Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,088
- 4,887
Traore amejizolea umaarufu mkubwa Duniani hasa kwa ulinzi wa rasilimali. Amekuwa na nguvu kubwa ya mapokezi kila anapokwenda. Amekuwa mwana mapinduzi anayetisha mabepari kwa misimamo yake.
Natambua Watanzania siyo wafuatiliaji wa siasa za nje, ila naamini ujio wa Traore ukifanyiwa matangazo vizuri nje ya nchi itakuwa sehemu yakitangaza nchi kiuchumi na kiutalii.
Katika mbinu za kuitangaza nchi tunayo kila sababu ya kuruhusu vyombo vyetu vya habari vifanye matangazo makubwa kuanzia mapokezi yake hadi hotuba zake.
Pia soma > Rais Ibrahim Traore wa Burkina Faso alikaa Jukwaa kuu na bunduki yake wakati wa uapisho wa Rais mpya wa Ghana
Tunapaswa kutumia fursa ya ujio wake kama njia ya kuifanya Duniani kufahamu ulinzi wa rasilimali zetu upo vipi na nini wafanye kuja kuwekeza.
Vyombo vya magharibi vitataka kumsikia anasema nini kuhusu nishati ! Vitataka kusikia anaeneza sumu gani kuwafanya waafrika wafikirie kujikomboa kwenye ukoloni Mamboleo. Fursa hii ina faida kwetu hasa pale tutakapounganisha matangazo ya nchi yetu na ujio wake.
Tunatakiwa kuitangaza Tanzania kwa kila opportunity tunayopata. Tuache kujifungia na ujamaa usio na tija. Chana wameweza na sasa wanajadiliwa Duniani kote, tutangaze nchi kibepari tuachane na ujamaa wakuabudi wazungu