Dalton elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 307
- 647
Katika hatua muhimu ya kukabiliana na shinikizo la mfumuko wa bei linalotokana na mwenendo wa uchumi duniani, Kamati ya Sera ya Fedha (MPC) imetangaza ongezeko la Kiwango cha Riba ya Benki Kuu (CBR) kutoka asilimia 5.5 hadi asilimia 6.
Uamuzi huu, umefikiwa wakati wa kikao cha MPC kilichofanyika tarehe 3 Aprili 2024 kwa kuzingatia tathmini ya mwelekeo wa uchumi iiliyofanyika mwezi Machi 2024.
Akitoa taarifa ya kamati hiyo katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya Benki Kuu Dar es Salaam mbele ya wakuu wa taasisi za fedha na vyombo vya habari, Gavana wa Benki Kuu, Bw. Emmanuel Tutuba amesema marekebisho ya CBR yatakayotekelezwa kwa robo ya pili ya mwaka huu, yaani Aprili hadi Juni 2024, yamo ndani ya wigo wa asilimia 2 juu na chini.
Hatua hii inaonyesha azma ya benki kuu katika kudumisha utulivu katika mabadiliko ya uchumi.
Tathmini ya MPC kuhusu hali ya uchumi duniani inaonyesha mwelekeo mzuri, huku uchumi wa nchi zilizoendelea na zinazoibukia ukiwa na mwenendo bora.
Akizungumza baada ya kutangazwa kwa CBR, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mabenki Tanzania, Bw. Theobald Sabi, aliipongeza Benki Kuu ya Tanzania kwa kuja na kiwango hicho kinachozingatia mazingira ya sasa hivi.
Pia aliishukuru Benki Kuu ya Tanzania kwa ushirikiano wake inaotoa katika maeneo mbalimbali yenye changamoto katika sekta ya mabenki, likiwemo tatizo la upatikanaji wa fedha za kigeni.