Good Father
JF-Expert Member
- Feb 28, 2014
- 10,323
- 18,538
Habari za asubuhi wanabodi.
Leo nitoe ya moyoni kuhusu huyu mkuu wa mkoa wa DSM.
Awali ya yote niweke wazi kwamba mimi ni mtu huru na sifungamani na chama chochote cha siasa hapa Tanzania, ninachoandika hapa ni maoni ya mtanzania wa kawaida tu.
Sina lengo la kumpaisha mtu, sina lengo la kumkejeli RC yeyote wala sitarajii kumkosoa mtu wala chama chake. Kama mtanzania naona natafakari pia ninayo haki ya kutoa maoni.
Niweke wazi kwamba tangu nimepata akili za kutambua mambo sikuwahi kuona RC anayejituma na mbunifu kama RC huyu wa DSM, ni wazi kwamba RCs wengi hukaa ofisini, huvizia mbio za mwenge na kushiriki vikao mbalimbali ambavyo huwanufaisha kwa posho, hii inafahamika, hatukuzoea kuona RC anatumia akili zake kwa kubuni vitu vyenye manufaa kwa jamii au eneo lake la utawala.
RCs walioko madarakani awamu hii wengi wao wamekua na kazi ya kupambana na watu wanaoishi kwenye mapori tengefu na hifadhi za taifa, wengine wamekua wakipambana na wanasiasa wa vyama pinzani (mnawafahamu).
Nirudi kwa RC Makonda; huyu RC ni kijana ambaye naweza kusema alistahili nafasi hiyo na pengine anastahili kua waziri wa wizara hata mambo ya ndani.
RC Makonda ameonesha ubunifu wa hali ya juu, amekua akifanya hivyo kila siku, anabuni miradi na mbinu mbalimbali za kuhakikisha mkoa wake unapata mchango wake wa moja kwa moja.
Nitaje machache tu, juzi kati ametafuta wadhamini wa kugharimia miguu bandia kwa ajili ya walemavu, amebuni mradi wa kujenga ofisi za walimu (hii ni kuboresha mazingira ya utendaji na hatimaye kuboresha taaluma ya wanafunzi mkoa wa DSM), Makonda ameenda mbali amebuni operation ya kuwapima afya wakazi wa DSM bure kabisa.
Hayo ni machache kati ya mambo mengi aliyobuni na anayobuni RC Makonda.
Inawezekana kabisa kwamba wengine mkaona RC Makonda hastahili kupongezwa, mimi nasema huyu jamaa amethubutu kuonesha umma kwamba kiongozi ni VISION sio umri, tuna mikoa isiyopungua 20 Tanzania bara lakini sijaona mkuu wa mkoa anayehangaika kuweka mambo sawa kama Makonda.
Huyu RC alituhumiwa kufoji elimu, nikitazama uwezo wake na tuhuma haviendani, kuna watu walisifiwa kua na elimu nzuri, vyeti safi lakini mbona sioni wakibuni mambo kama RC Makonda? Mbona sioni PhD zao zikitumika popote? Kweli elimu ni nyanja pana.
Ninaamini iko siku Makonda atakua Waziri tena katika wizara nyeti na atachapa kazi sana. (Jf inaishi na huu uzi mtakuja kuusoma yakitimia).
--------------------------------------
--------------------------------------
UPDATES:
Dar: Makonda atangaza neema kwa watumishi
Magari ya polisi aliyokarabati Makonda yanazidi kumpa kiki
Makonda kuweka umeme shule zote za msingi na sekondari jijini Dsm
Najua mtakosoa na kuponda maana sio kila mtu atapenda mawazo yaliyotofauti na mawazo yake.
Nawasilisha.
Amini usiamini, ukihitimu shule ndio utaanza masomo.