RC Makalla: Msako wa mifuko ya plastiki kuanza Jumatatu Agosti 29

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,616
13,301
RC MAKALLA: MSAKO WA MIFUKO YA PLASTIKI KUANZA JUMATATU YA AUGUST 29.

- Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango Ameelekeza msako wa mifuko ya Plastiki ufanyike Mikoa yote.

- Awataka Viongozi wa Masoko yote kutoa tangazo la katazo la uuzaji wa Mifuko hiyo.

- Wenyeviti wa Masoko waahidi kushirikiana na Serikali kwenye Operesheni hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ameelekeza operesheni ya kukamata Mifuko ya plastiki iliyokatazwa kuanza rasmi Jumatatu ya August 29 kwenye Masoko yote ya Mkoa huo.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo wakati wa kikao kazi na Viongozi wa Masoko yote ya Mkoa huo, Machinga na Maafisa Masoko ambapo pia ameelekeza msako wa kukamata Viwanda Bubu vinavyozalisha Mifuko hiyo kuanza Mara moja.

Aidha RC Makalla ameelekeza kila Wilaya kupitia Kamati za Ulinzi na usalama kuendesha Operesheni hiyo ambapo pia amewataka Maafisa Masoko kwa kila soko kutoa taarifa ya mwenendo wa zoezi Hilo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri husika kila siku.

Tayari RC Makalla amepata baraka zote za Operesheni hiyo kutoka kwa Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango ambae ameelekeza kila Mkoa kufanya Operesheni ya kutokomeza na kuzuia uingiaji wa Mifuko hiyo.

Pamoja na hayo RC Makalla ameelekeza Mamlaka za Udhibiti ikiwemo Baraza la usimamizi wa Mazingira NEMC na TBS kutoa tamko la maelekezo ya usimamizi kwa kila Mkoa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha Elimu inaendelea kutolewa.

Itakumbukwa kuwa mnamo tar 01/06/ 2019 Serikali ilitangaza marufuku ya Matumizi ya Mifuko ya plastiki na kufanikiwa lakini hivi karibuni Mifuko hiyo imeanza kurudi kwa Kasi jambo lililopelekea Serikali kutangaza Operesheni ya kutokomeza.

IMG-20220824-WA0014.jpg
IMG-20220824-WA0015.jpg
 
RC MAKALLA: MSAKO WA MIFUKO YA PLASTIKI KUANZA JUMATATU YA AUGUST 29.

- Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango Ameelekeza msako wa mifuko ya Plastiki ufanyike Mikoa yote...
Ajenda hii ni ya kupwa kujaa. Haijawahi kuwa endelevu. Tulishaanza vizuri kulishughulikia suala la plastiki lakini sasa hivi hali imerudi upyaa na sababu zisizo na mashiko kabisa.
Sasa mbona waziri Makamba amesema aliifuta Mifuko ya plastic nchini Tanzania?

Au mimi ndio sielewi
 
Kama tulishindwa jana leo tutaweza?
Ukiangalia ukumbi ulipotolewa tamko hauna shida kimazingira, wangeufanyia pale kwa uwanja wa kwa Mtogole huenda tamko lingekuwa halisi, lenye mashiko na linalohitaji utekelezaji wa dhati na sio hizi bla bla za kuhalalisha posho ya siku kwa waalikwa na mgeni rasmi.
 
Hawa watu wapo nyuma sana japo ni viongozi, hio mifuko iwepo na isizagae hovyo mitaani. Mifuko ya nailoni ni dili kwa wakusanya taka.

Inarudi viwandani watu wanazalishia industrial oil kupitia pyrolysis. Kilo moja ya mifuko chakavu ya plastic ni sh 400 ni wewe tu uwezo wako kukusanya na oda ya tani 300 kwa mwezi kama unaweza kusanya chukua Kazi hio.

Kwa tani moja wananunua kwa sh laki sita.
 
