RC Albert Chalamila: Gari lililobeba mitambo maalum liko njiani kwa ajili ya Uokoaji Kariakoo

Waufukweni

JF-Expert Member
May 16, 2024
1,190
2,891
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila amesema tayari gari maalum lililobeba greda na mitambo mingine linakaribia kufika Kariakoo kwa ajili ya kusaidia uokoaji wa Watu waliofukiwa na kifusi baada ya ghorofa kuporomoka ambapo amewataka Watanzania kutolaumiana kwa sasa bali kuweka nguvu kwenye kuokoa waliofukiwa.

Pia, soma: Ghorofa limeporomoka Kariakoo asubuhi ya leo Novemba 16

"Kama kuna vifo tutaendelea kuhabarishana lakini hadi muda huu hali ya usalama katika eneo hili ni kubwa na niwaombe Wafanyabiashara wote pamoja na Ndugu na Jamaa ambao Rafiki na Ndugu zao wapo kwenye jengo hili tuendelee kuwa na subira, hadi sasa tumefanya jitihada za kuleta mitambo, mnafahamu greda hauwezi kupitisha barabarani lazima ubebe kwenye gari maalum la mitambo na hadi muda huu lipo karibu kuja kusaidia uokozi"

"Niombe sana tuendelee kuwa na usikivu na ustahimilivu na Mh. Rais ametoa pole kwa waliopata na majanga, nitoe rai kwamba muda huu sio muda wa kulaumiana, ni muda wa kuwakoa wenzetu, jengo hili lina underground tunaambiwa wapo Watu ndani, baada ya muda tutatoa taarifa sahihi wangapi wamepatikana chini na wakiwa na hali gani, Vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama na Viongozi tupo hapa, tusilaumiane kwanza hadi tafiti zikianza tubaini chanzo"
 
Masaa yashapita zaidi ya manne alafu hapo ni kkoo kitovu Cha biashara nchi nzima, sasa huku mikoani si mtakuja baada ya wiki!!!

Haya sasa Wana kariakoo mkiwa dukani hakikisheni mna stock ya chakula na maji hata ya wiki maana nchi hii haieleweki lolote linaweza kutokea
 
Bi salam za pole na ahadi ya kugharamia mazishi aja tia neno badoo
 
Attachments

  • downloadfile-13.jpg
    downloadfile-13.jpg
    73.3 KB · Views: 3
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila amesema tayari gari maalum lililobeba greda na mitambo mingine linakaribia kufika Kariakoo kwa ajili ya kusaidia uokoaji wa Watu waliofukiwa na kifusi baada ya ghorofa kuporomoka ambapo amewataka Watanzania kutolaumiana kwa sasa bali kuweka nguvu kwenye kuokoa waliofukiwa.

Pia, soma: Ghorofa limeporomoka Kariakoo asubuhi ya leo Novemba 16

"Kama kuna vifo tutaendelea kuhabarishana lakini hadi muda huu hali ya usalama katika eneo hili ni kubwa na niwaombe Wafanyabiashara wote pamoja na Ndugu na Jamaa ambao Rafiki na Ndugu zao wapo kwenye jengo hili tuendelee kuwa na subira, hadi sasa tumefanya jitihada za kuleta mitambo, mnafahamu greda hauwezi kupitisha barabarani lazima ubebe kwenye gari maalum la mitambo na hadi muda huu lipo karibu kuja kusaidia uokozi"

"Niombe sana tuendelee kuwa na usikivu na ustahimilivu na Mh. Rais ametoa pole kwa waliopata na majanga, nitoe rai kwamba muda huu sio muda wa kulaumiana, ni muda wa kuwakoa wenzetu, jengo hili lina underground tunaambiwa wapo Watu ndani, baada ya muda tutatoa taarifa sahihi wangapi wamepatikana chini na wakiwa na hali gani, Vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama na Viongozi tupo hapa, tusilaumiane kwanza hadi tafiti zikianza tubaini chanzo"
View attachment 3153644

Limebeba camera kwa pic murua za chawaz kutoka Mars tusibiri nyama zipo chini
 
Back
Top Bottom