johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 94,157
- 164,595
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda ameibuka, baada ya Tumsime Ngemela kumtaja alipozungumzia tuhuma za kulawitiwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dk Yahya Nawanda.
Tumsime akizungumza na waandishi wa habari jana Julai 5, 2024 jijini Dar es Salaam, alimtuhumu Mtanda kwamba alimshawishi kufuta malalamiko aliyoyafikisha polisi dhidi ya Dk Nawanda.
Mtanda amesema anaviachia vyombo vya ulinzi na usalama kuchunguza tuhuma za yeye kuhusika kwenye sakata hilo.
Mtanda leo Julai 6, 2024 wakati wa hafla ya kutoa zawadi na sifa kwa wakaguzi na askari polisi waliofanya vizuri mwaka 2024, amesema amekuwa na ustahamilivu baada ya kusikia watu wakimsema vibaya mtandaoni.
Huku, akitaja 4R za Rais Samia Suluhu Hassan, Mtanda amesema yeye ni mstahamilivu wa kisiasa hana haja ya kujibu mtu yeyote kwa kuwa anajua tayari vyombo vya usalama vinafanya kazi yake.
“R ya pili resilience (ustahimilivu) wa kisiasa na hata sisi viongozi lazima tuwe wasitahamilivu… jana nilikuwa naona kwenye mitandao watu wanasema maneno ya ajabu, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza lelelelelele…
“Lakini kwa sababu mimi ni mstahamilivu wa kisiasa sina haja ya kujibu mtu yeyote ninachojua vyombo vya kisheria vinafanya kazi yake, Jeshi la Polisi lakini pia mamlaka nyingine zinaendelea na uchunguzi na kuingilia chunguzi hizo ni kuingilia misingi ya utawala bora,” amesema Mtanda.
Ametaka vyombo hivyo vya kiuchunguzi viachwe vitimize wajibu wake bila kuingiliwa ili visichelewe na kukwamishwa kutimiza wajibu wake.
“Hii ni kitu ambayo inaitwa ustahimilivu na sisi viongozi lazima tuwe hivyo, kiongozi wa kisiasa lazima awe na ngozi ngumu siyo unaguswa kidogo unaanza kulialia. Nimekuwa kiongozi nikiwa na miaka 17 nikiwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya leo nina umri mkubwa nimekuwa na experience (uzoefu) ya kutosha kwa hiyo ninao uvumilivu katika masuala ya uongozi na utawala bora,” amesema.
Akizungumza na wanahabari akiwa ofisi za Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Tumsime alidai alipigiwa simu na Mtanda aliyemweleza anahitaji kuonana naye, akamweleza kwamba yupo na polisi.
“Akasema wape simu akaongea nao na kuniamuru wanipeleke ofisini kwake. Tulipofika akawaambia polisi watoke nje, ili tuzungumze wawili, akaniambia kesho nikaifute kesi,” alidai Tumsime.
Alidai baada ya kuzungumza naye aliwaita askari polisi wakaingia ndani na akawaeleza makubaliano yamefikiwa ya kufutwa kesi.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa, Jeshi hilo Julai 5, 2024 lilipokea taarifa za uchunguzi wa vielelezo kuhusu madai ya Dk Nawanda kumlawiti binti huyo, kutoka maabara za uchunguzi wa kisayansi.
Tukio hilo linadaiwa kutokea Juni 2, 2024 saa moja usiku katika eneo la maegesho la moja ya baa mashuhuri jijini Mwanza.
Alidai aliingiliwa kwa nguvu kinyume cha maumbile kwenye gari dogo linalomilikiwa na mtuhumiwa.
Chanzo: Mwananchi
Pia soma
- RC Said Mtanda wa Mwanza hastahili kuwa kiongozi wa umma kwa kutaka kuzima kesi ya Binti Tumsiime anayedai kulawitiwa na Dkt. Nawanda