RC Makalla atoa onyo eneo la Muhimbili hospitali mwisho leo kufanyika biashara

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
24,284
28,180
29 October 2022
Dar es Salaam, Tanzania

RC MAKALLA ATOA ONYO ENEO HILI LA MUHIMBILI HOSPITALI |MWISHO LEO KUFANYIKA BIASHARA



Source : Dar es Salaam RS Digital


More info :

October 31, 2022 2 min read
Na Heri Shaban, TimesMajira Online, Ilala

RC Makala: Hospitali ya Muhimbili sehemu hatarishi kufanya biashara​

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala, amesema Hospitali ya Taifa Muhimbili ni sehemu hatarishi kufanya Biashara sababu ya kubeba magonjwa mbalimbali .

Mkuu wa Mkoa Amos Makala, amesema hayo katika Oparesheni ya safisha na Pendezesha Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Usafi eneo la hospitali ya Taifa Muhimbili Kata ya Upanga Magharibi .

“Eneo hili sio rasmi kufanya Biashara ni eneo hatarishi watu kuchukua magonjwa kwenda kwa Jamii, Mitaani, magonjwa hatarishi ” amesema Makala .

Mkuu wa Mkoa Makala amesema sehemu hiyo ambayo waliokuwa wakitumia wafanya Biashara sio sehemu rafiki kufanya Biashara , Daladala pia zinatakiwa kushusha na kuondoka mara moja .

Amesema kuanzia leo anaweka Kambi eneo hilo atakuwa anakuja kila wakati atasimamia masaa 24 hivyo amewataka Wafanyabiashara kuondoka sio sehemu Salama .

“Nakuagiza Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji kuanzia Leo simamia eneo hili sio rafiki kufanya Biashara wanapofanya Biashara wanabeba na magonjwa hatarishi aliwataka hospitali ya Taifa Muhimbili kuyalinda maeneo hayo Kipindupindu ni uchafu nawaomba Wananchi wa Ilala kuyapendezesha maeneo haya ” amesema.

Katika hatua nyingine amepongeza KAMPUNI ya Usafi ya Kajenjele ambayo inashiriki kampeni za Pendezesha Dar Es Salaam na kuunga mkono juhudi za kufanya Usafi Kila wakati eneo ambalo Serikali inazindua kampeni hizo Mkurugenzi wa Kajenjele anaacha Shughuli zake anajumuika pamoja ikiwemo kutoa magari ya usafi .

Wakati huohuo walijitoeza Wadau wa usafi akiwemo Diwani Mstaafu wa Upanga Magharibi Godwini Mbaga amesema atakabidhi shilingi milioni 1 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya kuunga mkono kampeni hiyo kabambe ambapo Mkuu wa Mkoa Amos Makala alimweleza Mbaga kuwa apeleke Ofisini kwa Kaimu Katibu Tawala Mkoa atampa pesa hiyo na kupewa risiti Maalum .
WhatsApp-Image-2022-10-30-at-11.07.48-AM-1024x682.jpeg
Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam Amos Makala Octoba 29/2022 amezindua usafi Eneo la Muhimbili Upanga Magharibi na kuwataka wananchi wasifanye biashara Eneo Hilo hatarishi Kwa afya watabeba magonjwa mlipuko (katikati )Diwani Mstaafu wa Upanga Magharibi Godwini Mbaga ameunga. Mkono kampeni za Usafi kwa kuchangia shilingi milioni 1
WhatsApp-Image-2022-10-30-at-11.07.52-AM-1-1024x682.jpeg
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala (Kulia) akiwa na wafanyakazi wa Kampuni ya Usafi Kajenjele na Mkurugenzi (Katikati)Kushoto Katibu Tawala Wilaya ya Ilala Charangwa Selemani wakati wa uzinduzi wa Usafi endelevu Upanga Magharibi Wilayani Ilala Octoba 29/2022
WhatsApp-Image-2022-10-30-at-11.07.54-AM-1024x682.jpeg
Katibu Tawala Wilaya ya Ilala Charangwa Selemani (Kushoto )akiwa na Wananchi wa Wilaya ya Ilala katika kampeni endelevu ya usafi Upanga Magharibi Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa Amos Makala 0ctoba 29/2022
 
Back
Top Bottom