RC Chalamila: Wafanyabiashara wa Kariakoo wajitafakari, migomo siyo suluhisho

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
93,081
162,316
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila ametoa tamko la kuwataka Wafanyabiashara wote wa Mkoa wa Dar es salaam kujiepusha na migomo na kila mmoja kujitafakari, hii ni baada ya kusambaa kwa taarifa jana kuhusu Wafanyabiashara wa Dar es Salaam na Mikoa mingine kupanga kugoma.



Akiongea Jijini Dar es salaam leo June 23,2024, Chalamila amesema “Masuala ya mgomo kwa Wafanyabiashara yasichukuliwe kuwa ni jambo la pamoja kila mmoja awe na tafakari ya kutosha kabla hajafikia wazo hilo la kufunga biashara, Mtu yeyote ambaye anaweza kuleta ubabe kutokusikilizana maana yake Serikali nayo inaweza kuamua kufanya hivyohivyo jambo ambalo hiyo sio falsafa hata kidogo ya Mh. Rais wa Tanzania”

“Wote tuungane kuijenga Dar es salaam, migomo sio suluhisho hata kidogo wala tusishabikie, mwisho wa mgomo inaweza ikawa ni vita ndogo ambayo ikamuathiri hata asiyekuwa na hatia”


Nawatakia Dominica njema 😃

Pia soma
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ameyasema hayo mapema leo Juni 23,2024 Kufuatia uwepo wa taarifa za uvumi wa mgomo wa wafanyabiashara wa kariakoo ambapo amewataka wafanyabiashara kuepuka kushiriki kwenye masuala yanayoweza kuleta uvunjifu wa amani na kurudisha nyuma uchumi ikiwemo mgomo huu kwani Serikali imeshashughulikia baadhi ya changamoto na inaendelea kushughulikia changamoto za wafanyabiashara hususani zile zinazohusu mabadiliko ya Kisheria

RC Chalamila amewataka wafanyabiashara kutambua kuwa mgomo sio suluhisho pekee la kutatua changamoto bali utaratibu bora wa kutatua changamoto ni kukaa mezani na mamlaka kujadili kwani mgomo huongeza chuki na wakati mwingine kusababisha uvunjifu wa amani

Aidha RC Chalamila amesema kuwa Serikali inatambua changamoto za wafanyabiashara na kada zingine za wafanyakazi na watumishi na inaendelea kuzifanyia kazi hivyo amewataka wafanyabiashara kushirikiana na Serikali kumaliza changamoto zao na kuepuka mihemko inayoanzishwa na watu wachache wasio kuwa na nia njema na Mkoa wa Dar es salaam na Taifa kwa ujumla

Sanjari na hilo RC Chalamila amesema ujenzi wa soko jipya la kariakoo na ukarabati wa soko liloloungua kuwa soko hilo linalojengwa kwa zaidi ya shilingi bilioni 28 lipo katika hatua za mwisho na kwamba Rais Dokta Samia atakuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa soko hilo na wafanyabiashara waliokuwepo zamani na wapya wataingia kwa utaratibu maalum utakaotolewa na uongozi wa soko hilo

Vilevile katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila amezungumzia oparesheini ya kuwaondoa wafanyabiashara za ngono (Dada Poa) inayofanyika Wilayani Ubungo na kusema kuwa Mila,Desturi na Tamaduni za Tanzania hazikubaliani na biashara hiyo ya ngono pamoja na ndoa za jinsia moja hivyo Serikali mkoani humo itaendelea kupinga vitendo
 
Mkuu wa mkoa wa DSM Albert Chalamila ametoa angalizo Kwa Wafanyabiashara kujitafakari na kujiepusha na migomo

Migomo siyo suluhisho jiepusheni nayo, amesisitiza Chalamila

Source: Ayo TV

Nawatakia Dominica njema 😃
Migomo ni suluhu ya mwisho juu ya matatizo wanayokabiliwa watu(Wananchi) endapo kama Kuna Serikali ambayo haina utamaduni wa kusikia vilio vya Wananchi wake.

Serikali ndio inapaswa kujitafakari kwamba kwa nini Wananchi wanaamua kutumia migomo kama njia ya utatuzi wa matatizo yao wanayokabiliwa nayo.
 
Mkuu wa mkoa wa DSM Albert Chalamila ametoa angalizo Kwa Wafanyabiashara kujitafakari na kujiepusha na migomo

Migomo siyo suluhisho jiepusheni nayo, amesisitiza Chalamila

Source: Ayo TV

Nawatakia Dominica njema 😃
Anadhani biashara inaendeshwa kwa domo kama siasa.

Lugha ya biashara ni debit and credit tu hakuna kuupiga mwingi na kububujikwa na machozi ya furaha kwa mama.

Serikali ya mama imeanza unyang'anyi kama mtangulizi wake.

Mkurugezi wa ilala kawaagiza watendaji wake mitaani kugakikisha wanakusanya Billion 30 kabla ya tarehe moja hawana pesa, wameiba pesa zote na hawana pesa za kuwafikisha mpaka watakapopokea pesa za bajeti mpya.

Mtaongea yote lakini solution ni kuyaondowa madarakani majizi ya ccm, na bahati mbaya tulionayo jeshi letu limeunganishwa kwenye mfumo wa kula keki, kwahiyo usitalajie jeshi kufanya chochote, walipewa fursa Magufuli alivyokufa CDF akampa Samia.
 
Back
Top Bottom