Status
Not open for further replies.

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,713
13,463
0BD73648-CA3A-447C-A1B2-7AA9DC311BC8.jpeg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Joseph Magufuli amefariki dunia.

Taarifa rasmi iliyotolewa kwa umma na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan kupitia Televisheni ya Taifa (TBC) leo usiku Machi 17, 2021 saa 5 usiku imeeleza kuwa Rais Magufuli amefariki dunia leo majira ya saa 12 jioni kwa maradhi ya Moyo akiwa katika Hospitali ya Mzena jijini Dar. Rais Magufuli alilazwa tarehe 6 Machi katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa tatizo la moyo wa mfumo wa umeme ambalo limekuwa likimkabili kwa takirbani miaka 10.

Nchi itakuwa katika kipindi cha maombolezo kwa siku 14 na bendera zitapepea nusu mlingoti

Tanzia(1).png





WASIFU:
Dkt, John Joseph Pombe Magufuli ni mwalimu na mtalaamu wa kemia akiwa na Shahada ya Uzamivu (PhD).

Kuzaliwa
Alizaliwa Oktoba 29 mwaka 1959 huko Chato mkoani Geita, Kaskazini magharibi mwa Tanzania.

Elimu
Magufuli alipata elimu ya msingi katika shule ya msingi Chato kuanzia mwaka 1967 hadi 1974.

Mwaka 1975 alijiunga na Seminary ya Katoke iliyo Biharamulo, Kagera kwa Elimu ya sekondari na kisha kujiunga na shule ya sekondari ya Lake iliyoko Mwanza hadi 1978 alipohitimu.

Mwaka 1979 alijiunga na shule ya Sekondari ya Upili ya Mkwawa, Iringa kwa ajili ya masomo ya kidato cha tano na sita na kuhitimu Mwaka 1981.

Mwaka 1981 hadi 1982 alisomea Stashahada (Diploma) ya Ualimu wa masomo ya Sayansi katika Chuo cha Ualimu cha Mkwawa, Iringa Masomo makuu yakiwa Kemia na Hisabati

Akiwa kazini, Magufuli aliamua kujiendeleza kwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mwaka 1985 hadi 1988 alipotunukiwa Shahada ya Ualimu katika masomo ya Kemia na Hisabati.

Mwaka 1991 hadi 1994 alisomea Shahada ya Uzamili ya Kemia (Msc. Chemistry) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Tanzania na Chuo Kikuu cha Salford, Uingereza

Mwaka 2009 alitunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) ya Kemia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Mafunzo ya Kijeshi
Kati ya Mwaka 1983 na 1984, Magufuli alipitia mafunzo ya kijeshi kwa mujibu wa sheria kwenye Kambi za Jeshi la Kujenga Taifa Makutupora - Dodoma, Makuyuni - Arusha na Mpwapwa - Dodoma.

Kazi
Baada ya kufuzu Stashahada ya Ualimu, alifundisha masomo ya Hisabati (Mathematics) na Kemia (Chemistry) katika shule ya Sekondari Sengerema kuanzia mwaka 1983.

Baada ya hapo akafanya kazi kama Mkemia katika Chama cha Ushirika cha Nyanza huko Mwanza hadi mwaka 1995.

Siasa
Nyota ya Magufuli liana kung’aa katika siasa, alipogombea na kushinda ubunge eneo la Chato mwaka 1995. Mwaka huo huo aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi, nafasi aliyohudumu hadi Mwaka 2000.

Baada ya uchaguzi Mwaka 2000, aliteuliwa kura Waziri wa Ujenzi, nafasi aliyohudumu hadi Mwaka 2006 alipohamishwa kwenda Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi alipokaa hadi Mwaka 2008.

Mwaka 2010, aliteuliwa kawa Waziri wa ujenzi kwa mara ya pili na kudumu kwenye nafasi hiyo hadi Mwaka 2015.

Urais
Mnamo Tarehe 12 Julai 2015, alichaguliwa kuwa mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Akiwa na Samia Suluhu Hassani kama mgombea mwenza.

