Rev Msigwa, Karibu CCM ila Usisahau hilli Ni Baada ya Dau Kifikiwa

Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
9,728
10,692
CCM inazidi KUVUNA. Hali tete Chadema.

Ukitafakari sana unaweza kudhani mpinzani halisi ni Luhaga Mpina kumbe Peter Msigwa ndiye CCM kindakindaki. Najua hujaelewa. Iko hivi; ndani ya CCM wanaamini Luhanga Mpina amekuwa mpinzani dhidi ya serikali ya CCM ambayo kimsingi ndiye iliyompa kibali cha kuwa mbunge ndani ya bunge la Tanzania.

Luhanga Mpina ukimsikiliza kwa umakini utaona ni mtu anaewaza kwa uhuru bila msukumo wa kichama. Kwake CHAMA ni bora zaidi kuliko serikali iliyoundwa na CCM, anaamini CCM sio sehemu ya malaika, wapo wahuni pia.

Ndo maana anaamini kuna uongo ambao WAZIRI ameusema bungeni na msimamo wake bado anausimamia.

Hebu angalia maelezo yake; anasema kwanza hajahukumiwa kwa haki, hukumu yake imetolewa kwa jazba na kinyume na haki. Haki ya msingi ilikuwa kusikilizwa, anasema alichohukumiwa nacho hakipo kikatiba, hakipo katika kesi za msingi ambazo alishitakiwa nazo na SPIKA kwa kamati husika. Lakini pia hajahukumiwa kwa kosa la kusema aidha uongo wa kumsingizia Waziri Bashe ama Bodi ya sukari.

Kwa maana nyingine Luhaga Mpina anatueleza kwamba alisema kweli, katika tuhuma zake dhidi ya Waziri wa Kilimo, Bashe anaamini ni za kweli. Hakuna uongo pale hata kidogo lwa maelezo yake, kwamba hoja zote dhidi ya Bashe ni za kweli. Ndo maana hukumu yake haijatokana na kusema Bashe amelidanganya Bunge. Ana hoja ya msingi.

Leo hii, wakati Mpina anasema anaelekea mahakamani kupinga hukumu yake ya kufunguwa vikao 15 vya bunge, anataka akapate ufafanuzi wa kisheria ni kwa namna gani amehukumiwa kinyume na utaratibu ambao Spika aliuelekeza kwa kamati ya Bunge.

Wakati huohuo, aliyekuwa mpinzani halisi nje ya CCM, Mch. Peter Msigwa, aliyekuwa Mbunge wa Iringa mjini na mwenyekiti mstaafu wa kanda ya Nyasa, amehamia CCM. KWANINI?

Madai yake ni kwamba Mbowe (Mwenyekiti wa Chadema Taifa) alitumia nguvu nyingi kumuondoa katika uongozi ikiwemo hila za uchaguzi dhidi yake. Alitoa madai mengi tu yaliyokihusu chama hicho kutumia nguvu nyingi kumuengua yeye na Tundu Lissu.

Kumuondoa Peter Msigwa kanda ya Nyasa ni hatari zaidi kwa chama kama chadema hasa nyakati hizi kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Peter Msigwa ana athari kubwa sana kwa chadema, kura zake za Iringa Mjini tayari zinahamia CCM soon, kwanini? Waliomuunga mkono walimuamini, wanampenda na kumheshimu, ikiwa na wao waliigundua hiyo HILA dhidi yake maana yake CHADEMA imepasuka tayari ukanda huo.

Pale kanda ya kaskazini, God bless Lema ameshajiondoa kwenye uchaguzi wa Kanda ya Kaskazini, hapohapo mkoa wa Arusha ngome ya Chadema kanda ya kaskazini yupo Makonda, unatarajia nini katika uchaguzi ujao? Wananchi wamuangushe Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo mstaafu wa CCM wamsaliti kwa kiwango hiki cha utoaji huduma na haki kwenye jamii?

Kuna mambo nataka kuwakumbusha tu hapa, zile kanuni za Bell; moto kwa vyovyote vile ukiugusa hata kwa bahati mbaya lazima ukuunguze. Moto kwa namna yoyote ile hata mtoto mdogo akiugusa lazima aungue. Moto hauna huruma na chochote kile kwa vyovyote vile utakupa majibu pale pale.

Kile ambacho Peter Msigwa amekifanya kuhamia CCM, na ambacho Luhanga Mpina anakifanya ni karata muhimu kwenye ustawi wa CCM kuliko uharibifu katika chama. Ikumbukwe kwamba Luhanga Mpina kuikosoa serikali ni kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi , maana anaowatetea ni wapiga kura wake waliompelekea Bungeni ambao kimsingi ndo mtaji wa CCM.

Kile ninachokiona katika hii drama ya Mpina kinamuimarisha zaidi Mpina na CCM kuliko utulivu atakaokuwa nao Spika pale jimboni kwake. Nadhani Spika katika hili asipokiwa makini anaweza kuiharibu ngome yake kule jimboni kwake.

