RC Makalla, Awapongeza Maafisa Lishe kwa kufuta rekodi mbaya ya lishe iliyokuwepo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,733
13,491
RC MAKALLA: DSM IMEFANYA VIZURI MKATABA WA LISHE.
IMG-20220722-WA0004.jpg

- Awapongeza Maafisa Lishe kwa kufuta rekodi mbaya ya lishe iliyokuwepo.

- Awaelekeza Wakurugenzi kuwawezesha Maafisa Lishe kutekeleza Majukumu yao na kutoa fedha kwa wakati.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Amos Makalla amewaelekeza Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa huo kuwawezesha Maafisa Lishe kutekeleza Majukumu yao na sio kuwaona hawana kazi kwa kuwageuza kuwa watu wa kuisaidia kwenye matukio ya dharura hususani Kamati za chakula kwenye mikutano.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo wakati wa kikao Cha tathimini ya utekelezaji wa mkataba wa Lishe ambapo amewapongeza Maafisa Lishe kwa kazi kubwa waliyoifanya kufuta tatizo la Lishe duni lililokuwa likiikabili Dar es salaam.

Aidha RC Makalla ameelekeza Halmashauri kutoa fedha za utekelezaji wa Lishe kwa wakati muafaka ili kuwezesha Maafisa Lishe kutekeleza Majukumu yao tofauti na Sasa ambapo pesa inatoka kwa kuchelewa.

Katika kikao hicho RC Makalla ametoa zawadi ya vyeti kwa Halmashauri zilizofanya vizuri kwenye suala la Lishe ambapo Manispaa ya Kigamboni imeshika nafasi ya kwanza ikifuatiwa na Halmashauri Temeke iliyoshika nafasi ya pili na Halmashauri ya Kinondoni nafasi ya Tatu.

Itakumbukwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan kipindi Akiwa Makamu wa Rais aliingia mikataba na Wakuu wa Mikoa kuhakikisha wanaondoa athari za utapiamlo katika maeneo yao.
 
Back
Top Bottom