Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron adai viongozi wa nchi za Afrika hawana shukrani

Strong ladg

Senior Member
Jul 15, 2021
113
323
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amedai kwamba viongozi wa nchi za Afrika hawana shukrani. Macron aliyasema maneno hayo mnamo tarehe 6 January 2025 wakati akiwahutubia wanadiplomasia wa Ufaransa wanaoiwakilisha nchi hiyo katika nchi mbalimbali.

Macron alisema kwamba mfano viongozi wa nchi za Sahel wanajua kwamba nchi zao "zisingekuwepo" kama Ufaransa isingepeleka majeshi yake kwenye nchi hizo kupambana na magaidi lakini hawana ujasiri wa kutoka mbele ya umma na kuishukuru Ufaransa.

Muda mfupi baadae, wizara ya mambo ya nje ya nchi ya Chad ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari ambapo ilisema inasikitishwa na mtazamo wa Ufaransa kuhusu nchi za Afrika na ikamwambia Rais Macron ajikite zaidi kushughulikia matatizo yanayowakabili raia wa Ufaransa.

Vilevile waziri mkuu wa Senegal Ousmane Sonko kupitia mitandao ya kijamii alimjibu Rais Macron kwa kumwambia kuwa Ufaransa haina uwezo wa kuilinda nchi yeyote na kama isingekuwa maaskari kutoka Afrika waliokwenda kupigana upande wa Ufaransa wakati wa vita kuu ya pili ya dunia, hadi leo Ufaransa ingekuwa chini ya utawala wa Ujerumani.

Inawezekana Ufaransa ndio nchi ya Ulaya inayopoteza ushawishi kwa kasi barani Afrika kwa sasa. Hii ni kutokana na mapinduzi yaliyozikumba baadhi ya nchi za Afrika Magharibi katika miaka ya hivi karibuni pamoja na kuongezeka kwa umaarufu na ushawishi wa viongozi wa nchi zinazounda umoja wa nchi za Sahel ( AES).
 
Wenzie walishtuka mapema wakabadili mbinu, he is too late
 
Just imagine kijana anafanya mapenzi na mwanamke ambaye ana mtoto mkubwa kumzidi yeye, just imagine. 😃 joke
Unasemaa ? 😂 joke tu
images - 2025-01-07T105744.856.jpeg
images - 2025-01-07T105708.389.jpeg
 
Back
Top Bottom