Rais Samia: Ukimya wangu siyo Ujinga na Kuropoka kwao siyo werevu

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,944
10,591
RAIS SAMIA“Niliwahi kusema na hapa nataka nirudie tena kwa msisitizo, Ukimya wangu sio ujinga, na wala kuzungumza sana kwa wale wanaozungumza sana sio uelevu hata kidogo, kuzungumza sana ni udebe tupu tu haliachi kuvuma lazima litavuma na anaenyamaza kimya sio mjinga ni mtu anayetafakari mambo, kwa hiyo Ukimya wangu si ujinga na kuropoka kwao sio uelevu”

 
Ndugu zangu Watanzania,

Kwa hakika leo hii Rais Samia ametoa hotuba nzito sana,hotuba ya karne,hotuba ya mamlaka ,hotuba ya viwango ,hotuba yenye kugusa kila kitu,hotuba ya Amiri Jeshi Mkuu na Mkuu wa Nchi,hotuba yenye kujiamini na UKWELI mtupu,hotuba ya kijasiri,hotuba yenye kutetea hadhi na heshima ya Taifa letu,hotuba yenye kuonyesha namna kiongozi anapaswa kuwa na hotuba yenye kuonyesha njia.

Ni hotuba ambayo nawashaurini watanzania wote muitafute na kuisikiliza yote yenye Dakika 57.Rais Samia ni kiongozi imara ,jasiri,madhubuti,shupavu na mwenye msimamo usiyo yumba wala kuyumbishwa. Ameonyesha ni kwanini mamilioni ya watanzania wanataka aendelee kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.Ameonyesha ni kwanini kati ya wanawake wengi waliopo hapa Nchini alipewa yeye nafasi ya kuwa Mgombea Mwenza Mwaka 2015.

Leo katika hotuba nzito na yenye kugusa hisia za watu amesema kuwa Ukimya wake siyo Ujinga na wala kuropoka kwao siyo werevu. Amezungumza haya katika kukemea na kuweka msimamo wake na serikali yake kuwa hata kuwa tayari hata kidogo kumvumilia wala kumfumbia macho mtu yeyote yule atakaye taka kuharibu amani na utulivu wa nchi.

na kwamba wale wanaofanya kazi ya kuropoka kujaribu kuchochea machafuko au kuvuruga amani au kuleta uasi au kuleta uchonganishi na kuvuruga tunu yetu ya amani watashughulikiwa haraka sana kwa mujibu wa sheria . Na kwamba waache mara moja kwa kiwa intellegensia ya Nchi hii ni kubwa sana na kamwe hawawezi kupanga kufanya maovu yao pasipo au bila serikali kujuwa na kupata taarifa na mipango hiyo.

Rais wetu ameapa kuwa atalinda tunu ya amani ya Nchi Hii kwa gharama zote. Na kamwe hatamvumilia mtu yeyote yule atakayejaribu kuichezea amani yetu.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Speech ya samia leo ni declaration, yaani rasmi kawapa leseni akina Mafwele wenzake kuendeleza utekaji, kujeruhi, kupoteza na kuua wapinzani na critics wa utawala.

Watanganyika tujiandaeni ngoma hii bado mbichi kabisa,mpaka kufika Dec/2025 kila nyumba bara itakuwa na msiba usoisha.
 
Speech ya samia leo ni declaration, yaani rasmi kawapa leseni akina Mafwele wenzake kuendeleza utekaji,kujeruhi,kupoteza na kuua wapinzani na critics wa utawala. Watanganyika tujiandaeni ngoma hii bado mbichi kabisa,mpaka kufika Dec/2025 kila nyumba bara itakuwa na msiba usoisha.
Naona waropokaji mmeanza kupiga mayowe yenu hapa.Maana mlikuwa mnajifanya muda wote kutoa maneno machafu na ya hovyo hovyo tu bila ushahidi wa aina yoyote ile
 
Kashaanza kuchanganyikiwa sasa huyu mama

Shida ya huyu Maza analazimisha kupendwa lakin ukweli utabaki kwamba raia hawampendi
Hivi kuna mtu anaweza kumfikia Rais Samia kupendwa hapa Nchini? Nani anapendwa hii nchi kama ilivyo kwa Rais Samia?
Screenshot_20240805-224054_1.jpg
 
RAIS SAMIA“Niliwahi kusema na hapa nataka nirudie tena kwa msisitizo, Ukimya wangu sio ujinga, na wala kuzungumza sana kwa wale wanaozungumza sana sio uelevu hata kidogo, kuzungumza sana ni udebe tupu tu haliachi kuvuma lazima litavuma na anaenyamaza kimya sio mjinga ni mtu anayetafakari mambo, kwa hiyo Ukimya wangu si ujinga na kuropoka kwao sio uelevu”
Rais Samia acha ngonjera nchi inateketea kwa ujinga wako!
 
Back
Top Bottom