Tarehe 29 Oktoba 2015 alitangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ushindi wa kura 8,882,935 sawa na 58.46%.

Magufuli aliapishwa kama Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 5 November 2015.

Muhula wa Pili
Mnamo tarehe 30 Oktoba 2020, Tume ya Uchaguzi Tanzania ilimtangaza John Pombe Magufuli kama rais kwa muhula wa pili kwa kupata kura milioni 12.5 hiyo ikiwa ni sawa na asilimia 84 akiwa amemshinda mshindani wake wa karibu, Tundu Lissu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) aliyepata kura milioni 1.9.

Baadhi ya Nukuu zake:
"Ni nafuu wakuchukie... uonekane wewe sio Mwanasiasa mzuri (Unpopular) kwasababu sikuja kutafuta Mchumba. Nimekuja Kufanya kazi za Watanzania." - Septemba 7, 2017


Soma pia:

1) Nukuu toka kwa Rais Magufuli (QUOTES)

2) Magufuli: Kila atakayetaka kuiokoa nafsi yake atapoteza...


VIDEO:




Baadhi ya Hotuba zake:

Hotuba ya Rais Magufuli kufungua Bunge la 12: Utumbuaji majipu utaendelea ili kuhakikisha Watumishi wanatenda kazi kwa mujibu wa Sheria na Kanuni - Novemba 13, 2020

Bungeni Dodoma: Rais Magufuli avunja Bunge la 11. Asema ajira 6,032,299 zimetengenezwa, Viwanda vipya 8,477 vimeanzishwa - Juni 16, 2020

 
Samia Suluhu akiwa kama Rais ajae, ana uwezo wa kuturudisha kwenye nchi ya maziwa na asali au kuendeleza ubabe wa toka 2015.

Afufue uchumi uliosinyaa na kuleta sera nzuri zenye kuleta ustawi na mshikamano wa taifa letu. Palipo vunjika aunganishe, walioumizwa wapewe faraja.

Pia tusidhihaki wapakwa mafuta.

JPM apumzike anapostahili.
 
Apumzike kwa Amani

Kila jambo na wakati wake lakini yote hayawezi kututenga na upendo wa Mungu

Kuna wakati wa Furaha, huzuni, Mateso, Shida na Mahangaiko. Yote hayo tunayopitia hayawezi kututenga na upendo wa Mungu

Nitakulilia Mungu wangu daima wakati wa shida, Raha, Taabu na Furaha, Nitaziungama dhambi zangu daima mbele yako

Wote tupo safarini, Safari yetu ni moja na hapa Duniani tunapita

Tuishi kwa upendo, kusaidiana na kuombeana wakati wote bila kujali tofauti zetu za kimaisha, kisiasa au kiuchumi

Eee Bwana Tuhurumie, Tuhurumie tunajileta mbele yako kwani sisi ni wakosefu kwa mawazo, Maneno na vitendo, Tufanye kuwa watu wapya maishani mwetu kwa msamaha wako

Eee Bwana wewe ndie Wajua maisha yetu dakika moja ijayo, Hakuna yeyote ajuae kesho yake kama ataamka mzima au mfu

Tuhurumie sisi wakosefu, Tusamehe dhambi zetu
 
Alikuwa na mema yake na mabaya yake, kama tulivyo wengine wote. Apumzike kwa amani anapostahili.

Taarifa nzito kwa kweli, halijawahi kutokea hili kwenye nchi yetu Rais kufariki akiwa madarakani, Mungu atuvushe salama.

Nimekumbuka maneno ya Mfalme Suleiman alipoulizwa na Mungu nikupe nini, akamjibu naomba hekima niwaongoze vizuri hawa ulionipa.
 
Maisha ni fumbo.

Tumia muda wako kufanya mazuri kwani siku moja utapotea kama nukta moja ya mchanga baharini na kitakachobaki ni historia yako iwe ya mabaya au mazuri.
Hata kama ulimchukia au kumpenda ila kifo ni kifo. upendo na chuki vyote havina faida sasa hivi.
Binadamu wenye moyo watanielewa.

Sifurahii wala Sisikitiki.

Have a good sleep mr. president.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom