Rasmi: UKAWA imeshakufa kibudu

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
25,253
36,508
Wiki chache zilizopita nilifanikiwa kumuona na kumsikiliza Maalim Seif katika kipindi cha luninga cha ahsubuhi akielezea yanayojiri Zanzibar na Chama chake cha CUF. Kituo hiko hiko kesho yake walimualika Prof Lipumba na kuhojiana naye kuhusu yale waliyomuuliza Seif.

Hayo yamejiri kama matokeo baada ya washirika wa Seif katika UKAWA kuamua kuingilia uhuru na demokrasia ndani ya chama cha CUF huku ilihali wanapalilia mgogoro na kuutukuza ubaguzi mkubwa na wa wazi anaoufanya Seif na wenzake.

Naam, UKAWA kirefu chake ni Umoja wa Katiba ya Wananchi ambapo lengo lake lilikuwa ni kuhakikisha maoni ya wananchi katika Katiba mpya (rasimu ya Warioba) yanaheshimiwa. Lakini kilichotokea ni hadaa kwani hata kabla hawajaunda huo Ukawa tayari viongozi hao walisimama kidete kuipinga rasimu ile ile kabla haijawasilishwa Bunge la Katiba.

Baada ya UKAWA kuundwa ikaonekana ndiyo namna pekee ya kuunganisha nguvu ya kisiasa dhidi ya CCM ili kuitoa madarakani. Lakini ukiwauliza watukufu wa Ukawa nini malengo yao watakujibu kwa kuhubiri mapungufu ya CCM na kasoro zake huku wakiapiza kurekebissha changamoto hizo. Kwa sisi wenye akili tunag'amua kwamba hapo hakuna jipya kwani unaposema unatarajia kutatua matatizo bila kuwa na mpangokazi ni sawa na kutegemea kudra kwenye jambo ambalo ni lazima juhudi ifanyike.

Tunashuhudia leo namna injini za propaganda zinavyofanyakazi mitandaoni na vyombo vya habari katika kuchafuana wenyewe kwa wenyewe na wanavyojiundia udiktekta kwenye vyama vyao. Unapokuwa katika vyamba vya UKAWA na ukafanikiwa kuwa kiongozi wa umma basi wewe unakuwa na cheo cha kuwa msemaji wa chama na UKAWA. Hakuna nidhamu wala mpangilio.
Unakuta kiongozi anaongea maneno ya hovyo hata kufikia kiwango cha kutukana lakini hakuna anayekemea wala kuwarejesha katika mstari.

Badala ya kuunga mkono maendeleo, leo hii UKAWA imekuwa mstari wa mbele kupinga maendeleo na hata kupropagate dhidi ya mipango yote ya serikali kuwaletea maendeleo wananchi.


Ikumbukwe, Dr. Slaa alijitoa kwa kiwango cha juu kujenga upinzani wenye tija lakini alipoona kuna gia mbovu zilizolazimishiwa kubadilishiwa hewani akajiweka pembeni na hawakumuacha hivi hivi walimtukana na kumdhalilisha vya kutosha.
Leo wanapambana na Lipumba ambaye ni muasisi wa huo umoja wao

Wasichokijua wananchi ni kuwa injini nyuma ya mchezo huu wote ni Lowassa na Mbowe ambao kila mmoja kwa wakati wake alitumia njia za kuchafua wenzake wanaoonekana wana juhudi za kuimarisha vyama walivyokuwemo.

Mimi ninachokijua ni kwamba UKAWA imebaki jina, imekuwa ni kigenge cha kupata public sympathy na siyo tanuru la kupika viongozi na kuleta utunduizi wa hoja za kuwasaidia wananchi.

Wanadandia matukio
wanadandia hoja
wanadandia sera
wanadandia treni kwa mbele

Msanii
 
Wewe uko ktk kumtetea Dr Mihogo, katiba, Ukawa, CCM au kama Ukawa imeshakufa sioni sababu ya kupoteza muda kuongelea vitu vilivyokufa otherwise ungekuwa unatupa historia yake namna ilivyokuwa.
 
Wewe uko ktk kumtetea Dr Mihogo, katiba, Ukawa, CCM au kama Ukawa imeshakufa sioni sababu ya kupoteza muda kuongelea vitu vilivyokufa otherwise ungekuwa unatupa historia yake namna ilivyokuwa.
Historia utabaki nayo wewe na wachache walioitumia kuwachangisha watanzania kwa kuwahadaa kuchangia operesheni za ukombozi kumbe walaji.

