Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,042
- 10,779
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete, amewaagiza Maafisa Utumishi wa Halmashauri zote nchini kuacha tabia ya kukaa ofisini badala yake watembelee ofisi za watumishi zilizopo katika Kata na Vijiji ili kutatua changamoto za watumishi.
Aidha, Kikwete amepiga marufuku tabia ya baadhi ya maafisa utumishiukutoa vibali vya kusafiri kwa watumishi kwenda Jijini Dodoma katika Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa ajili ya kufuatilia masuala yao binafsi ya kiutumishi ilihali kazi hiyo ni ya Maafisa Utumishi hao.
"Acheni ile tabia ya kuonekana miungu watu, tatueni matatizo ya watumishi" amesisitiza Mhe. Kikwete.
Amesema watumishi hao hufika Dodoma kwa ajili ya kufuatilia kupandishwa madaraja, kubadilishiwa miundo na kada, kudai malimbikizo ya mshahara, kuwa vitendo hivyo vinawanyima fursa wananchi kuhudumiwa na watumishi hao waliolazimika kusafiri.
Mhe. Kikwete ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Bunda, ikiwa ni siku yake ya tatu ya ziara anayoendelea kufanya mkoani Mara ambapo amewataka Maafisa Utumishi hao kuleta matumaini kwa Watumishi wenzao.
Chanzo: EATV