'RI CHUN-HEE' Mtangazaji wa vifo vya viongozi na silaha za Korea Kaskazini

Juma Wage

Member
Sep 8, 2023
88
246
KOREA Kaskazini ni taifa huru baada ya kugawanyika kwa nchi ya Korea mwishoni mwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

Awali eneo lote la Korea lilikuwa koloni la Japan kuanzia mwaka 1910 hadi 1945.

Mwisho wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia, Jeshi la Russia lilivamia eneo hilo upande wa Kaskazini na Wamarekani waliingia kusini, kwa lengo la kuyaondoa majeshi vamizi ya Japan.

Vita baridi ilikuza joto la uadui kwa Korea na kuigawa katika pande mbili, ambapo kila pande ilianzisha serikali kufuatana na itikadi yake.

Russia walisimika serikali ya kikomunisti eneo la Kaskazini na Wamarekani waliimarisha serikali ya kibepari eneo la kusini.

Kiongozi mkomunisti, Kim Il Sung, alishika mamlaka ya kutawala Korea Kaskazini, iliyokuwa ikiongozwa chini ya chama kimoja.

Alipofariki dunia mwaka 1994 mwanaye Kim Jong IL alichukua nafasi yake hadi alipofariki Desemba 17 mwaka 2011 ambapo nafasi hiyo ilichukuliwa tena na mtoto wake Kim Jong Un.

Kim Il Sung aliunda itikadi ya Juche ikiwa na falsafa ya kuendeleza ujamaa.

Taifa hilo limeingia kwenye msuguano mkubwa na Marekani kutokana na mwenendo wake wa kufanya majaribio ya silaha za nyuklia.

Idara ya Ulinzi ya Marekani "Pentagon" inaamini kwamba Korea Kaskazini inamiliki makombora sita aina ya KN-08 ambayo yanaweza kuisambaratisha Marekani.

Novemba 17, 2022 Rais Kim Jong Un, aliutangazia umma kuwa matengenezo ya Kombora lao jipya linaloruka kutoka bara moja hadi jingine yamekamilika na akalifanyia majaribio.

Kwa wenye kumbukumbu au waliokula chumvi nyingi watakumbuka kuwa mpango wa kutengeneza makombora ya kisasa wa Korea Kaskazini ulianza kwa kutengeneza Skadi mwaka 1976.

Ilipofika mwaka 1984, taifa hilo liliyabadilisha jina makombora hayo na kuyaita "Hwasong."

Sio tu, makombora ya masafa marefu, Korea Kaskazini pia ina makombora ya masafa mafupi ambayo yanaweza kulenga taifa jirani la Korea Kusini ambalo uhusiano wao kwa sasa umeanza kuimarika tangu alipoingia madarakani Rais Moon Jae In.

Kombora la " Hwasong 5" na "Hwasong 6" ambayo pia hujulikana kama Skadi B na Skadi C yana uwezo wa kwenda kilomita 300 hadi 500 kwa mujibu wa kituo cha Marekani kinachofanya tafiti za kuzuia kuenea kwa nyuklia.

Silaha hizo za Korea Kaskazini zimekwishajaribiwa na kupelekwa katika maeneo yanayohitajika tayari kwa vita.

Mbali na Skadi kuna aina nyingine ya kombora liitwalo "Nodong" linaloweza kusafiri urefu wa kilomita 1,000 na kumuangamiza adui.

Wachambuzi wa Silaha na Medani za kivita wanasema kwamba makombora hayo yanaweza kupiga maeneo yote ya Korea Kusini na jirani zao Japani.

Katika maonesho ya silaha zake, mwaka 2010 Korea Kaskazini ilionesha kombora hilo linalofika urefu wa kilomita 1,600 ambalo linaweza kupiga kambi kadhaa za Marekani zilizopo katika eneo la
Okinawa.

"Nodong" haikuwa funga kazi, Korea Kaskazini wana kombora lingine liitwalo "Musudan" lililojaribiwa 2016.

