RC Mbeya kuwawajibisha Viongozi wa Halmashauri zitakazopata Kipindupindu

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,591
8,817
Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Juma Homera ameziagiza halmashauri zote mkoani humo kuzingatia usafi wa mazingira ili kujikinga na ugonjwa wa kipindupindu katika msimu huu wa mvua na eneo ambalo ugonjwa huo utalipuka, viongozi watawajibishwa.

Homera ametoa agizo hilo leo Jumamosi Desemba 31,2023 wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa ikiwa ni siku ya usafi wa mazingira wa mwisho wa mwezi huku akisisitiza jiji limekuwa katika hali mbaya ya uchafu.

“Naagiza maofisa afya, wakurugenzi na wakuu wa wilaya kuhakikisha kila eneo linakuwa safi vinginevyo atachukua hatua kwa ambaye eneo lake litakuwa chafu au kuibuka kwa kipindupindu.” amesema Homera.

Kaimu mkurugenzi wa jiji la Mbeya, Trifonia Kisiga amesema suala la usafi limerejeshwa kwenye ngazi ya kata ambako watendaji wa mitaa hukusanya tozo kwa kushirikiana na wenyeviti wa mitaa .

“Kwa sasa suala la ukusanyaji taka limerejeshwa kwenye ngazi ya kata zikikusanywa kuna utaratibu maalum wa magari kuzipitia kisha kuzipeleka kwenye dampo kuu eneo la Nsalaga nje mji,”amesema.

Ofisa Mazingira wa Jiji, Nimrod Kiporoza amesema wameondoa mfumo wa kutupa taka kwenye maguba ili kupunguza gharama za uendeshaji ambazo zilikuwa zinatolewa na jiji na badala yake wamepata wazabuni ambao wanaziondoa kwa kutumia magari maalumu.

“Kuna utaratibu wa kuondoa taka licha ya kuwepo kwa changamoto ya wananchi kutupa ovyo na kusababisha jiji kuwa katika hali mbaya ya usafi licha ya kutoa elimu ya mara kwa mara,” amesema.

Hivi karibuni, Spika wa Bunge na mbunge Mbeya Mjini, Dk alieleza kusikitishwa kwake kwa hali ya uchafu wa mazingira unaosababishwa na utupaji taka ovyo hali ambayo inahatarisha usalama wa afya za jamii.

Dk Tulia ambaye alishuhudia mrundikano wa taka soko la wafanyabiashara la Sido ambazo zilipelekea kufunga barabara iendayo Kituo cha Mabasi ya Chunya kwenda Mwanjelwa

Mwenyekiti wa wafanyabiashara soko la Sido, Huruma Nsangalufu amesema kuondolewa kwa maguba katika soko hilo kumechangia ongezeko la uchafu na wafanyabishara kuwa hatarini kuugua magonjwa ya matumbo kutokana na mazalio ya nzi.

“Nishauri jiji katika maeneo ya masoko warejesha mfumo wa maguba kwani kwa sasa hali ni mbaya zaidi taka zinatupwa kiholela ni vyema kuchukua tahadhari kabla ya hatari kutokea,” alisema Dk Tulia.

MWANANCHI
 
Back
Top Bottom