Venus Star
JF-Expert Member
- Dec 6, 2018
- 25,969
- 77,251
UTANGULIZI
Leo wana JF nimependa niweze kuwapa somo la kurejesha kumbukumbu. Nimekuwa nikifanya hivyo kwa muda wa miaka 15 sasa. Kuna baadhi ya kumbukumbu nimeweza kuzirejesha.Somo langu la leo ni kuhusu sisi watu au kuhusu viumbe vilivyo na uhai.
Kwanza kabisa: Sisi watu tunaoishi hapa duniani tupo katika sehemu kuu mbili:-
- Ulimwengu wa Damu na Nyama
- Ulimwengu wa Roho
Na ulimwengu wa Roho umegawanyika katika sehemu kuu mbili:-
- Nafsi
- Roho
ULIMWENGU WA DAMU NA NYAMA
Ulimwengu huu tumekuja kwa Temporary Existence kwa lengo kubwa la Soul browsing sites. Sasa ili nafsi iweze kupata hisia kwenye Ulimwengu wa Damu na Nyama ikatengeneza mwili ambao utakuwa kama medium of communication kati ya Ulimwengu wa Damu na Nyama na Mtu.Ulimwengu wa damu na nyama upo na Elimu yake na Sisi tunajaribu kuuelezea kwa namna ya tunavyouona. Lakini kwa sasa katika somo hili sitaelezea sana kuhusu jambo hili.
ULIMWENGU WA ROHO
Ulimwengu wa Roho ndio maisha yetu yalipo, ndio uhalisia wetu ulipo. Nafsi huwa inaenda kufanya exploration katika existence tofauti tofauti.NAFSI NI NINI
Tunapoongelea Nafsi tunaongelea mambo makuu matatu:- Ufahamu
- Hisia
- Utashi
Na mimi katika mada hii nitaongelea sana kuhusu Ufahamu (Hisia na Utashi) nitaongelea siku nyingine. Maana leo ninataka kufundisha namna ya ku retrieve kumbukumbu zilizohifadhiwa kwenye ufahamu.
KABLA YA KUWEPO HAPA DUNIANI TULIKUWA TUNAISHI
Kama nilivyoeleza hapo awali kuwa hapa katika ulimwengu wa damu na nyama tupo kwaajili ya kupata exposure of Existence na tukimaliza kufanya kazi katika huu ulimwengu tutaenda katika ulimwengu mwingine au tunaweza kurudi katika ulimwengu huu.Kumbukumbu zetu zinakuwa zimehifadhiwa katika ufahamu
KWANINI TUNASHIDWA KUPATA KUMBUKUMBU ZA YALE TULIYOPITIA?
Kwanza tunatakiwa tuelewe. Mtu anapozaliwa hapa duniani tayari anakuwa yupo na Ufahamu,Baadae inapoanza udadisi anakuwa anajifunza vitu mbalimbali. Ili kuwa na total exploration ya Ulimwengu wa Nyama, Nafsi inatengeneza concetration kubwa kwenye ulimwengu huu wa sasa.
Kwahiyo kuna kuwa na nafasi ndogo sana ya kuweza kufuatilia ulimwengu wa roho. Mtoto ataanza kujifunza na kisha kupata Elimu katika mambo mbalimbali. Na elimu hiyo inawekwa kwenye Kumbukumbu ndani ya Nafsi.
Kwa sababu concentration kubwa ipo kwenye ulimwengu wa damu na nyama, mtu huyo baada ya kupata elimu (Education) atapata (Maarifa) Knowledge na baada ya kuitumia hiyo Knowledge -> atapata Skill (Ujuzi). Na baada ya kutumia Skill hiyo kwa muda atakata Experience (Uzoefu) na baada ya kutumia uzoefu huo kwa muda atapata Wisdom (Hekima).
NGOJA NIISHIE HAPO kwa SASA NITAENDELEA.