Majaribio yanapofanyika, yupo mwanamke mmoja ambaye hutangaza kwa hisia kali huku akitumia lugha iliyojaa maneno ya msisitizo.

Inasadikika kwamba umri wa mtangazaji huyo ni 79, amekuwa akipewa jukumu la kutoa matangazo muhimu ya taifa la Korea Kaskazini.

Mtangazaji huyo hutumiwa kutoa tahadhari kuhusu uovu wa nchi za Magharibi na majaribio ya nyuklia au makombora pindi yanapofanyika.

Jina la mwanamama huyo ni Ri Chun Hee ambaye amewahi kulia, kucheka na kusema kwa sauti kali katika runinga ya taifa la Korea Kaskazini kwa kipindi cha zaidi ya miaka arobaini aliyofanya kazi.

Hupendelea kuvaa vazi la Kikorea la “Chima jeogori” pindi anapotangaza kufanyika kwa jaribio la bomu la Haidrojeni.

Mara zote huonekana amevalia mavazi meusi huku akitekwa na huzuni kali iliyomtoa machozi wakati akitangaza vifo vya viongozi wa Korea Kaskazini.

Inaarifiwa kwamba, Kim Jong Un humtaka awasilishe binafsi ujumbe wa chama chake duniani.

Hadi sasa mwanamama huyo ndiye aliyetangaza vifo vya viongozi wa awali, Kim Il-Sung na Kim Jong-Il.

Februari, 2016, Ri Chun - hee alitangaza kufanikiwa kwa Korea Kaskazini kurusha satelaiti ya kuzunguka dunia kwa kutumia roketi.

Tukio hilo lilishutumiwa kama njama ya kufanyia majaribio ya kombora la masafa marefu.

Pia, huzungumza kama mtu mwenye mamlaka akifikisha ujumbe wa viongozi wa Korea Kaskazini.

Chun Hee huishi Pyongyang na kuonekana kwenye runinga akiwa na watu wengi wanaomtazama, kupiga makofi na wakati mwingine kulia.

Mwaka 2019 alitangaza nia ya kuacha kazi ya utangazaji na kuwapa mafunzo watangazaji wengine wa kike kutangaza habari za taifa.

Chun Hee anadaiwa kutembelea migahawa bora zaidi na vituo vya burudani vya Pyongyang.

Ndimi Juma Wage
Dodoma
Septemba 11, 2023.
 
Ni sawa ila hao waendelee kujitekenya wacheke wenyewe.
Kwa Japan haongeagi sana mpk ifike kwenye mtanange rasmi.
Na Hawalii ni bonda nikubonde.
Hawataji silaha wala nchi adui na hawana hata idea ya kusema nchi gani ni adui yao.
 
Ni sawa ila hao waendelee kujitekenya wacheke wenyewe.
Kwa Japan haongeagi sana mpk ifike kwenye mtanange rasmi.
Na Hawalii ni bonda nikubonde.
Hawataji silaha wala nchi adui na hawana hata idea ya kusema nchi gani ni adui yao.
China ni adui wa japan, Japan kila siku anaweweseka kujihami dhidi ya China hata hao Korea wawili kiasilia hawampendi kabisa Japan.

Historia ya Japan inamfanya asipendwe na majirani zake kutokana na alicho wafanyia wanaliana timing tu siku kikinuka watafanyiana revenge
 
Ni sawa ila hao waendelee kujitekenya wacheke wenyewe.
Kwa Japan haongeagi sana mpk ifike kwenye mtanange rasmi.
Na Hawalii ni bonda nikubonde.
Hawataji silaha wala nchi adui na hawana hata idea ya kusema nchi gani ni adui yao.
Japan hana nguvu kwa sasa alidanganywa na US na ule mkataba wake wa kumlinda akaacha wekeza kwenye silaha ndio maana hata mchina anamnyanyasa siku hizi.
 
Kwanini Japan huwa haionekani kwenye medani za kimataifa ni kama imejificha hivi!!
 
Back
Top Bottom