RC Gambo ameivua nguo serikali na mamlaka iliyomteua

tethering

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
331
139
Kwa baadhi ya vitendo au maamuzi yanayofanywa na huyu kiongozi kwa kutumia cheo chake yananifanya niamini kumbe hata mimi naweza kuongoza vizuri na kwa busara kuliko huyu.

Kitendo cha kukamata watu walioenda kufarijiana kwa msiba uliotokea eti ni mkusanyiko usio halali eti hauna kibali, hata atumie hoja nyingi kias gani kujisafisha ukweli utabaki palepale
Ameivua nguo serikali na mamlaka iliyomteua.

Kitendo hiki kimepanda chuki juu yake kwa sababu kuna watu wengi wapo nyuma ya waliokamatwa mfano wale viongozi wa dini. Yaani hapo wisdom empty hata kama itatumika jiki kusafisha hilo halitoki kwenye mioyo ya watanzania.

Hata kama nitakamatwa mimi mtoa hoja, bado ukweli utabaki hapo na cheo chako ni dhamana tu kesho tutakuwa wote huku mtaani. Sidhani kama alifikiri vizuri impact ya kitendo hiki, bado najiuliza hivi asingewakamata na kuwalaza polisi kwani kuna madhara yangetokea?

Jambo la pili ni kuhusu rambi rambi..

Najiuliza; Je, kama serikali inatumia rambirambi kinyume na matakwa ya waliotoa rambirambi na yenyewe ipo tayari fedha inazotuma kwenye halmashauri nchini zitumike kinyume na maelekezo?

Nakumbuka mara kadhaa waziri mkuu amekuwa akitoa onyo kali kwa viongozi kunapokuwa na fungu fulani limetolewa kwa shughuli fulani kwamba zitumike kama ilivyopangwa.
 
 
Bashite na Gambo ni kielelezo tosha cha vijana wasiojua kuongoza.
 
Wakati mwingine mapenzi ya jambo au kitu fulani huwa hayaoni kabisa mf unaambiwa mtu au kikundi fulani wanachanganya siasa ktk misiba hutakubali kwa kuwa Tayari unamapenzi na mtu au kundi fulani lakini hata kwa akili ya kushikiwa tu kwanini unakwenda kutoka rambi rambi ubebe na waandishi na sehemu kubwa ya viongozi kutoka kundi fulani inamaana hawakuridhika siku ya kuagwa miili yavwapendwa wetu walipowakilishwa na Mwenyekit wao? jariibuni kujiongeza .
 
Kwa hili Gambo amedhihirisha hawezi kuongoza ndio maana Kikwete akiwa rais alimuondoa kwenye kazi kama mkuu wa wilaya ya Korogwe, hili zoezi la kuokota waliokosa kura za maoni ndio limemuibua huyu jamaa hata Magu atamchoka, full kukurupuka, hana busara kabisa,
 
Viongozi wetu hawa ilikuwa ni muhimu sana kufanyiwa interview kwanza hata kwa maswali madogomadogo kuona kama wana uwezo wa kukalia viti vyao vya wanaojua kusoma na kuandika, ofisi imekua kama bafu unachagua jiwe gani la kusugulia miguu ulitumie!!!!
 
Kwamtazamo
Wangu hiyo ni hoja nyepesi sana ukilinganisha na impact ya kitendo alichofanya rc
To be honest ulemsiba ni mkubwa
Vyombo vya habar kuwepo siojambo geni
Hata serikali hutoa msaada mbele ya vyombo hivyo
 
Hivi hawa jamaa wanajua kama kuna maisha baada ya utumishi wa umma? au wataenda kuishi sayari tofauti..hata kama ni kulinda kibarua sio kwa kujitoa ufahamu
 
Hakuna chochote kilichofanywa na RC Gambo cha kuivua nguo Serikali. Serikali is bigger than that.

Kimsingi alichokifanya RC Gambo hakikuzoeleka kwa wanasiasa "opportunists" wengine ambao kutoa neno misiba kwao ni agenda.

Tunahitaji RCs ambao wako Genuine kama Gambo.
 
..Sidhani kama alifikiri vizuri impact ya kitendo hiki, bado najiuliza hivi asingewakamata na kuwalaza polisi kwani kuna madhara yangetokea?

Uwezo wa kufikiri wa hawa vijana ni mdogo sana. Hakukuwa na haja ya kulikuza jambo lile mpaka kuwalaza ndani tena kwa siku mbili. Chuki inayopandikizwa ni ya hatari sana.
 
Ngoja mletewe Mh. Steven Wasira kuwa Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro ndio mtakapoelewa hizi ni zama gani!

..tatizo la hawa watoto hawaelewi jinsi ya kuenenda kama viongozi wa serikali.

..Mzee Wassira pamoja na matatizo yake yote hawawezi kufanya mambo ya hovyo-hovyo kama tunayoshuhudia toka kwa hawa watoto.

..hawa watoto madaraka yamewazidi kimo. Ukiwasikiliza unajua kabisa hawajawiva kiongozi. Ukisoma statement zao ambazo ni official utagundua hawaelewi mipaka na uzito wa dhamana walizopewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…