Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,106
- 10,178
MKUU wa Mkoa wa Manyara, Makongoro Nyerere, ameahidi kutumia gharama yoyote ya fedha kupeleka nyama kwa wawindaji, waokota matunda na warina asali wa jamii ya Wahadzabe, ili kuwashawishi wajitokeze kushiriki sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.
Wahadzabe hao ni wale wanaoishi katika Kitongoji cha Domanga kilichoko Kata ya Eshkesh katika Wilaya ya Mbulu.
Makongoro alitoa ahadi hiyo jana, wakati akizungumza na jamii hiyo ili kuwahamasisha kujitokeza kwa wingi katika sensa hiyo.
"Mwaka ujao itakuja sensa ya watu na makazi, nitawaletea nyama za kutosha ila mje wote kuhesabiwa," aliahidi Makongoro.
Aidha, alisema sensa ina umuhimu mkubwa, kwa kuwa inalenga kupata takwimu sahihi zitakazoisaidia serikali kupanga mipango yake ya maendeleo.
"Watu wa hapa mnapenda nyama sana safari ijayo tutakula nyama wee acha tu mjitokeze sana mhesabiwe," alisema Makongoro.
Aidha, Makongoro, alisema serikali inapopata takwimu sahihi za watu na makazi, ndipo inapata mwanga mzuri wa kuwaletea huduma za kijamii kama vile maji, shule, zahanati na barabara kulingana na idadi yao.
Vile vile, Makongoro aliwashukuru Wahadzabe, kwa kuitikia wito wa kukubali kuhesabiwa katika sensa ya majaribio.
Mratibu wa Sensa Mkoa wa Manyara, Gidion Mokiwa, akitoa taarifa kwa kamati ya sensa ya mkoa huo, alisema katika sensa ya majaribio iliyofanyika Septemba 11, mwaka huu, kaya 104 za Kitongoji cha Domanga zilihesabiwa na kuyafikia majengo 97.
Mokiwa, alitaja miongoni mwa mafanikio kuwa ni uwapo wa utayari mkubwa wa wananchi kuhesabiwa hususani kwa makundi yote, ushirikiano mkubwa wa viongozi wa kata na kijiji, uwapo wa ushirikiano wa wanakamati kuanzia mkoa hadi kijiji na ushiriki wa kiwango cha juu cha Wahadzabe.
Pia mratibu huyo alivitaja vikwazo pia kuwa ni ukubwa wa kitongoji, idadi kubwa ya wanakaya, tatizo la lugha kwa baadhi ya maeneo ya kitongoji, baadhi ya wananchi kuwa na uelewa mdogo wa umuhimu wa sensa na malalamiko ya kutopatikana kwa baadhi ya huduma za jamii ndani ya kitongoji.
Kwa upande wake, Diwani wa Eshkesh, Rumay Bajuta, alisema kazi hiyo ya sensa ya majaribio katika kitongoji hicho, ilienda vizuri na watu walifurahi kuchinjiwa nyama pori.
NIPASHE