Mimi nawaeleza kuwa mmeshakwisha na kila mnalolishika linawaponyoka.

Ubinafsi na uchu wa madaraka uliopitiliza ndilo kaburi lenu
 
Ingekuwa vizuri kama ungefafanua uhai wa mbadala wake - Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambayo over 80% ya wanachama wake - huko kwenye matawi na mashina hawatarajii kumwona mwenyewekiti wao anytime soon kwa sababu anajua sehemu nyingi ccm iliiba kura. Kilichobakia ni kwamba kila anapopata Kipaza sauti kwenye mikutano ya Chama ni kulia lia tu Lowassa Lowassa. Uwanja ni wako.
 
Hao walishaisha.Yupo Mzee mmoja wa mvi sasa hivi anahangaika hangaika akidhani 2020 ataipata tena neema ya 2015.Amuulize Dr Slaa.Atalia kilio cha mbwa.
Nilipigwa butwa kusikia Tanzania ni nchi ya mia hamsini na kitu kwa kuwa na wananchi wasiokuwa na furaha tunapitwa hata na nchi zilizo na migogoro ya vita inawezekana watafiti wakitafiti pia na nchi gani zina mbumbumbu wengi duniani basi Tanzania yetu inaweza ikawa nchi ya kwanza kuwa na mbumbumbu wengi.Hiki chama kuendelea kuwa madarakani kwa sababu za kukosa katiba na tume huru ya uchaguzi na bado tunawaza mambo ya uchaguzi ni jambo la fedhea sana na linatia walakini kama akili zetu zina akili.Sijui kama akili zetu zinafikiria sawa sawa.Ebu fikiria kama mwenyekiti wa chama tawala ndie ana mamlaka ya kumteua mwenyekiti wa tume ya uchaguzi.Hivi hapo kuna uchaguzi kweli au ni uchafuzi tu.Nchi nyigine ungekuta kishanuka.Huwezi kuwafanya watu mbumbumbu kiasi hicho.Iwepo katiba na tume huru uone fisiem kama itashinda.Tutaambulia mabomu nchi nzima.
 
Wewe uko ktk kumtetea Dr Mihogo, katiba, Ukawa, CCM au kama Ukawa imeshakufa sioni sababu ya kupoteza muda kuongelea vitu vilivyokufa otherwise ungekuwa unatupa historia yake namna ilivyokuwa.
Anaendeshwa na hisia hasi huyo. Apuuzwe hadi apauke mdomo kwa kupayuka.
 
Cheti
Bashite
Rambirambi
Kulilia Mic za Misibani

Ndo Sera yetu.
Umekosea kuzipanga. Rambirambi ndiyo hatari zaidi. Mkisikia hiyo kitu mnaweweseka kama vibiriti ngoma. Na kila hoja ya utetezi mnayokuja nayo mnapigwa mwiko wa pua. Wala rambirambi wakubwa ninyi! Khaaa! Ptuuuuuu!
 
Miundombinu inaboreshwa
Elimu bure
Ufisadi unakomeshwa
Wabadhirifu mnashughulikiwa
Niseme zaidi?

Labda miundo mbinu inayojengwa kwa.pesa za Rambirambi. Wabadhirfu wa miaka 20 ilikwisha ndiyo Marais Leo,unategemea ubadhirifu kwisha.

Wala rushwa wa Jana ndiyo Mawaziri wa Leo,kwa nini msiletewe TT kwa bei ya kutuua.

Adui wa CCM Siyo Upinzani ni Wanachama wenyewe, piganeni ndani ya Chama chenu,waamvieni watawala ukweli msipige makofi hata kwenye upupu.

UKAWA ikifika si ndiyo furaha ya CCM?? Si ndiyo sababu ya Kuwekwa Lipumba ajue CUF ili CCM ishinde au?Kuna sababu gani ya kulipa millions of money Lipumba kama siyo kuua CUF.

Pole sana.
 

Tatizo unayoyaongea ndiyo hapo ndani ya Chama Chako CCM! Ubinfsi na uchi wa Mali ndivyo vinavyowaponza.

