Rais wetu amelewa madaraka, amesahau kuwa yeye ni Rais wa Watanzania na ni lazima atusikilize na apange kulingana na matarajio yetu. Nafikiri ni wakati muafaka sasa watanzania kuanza kuzitafakari kauli za Rais kwa kuwa zina athari kwa maisha yetu.
Haiwezi kuwa sawa eti kwa kuwa alikwenda kuchukua fomu mwenyewe anaweza kufanya atakavyo. Ni lazima awe tayari kujibu hoja zinazomkabili Makonda, akumbuke yeye ndiye aliyeanzisha mchakato wa uhakiki wa vyeti na makonda ni mtumishi wetu anayelipwa kwa fedha za Watanzania.
Nilitarajia nisikie Rais hatamchukulia hatua kwa kuwa tuhumu alizoelekezewa hazina ukweli wowote na siyo kuonyesha ubabe na kiburi kilichokithiri.