RC wa Mwanza, John Mongella naye ni Jipu. Litumbuliwe ama lijitumbue lenyewe haraka sana

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,388


Kuna kila dalili za viongozi wa sasa kucopy na kupaste tabia mbaya ya kuhamisha mtu anayevuruga katika eneo moja na kumpeleka eneo jingine. Nimesikitishwa sana na kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kumhamisha RPC na kumpeleka Mbeya eti kwa madai kuwa Mbeya haina Changamoto nyingi kuliko Mwanza. RPC hajaondoka peke yake bali na wasaidizi wake pamoja na Afisa Usalama wa Taifa. Hii ni fedheha kubwa kwa Mongella kwani ulichofanya ni sawa na kuondoa kinyesi chumbani kwako kwa madai kinatoa harufu kali na kukipeleka kwenye sebule ya jirani yako.

Hakika hii ni fedheha kubwa sana na ni aibu kwake. Nani asiyekumbuka jinsi Mbeya ilivyokuwa inakumbwa na matukio kadhaa ya Ujambazi enzi zile tangu Suleiman Kova akiwa RPC na muda mfupi baada ya kuondoka kwake? Nani asiyejua hilo? John Mongella, hivi unajua kwa nini ujambazi na matukio ya kipuuzi kama yale ya kuchuna ngozi watu yalishamiri sana enzi hizo na sasa yamekomeshwa? Kwa nini Mbeya unawapelekea mzoga uliowashinda kula wana Mwanza? Unataka Mbeya waanze kuishi tena kwa hofu ya kuchunwa ngozi?

Rais wangu Magufuli, naona sasa hawa wakuu wako wa Mikoa hasa wale waliokuwepo enzi zile wanaonekana kutaka kukuharibia. Inaonekana ndani yao wana ajenda ya siri ya kutaka kukuharibia ili ionekane haufanyi kazi. Kitendo cha kumhamisha RPC aliyeshindwa kazi Mwanza na kumpeleka Mbeya ni kuendeleza yale yale yaliyokataliwa na wananchi. Nakumbuka kwenye mikutano yako ya kampeni ulilieleza bayana hilo kuwa hutamhamisha mtu anayevuruga kwenye eneo jingine. Inasikitisha sasa kuona baadhi ya viongozi na watendaji wako wameanza kukiuka yale uliyoahidi na uliyoanza kuyatekeleza kwa nguvu zako zote na wananchi tunakuunga mkono.

Kama Mongella una ushahidi kuwa viongozi hao uliowatimua wamechangia kwenye matukio kadhaa ya ujambazi ama wameshindwa kuchukua hatua, suluhisho si kuwahamisha bali washughulikiwe kama wengine wanavyoshuguulikiwa. Sheria ni msumeno. Si wakiguswa watu wa kada nyingine wanashughulikiwa kwa nguvu kubwa ila wakiguswa wa kada nyingine mnawahamisha. Hiyo inajenga double standard ambayo haitakiwi katika utawala huu wa awamu ya tano.

Nawasilisha.
 
Mongella ana uwezo kwa kubadili RPC, au Afisa usalama wa Taifa. Nadhani kuna mamlaka zinahusika, sio RC..Usimsingizie
 
Mongella ana uwezo kwa kubadili RPC, au Afisa usalama wa Taifa. Nadhani kuna mamlaka zinahusika, sio RC..Usimsingizie
Sijamsingizia bali nimeandika mada hii kulingana na taarifa iliyotolewa
 
Mkuu, Mkuu wa Mkoa hana mamlaka kisheria kumhamisha RPC. Mwenye mamlaka hayo ni IGP. Halafu pia hana mamlaka ya kumhamisha afisa yoyote wa Usalama wa Taifa hata awe wa Wilayani.
 
Elimu ya Uraia ni muhimu!!! sasa tangu lini RC akamuamisha RPC, na huko anakompeleka RPC wake atapangiwa na nani...
 
Hujui ulichokiandika!
 
Lizaboni leo umebugi mbaya! kumbe uwezo wako ni propaganda tu! mkuu wa mkoa kuhanisha RPC kwenda mkoa mwingine are you serious?
 
Mleta mada ana hangover ya viroba vya jana. Hii ni dalili kuwa utumbuaji majipu wa mpendwa wetu JPM umewachanganya vijana wa Lumumba sasa hawana pa kushika.

RC na RPC wapi na wapi? Hivi elimu ya uraia hapo Lumumba hampeani. Lakini pia tuliambiwa utumbuaji majipu ukiwa mkali na sisi wananchi tuzidishe maombi kwa raisi wetu. Mtumishi wa umma kuhamishwa ni kawaida kama Kamugisha hataki kwenda Mbeya kama kweli kahamishwa ni aanzisha kampuni yake ya ulinzi tu
 
jamani huyu kamugisha majambazi sijui yanamtafuta nini? hata alivyokuwa shinyanga majambazi yalishamiri kweli, watu waliporwa mali zao mchana kweupe kiduka cha mpesa kikiwa wazi saa moja jioni tayari yameshafika, kahamishiwa mwanza yaleyale watu wanapigwa risasi mchana mchana na majambazi, nahuko mbeya yatamfuata tu.
 
Lizaboni leo umebugi mbaya! kumbe uwezo wako ni propaganda tu! mkuu wa mkoa kuhanisha RPC kwenda mkoa mwingine are you serious?
Hapana Mkuu. Nipo sahihi ka asilimia 100. Aliyetangaza uamuzi huo ni RC John Mongella. Hajasema uhamisho huo umetolewa na nani. Kwa vile yeye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, na kwa kuwa yeye ndiye aliyetutangazia kua wamehamishwa watendaji hao, naamini kuwa uhamisho huo umetokana na maamuzi yake. Hoja ya msingi hapa ni kwamba kama mtu kavuruga eneo moja asihamishiwe eneo jingine. Atumbuliwe hapo hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…