Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,211
- 3,611
Kuna malalamiko mitaani na kwenye mitandao ya jamii kama Insta kuhusiana na mchakato (unaotafsiriwa kama ni dhalimu) wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA kuendesha ajira kwa mfumo ambao unasemekana UMEKOSA UWAZI na kuzua hofu ya ufisadi wa ajira kupata kutokea kwa miaka 8 iliyopita.
Inayoitwa serikali ya awamu ya 5 ilirudisha ajira za TRA Utumishi ili kutenda haki kwa Watz wa madaraja yote ya maisha kufuatia malalamiko yaliyokithiri ya Mamlaka kutokuwa na uwazi katika kuajiri.
Awamu ya 6 ikatengua uamuzi huo na kuirejeshea TRA mamlaka ya kuajiri itakavyo, anasema mhanga mmoja wa ajira zilizohitimika hivi karibuni.
Anaendelea kusema TRA ilitangaza nafasi kwenye ukurasa wake, ikachuja waombaji na kutangaza majina yao kwenye ukurasa wake pia, ikachuja tena mara ya pili na kuita wasailiwa kwenye ukurasa wake.
Usaili ukafanyika kwa awamu 2 za mtihani na mahojiano. Matokeo ya usaili hayakutangazwa kokote kwa uwazi kuonyesha nani amechaguliwa na nani hakuchaguliwa.
Kwamba waliochaguliwa walipewa taarifa kwa baruapepe kila mmoja kivyake jambo ambalo linalalamikiwa kwamba limekosa uwazi.
Kwamba baadhi ya waliokosa wakapata habari tu kutoka kwa wenzao waliochaguliwa kwamba tayari wako kazini baada ya kumaliza mafunzo.
Hali hii ilitishia kuirejesha Rwanda kwenye kimbari ya 2 baada ya kimbari ya 1 na Mhe. Rais Paul Kagame hakulifumbia macho hata kidogo na kuchukuwa hatua za makusudi na za dharura kusahihisha mwelekeo wa taifa ikiwemo kwenye suala zima la ajira ambalo lilighubikwa na ukabila. Akaondoa dai la kabila kwenye nyaraka zote za nchi kwa sekta zote 2 rasmi na binafsi.
Tusipochukua hatua kujikosoa kama taifa iko siku tutapewa haki kikabila, iko siku tutapewa haki kwa ukanda, iko siku tutapewa haki kwa kigezo cha ukazi wa pande 2 za muungano, iko siku tutaajiri kwa kuangalia itikadi za kisiasa na kadi za uanachama wa vyama vya siasa kutumika kama moja ya viambatanisho vya nyaraka za kuomba ajira.
Binafsi nashauri ajira hizo zitenguliwe zoezi lianze upya kwa kuweka chombo huru cha kuisimamia TRA inaporudia kuajiri upya hadi hapo Utumishi itakapokasimiwa rasmi dhamana na jukumu hili adhimu kwa ustawi na utangamano wa taifa.
Rais tengua uamuzi wako rudisha ajira za TRA Utumishi.