Rais Xi Jinping wa China atoa hutuba kwenye mkutano wa kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwa CPC

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,094
1,094
1.jpg

Mkutano mkuu wa kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) leo umefanyika hapa Beijing. Rais Xi Jinping wa China ametoa hotuba muhimu kwenye mkutano huo.

Kwenye hotuba yake, rais Xi ametanga kuwa China imetimiza lengo la kwanza la karne, yaani kujenga jamii yenye maisha bora kwa pande zote.

Amesema hii inamaanisha kuwa China imetatua tatizo la umaskini uliokithiri nchini China na inaelekea kutimiza lengo la pili la karne la kuijenga China kuwa nchi ya kisasa ya kijamaa yenye nguvu katika pande zote. Amesisitiza kuwa China imepita vipindi vya kujikomboa, kutajirika na kuwa na nguvu kubwa, na sasa mchakato wa ustawi tena wa taifa la China haupinduki.

Amesema maendeleo ya China yatatoa fursa kwa dunia nzima, na China itashikilia njia ya kujiendeleza kwa amani, kukuza ujenzi wa uhusiano wa aina mpya wa kimataifa, ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja, na kusukuma mbele maendeleo yenye kiwango cha juu ya “Ukanda Mmoja, Njia Moja”. Pia amesisitiza kuwa, China siku zote ni mjenzi wa amani ya dunia, mchangiaji wa maendeleo ya dunia, na mlinzi wa utaratibu wa dunia, na Chama cha Kikomunisti cha China kitashikilia kufanya ushirikiano wa kunufaishana na kupinga umwamba.

Rais Xi amesema uongozi imara wa CPC unatakiwa kulindwa, kwani uongozi wa Chama hicho ni sifa ya kimsingi ya Ujamaa wenye Umaalum wa China na kutoa nguvu kubwa kwa mfumo huo. Ameongeza kuwa uongozi wa CPC ni msingi na damu ya Chama na nchi, na una uhusiano wa karibu na maslahi na mustakbali wa watu wote wa China.

Amesema daima CPC kinawakilisha maslahi ya kimsingi ya wananchi, na kuishi kwa kutegemeana na wananchi, na hakina maslahi yoyote maalum, na kamwe hakiwakilishi maslahi ya kundi lolote lenye mamlaka, na watu wenye hadhi maalum. Ameongeza kuwa, jaribio lolote la kutenganisha chama hicho na watu wa China kwamwe halitafanikiwa. Pia amesisitiza kuwa, CPC lazima kizingatie madhumuni ya kimsingi ya kuwahudumia wananchi kwa moyo wote, kufuata msimamo wa wananchi, na kuhimiza mchakato wa maendeleo ya pande zote ya binadamu, pia kuhakikisha wananchi wote wanapata maendeleo makubwa zaidi na kutajirika kwa pamoja.

Aidha, rais Xi amesema kamwe Wachina hawataruhusu nguvu yoyote ya kigeni kuwaonea, kuwakandamiza au kuwatweza, na mtu yeyote atakayejaribu kufanya hivyo atakumbana na ukuta mkubwa wa chuma uliojengwa na watu zaidi ya bilioni 1.4 wa China. Amesema China haijawahi kuonea, kudhulumu, au kuwatisha watu wa nchi nyingine yoyote, na kamwe haitafanya hivyo. Amesema siku zote China imekuwa ikifanya kazi ya kulinda amani ya ulimwengu, kuchangia maendeleo ya dunia, na kulinda utulivu wa kimataifa, na ametoa mwito wa kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakbali wa pamoja.
 
Tusipokuwa makini CCM anaweza akafikia rekodi ya kutawala muda mrefu kama CPC, or even kuvunja rekodi yake.
 
Ila CPC wao wako Madarakani kwa sababu kuna vitu vimefanyika na vinaonekana.

Fikiria sisi ndani ya miaka 60 bado kabisa, watoto still wanakaa chini, Huduma za afya ni Duni, so CCM wataendelea kubaki Madarakani kiujanja ujanja na sio kwa sababu kuna vitu wanafanya.
 
Hakika PRESIDENT Xi ni mwamba na jabari katika siasa za China na Ulimwengu. Ni yeye na Mao ze Dong peke yao, ambao mawazo yao binafsi yaliingizwa kwenye katiba ya nchi.
China hii, ina ubabe mkubwa wa kiuchumi, kiteknolojia pamoja na kijeshi, ina watu karibu kila nchi ulimwenguni wakifanya biashara na ujenzi wa miundombinu mbalimbali.
Haishangazi kuona wachina chini ya chama chao cha CPC, wakimpa uongozi wa maisha president Xi kutokana na makubwa aliyoyafanya. Africa isipojifunza kwa China, tutabaki watu duni mpaka dunia iishe.
 
Tusipokuwa makini CCM anaweza akafikia rekodi ya kutawala muda mrefu kama CPC, or even kuvunja rekodi yake.
Tatizo sio kubailisha madaraka Kama fashion, je ni nani huyo anayeweza kuwa mbadala wa tunachokipigania
 
Ila CPC wao wako Madarakani kwa sababu kuna vitu vimefanyika na vinaonekana.

Fikiria sisi ndani ya miaka 60 bado kabisa, watoto still wanakaa chini, Huduma za afya ni Duni, so CCM wataendelea kubaki Madarakani kiujanja ujanja na sio kwa sababu kuna vitu wanafanya.
Hivi tu CCM anavyo endesha nchi wanaojiita wanaharakati wanalalamika, je wakiendesha nchi kama China, iatakuwaje ........?Sababu China ina aina ya demokrasia ya peke yake.
 
kipande hichi huyu rais wa super power ajae kaongea kisuper power mnoooo

Aidha, rais Xi amesema kamwe Wachina hawataruhusu nguvu yoyote ya kigeni kuwaonea, kuwakandamiza au kuwatweza, na mtu yeyote atakayejaribu kufanya hivyo atakumbana na ukuta mkubwa wa chuma uliojengwa na watu zaidi ya bilioni 1.4 wa China. Amesema China haijawahi kuonea, kudhulumu, au kuwatisha watu wa nchi nyingine yoyote, na kamwe haitafanya hivyo. Amesema siku zote China imekuwa ikifanya kazi ya kulinda amani ya ulimwengu, kuchangia maendeleo ya dunia, na kulinda utulivu wa kimataifa, na ametoa mwito wa kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakbali wa pamoja.

Sent from my SM-J5108 using JamiiForums mobile app
 
Strong statement from strong leader
 
Sio CPC ni CCP

Na sijui nakaa nasikiliza hotuba ya haya mavichaa sijui natolea wapi?

Linchi ukikosea hakuna cha mahakama unachinjwa hadharani

Hakuna due process,Xi asipokupenda from no where unauawa

Fvck communists
Je huko kwa mabest wa mabeberu Saudia wanasemaje......
 
Amesema maendeleo ya China yatatoa fursa kwa dunia nzima, na China itashikilia njia ya kujiendeleza kwa amani, kukuza ujenzi wa uhusiano wa aina mpya wa kimataifa, ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja, na kusukuma mbele maendeleo yenye kiwango cha juu ya “Ukanda Mmoja, Njia Moja”. Pia amesisitiza kuwa, China siku zote ni mjenzi wa amani ya dunia, mchangiaji wa maendeleo ya dunia, na mlinzi wa utaratibu wa dunia, na Chama cha Kikomunisti cha China kitashikilia kufanya ushirikiano wa kunufaishana na kupinga umwamba.
“UJENZI WA JUMUIYA YA BINADAMU YENYE HATMA YA PAMOJA “
 
Back
Top Bottom