Hakuna mwanasiasa asiye taka kutawala.Kama hamna uchi wa madaraka acheni kugombea nafasi zozote za Uongozi! Lakini kwa sababu ni Ilani yenu hata kuua mbaya ili mpate Uongozi,na mifano ipo!

Kama ni rushwa CCM mmeshika number,kama ni mauaji ya RAIA wasio na hatia CCM kutumia polisi mmeshika number,matumizi mabaya ya Katiba na sheria CCM mmeshika number,kama matumizi mabaya ya Madaraka CCM mmeshika number.

Nilitegemea uionue CCM ili Watanzania labda tunaweza kuangalia Tena lakini kila siku ni Upinzani tu utadhani hao Ukawa umewaibia mume.
 
Imekaa poa sana kwa CCM kama ni kweli.
 
Bilioni Nane za Kivuko kibovu Waziri wa miundo mbinu,Barabara chini ya viwango Waziri wa miundo mbinu,baada ya mvua kidogo tu hata Barabara za Mwendokasi zina mashimo,waziri wa miundo mbinu,uuzwaji holela wa nyumba za serikali waziri wa miundo mbinu,bongo ya kujengewa hoteli mkabala na maeneo ya Geita waziri wa miundo mbinu!

Halafu huyu ndiye Rais leo ,tunaletwa Q400,tunajenga International Airport Chato,ndege Bomu kwa $224 milioni,halafu ati Ufisadi Lowassa maweeeeee,tengenezeni ndani ya CCM, kemeeni maovu,msijipe hope kwamba Watanzania hawaoni kwa kuleta vituko humu,Watanzania wanajua mnatenga pesa za Uchaguzi 2020 kwa gharama za maisha ya Watanzania.

Hakuna Maji ,elimu mbovu afya pumbavu,fanyeni yenu safisheni CCM kuna shida ndani ya system.Msiharibu sifa za watu kwa gharama kubwa.

mke wa mwizi wa Escrow mmempa Ubunge wa kuteuliwa,halafu rushwa inapiganwa kweli hapo??

Mkuu wa Mkoa ndiye mpiga madeal anaiba hata pesa za rambirambi, ati zijenge miundo Mbinu, wafanyabiashara wananyang'anywa pesa na Mali zao halafu ati madawa ya kulevya, semeni Madaraka ya kulevya.

Hakika JKN akifufuka leo Ukiona CCM aliyoijenga atakufa tena kwa shock.
 

Kama Maendeleo ni kuiba na kula pesa za Rambirambi ni sawa maana huku kwetu ni Laana kula pesa za rambirambi.

Kama Maendeleo ni kuweka Viongozi wa upinzani Jela basi mmefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Kama Maendeleo ni kuweka Viongozi wa dini Mahabusu hiki nacho mmefanikiwa.

Lakini kama Siyo basi rudi kajenge CCM achana na Ukawa maana Ukawa siyo Chama cha Siasa.
 
Hao walishaisha.Yupo Mzee mmoja wa mvi sasa hivi anahangaika hangaika akidhani 2020 ataipata tena neema ya 2015.Amuulize Dr Slaa.Atalia kilio cha mbwa.

Nilidhani UVCCM kuna wenye akili kumbe wote akiondoka nao JKN,hivi kwa Serikali ya CCM kutwa kucha kupiga kelele na Upinzani ndiyo Maendeleo?? Rais akiongea kila maneno mawili moja ni Lowassa.40% ya hotuba ni jina la Lowassa hivi hamuoni kuna shida mahali?

CCM inazo nguvu zote imshtaki basi.Huyo Kitilya kawashinda kila siku ushahidi unatafutwa mwisho wa siku Kitilya atatoka na mtamlipa zaidi ya pesa alikwisha INA.UVCCM hamuliangalii hilo kwamba kodi zetu kama wana nchi zinatumika vibaya au hamjiulizi kwanini kesi haiendelei,mko busy Ukawa,Lowassa,Chadema tengenezeni kwenu kwetu tuaxhieni kama kuna bomoka si nafuu yenu.!
 
kwa hiyo mnajiona wajanja na mmewin baada ya kupandikiza mgogoro CUF,

na mnajiona wababe sana kwa kuzuia upinzani usifanye siasa
ngojeni muda utafika ndo utajua kama tupo au. tumekufa.
 
Same old crap!Siku nyingine usipoteze muda kuandika,search utapata uzi unaoendana na idea yako kisha pachika!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…