Kwa rai yangu, Luhanga Mpina kama CCM itamuunga mkono itakuwa imechukua point zote tatu muhimu kwa wananchi na wapiga kura kuliko ambavyo CCM ikiamua kumuadhibu kwa aidha kumuengua chamani ama baadae katika kura za maoni jimboni kwake. Kwa uhalisia jimbo la Mpina hadi sasa ni la Mpina kwa namna yoyote ile hata akigombea bila kuwa na chama chochote atapita bila kipingamizi. Uzoefu unaonesha Luhanga Mpina ndiye mbunge mwenye kura nyingi zaidi kuliko mbunge yeyote kutoka mkoa wa Simiyu.

Hii sio kwa sababu anapita kwa bahati mbaya, Luhanga Mpina ni mpambanaji wa kweli, msema kweli, na muaminifu. Jimboni kwake wanamuamini na kumheshimu, moja ya sababu za kwanini anaaminika ni kwa sababu anateleleza ahadi zake.

Kwa huu mtaji wa hawa watu wawili niliowagusia hapa ni ishara kwamba CCM imejizolea kura zaidi kuliko Chadema & Co.

Ukipanic, napost tena.
Msigwa karibu CCM lakini usisahau kwamba hili ni baada ya "dau" kufikiwa. Unajua kwanini? Ni kwa sababu uliamini kila anaehamia CCM anahamia baada ya kununuliwa. Leo utaambia nini watu waamini wewe hujafikiwa "DAU", ulisema waliohamia CCM wamehamia baada ya utumbo mpana kukosa "lishe", leo wewe tuko pamoja kuimba nyimbo za "kuupiga mwingi".

Moja ya maswali yangu kwako ni haya yafuatayo;
1. Lini CCM imeacha kununua watu hasa viongozi kutoka vya vya upinzani?

2. Umehamia CCM kwa sababu ni sehemu sahihi ya kuwahudumia wananchi kwa kuwapelekea maendeleo?

3. Umehamia CCM kwa sababu ni chama chenye misingi bora ya utawala bora ama na huku ukikatwa jina utakimbilia CHAUMA?

4.Tukuamini katika Peter Msigwa yupi, yule aliyesema hakuna mtu msafi ndani ya CCM au huyu anaesema ni Peter Msigwa mpya ila aliyeingia katika chama chakavu ambacho hakika kiongozi msafi na kinapaswa kustaafishwa?

5. Uliwagi kusema CCM imechoka na kuiita Chama chakavu ambacho kimastahili kuondolewa madarakani baada ya kuhudumu kwa miaka yote tangu uhuru wa nchi hii na hakuna unafuu wa maisha kwa Mtanzania na hivyo kuhitaji chama mbadala ili watanzania wapate maendeleo stahiki? Je wewe utakuja na agenda zako za kukibadili chama hiki kuwa kipya au utanyamaza ili upate nafasi za upendeleo za uongozi utulie ujiondokee na pensheni za uzee?

Point to note: Huku ndani ya CCM hakuna kupiga sana kelele, huku ukipiga kelele ni kama kutishia kujirusha ghorofani ambako mvua inanyesha, ukitishia unaachwa uanguke wengine wachukue nafasi yako pale juu, huku ni ku-snitch-iana tu. Utazimudu hizi gharama?

Huku huwezi kuonekana hadi uwe CHAWA, wale unaoona wana akili nyingi, huku CCM wamejaa lakini wakiingia tu maofisini, AKILI wanaziacha mlangoni, wanaongeza nguvu ya VIGANJA kwa ajili ya kugonga meza na kupongeza. Mawazo ya mkubwa ni ya kutukuka hata kama utaelekezwa kibla unatakiwa ukubaliane na usubiri HURUMA ya wakubwa unusurike, au usubiri taarifa imfikie akiwa AMESHIBA anaweza kukusamehe.

Kwa kifupi huku tunaishi kwa kuviziana, ukikosea kidogo tu, mwenzako anakufitini unafukuzwa halafu kilaza mwingine anapewa nafasi yako. Usisahau huku hatuna tofauti na watoto waliopo jandoni, ni marufuku kumkosoa mkubwa yoyote yule.

Nakukaribisha Mchungaji Peter Msigwa, karibu sana ila nakuomba sana, ile imani yako ilinde, ikiwa uliamini kutenda haki ni wajibu wako, usijiingize katika mijadala ya nani anafaa au nani hafai, tunajuana, unaoongea nao na watakaokusntch ni haohao. UTATOLEWA nje ya "KEY" kabla ya jogoo kuwika maana wanaamini umekuja kuchukua nafasi ya mtu.

Huku huwa tunaishi na kanuni moja tu, trust nothing, suspect every thing. Ukizubaa umepigwa.

Abdoulquarim Malisa
Mjumbe CCM
KINONDONI
DSM
30 June 2024
 
mbowe amecheza faulo mbaya sana.hata sugu hatashinda uchaguzi hata jimbo la mbeya likigawanywa, na iringa yote hakutakuwa na mbunge wala diwani wa chadema.
 
Asante kwa ujumbe mzuri.
 
CCM kumbe nako kuna watu wenye point eeh? Wewe ni nusu chawa kwa uelewa wangu. Kwa kifupi Msigwa tayari tumemjua n nani? Na alikuwa anatafuta nn Chadema. Ukitaka umaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…