A
Anonymous
Guest
Kwa kipindi kirefu sasa rais wetu, mama Samia Suluhu Hassan amekuwa akihangaika kubuni mbinu mbalimbali kwa lengo la kutatua kero za wananchi.
Sisi wananchi wa kata ya Lukobe, Morogoro tunathamini na kuunga mkono juhudi hizo. Ila kwa bahati mbaya kuna baadhi ya watendaji wake hawathamini juhudi hizo na ni kama kuna hujuma za makusudi.
Hili linadhihirika kwa watendaji wa ngazi zote za serikali kuanzia kitongoji (Mgudeni) hadi mkoa (Morogoro) ambapo miradi karibu yote haikamiliki na hakuna hata ufuatiliaji wala uwajibishwaji.
Kwa ufupi; barabara zetu hazipitiki kwa sababu zina mitaro na sio mashimo, yaani hakuna hata ukarabati wa kawaida. Kinachosikitisha zaidi ni upigaji wa wazi (hata maamuma anang'amua) wa pesa za miradi na hakuna uwajibishwaji. Hayo yapo katika miradi mbalimbali ambayo utekelezaji wake hauridhishi hata chembe ikiwemo ujenzi wa mfereji wa kuzuia mafuriko kandokando ya barabara kati ya Kwawagogo hadi Mgudeni ambapo pesa imeliwa na sasa mifereji imegeuka mahandaki na mazalia ya mbu.
Mradi mwingine dhaifu ni wa mamlaka ya maji (MORUWASA) ambapo imechimba mitaro ya kupitisha bomba za maji kando kando ya mifereji (mahandaki) iliyotelekezwa na TARURA na kwa pamoja wamevuruga kabisa hata njia za miguu hivyo kukatisha kabisa mawasiliano ya barabara kati ya mgudeni na sehemu za jirani.
Mbali na miundombinu mibovu, kata ya Lukobe imesharipotiwa katika vyombo mbalibali kuwa kinara cha uhalifu na hakuna hatua madhubuti zinazochukuliwa.
Kwa ujumla wananchi tumechoka ila hatuna pa kukimbilia. Tunaomba raisi wetu, Mh. Dkt Samia Suluhu angalau atusaidie kuwaamsha viongozi wetu waliolala.