duniani yapungua, Tanzania yafikia watoto 5 kwa mwanamke mmoja

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,516
3,806
Ripoti ya mwaka 2018 iliyotolewa na Benki ya Dunia inaonyesha kila Mwanamke duniani hadi mwaka 2016 anajifungua wastani wa chini ya watoto 2.5

Idadi hiyo ni kama nusu ya ilivyokuwa katikati ya miaka ya 1960 ambapo Mwanamke mmoja alikuwa anajifungua watoto watano

Kiwango cha uzazi kinawakilisha idadi ya watoto ambao watazaliwa na Mwanamke ikiwa ataishi hadi mwisho wa miaka yake ya kuweza kubeba mimba na kuzaa watoto kwa mujibu wa viwango vya uzazi wa mwaka maalum

Katika mataifa yaliyoendelea kiviwanda, ripoti hiyo imeonyesha Mwanamke anazaa watoto wachache kuliko inavyotakiwa duniani huku katika mataifa maskini matokeo ni kinyume

Aidha, katika mataifa 43 wanawake wanakozaa angalau watoto wanne, mataifa 38 ni ya Afrika na kubainishwa kuwa idadi hiyo kubwa ya uzazi inatokana na ukosefu wa elimu na kinga wakati wa ngono

Kwa nchi ya Tanzania ripoti hiyo inaonesha kuwa wastani wa mwanamke mmoja kuzaa katika miaka ya 1960 ilikuwa ni watoto 6.8 ila kwa mwaka 2016 ni watoto watano

3.PNG
 
Nchi ya hiii ya Tanzania ni pumbavu sana. Ilitakiwa iwe na idadi ya watu milinion 30 lakini kwa kupenda mapenzi. Tumejikuta tuna watu wengi wasiokuwa na weledi wala kuweza kuwamudu
 
Nchi ya hiii ya Tanzania ni pumbavu sana. Ilitakiwa iwe na idadi ya watu milinion 30 lakini kwa kupenda mapenzi. Tumejikuta tuna watu wengi wasiokuwa na weledi wala kuweza kuwamudu
Acha uwongo.tanzania tulitakiwa tuwe zaidi ya million 100
 
Back
Top Bottom