Rais, Wakazi wa Kilimanjaro tumekukosea nini? Kwanini tukuombe radhi?

General Mangi

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
15,303
23,055
Nimeshangazwa na kauli ya Rais juzi kwa wakazi wa KLM kuwa ametusamehe.

Nikauli ambayo inaonesha wazi Rais alikuwa na nyongo kubwa moyoni mwake juu ya wakazi hawa.

Inabidi Mh Rais utueleze wazi tumekukosea nini mpaka itutake kuomba radhi.

Binafsi siamini kwamba wale watu waliokuja na masale walikuwa na nia ya dhati kufanya hivyo zaidi ya kushinikizwa kufanya hivyo.

Nina uhakika hata ukiwauliza hawawezi kujibu ni kosa gani walilotenda mpaka kufikia hatua ya kuomba radhi.

Hivyo Mh Rais inabidi uweke mambo sawa na kuondoa kisasi cha muda mrefu kwa watu hawa.

Embu tueleze tuweze tambua kosa letu sisi wakazi wa KLM.

Wasalam.
 
Nilijua hili litakuja tu...ha ha ha haaaaa

Waliyabeba akayaona akawasamehe

Hapa kazi tu
 
Nikijua hili litakuja tu...ha ha ha haaaaa

Waliyabeba akayaona akawasamehe

Hapa kazi tu
Kuna kauli zilikuwa zinaelezwa juu ya teuzi za Rais kuhusu watu wa kaskazini.
Teuzi zile zilionyesha dalili ya mbaya.
Nahisi ndio sababu ya wakazi hawa kushinikizwa kubeba masale.

Lkn bado sijajua ni kosa gani tumemkosea Rais
 

Kosa lenu ni kuichagua Chadema, na hili halisameheki subirini maumivu.
 
Labda teuzi toka kaskazini zimepungua na wengi wao wanaongoza kwa kutumbuliwa kutokana na ufisadi so wanaomba huruma ya mkulu
 
Kuna kauli zilikuwa zinaelezwa juu ya teuzi za Rais kuhusu watu wa kaskazini.
Teuzi zile zilionyesha dalili ya mbaya.
Nahisi ndio sababu ya wakazi hawa kushinikizwa kubeba masale.

Lkn bado sijajua ni kosa gani tumemkosea Rais
Masale ni nini hiyo?
 
Kuna kauli zilikuwa zinaelezwa juu ya teuzi za Rais kuhusu watu wa kaskazini.
Teuzi zile zilionyesha dalili ya mbaya.
Nahisi ndio sababu ya wakazi hawa kushinikizwa kubeba masale.

Lkn bado sijajua ni kosa gani tumemkosea Rais
Mimi ni Mchagga, hatuna maua zaidi ya masale mara zote tangu zama za kale huwa ndilo jani linalo tumika kupokea wageni japo sale lina kazi zaidi ya hiyo.
Siamini kama ni kweli wale watu walibeba lile jani kuomba chochote toka kwa Mh. Rais. Nasema hivyo nikiamini mila yangu. Sale la kuomba radhi hali peperushwi. Linabebwa kwa unyenyekevu. Ukili peperusha unashangilia.
Nawaomba msiojua mila zetu msituharibie mila. Maana Lumumba akili zenu zinawatosha wenyewe.
 
Ni jani la jadi ambalo hutumika kuomba radhi.
Inasemekana ukikataa msamaha huo basi utapata pigo kali.
Ni jani la amani.
Sale lina maana zaidi ya kuomba radhi, pia hutumika kushangilia. Jani la kuomba radhi hubebwa kwa heshima na halipeperushwi. Na ili iwe ombi limekubaliwa lazima anaeombwa alipokee. Je?? Mh. Rais alipokea hilo jani?? Naomba tena msituharibie mila Maccm.
Watafuteni wazee wa Kichagga wawape darasa.
 
Kwani kosa lenu hamlijui?

Kwake yeye Magu kuchagua upinzani ni sawasawa na kosa la uhaini!

Sasa inakuwaje kwenye Katiba ya nchi inabainisha kuwa nchi ipo kwenye mfumo wa vyama vingi, kama anaona wananchi waliochagua upinzani ni wahalifu zaidi ya majambazi?

Ni bora tu Mkuu wetu apeleke muswada bungeni wa kuirejesha nchi yetu kwenye mfumo wa chama kimoja ili aweze kussuzika moyo wake!
 
Kwa hiyo kosa lao ni kutenda kwa mujibu wa katiba?
 
Mnakuwa waoga JPM hapendi Wachaga. Sio kosa lake. Kaamini vile sis inatuhusu. Ukichukiwa usilazimishwe upendwe. Kaa na Mungu wako inshallah siku zaenda. Mungu atamuuliza wslikukosea nini. Hawakunichagua, basi na mimi sitakuchagua amen.
 
Nadhani swali hili ungaliwauliza hao waliokuja kumlaki na Masale, rais alidokezwa tu maana ya hayo Masale na kama walishinikizwa lawama zielekezwe kwa waliofanya njama hizo. Lakini kwa kuangalia mavazi wengi ya wale waliashiria ni wana CCM, labda kuna makosa waliyofanya na walistahili msamaha wa Mwenyekiti wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…