Ishu ya taka za plastic ilikuwa kero back na sio now days. Hata nashangaa TRA bado wamebase na ant dumping principal ya kizamani kweli kweli kabla ya recycling industry haijaja.

Magari machakavu yanakuwa recycled waache maushuru ya kipumbavu kukomoa watu waaingize magari yakichoka yanasagwa chuma chakavu wanapress kama marobota yanarudi tena nje kuzalisha bidhaa.

Kama ilivyo taka za plastic nazo zinafungwa kwenye marobota watu Wana exports nje wanapata utajiri Mkubwa Sana.
 
Waziri recycling industry ya TANZANIA inakua KILA siku wala usiumize kichwa juu ya takataka za plastic, mateja wanafanya Kazi nzuri Sana za kusafisha mji, we cha msingi wape uwezo veta wazalishe mashine za kusaga plastic angalau KILA mtaa zikiwepo zitasaga takataka zote za plastic soko la chenga chenga za plastic zilizosagwa ni unlimited hapa nchini na nje ya nchi.

Kama kiwanda kimoja tu Mwanambaya Mkuranga kinataka tani 300 kwa mwezi na vipo viwanda vingi tu vinanunua taka za plastic na vyuma chakavu. Jikiteni zaidi kwenye kuzalisha ajira kupitia recycling industry.
 
Walifanya kosa kuruhusu ile mifuko laini inayokua haina rangi au tuite nyeupe. Changamoto yake inaanza kuonekana sasa
 
Huu mzigo upo nipe konekisheni ya hivyo viwanda..tusaidie kulinda mazingira

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Nenda Mwanambaya Mkuranga kiwanda cha Wachina mkono wa kushoto kama unaenda Mkuranga jirani na kile cha Wachina wanachozalisha ndala na sendos.

Plastic ngumu iliyosagwa tani moja wanachukua kwa sh milioni moja na nusu.

Chupa za maji zisizosagwa kwa tani ni sh milioni moja na elf 50.

Wanachukua pia viroba, nailoni,mabomba ya plastic yaliyosagwa fika kiwalani kwa Guru utapata soko.
 
Kwahiyo mpaka wasubiri kiongozi wa juu atoe agizo, wao wenyewe hawaoni.

Kutangaza tarehe kunalenga nini?

Kwanini wasifanye msako wa kushitukiza ili waondoe tatizo badala ya kutishia watu ili waifiche mifuko.
 
Walifanya kosa kuruhusu ile mifuko laini inayokua haina rangi au tuite nyeupe. Changamoto yake inaanza kuonekana sasa
Hizo soft ata Tanzania kuna viwanda vinazalisha shida ni kwamba wanashindwa ushindani na soft zinazotoka nje sababu ya bei ni ndogo na hizo ndio ambazo zinasambaa Sana mitaani
 
RC MAKALLA: MSAKO WA MIFUKO YA PLASTIKI KUANZA JUMATATU YA AUGUST 29.

- Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango Ameelekeza msako wa mifuko ya Plastiki ufanyike Mikoa yote...
mifuko wanayozungumzia ni ile ya zamani au hivi vipasel ambavyo hata ukinunuwa nyanya unawekewa?Mfano wa vile vya kuwekea bisi?

Nawakumbusha wasisahau kuagiza ufanyike msako kwa madereva wazembe na magari mabovu.
 
Kuna baadhi ya mambo magumu kuelewa au kuna siasa ama agenda nyuma yake.Nchi zinazotakiwa kuwa mstari wa mbele kulinda mazingira ni nchi zenye idadi kubwa ya watu.China hadi leo mifuko ya plastiki inatumika,wana recycle,so hata Tanzania inawezekana kutafuta njia bora ya kutatua tatizo bila kuongeza gharama kwa mwananchi wa chini.Mifuko isiyo ya plastiki ni bei gani?Hii agenda ya maziingira ianze na nchi wazalishaji wakubwa wa platiki kuliko kuanza na nchi watumiaji wadogo wa plastiki
 
Back
Top Bottom